Wadau, nimejaribu kufuatilia matukio ya hivi karibuni na coverage yake ninaona kama sisi tuliokuwa wagumu kuamini kama ZZK anatumiwa na mahasimu wa CHADEMA, kuanza sasa kuamini kuwa ni kweli huyu bwana anatumiwa.
Matukio ya kupigiwa chapuo kwa nguvu na wana CCM, na kupata corerage kuubwa kwa msaada wa wana CCM, inatupa wasiwasi sisi matomaso na kupata majibu dhahili kuwa sasa tunaona ZZK akiwa upande wa pili na akitumiwa kweli kuiangamiza CHADEMA, Tumeona coverage ya Star TV, na redio pamoja na magazeti kadhaa ambayo kwa kawaida ni vyombo vya habari hasimu kwa CHADEMA, sasa dhahili vikimuunga mkono na kutoa coverage ya bure, kama ni bure kweli, kwa ZZK and company, kweli sasa tumeanza kufunguka macho na kuona jinsi bwana Zitto alivyo na mpango mkakati wa kuiangamiza CHADEMA.
Maandamano na mikutano ambayo asilimia 90 ni wana CCM wa mkoa especially wa Kigoma yanatia wasiwasi, je Zitto hajui kuwa wanachama wa CCM ndio wana mbackup? Kama anajua lengo lake ni nini? Je anadumisha chama au anasambaratisha chama?
Kwa viongozi wa CHADEMA mikoani na mawilayani, ninajua wengi wenu mtakuwa mmepata pesa japo kidoogo kutoka kwa wale waendesha mpango wa ondoa CHADEMA, Mwigulu and the likes, lakini jueni tuu, mambo ya usaliti mwisho wake daima sio mzuri! Tunajua baadhi ya misemo ya viongozi wa juu wa CHADEMA ni kula CCM kura CHADEMA, hebu changanyeni akili na mle tuu CCM, kama wakiwaletea vijihela vyao, lakini roho ya uasi muachane nayo kabisa, ZZK you are a backslider, slide back and come into your senses common!
Maajabu, thread plus vitu vingi tuu, wawakilishi wakuu ni wana CCM, Tunaona mtu kama Mohamed Mwaupete, Hamm-d, Mwampamba, Machange, Ifweero na wengine wa design hiyo ndio haswa wanaopata habari za kina toka kwa zitto, kwanini? Je organizers wa mikutano ya Zitto ni wana CHADEMA? Hebu jiulizeni ndugu, kama ni wanaCCM ni kwanini? Au ni kwa sababu Zitto ni mzalendo, kweli inaweza ikawa ni hivyo?
Sasa kwa kamati kuu, kosa kubwa mnalolifanya ni kuacha hili jambo lidumu kwa muda mrefu, hebu fanyeni mambo kwa haraka na yaishe kuliko kukaa hivi huku adui akitekeleza mambo yake kwa umakini, mnatakiwa musurprise msisubili surprise! Fanyeni haraka , kama ni kumfukuza mtuhumiwa on which naona ndio best option fanyeni hivyo, na kama ni msamaha kama mtaweza fanyeni hivyo, kukaa kwenu kimya mnakiangamiza chama! Mnakumbuka ya NCCR Tanga? Mkutano wenu unaweza ukatibiliwa na Mayuda watakaowasaliti kwa tamaa za hela hivyo utabiri wa Sheik Wassira kuwa chama kitasambaratika kabla ya 2013 ukawa kweli!
Nawasilisha!