Dr.Slaa: Zitto anaweza kufukuzwa kabisa

Dr.Slaa: Zitto anaweza kufukuzwa kabisa

Status
Not open for further replies.
Tangu lini mjinga akaujua ujinga wake. Povu linawatoka nyie mnaodai Zitto kaonewa, Zitto maarufu kuliko CHADEMA, Zitto maarufu kuliko Dr Slaa yote haya yanawahusu nini? Ndani ya chama chenu kuna matatizo kibao mpaka kufukuzana Uwaziri kwanini hamyashughulikii na kuyamaliza? Kutwa kucha Zitto hivi Zitto vile blah blah blah. Sijamsikia kiongozi yoyote ndani ya MACCM akiwemo Kikwete ambaye inasemekana ni marafiki wakubwa Mang'ula, Kinana, Nape, January au mwingine yeyote aseme kuna opportunity hapa ya kuimaliza CHADEMA kwa kumpa uanachama Zitto ambaye ni maarufu kuliko CHADEMA na pia ni maarufu kuliko kiongozi yeyote wa CHADEMA. Povu zinawatoka ili abaki CHADEMA. Mmeshawahi kujiuliza kwanini Kikwete, Mang'ula, Kinana, Mwigulu, Nape, Pinda hawachangamki katika kumsajili Zitto ili naye ajiunge na MACCM!? Tafakari kwa kina badala ya kuendelea kutoa povu.


umekamatwa mkuu

matusi na povu la nini?? kama umeamua kuweka akili mfukoni kwa chuki zako kwa zitto

sio wote wajinga
 
Zitto Kabwe
Tatizo la baadhi yetu ni kuishi maisha ya uongo na fitna.

Sina tatizo na Dr Slaa. Ni Katibu Mkuu wa chama na amefanya mengi mazuri kufikisha chama hapa.

Sasa hivi watu wanajitahidi sana kuchochea kwa kugeuza maneno ionekane kwamba nina tatizo na Katibu Mkuu wangu.

Ziara yangu Kigoma haikuwa 'kumjibu Dr Slaa' kama inavyosemwa. Sina cha kumjibu Katibu Mkuu wangu. Ninalo jukumu kama mwanachadema kutoa maelezo kuhusu tuhuma dhidi yangu na pia kuongea na wananchi kuhusu matatizo ya nchi yetu.

Hayo sio majibu kwa Dr Slaa kwa sababu ni uonevu kusema Dr Slaa ni Kamati Kuu.

Mimi nitaendelea kutumikia wananchi wa Kigoma na watanzania wote kama mwanachadema na Mbunge. Anayesema naidhoofisha Chadema ni muongo na apuuzwe.
 
Huyu mzee gongo anayobitetea inamponza, maana hawezi kuutubia mkutano bila kunywa gongo na hii ni hatari kwa Chama maana kuropoka kumepita kiasi.
 
Zitto Kabwe
Tatizo la baadhi yetu ni kuishi maisha ya uongo
na fitna. Sina tatizo na Dr Slaa. Ni Katibu Mkuu
wa chama na amefanya mengi mazuri kufikisha
chama hapa.
Sasa hivi watu wanajitahidi sana kuchochea kwa
kugeuza maneno ionekane kwamba nina tatizo
na Katibu Mkuu wangu. Ziara yangu Kigoma
haikuwa 'kumjibu Dr Slaa' kama inavyosemwa.
Sina cha kumjibu Katibu Mkuu wangu.
Ninalo jukumu kama mwanachadema kutoa
maelezo kuhusu tuhuma dhidi yangu na pia
kuongea na wananchi kuhusu matatizo ya nchi
yetu. Hayo sio majibu kwa Dr Slaa kwa sababu ni
uonevu kusema Dr Slaa ni Kamati Kuu.
Mimi nitaendelea kutumikia wananchi wa
Kigoma na watanzania wote kama
mwanachadema na Mbunge. Anayesema
naidhoofisha Chadema ni muongo na apuuzwe.
 
Ni udhaifu mkubwa kushindwa kumfukuza Zitto.
Ukweli mchungu, Pia tunashukuru sana kwa Kamati kuu kutudhihirishia na kuthubitishia kauli ya Zitto kuwa "ZITTO NI CHADEMA NA CHADEMA NI ZITTO".

samahan Mkuu kwa kwenda nje ya mada lakin.
 
Last edited by a moderator:
Hizi ni kauli za kisiasa tu ukweli Slaa na Mbowe hawapatani na Zitto.

Umesahau ni za kisayansi, mantinki na kiuelewa zaidi hakuna kupatana na WASALITI wanaopatana nao ni wale wasioelewa wasiliti walichofanya au kutaka kufanya wakanaswa
 
Atamuheshimuje mtu ambaye hajiheshimu?Viongozi wa CDM hawajiheshimu ndio maana hawaheshimiwi na mwana CDM yeyote mwenye akili timamu
Mjinga hajijui pole sana Gamba on duty
 
So far zito nni mkubwa kwenye chama,na ninavyoona chadema hawana uwezo wa kumfukuza.
 
Kwani kwa kumfukuza Zitto kwenye chama chama cha CDMkitapata faida gani au Zitto kuwepo chamani kuna sababisha hasara gani kwa CDM?Nadhani ni bora kuangalia pros and cons…, kumvua uongozi kidogo kuna make sense,lakini kumfukuza uanachama kuna faida gani kwa CDM?? Zaidi ya kutufanya tuaminikuna majungu, fitna na chuki binafsi zinazoendelea kati ya viongozi wa CDM na Zitto?
Kumbukeni ali wanadi vijana majimboni kwao mpaka wakapatakura za wananchi wakawa wabunge wa CDM… tulimjua Zitto kabla ya wabunge wenginewengi wa CDM waliopo mjengoni sasa hivi, watu tunahitaji maelewano na umoja kwaviongozi wa CDM sio hizi blah blah.
Sasa mkifukuza uanachama na ubunge wa CDM aliopewa nawananchi nao mtamvua ??? Sasa hapo ndio mtakapo onyesha kwamba pipo power ni kawimbo tu kama kale ka ari zaidi na nguvu zaidi
CCM na uozo wao wote na makundi lakini walau hadharaniwanaonyesha mshikamano (of course ukiacha uvccm wanaokabana kabali mbele yakadamnasi na wamama wanaopeana makavu live), wanavuana madaraka kimya kimya nakuendelea kuvumiliana kama wanachama, wabunge wao wanavuliwa uwaziri, unaibukatibu, uwaziri mkuu etc lakini sio unachama, hii walau inaonyesha heshma kwachaguo la wananchi…wamepitiliza kiasi cha kuwavumilia mpaka wanaopaswakupelekwa mahakamani….
Kwa mwendo huu CCM will be flying high in 2015, sijuitukimbilie wapi masikini sisi!
 
BABU wewe tulia tu hio
ya ZZK ni trela Subiri picha kamili hio ndio habari ya mujini! Jiandae
kurudi KARATU huo UKATIBU MKUU Unauachia siku si nyingi.

na wewe unautaka ukatibu mmkuu kweli Viloba vinatuhalibia vijana.
 
Hujitambui weye!!! Fuatilia mijadala kwa kina ili uelewe kinachoendelea badala ya kukurupuka na kuropoka ropoka bila mpango. Upo ushahidi wa kutosha kuhusu usaliti wa Zitto humu ndani kaupitie kwa utulivu badala ya kutoa povu bila mpango.
siko narrow minded kama wewe kibavicha, naangalia mambo kwa mapana yake.
kabla ya 2009 Zitto alikuwa mtakatifu na hero kwa chadema ila alipoenda kuchukua form ya kumchallange mkwe wa hayatulah mtei ndo tunaona haya yote. na tangu kipindi kile mpaka leo bado mnaendelea kumchafua. we all know. tatizo ni uenyekiti. Zitto ni yuleyule ila mnamchafua kwa makusudi. siamini kama kweli kuna mkono wa ccm. hatujasahau yaliyomkuta chacha wangwe kwa kumchallange mkwe wa hayatulah mtei.
kama mbowe anajiamini katika uongozi wake kwa nini amhofie zitto wakati kapu lakura bado lingembeba?
hata kama hatujui kusoma hata picha ukutani hatuioni? funguka, otherwise utatumika sana.
 
Hamasa imepungua kutokana na malumbano yanayo endelea ndani ya chama huku hakuna kiongozi anaye onesha kupata busara ya kuutatua mzozo huu. Kwa maoni yangu ni kwamba hata Dr. Slaa ni tatizo.

Sielewi ni vipi katika mazingira ya sasa yalivyo kama Zitto akiomba kufanya mkutano kwa taratibu za chama atakubaliwa! Na ktk mazingira haya sioni hata uwezekano wa CDM hata ikimvua uanachama Zitto kama watafanikiwa kumuondoa Bungeni. Wajifunze kutoka kwa Kafulila na NCCR MAGEUZI na Hamad Rashid na CUF.
mkuu hao ni sikio la kufa,
ukiangalia haya mambo kwa mapana yake utayaelewa yafuatayo.
kabla ya 2009 Zitto alikuwa mtakatifu na hero kwa chadema ila alipoenda kuchukua form ya kumchallange mkwe wa hayatulah mtei ndo tunaona haya yote. na tangu kipindi kile mpaka leo bado mnaendelea kumchafua. we all know. tatizo ni uenyekiti. Zitto ni yuleyule ila mnamchafua kwa makusudi. siamini kama kweli kuna mkono wa ccm. hatujasahau yaliyomkuta chacha wangwe kwa kumchallange mkwe wa hayatulah mtei.
kama mbowe anajiamini katika uongozi wake kwa nini amhofie zitto wakati kapu lakura bado lingembeba?
hata kama hatujui kusoma hata picha ukutani hatuioni? wafunguke, otherwise watahangaika sana.
 
Who the hell is he to even be a threat anyway?

Damn it!! ask babu bahau will tell all! They boy is big no question about it! ain't ----ing nobody gonna stop him!! He is an avalanche!! do you know why all those suckers can't sleep??? !! he is big and he can be whoever he want to be so if you suckers can't stand him just suck it!!! he raised on his own way; Chadema didn't do a thing! his people loved him so much wherever he they will go; so you hatters drop dead and go to hell!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom