Dr.Slaa: Zitto anaweza kufukuzwa kabisa

Dr.Slaa: Zitto anaweza kufukuzwa kabisa

Status
Not open for further replies.
Dr.W.Slaa anajaribu kisema kila kinacho fanywa na wanao mpenda na kimuunga mkono zitto basi kime andaliwa na zitto?

Dr.W.Slaa atwambie ni kipengele gani na ni sheria hipi inatoa nafasi mtu kuhukumiwa kwa kosa la mwingine?

Dr.W.Slaa anajaribu kusema kamati kuu yote itakubaliana na mawazo yake ya kumfukuza mtu kwa kuwa wafuasi wake wanataka kuandamana na wameandaa document za kusaini?

Dr.W.Slaa anajaribu kutwambia kamati kuu yote ina fikiri kama yeye na itafanya maamuzi kilingana na matakwa yake?

Dr.W.Slaa anajaribu kusema wafuasi wake wanao mtukana zitto au watu wengine huwa ana watuma?
Dr.W.Slaa kwanini unajaribu kuonesha umeiweka kamati kuu mfukoni.
ZIto mla rushwa, anatumiwa na CCM kubomoa chama, wewe si mwana mapinduzi, kaboreshe sera za chama chenu, acha kufukuza mawaziri sio suluhisho. Dhaifu wakubwa.
 
nafikiri anachofanya zzk sio sahihi kwa afya ya chama anachodai kukipigania nafikiri analipa fedha za magamba kwa style hii mpya
 
hivi, kama cmd mnaweza kumfukuza zzk naomba mniambie mnacho subiri?
 
nguvu ya mamba iko ku mayi.hebu aende mwanza,arusha mbeya iringa tuone.awahonge waha hukohuko cdm mwendo mdundo hana jipya subiri wamtimue ndo mtajua nani maarufu kati ya cdm na zzk.wanafiki wanaomdanganya itakula kwenu mmoja kasha timuliwa uwaziri ambae walikuwa lao moja.afukuzwe tu
 
Who the hell is to even be a threat anyway?

He is a threat na ndio maana hatoki kwenye midomo yao, yani hawaishi kumtaja. Kama wanaona he is not a threat then kwanini wazidi kumpandisha kwa kumuongelea kila kukicha, to hell with politics
 
Dr.W.Slaa anajaribu kisema kila kinacho fanywa na wanao mpenda na kimuunga mkono zitto basi kime andaliwa na zitto?

Dr.W.Slaa atwambie ni kipengele gani na ni sheria hipi inatoa nafasi mtu kuhukumiwa kwa kosa la mwingine?

Dr.W.Slaa anajaribu kusema kamati kuu yote itakubaliana na mawazo yake ya kumfukuza mtu kwa kuwa wafuasi wake wanataka kuandamana na wameandaa document za kusaini?

Dr.W.Slaa anajaribu kutwambia kamati kuu yote ina fikiri kama yeye na itafanya maamuzi kilingana na matakwa yake?

Dr.W.Slaa anajaribu kusema wafuasi wake wanao mtukana zitto au watu wengine huwa ana watuma?
Dr.W.Slaa kwanini unajaribu kuonesha umeiweka kamati kuu mfukoni.

Ndugu Ruta utasubiri sanaaaa kupata hayo majibu. Kwa mawazo yangu binafsi ninaona kama kufukuzwa si lazima wajumbe wote wa CC wakubaliane ila perc kama majority ifikiwe! Hata wakati maumuzi ya CC yaliyopita si kwamba wote walikubaliana ila majority walisema ni sawa. Huyu jamaa inabidi aondoke kama si leo hata kesho na kama CDM kufa ife kuliko kuwa na mtu wa namna hii. Haya ni mawazo yangu kama utanihukumu fanya hivyo ila huyu jamaa haitajiki na kama akienda ccm si muda mrefu atakuwa kiberiti cha njiti tu.
 
what zitto is doing is not acceptable in modern politics,asijione bila yeye chadema utakufa,thats day dreaming.anajimaliza politically.
zitto imetuangusha vijana,umekubali kununuliwa kuivuruga cdm,upinzani unayuba coz of your selfishness,what a shame!
 
Ninapomuona Zitto wa kawaida ni pale hajifunzi frm past experience ya waliwahi fukuzwa CDM na hata vyama vingine. Zaidi ni pale vitangulizi vyake vimepotea kabisa, i.e Juliana Shenzi et al.

kila mtu ana maisha yake, kumbe kuandiwa magazetini kila siku ndio ujanja?? believe me , hao unaowasema wako kimya ndio wanaokula nchi na kusaza, wewe endekeza ujinga wa kuandikwa kila siku

ama kweli
 
Viongozi wa CDM, Kuchukua hatua sahihi kuhusu Zitto " is Now or Never!"
 
Chadema ili kukata mzizi wa fitina mfukuzeni basi Zitto.
Hivi Ritz ndani ya CCM una bifu na Kamati Kuu ya CCM, unaenda Kigoma kufanya Mkutano Mabango yana wadhalilisha viongozi wa CCM na mabango yote hayana bendera ya CCM bali ya Taifa (Ila huna cheo chochote serikalini cha kukupa status ya kututumia bendera ya Taifa) na unasema unaipenda CCM sana ila unapambana dhidi ya uhafidhina ndani ya CCM, na isitoshe unadai wewe utakuwa wa mwisho kutoka CCM kwa hiyari yako siyo kufukuzwa, hivi CCM hii unayoijua wewe unadhani itakufanyaje?????
 
Katibu wa Chadema Wilaya ya Kasulu ameufahamisha Umma wa Watanzania wote kuwa Mkutano wa CHADEMA Kasulu ni halali,na ujio wa Zitto Kabwe kwenye Mkutano huo upo kihalali kwa kufuata misingi ya katiba ya Chadema.
Akizungumza moja kwa moja kutoka kasulu kwenye Mkutano wa Chadema uliokuwa unarushwa Live na Redio kadha ikiwamo Kwazulu,Katibu wa CHADEMA Bwana. MASOUD aliwafahamisha wananchi kuwa Zitto amefika KASULU kwa Mwaliko wa Chama kwa kufuata hatua zote.
Masoud alilazimika kufungua Katiba ya CHAMA hadharani(Star tv) na kusoma majukumu ya Wabunge wa chama ambapo moja wapo ni kujenga na kueneza sera za chama maeneo yote ya nchi Lakini Mbunge huyo atakwenda nje ya jimbo lake kushiriki shughuli za kisiasa kwa Mwaliko wa uongozi husika wa Jimbo husika.
Hivyo uwepo wa Zitto Kasulu ni halali na umefuata kanuni za Chama,Katibu aliongeza kuwa wanajisikia furaha kwa Zitto kukubali kufika Kasulu licha ya kutingwa na majukumu ya kujenga nchi,"Mh.mbunge wananchi wako wanakiu sana kusikia
 
ZITTO amechanganyikiwa, kwa sasa anapokea kila ushauri, ni vema afukuzwa uanachama ili apumzike kiakili, kwa sasa anahisi anaweza ku-rescue hali kumbe anatumia njia mbaya kuzidi hata ubaya wa WARAKA uliomfikisha hapo, kwa sasa nanavyunja miiko ya uongozi iliyowekwa CDM, sidhani kwa sasa kama ataweza kujitetea kunasuka katika tope alilojizamisha.tope hilo wasukuma wanaita ikomelo
 
Miaka ya nyuma wakati Dr wenu wa canon anagombania urais niliwahi kusema huyu hafai kuwa rais amejaa udikteta, maisha ya kugawa watu na anapenda kuabudiwa. Hata ile taasisi anayoiongoza pale dar kama chairman katika bodi anaiendesha kama yeye ndio kila kitu. Anaabudiwa kama mungu na hadi jamaa zake wakifika pale wanakuwa kama waungu. Huyo katibu wenu wa chama chenu ambaye anatoa tamko kama hili halafu unaiita chama hichi ni cha demokrasia yenye kuleta maendeleo. Demokrasia hiyo haipo huko labda demokrasia ya utopia yenye kuishi katika nadharia za zidumu fikra za mwenyekiti hakuna mwengine zaidi.

Stephen Wassira aliona mbali na kauli yake itatimia haswa wakimfukuza Zitto. Fukuzilieni mbali msaliti huyo wengine sisi tushangilie mwisho wa chama cha utopian :cool2::spy::rip:
 
Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Dr.Wilbroad Slaa amesema Zitto anaweza kufukuzwa kabisa na amewaonya wafuasi wake waache kutumika kwa kusainishwa document fake, "nawaonya mnaomshauri mnaweza kumpoteza huyu kijana", alisema Dr.Slaa.

Pia, Dr.Slaa amesema yeye kama katibu mkuu hajatoa form zozote zinazodaiwa kuoka makao makuu ambazo zinasambazwa ili zisainiwe.

Dr. Slaa katoa kauli hiyo leo mkoani Tabora wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara.

CHANZO:ITV

Babu ameshaona Kigoma kimenuka! ameambiwa Zitto ana safari za kupita hukohuko anakopita Slaa kumgaragaza kama alivyofanya kigoma.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom