Zito sio mtu wa kuaminiwa kwa madaraka makubwa iwe ndani ya Chama ama madaraka makubwa ya Kitaifa,Mpaka sasa ZZK ameprove failure ndani CHAMA CHAKE. Izingatiwe kwamba mtu wa nia mbili siku zote hutangatanga katika maamuzi yake,Zito anaonesha kuipenda CHADEMA na kwa wakati huo huo kwa usalama wa tumbo lake Na kwa kutafuta kujiongezea umaarufu anaitumikia CCM kwa kufuata maelekezo yote bila kukosea,Ni vigumu mtu aina hii ya akina Zito kutimiza ndoto zake,Na mwisho wa yote ni kukataliwa na pande zote na kubakia kama Garasha mbele ya UMMA WA WATANZANIA.
Tusisahau sio tu uwezo wake Zito ndio uliomfanya akubalike sana hasa kwa Vijana bali Kule kuji-conect na chama makini na sahihi chenye kujali maslahi ya Wananchi kumechangia kwa 75% kujenga na kumtangaza ZZK kukubalika kwa UMMA.
Shida kubwa aliyonayo Zito ni kujiamini sana kunako changanyikana na KIBURI CHA FEDHA,KIBURI CHA UMAARUFU NA TAMAA YA MADARAKA Huku akitabainisha wazi kukosa minofu ya Uaminifu na Uadilifu ndani ya chama chake. Shauku na matamanio ya kutaka kufikia ndoto yake vinam-drive ovyo mpaka kumtoa nje mwendo halali uliosimikwa kwenye misingi ya UADILIFU na kubakia kufuata MISISIMKO inayoletwa na kiu yakutaka kushika nafasi fulani kubwa ndani chama ama Kitaifa.
Ni wazi tena ni ukweli usiyopingika kijana huyu ana Ndoto kubwa kwa siku zijazo ila kwa kukosa Hekima,Utulivu (SUBIRA) amejikuta ameangukia mikononi mwa watu wabaya wenye kujionesha wema macho pake mwenyewe kumbe ni nyoka wenye sumu kali walioshindikana kuvuana magamba. Wako hapo pamoja na Zito kwa kusudi moja kubwa KUIZIMA NDOTO KUBWA YA ZITO,Nitawapa mfano wa mdudu mmoja:- Kwa Lugha ya Kabila langu mdudu huyo anaitwa CHALUNGU.Mdudu huyo hupenda sana kuchimba shimo ama katikati ya njia au kando ya njia na kufanya kashimo (katundu) hako ndio makao yake ya kuishi,Na mdudu ni maarufu sana kwa jina la Kinyaturu CHALUNGU kama nilivyomtaja hapo juu. Tulipokuwa Watoto kila tulipoona nyumba ya CHALUNGU tulifanya hima kuhakiki tumemtoa nje ya nyumba yake hio.Kazi ya kumtoa CHALUNGU ni rahisi sana,unapaswa uwe na zana zifuatazo Macho,mdomo ,Mate,Mikono na Unyasi mwembamba mrefu kwa wastani.
Ukishaukata huo unyasi utautafunatafuna kwa kuulainisha mwisho wa Ncha kisha utauingiza kwenye lile shimo aliko CHALUNGU,mara atakatambua kuna jambo jipya limeingia ndani nyumba yake kwa hasira atang'ata ule unyasi kisha CHALUNGU ATAUSUKUMA kwenda juu ili kuhakikisha kautoa nje ya makao yake,kwa kuwa CHALUNGU hajui kinachoendelea juu ya silaha hio aina ya Unyasi atabakia kuung'ata kwa hasira,Hatimaye mmoja ya vijana akiwa na wenzake watagundua CHALUNGU yupo kwa ishara ya unyasi kucheza cheza huku ukitolewa nje kwa kuja juu.
Kabla CHALUNGU hajautoa huo unyasi kijana mmoja kwa haraka sana ataushika unyasi na kuuvuta kwa haraka kwa vile CHALUNGU AMEUNG'ATA TENA BADO AMEUNG'NG'ANIA KINYWANI MWAKE watafanikiwa kumtoa nje ya nyumba yake huku wakimbamiza chini ya ardhi ngumu njiani.
Baada tu ya kufanikiwa kumtoa CHALUNGU nje ya nyumba yake Kijana au Vijana watacheka kwa dharau na kufurahia kazi walioifanya ya kumtoa CHALUNGU ndani ya makao yake sahihi.Wamemuweza hawezi kurudi tena huko nguvu zake zimekwisha kwa kubamizwa chini ya Ardhi ngumu,hana ujanja tena wakurudi mwenyewe kwenye shimo lake (hio nyumba ya CHALUNGU) Sasa atapigwa na jua kali na kwa kuwa mafuta mengi mwilini mwake atakufa kwa joto kali la jua,Pia sisimizi watamshambulia na kumwuua kabisa na kuitafuna Nyama yake,huo ndio utakuwa mwisha CHALUNGU yule mwenye Kichwa kigumu na mwili laini,Vijana mtaani watabakia na msemo tu,SASA CHALUNGU BASI-KWISHA HABARI YAKE.
"ZITO ZUBERI KABWE TAFADHALI JIFUNZE KWA MDUDU CHALUNGU"
Zito unakumbuka jinsi ulivyoanza siasa kwa mara ya kwanza? kwa vyovyote vile wewe huwezi kuwa mtu mkuu na maarufu kuliko CHADEMA uliyoikuta. Mimi nikukumbushe jambo hili; Usisahau katika Ndoto zozote alizonazo mtu awaye yote kwenye maisha yake ANAHITAJI WATU SAHIHI ILI KUFIKIA LENGO NA HATMA NJEMA YA NDOTO ZAKE.
Zito unaonekana umejisahau umejiruhusu kuingia mikononi mwa watu wanaotamani Vipawa vyako wanakuchekea, huku wanakutumia isivyostahili, Wanakusifia kinafiki wewe ni Kichwa sana mpaka kufikia nawe kubweteka wakati kiukweli wewe bado ni kijana mwororo sana kwenye siasa za Nchi yetu,Bado unahitaji uangalizi mzuri na Mashauri ya watu wengine walikutangulia kwenye mambo ya siasa.Na watu hao sahihi wanapatikana kwanza CHADEMA kabla ya kuinua macho kwenye vyama vingine kikiwemo CCM WANAOONEKANA KUKUPENDA SANA KWA WAKATI HUU.Zito wewe sio wakuwapuuza CHADEMA, maana wao ndio wamekufanya uwe kama ulivyo sasa.Baadhi ya Wana CCM na watu wa TISS wanakufurahia na kukushabikia kwa sababu wamekukuta uko ndani ya nyumba salama CHADEMA.
Zito wa Kabwe kwanini umekubali kirahisi vile kulainishwa kwa vijisenti kwa kutumainishwa makubwa wakati wewe mwenyewe una ndoto kubwa na ndio inayotafutwa KUZIKWA MAPEMA KABLA YA KUTIMIA? Hivi ni kweli hii inaingia Akilini??? CCM ndio wanaokupenda kuliko CHADEMA? Mahusiano hayo mmeanza nao lini? Hivyo ulivyo ndo walivyokukuta umesoma na kupendeza na umaarufu huo? kama sivyo kwanini leo wakusifie? KIJANA SHITUKA!!! LA SIVYO IMEKULA KWAKO.
Zito unapaswa kuelewa kanuni ya maisha iko hivi.Ukipendwa Jipende,Ukithaminiwa Jithamini,Ukiaminiwa Aminika.
Kwa mwenendo anayoenda nayo Zito sitashangaa akituachia Hadithi kuwa Tulikuwako na kijana machachari ajuaye kujenga hoja (ZITO) Lakini kwa kukosa SUBIRA,UAMINIFU NA UADILIFU ALISHAWISHIKA KIRAHISI AKATUMIKA VIBAYA CHADEMA WAKAMDAMPO CCM WAKACHEKELEA WANANCHI TUKAMSAHAU MPAKA WA LEO,NACHELEA YASIJE KUMKUTA ZITO ZUBERI KABWE YALE YALIYOMKUTA MR.KABURU ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) Mwenye macho na Masikio na asome na kulielewa Andiko hili la 12STONE MwanaJF mwenzenu, Nawasilisha.
Mungu akitujalia kuiona 31 Dec. 2013 na Kuingia Jan.1,2014 WOTE TUWE NA SHUKRANI KWAKE MOLA.