kyannala nabiso
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 645
- 143
mbona watu wengine mnapenda kubishana upumbavu kama watoto matahira lol!
Ukitaka kujua ukweli wa mtu ni kwenye Fedha.
Hapa ndipo huwa nawashangaa sana hawa ndugu zangu wanaoamua kuchukua nafasi ya kutetea uhalifu eti tu kwa sababu ya mtu mwingine kuufanya. Swali langu la msingi ni hili kuna sababu gani sasa ya kubadilisha uongozi kama hawa tuliowaamini nao wako hivyo hivyo kama waliopo sasa au tunataka kubadilisha watu ili nao wale, waibe?
Nilisema hivi hivi kwenye tuhuma ya Lema na mpaka leo hajatoka hadharani kukanusha ila atakuja siku moja kutolea ufafauzi kama ilivyotokea kwa Dr. Slaa leo wakati hizi tuhuma ziliwekwa hapa miezi saba iliyopita. Alikuwa wapi wakati huo kutolea ufafanuzi huu?
Hello Great Thinkers!!
kuanzisha hoja za kitoto kuwa mwenyekiti anakopa (SHAME!!) "[......] hana Mke kaiba mke wa Mtu" .
Chama makini ni CCM ambacho wanakwiba pesa za Umma. mtueleze kwanza assets zote za viwanja vya mipira na majengo ambayo Watanzania wote tulishiriki kuvijenga pesa zake ziko wapi?Tatizo siyo kurudishwa kwa mkopo tu, tatizo ni kanuni, mwongozo na taratibu zipi ndani ya chama zilitumika kumpatia huo mkopo na malipo ya nan wa girlfriend wake
Huoni kama kuna hoja ya kujibiwa ukizingatoa CHADEMA inataka kuudhihilishia uuma wa Watanzania kama ni chama makini katika utendaji wake
Toka lini chama kikawa mkopeshaji wa unsecured loan. Kanuni, mwongozo na taratibu zipi za chama zinatoa uwezo wa maofisa wa fedha ndani ya chama kutoa unsecured loan kwa wanachama
Hello Great Thinkers!!
Nimeanza na salamu ya kizungu kidogooo kuonyesha msisitizo! Hoja kweli imekuwa dhaifu hasa kutoka kwa wanachama wenzangu wa CCM. Sisemi hakuna mabaya Chadema yatakuwepo saana tu japo kwetu mabaya ni mengi zaidi ya mazuri. Kama kuna kitu wenzetu wa upinzani wanafanya ni suala la kumvua uanachama yeyote ambaye si mwadilifu au anaonekana sio mwadilifu labda kwa sababu hawana dola hivyo hawana mahala pa kumweka azidi kuishi..
Rejea issue ya NAPE MNAUYE na sakata la Jengo la CCm alipobaini ukweli wa mambo na ufisadi ambao alidai ulikuwa ukisimamiwa na kamati ya udhamini ikiongozwa na Mh. Lowasa. Makamba Senior ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu wa Chama alimsimanga sana kijana kwa kuongea nje ya vikao na pia akavuliwa uanachama wa UVCCM kama kukumbukumbu zangu ziko sawa. Baada ya hapo sasa NAPE akapewa ukuu wa Wlaya Masasii..kisa amesema ukweli akatimuliwa uanachama na kwa sababu labda ayajua mengi mkuu wa kaya akampa ukuu wa Wilaya. Lakini mwenye mamlaka ya uongozi wa Chama ni Mwenyekiti na Katibu pamoja na Kamati zao zilizochaguliwa kihalali. Hivyo CHADEMA kuwafukuza uanachama wale wenye kuvuruga taratibu za chama lawama zisiwe kwa Mbowe wala Dr. Tlaa (Slaa) kama wao bali kama viongozi kwa vyeo vyao. Yaani mwenyekiti na Katibu. Na kama CCM tungekuwa tunafanya hivii nadhani tungekuwa na watu wazuri sana wanaobakia Chamani.
Hivyo basi nahitimisha bila kukuchosha msomamaji wa waraka huu usio rasmi kuwa, kwa kurudia hivi..tutaiua CHADEMA kwa kumaliza ufisadi Tanzania na si kuanzisha hoja za kitoto kuwa mwenyekiti anakopa (SHAME!!) "ooh anakadi mbili hana Mke kaiba mke wa Mtu" Hapana WanaCCm tuungane na upinzani wa hoja sio kingine na hata kuwaunga mkono zile hoja zenye msingi tu..na maendeleo tutayaona. Sio kila lisemwalo ni baya ama zuri! Kuna mabaya tuyaache na kuyakosoa na mazuri tuyaendeleze.
Kama ulikuwepo yaani mimi ndio sioni wala sisikii, hapa naomba uhai tu, kura yangu ya Urais 2015 ni kwa Dr Slaa na si vinginevyo, ila Tshirt na Kanga na pesa za Magamba kama kawaida nitachukuwa, pesa nitatafuna Tshirt na kanga na kopelo nitatowa msaada kijijini kwa wasio na nguo za kujistiri.
Weka ushahidi kuonyesha kwamba sio 140 ni 20, na ushahidi kwamba zimelipwa zote...kwa hiyo yaya analipwa na chama?
Mkuu sehemu unayotoka watu huwa wana misimamo ya uhakika kwa vile wanakula kamongo.Una mfano hai wa mwanasiasa aliyewahi kukopeshwa na taasisi za kifedha based on malipo/mshahara anaopata kutokana na utumishi wake katika chama cha siasa? Kwamba amekopeshwa kwa dhamana ya chama anachokitumikia. Usinitajie wafanyabiashara ambao ni wanasiasa.
Tuntemeke alilalamika kuwa hairuhusiwi kukopa? Hao masalia wengine, wana uthibitisho kuwa taratibu hazirUtaratibu gani ulitumika kumkopesha? Je, viongozi wengine pia wanaruhusiwa kukopeshwa? kwa utaratibu upi?
Kwanini TUNTEMEKE alivyotoa tuhuma hizi kwa mara ya kwanza mwaka 2011 alipigwa ban wakati inaonekana kweli wakati huo deni lilikuwepo? - Tuntemeke aombwe radhi, to be fair...
Tuhuma zimeendelea kuwepo kwa sababu hazikujibiwa.
Kimsingi kama ni vita huwezi kujibu kila hoja, yawezekana ni mbinu ya kumtoa kwenye hoja za msingi na kumuelekeza kwenye malumbano yasiyo na tija, kama kuna hoja zenye maslahi kitaifa hana budi kuzijibu kama ni sahihi kufanya hivyo public, lakini kama zinapaswa kujibiwa kwa taratibu za chama tusianze kuwa wajinga maana hata masalia, juliana nk walipaswa kutoa hoja zao kwenye vikao, kwahiyo si busara kila jambo tutake ufafanuzi hapa jukwaani wakati kuna utaratibu wa chama kushulikia mambo mbalimbali.Kwanini hataki kujibu hoja zote zilizoelekezwa kwake na masalia? Kuanzia za magafu wa mwanza, mwampamba wa mbozi, juliana na kisandu? Kwanini anachagua anayopenda yeye? Nadhani katibu mkuu anapaswa kuufahamisha umma kwa uwazi zaidi kuhusu haya mambo..
Tunawashwa kama vile yeye Dr Slaa alivyowashwa na fedha za EPA na Kagoda.Mkopo ulitolewa na ukarudishwa, tatizo lenu nini? Mbona mnawashwa pasipo sababu!!
Sioni hata hoja ya kujadili hapa. Chama kilimkopesha mtumishi wake na ameshalipa. Hakuna issue tena ya kujadili hapa.
Options
Willibrod Slaa
Hoja ya kujikopesha kwa sura ya ufisadi ni "mfu" nimetamka nilikopa 20 kwa kuwa watumishi wa vyama hawawezi kukopa kwingine. Aidha siyo 140 Million. Zote 20 m zililipwa awamu ya mwisho June 2012. Hivyo hakuna deni la chama tena.
2. Josephine hajawahi kulipwa hata senti mmoja na chama kwa ziara za Mikoani, wala kwa shughuli yeyote ile isipokuwa wakati wa kesi Arusha alipokuwa na mtoto wa miezi 3 na tulihitaji yaya
Options
Willibrod Slaa
Hoja ya kujikopesha kwa sura ya ufisadi ni "mfu" nimetamka nilikopa 20 kwa kuwa watumishi wa vyama hawawezi kukopa kwingine. Aidha siyo 140 Million. Zote 20 m zililipwa awamu ya mwisho June 2012. Hivyo hakuna deni la chama tena.
2. Josephine hajawahi kulipwa hata senti mmoja na chama kwa ziara za Mikoani, wala kwa shughuli yeyote ile isipokuwa wakati wa kesi Arusha alipokuwa na mtoto wa miezi 3 na tulihitaji yaya
[/QUOTE
kwanza kabisa ningependa kumkosoa slaa kwa maneno yake aliyosema watumishi wa vyama vya siasa hawawezi kukopa kwingine zaidi ya ndani ya vyama vyao. Hii si kweli na ni uongo dhahiri, kwa sasa watumishi wa vyama wanakopeshwa na mabenki mengi tu, Nenda crdb, nmb, nk wanakopesha na wengine mpaka hivi Leo wana mikopo wa vyama vingi tu km ccm, Cuf, nccr , nk. Hapa yaonyesha kuna kilicho jificha nyuma ya pazia, na yawezekana alitumia madaraka yake kujikopesha, si bure.
chama ni kama organisation nyingine tu. kina haki ya kutoa mikopo kwa wafanyakazi wake kulingana na sera zilizowekwa na chama husika. Huwezi chukua mkopo wa Mbowe ambao ni secured ukaanza kusema mbona yeye kakopeshwa? huo utakua uendaw.... .
Wewe tuambie ni taratibu zipi zinawakataza kutoa sababu hilo ni suala la sera tu( Policy). Kila chama kama taasisi zingine kina sera zake za fendha (Financial Policies) ambazo zina baraka ya msajili wa vyama So tusikurupuke kama hatujui za CDM zipo vipi. CLOSED
Hebu tupe kwanza kwa ufupi personal affairs za Rais wetu aliyepo Madarakani JK, maana Ridhiwani ana Mama yake, Miraji ana Mama Yake na Salma Kikwete ana watoto wake, halafu tumalizie na masaibu ya Babu Seya huenda ukafanikiwa kuniondowa Wazimu wa kumpenda Dr Slaa, kiasi kwamba nimeshamuandalia kura yangu.namchukia kwa sababu tatu za msingi
1- alizaa watoto wawili akiwa padri. alilisaliti kanisa kwa kwenda knyume na kiapo alichoapa. hii inaonesha tukimpa urais hata sisi anaweza kutuingiza mjini kwa kuapa kuilinda katiba kisha akafanya vinginevyo.
2- alimuiba mke wa mtu na kuzaa nae. yeye amesoma dini hadi kuitwa dkt. ni padri. kwa nini afanye hivi! hana muamana wa kupewa nchi yetu!
3- akiwa jukwaani huwa anaongea mambo mengi ya uongo. hata kama siasa ni uongo lkn wa kwake umezidi. orodha ni ndefu lkn kwa leo naishia hapa
Mbona hoja zote hizi zilishajibiwa na hata waasisi wa hizi propaganda walishahama huko ndio maana kila kukicha wanakuja kwa staili mpya, wewe bado umebaki huko? Go back and read sidhani kama utabaki ulivyo.namchukia kwa sababu tatu za msingi
1- alizaa watoto wawili akiwa padri. alilisaliti kanisa kwa kwenda knyume na kiapo alichoapa. hii inaonesha tukimpa urais hata sisi anaweza kutuingiza mjini kwa kuapa kuilinda katiba kisha akafanya vinginevyo.
2- alimuiba mke wa mtu na kuzaa nae. yeye amesoma dini hadi kuitwa dkt. ni padri. kwa nini afanye hivi! hana muamana wa kupewa nchi yetu!
3- akiwa jukwaani huwa anaongea mambo mengi ya uongo. hata kama siasa ni uongo lkn wa kwake umezidi. orodha ni ndefu lkn kwa leo naishia hapa