Dr Slaa ajibu tuhuma dhidi yake

Dr Slaa ajibu tuhuma dhidi yake

Status
Not open for further replies.
Willibrod Slaa


"Hoja ya kujikopesha kwa sura ya ufisadi ni "mfu" nimetamka nilikopa 20 kwa kuwa watumishi wa vyama hawawezi kukopa kwingine. Aidha siyo 140 Million. Zote 20 m zililipwa awamu ya mwisho June 2012. Hivyo hakuna deni la chama tena.
2. Josephine hajawahi kulipwa hata senti mmoja na chama kwa ziara za Mikoani, wala kwa shughuli yeyote ile isipokuwa wakati wa kesi Arusha alipokuwa na mtoto wa miezi 3 na tulihitaji yaya"



Wewe Mzee hoja siyo kwamba umekopa na kurudisha, hoja hapa ni je kwa mujibu wa Katiba, Kanuni, Miongozo na Taratibu za Chama cha Chadema kuna utaratibu wa mwanachama au Kiongozi kukopo na kisha kurejesha? kama upo ni acha wanachama wa kawaida je ni Viongozi wangapi wameshawahi kukopesha na CHADEMA kisha wakarejesha? weka wazi hapa na siyo kulete hadithi za ni kweli nilikopa sasa nimerudisha hiyo siyo hoja. Hoja hapa umetumia Ibara ya ngapi ya Katiba ya CHADEMA kukopa? au umetumia Kanuni namba ngapi ya Kanuni za CHADEMA kukopa, au umetumia kipengele cha ngapi cha Taratibu au Miongozo ya CHADEMA kukopa?.

Lakini pili unaposemanimetamka nilikopa 20 kwa kuwa watumishi wa vyama hawawezi kukopa kwinginesikuelewi, hivi hakuna Taasisi za kukuwezesha wewe kukopa? Mbona Mwenyekiti wako Mbowe alikopa NSSF. Kuna Mabenki, kuna SACCOS n.k lakini hizo zote haziwezi kukukopesha ila umeona CHADEMA ndiyo inaweza kukukopesha eti?
Ni aibu kubwa sana kwa Kiongozi anayesema ni mtetezi wa kupiga ufusadi wewe ndo umekuwa mstari wa mbele kuchochea ufisadi. Ufisadi siyo kuiba pesa tu hata kuzitumia au kukopeshwa kinyume na Taratibu zozote hata kama umezirejesha.

NATAKA KUKUONA UNATOKA HADHARANI na kuwaambia wanachama wako kuwa umekiuka Katiba, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya CHADEMA.Ninaposema CHADEMA ni NGO unaweza kusimama na kusema siyo hivyo? kama siyo NGO au SACCOS unawezaje kwenda kukopa kwenye Chama cha Siasa. Hivi kumbe CHADEMA ni CHAMA CHA MAENDELEO NA DEMOKRASIA kwa maana ya kuweza kukopeshana?

Wanachama wa CDM amkeni hizi ni zile kidogo zilizojulikana hiyo mijihela ya M4C waulize inakwenda wapi?Tazama na hii unayomtetea Mzinifu mwenzako Josephine"isipokuwa wakati wa kesi Arusha alipokuwa na mtoto wa miezi 3 na tulihitaji yaya" haya ni mambo ya Kitoto ambayo hayatakiwi kufanywa na Kiongozi wa ngazi ya juu kama wewe. kwa hiyo Katiba au Taratibu za Malipo za CHADEMA zinasemaje kwa mtu ambaye siyo Kiongozi wa chama lakini mume au mkewe ni Kiongozi wa Chama. Kama mtu huyo siyo Kiongozi eti kwa sababu ana mtoto na kwa kuwa anahudhuria kesi basi alipwe pesa na CHADEMA kwa kuwa mumewe ni Kiongozi ili aweze kuhudhuria kesi? HUU NI UPUUZI MWINGINE wa matumizi mabaya ya Fedha za Chama.

Mzee, hili ni scud missile!
Huyu babu wa CHADEMA kesha kosa moral authority
 
sramble,

Maneno yako yanalingana kabisa na jina lako-scramble. Kwa watu wa data na microwave signals wanajua maana ya scrambled signal kuwa ni signal ambayo imevurugwa au kuchafuliwa ili usiweze kujua kilichoko ndani.Ni uchafu au takataka tu hakuna kinachoeleweka.

Baada ya kusema haya nakuja kwenye hoja. Wazungu siku zote wanasema intelligent mind discuss issues while foolish mind discuss people.Msemo huu unaenda moja kwa moja kwa mijtu yote ya Magamba-CCM na mishabiki yake. Kwamba ni jambo la kusikitisha na kushangaza mijtu mizima na kengele zao inaacha KUJADILI ISSUES ZA KITAIFA BADALA YAKE INAKAAA KUMZUNGUMZIA MTU-DR.WILBROAD PETER SLAA!!!Shame on you bastards. Kuna issue za kitaifa ambazo ni very hot kwa sasa kama hii ya GESI ASILIA YA MTWARA/LINDI ilivyo kaa vibaya! Badala ya mijitu ya CCM inayojidai kuwa imeshika dola kukaa na kutafakari namna ya kuuzima moto wa Gesi asilia ya Mtwara imekalia kumjadili Dr. Slaa!!!....
Kweli wewe punguani, wewe je unamshikia kengele zake Dr?
 
unahitaji viongozi wa dini wakuombee.

Wewe ambaye unaleta habari za kizushi na uongo ndiye unatakiwa uombewe na viongozi wako wa dini!
Yaelekea umepagawa na pepo la uongo na la usengenyaji.Ushindwe na ulegee.
 
Tunawashwa kama vile yeye Dr Slaa alivyowashwa na fedha za EPA na Kagoda.

Dr Slaa alitoa ushahidi wa tuhuma zake kwa hao waliochota fedha za EPA na KAGODA, na nyie pia toeni ushahidi kuwa taratibu na kanuni hazikufuatwa katika kupewa huo mkopo.Dr Slaa alisababisha walioiba kufatiliwa na kushtakiwa mahakamani, lakini ninyi mnakua mnapiga kelele za bure.

Suala lipo wazi, toeni ushahidi wenu tuujue ukweli ili tujue hatua zakuchukua. Tatizo lenu nini sio wanachama wa CDM, sisi wenye chama tumeridhika yeye kupata huo mkopo na tunafurahi kwamba alirudisha kwa wakati kama tulivyokubaliana.
 
Kweli wewe punguani, wewe je unamshikia kengele zake Dr?

masopakyindi,

Wewe ndiye punguani wakhedi! Mtu usiyeweza kutofautisha kati ya issue na mtu! Kama umeacha hoja za msingi zinazorihusu Taifa hili ukaanza kumzungumza mtu then wewe ni mmoja ya mapunguani wa CCM!!!
You're one of those fools discussing peope instead of discussing issues!
 
Viongozi wa vyama vya siasa wangekuwa hawawezi kukopa Mbowe angekuwa hadaiwi na NSSF. Yaani na wewe unadanganyika haraka na kirahisi namna hiyo?! au ndio ile mtu akipenda chongo huita kengeza? Mikopo ipo kwa watu wote wanaokopesheka.Kama hakopesheki basi tatizo ni lingine lakini siyo kwa kuwa ni mwanasiasa. By the way, Slaa na mshahara wa milioni 7 alikuwa na ulazima gani wa kuchukua tena milioni 20 za chama?
Usijibu kihuni mkuu Mbowe yeye hakopi kama Mbowe anakopa kama kampuni ambayo inamiliki bilicanas na mbowe hotels. Dr. Slaa anaposema viongozi wa siasa vigumu kukopa anamaana benki either uweke dhamana ya mali au kama ni muajiriwa lazima iwe ajira ambayo ina mkataba maalumu ili kuguarantee urejeshaji, sasa katibu mkuu wa chama hana mkataba maalumu anaweza kuondolewa muda wowote na bosi wake sasa akakope kivipi. Kabla hamjaongea mjiridhishe kiutafiti na hoja unazoongelea.

Issue sio mshahara mkubwa ni nature ya contract ndio inaamua ukopeshaji wako. Wabunge wanakopa kwakuwa wanaguarantee ya serikali na uhakika wa miaka mitano.

Kama unahitaji kujua zaidi kaulize wafanyakazi wa ofisi za Umoja wa Mataifa ambao ni local na wanamishahara mikubwa ila wako under service contract je wanaweza kukopa benki kwa guarantee ya ofisi zao?
 
WanaJF,
Nilidhani walioko humu ni great Thinkers. Nilisema hakuna hoja ya kujibiwa hivo sina muda wa kupoteza kujibu hoja za kufikkirika. Ni jukumu la mwenye kuleta hoja kutoa ushahidi si jukumu la mtuhumiwa. Ndio maana wakati wa EPA/B0T. Nilitoa account no, bank husika, majina ya wahusika, tarehe ya transaction na kadhalika. Kama ni kutamka anybody anaweza kutamka chochote hat a kichaa. Hivyo watanzania, nikikaa kimya maana yake nimepuuza kwa kuwa hakuna hoja ila wanaoleta wanadhamira tu ya kutuondoa kwenye hoja za msingi. Nagpenda kwa Mara ya mwisho niwahakikishie woe wenyewe mapenzi MEma Chadema iko makini, yote tunayofanya ni kwa mujibu wa taratibu zetu tulizojiwekea. Iwapo mwenye nia Njema anahitaji kufahamu jambo milango ya makao makuu yako wazi saa zote alimradi unafuata taratibu za kawaida za kiofisi.

Babu, Juliana Shonza kakutoa pangoni. bila yeye kuweka hadharani usanii wako ungeendelea kufyonza tu.

Bado kuna bomu lingine linaandaliwa la jinsi womanfriend wako Josephine anavyotumia NGO ya IGEHETA kwenye shughuli za siasa na kula pesa za CHADEMA.

wewe mtu mzima unalipwa mshahara sh. milioni saba bado unaenda kujikopesha pesa za walalahoi walioichangia M4C huku wakiamini pesa hizo zinaingizwa kwenye harakati, kumbe wewe unaenda kufanyia anasa!

Hii ndio imesababisha hata Lema mmeshindwa kumchukulia hatua kwa kuingia mitini na pesa za M4C.

Halafu babu unaonekana huna marafiki, yaani milioni 20 tu unakosa mtu wa kukuazima!!! Watu wanaodanganyika na porojo zako wanazidi kupungua kila siku...
 
Last edited by a moderator:
Babu, Juliana Shonza kakutoa pangoni. bila yeye kuweka hadharani usanii wako ungeendelea kufyonza tu.

Bado kuna bomu lingine linaandaliwa la jinsi womanfriend wako Josephine anavyotumia NGO ya IGEHETA kwenye shughuli za siasa na kula pesa za CHADEMA.

wewe mtu mzima unalipwa mshahara sh. milioni saba bado unaenda kujikopesha pesa za walalahoi walioichangia M4C huku wakiamini pesa hizo zinaingizwa kwenye harakati, kumbe wewe unaenda kufanyia anasa!

Hii ndio imesababisha hata Lema mmeshindwa kumchukulia hatua kwa kuingia mitini na pesa za M4C.

Halafu babu unaonekana huna marafiki, yaani milioni 20 tu unakosa mtu wa kukuazima!!! Watu wanaodanganyika na porojo zako wanazidi kupungua kila siku...

Mkuu wangu ZeMarcopolo,

Hivi kina Molemo, Crashwise, Mungi, Matola, Mohamedi Mtoi, na Pro-Chadema JF wanashindwa kuchanga laki mbili kila mtu wakampa Dr Slaa mpaka akope pesa za ruzuku.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,
Dr. Slaa amekubali kama amepewa mkopo, tatizo letu ni kwa njia zipi alipata huo mkopo kwa sababu hakuna kipengele katika uendeshaji wa CHADEMA kinachoainisha na kururuhusu ofisa wa fedha wa chama kutoa mkopo kwa wanachama na kama kipo kama unavyodai basi kisemwe. Kama hilo nalo haliwezekani basi hakuna haja ya kuendelea kuliongelea kwa sababu limeeleweka katika macho ya watu wenye fikra pana.

Nafikili tukubali kutokubaliana kwa sababu badala ya kunijibu swali langu la msingi, unachofanya ni kuniuliza tena.

Unachokosea ni kumchukulia Dr Slaa kama mwanachama katika hiyo kesi, sisi wanachadema Dr Slaa tunamchukulia kama mwajiriwa (pamoja na uanachama wake), tumemuajiri kwa nafasi ya ukatibu mkuu wa chama. Tunamlipa mshahara na akitaka mkopo tunampa kwa makubaliano kwamba atarudisha, nafikiri hata wewe unapofanyia kazi unaruhusiwa kukopa, kama hawakukopeshi pole sana.

Suala linalowachanganya nyie ni mkopo kwa Dr Slaa kama mwanachama, kitu ambacho sio sahihi. Hakuna utaratibu nchi nzima kwa mwanachama wa Chadema kukopa hela za chama na Chadema haijawahi kufanya hivyo. Chadema haijawahi kuwakopesha wanachama na haitakuja kuwakopesha wanachama wake, ila inaweza kuwakopesha waajiriwa wake kama wanakopesheka. Huo ni utaratibu wa vyama vya siasa vingine na pia ni utaratibu wa waajiri wengine.
 
Magamba na masalia hawa watu ni lazima tu watakuwa na mapepo na bila shaka wanahitaji maombi kabisa, hoja za kijinga yanashadadia tena kama haya magamba 2 humu JF Mingoi na ZeMarcopolo yanajifanya yana uchungu na chama kumbe njaa tu zinayasumbua.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu ZeMarcopolo,

Hivi kina Molemo, Crashwise, Mungi, Matola, Mohamedi Mtoi, na Pro-Chadema JF wanashindwa kuchanga laki mbili kila mtu wakampa Dr Slaa mpaka akope pesa za ruzuku.

Tatizo ni kwamba hata wao inaonekana walikuwa hawajui juu ya huu usanii wa dr. Slaa. Ndio maana hata kumtetea wanashindwa.
Dr. slaa amejifanya kujibu hii hoja kabla ya kikao cha kamati kuu cha weekend kwa sababu anajua hoja hii italetwa sasa anataka kudesa majibu ya kutoa. hata hivyo, vidhibiti vyote vipo kuwa alichukua 140 mil kwa hiyo anaweza kujitapa kwenye facebook lakini ikijadiliwa kwenye kamati kuu atachemsha.

Yaani watu walalahoi wanachangia kipato chao kidogo kwa ajili ya M4C halafu yeye anachukua hizo pesa kumpekea mpenzi wake josephine. Huu sio tu ufisadi bali pia ni DHARAU. Na ndio maana Lema naye kajichotea na hawawezi kumgusa!!!
 
sramble,

Maneno yako yanalingana kabisa na jina lako-scramble. Kwa watu wa data na microwave signals wanajua maana ya scrambled signal kuwa ni signal ambayo imevurugwa au kuchafuliwa ili usiweze kujua kilichoko ndani.Ni uchafu au takataka tu hakuna kinachoeleweka.

Baada ya kusema haya nakuja kwenye hoja. Wazungu siku zote wanasema intelligent mind discuss issues while foolish mind discuss people.Msemo huu unaenda moja kwa moja kwa mijtu yote ya Magamba-CCM na mishabiki yake. Kwamba ni jambo la kusikitisha na kushangaza mijtu mizima na kengele zao inaacha KUJADILI ISSUES ZA KITAIFA BADALA YAKE INAKAAA KUMZUNGUMZIA MTU-DR.WILBROAD PETER SLAA!!!Shame on you bastards. Kuna issue za kitaifa ambazo ni very hot kwa sasa kama hii ya GESI ASILIA YA MTWARA/LINDI ilivyo kaa vibaya! Badala ya mijitu ya CCM inayojidai kuwa imeshika dola kukaa na kutafakari namna ya kuuzima moto wa Gesi asilia ya Mtwara imekalia kumjadili Dr. Slaa!!!

What is 20 million Tshs. hata kama zingelikuwa hizo 140m! Mbona kama nyie CCM mna uchungu na hela ya walipa kodi wa Tanzania hamuhoji kuhusu Ufisadi uliopo serikalini kuanzia maswala ya EPA,DEEP Green,Meremeta na Mabilioni ya Shillingi yaliyoko kwenye offshore accounts huko Uswiss???Kuna watu wanadaiwa mabilioni lakini hakuna anayepiga kelele.

Sijui ni kipi cha ajabu kwa mtu kukopa fedha ya chama na baadaye kuirudisha! Kama mtu anaweza kukopeshwa na Kanisa na baadaye akarudisha hiyo pesa kuna tatizo gani?? Mbona hata wafanyakazi wa serikali na mashirika ya umma hukopeshwa na waajiri wao mishahara 3,2 au 1 kutegemea na mhitaji na baadaye akakatwa polepole kutoka kwenye mshahara wake na deni likaisha!!

Watanzania tunatakiwa kubadilika. Huu ushabiki wa kishenzi wa kushabikia kitu cha kipuuzi ili kumchafua mtu na ilhali hakina tija yoyote kwa jamii na Watanzania kwa ujumla wake ni ufisadi wa aina yake. Hivi kuna viongozi wangapi wa Serikali ya CCM wanaofanya madudu kila kukicha???Lakini kwa vile wao wameshika patamu mambo huwa wanayafunika kwa kutumia njia za kibabe ili wasiumbuliwe. Napenda niwahakikishie enyi wanafiki na wazushi wa chama Twawala siku inakuja muda si mrefu ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe. Mbona kila jambo litawekwa hadharani na sijui mtaficha wapi nyuso zenu!!

Pole sana Dr. Slaa. Kwa Watanzania na all Great Thinkers wenye akili timamu wanajua ukweli kuhusu wewe na wana Imani kubwa na wewe hadi 2015. CCM wanalijua hili na ndiyo maana kwa sasa majeshi yao yote yamehamishiwa CDM na nia ni kummaliza Slaa ili kwenye GE 2015 washinde kiulaini. Wanajua ulivyowapa tabu wakti wa GE 2010 ambapo ilibidi watumie UWT,Polisi na NEC kuvuruga matokeo ili kuinusuru CCM. Wanajua kuwa wasipofanya hivi kwa sasa ili kukuchafua na wakijua kuwa 2015 tutakuwa na Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi hawataingia Ikulu!!!

Nina amini Mungu yuko pamoja na wewe na Mungu atakuwa amekwisha kuwaandalia Rais aliye bora kabisa kutoka CHADEMA come 2015. Tusubiri.

Nafikiri msemo wako ulouweka mwanzoni mwanzoni kama utawasuta wengi! Kwa sababu wamo watu wengi hawajadili ishu za kitaiga humu, watu wamemkamia JK. Mana nimeona thread JK yupo france basi ule mwamvuli haujamfunika wote tayari watu wameanza kujadili, kama si ujinga ni nini? Hivi baada ya kuapishwa rais nchini marekani mnakaa kitako mkisikia kuwa republican wameweka mikutano ya kupinda upinzani? Tanzania imeinekana ni nchi wa wajinga, watu wamezama katika siasa, kila kitu siasa, siasa katika kila ofisi, katika kila tukio kina siasa, leo boda boda akiwa chadema akigongwa tu mara itakuja siasa, mtu anaweza kususia asinunue kitu kutoka duka flani kisa tu yule chadema huyu ccm! Nchi yenye watu wapuuzi sana, ndio maana watu wanakuja kuekeza na kuchukua mali wakisepa nazo, sisi tunakaa na siasa uchwara!
 
Jamani sisi tunampenda tumempa majukumu tumemkopesha amelipa na akitaka kukopa tena tunamkopesha tusimtunze Dr Slaa tumtunze nani.
 
Weka ushahidi kuonyesha kwamba sio 140 ni 20, na ushahidi kwamba zimelipwa zote...kwa hiyo yaya analipwa na chama?

Tujifunze kusoma na kuelewa kabla ya kukurupuka. Dr Slaa ameandika kuwa Josephine ndiye aliyelipwa na sio yaya.
 
Kwanini hataki kujibu hoja zote zilizoelekezwa kwake na masalia? Kuanzia za magafu wa mwanza, mwampamba wa mbozi, juliana na kisandu? Kwanini anachagua anayopenda yeye? Nadhani katibu mkuu anapaswa kuufahamisha umma kwa uwazi zaidi kuhusu haya mambo..

halafu...?
 
Dr.W.Slaa,

Hakuna ambaye anataka kukutoa kwenye hoja ya msingi. Ili la kukopa ruzuku ya chama wewe unaona siyo hoja ya msingi.

Naomba kufahamu ndani ya Chadema mna utaratibu wa kukokopeshana pesa za ruzuku ya chama.

Unapokea milioni 7 kwa mwezi halafu unasema hakuna wa kukopesha ndiyo maana umeamua kujikopesha.

Juliana Shonza bila kuwambia wananchi tusingejua kama umekopa pesa ya chama kwa matumizi yako binafsi.
Kinachokushangaza hapo ni nini?Utaratibu wa vyama kusaidia viongozi wa chama ulianzia CCM kutokana na kusaidia viongozi waadilifu.Mwl Nyerere alijengewa na CCM nyumba butiama,Katibu Mkuu Mzee Kawawa alisaidiwa na chama nyumba ya madale na Philip Mangula aliuziwa nyumba osterbay kwa masharti nafuu na serikali ya Benjamin Mkapa.Hivyo sioni cha ajabu kwa CHADEMA kumkopesha Dr Slaa fedha kwa ajili ya kumsaidia kwenye shughuli zake za kimaendeleo.
 
Babu, Juliana Shonza kakutoa pangoni. bila yeye kuweka hadharani usanii wako ungeendelea kufyonza tu.

Bado kuna bomu lingine linaandaliwa la jinsi womanfriend wako Josephine anavyotumia NGO ya IGEHETA kwenye shughuli za siasa na kula pesa za CHADEMA.

wewe mtu mzima unalipwa mshahara sh. milioni saba bado unaenda kujikopesha pesa za walalahoi walioichangia M4C huku wakiamini pesa hizo zinaingizwa kwenye harakati, kumbe wewe unaenda kufanyia anasa!

Hii ndio imesababisha hata Lema mmeshindwa kumchukulia hatua kwa kuingia mitini na pesa za M4C.

Halafu babu unaonekana huna marafiki, yaani milioni 20 tu unakosa mtu wa kukuazima!!! Watu wanaodanganyika na porojo zako wanazidi kupungua kila siku...

Nyie nao mnatuletea ukomedy tu,,,.........ambacho hujaelewa nini??????????kakopa ndio si karudisha ufisadi uko wapi sasa??????? ameonyesha ni mtu anayekopesheka. ni yale yale akikopa kwa rafiki yake au kwa chama chake kwa baba yake alimradi karudisha.we hujawahi kuona mwajiriwa anakopeshwa na mwajiri wake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom