Dr Slaa ajibu tuhuma dhidi yake

Dr Slaa ajibu tuhuma dhidi yake

Status
Not open for further replies.
Kumbe wewe ni mtu usiye na hoja kiasi hiki

Mkuu hili swala mbona mmechelewa sana kulitolea jibu.
Halafu, ni sheria gani inayompkataza mwanasiasa kukopa.
By the way, Slaa na mshahara wake wa mil. 7 anashindwa kupata rafiki akamuazima mil. 20 tu!!! Kulikuwa na ulazima gani kuchukua pesa za ruzuku za chama halafu mnaenda kuwaambia walalahoi wachangie chama?
 
Viongozi wa vyama vya siasa wangekuwa hawawezi kukopa Mbowe angekuwa hadaiwi na NSSF. Yaani na wewe unadanganyika haraka na kirahisi namna hiyo?! au ndio ile mtu akipenda chongo huita kengeza? Mikopo ipo kwa watu wote wanaokopesheka.Kama hakopesheki basi tatizo ni lingine lakini siyo kwa kuwa ni mwanasiasa. By the way, Slaa na mshahara wa milioni 7 alikuwa na ulazima gani wa kuchukua tena milioni 20 za chama?
Ndugu yangu ZeMarcopolo,
Unasahau kitu kimoja. Hata kabla hajaingia siasa Mbowe alikuwa ni mfanyibiashara mwenye mali zisizohamishika. Kwa hiyo anaweza kupata mkopo. Tungemuuliza Maalim Lipumba juu ya uzoefu wake kwa sababu huyu, kama Mzee Slaa, hana biashara. Kama Lipumba atasema kuwa ni rahisi kwake kupata mkopo, ingawa kazi yake ni full time mwanasiasa, basi tamko la Slaa litakuwa na mushkeli. Hata mwenye mshahara wa milioni saba hukopa. Labda kuna dharura ilitokea. Lakini the point is alishalipa.
 
Deni limeshalipwa, tena imepita miezi saba sasa. What is the issue? Sijui na siwezi kuhukumu madai kuwa watumishi wa vyama vya siasa hawaruhusiwi kukopa. Lakini nisingekurupuka na kusema ni uwongo kabla sijafanya utafiti. Let us give him the benefit of the doubt until proven otherwise. Lakini naona wenzangu mna haraka ya kutoa hukumu na kukimbilia conclusion kuwa asiaminiwe kupewa Ikulu. Leo ikulu inakaliwa na mwizi wa mali za umma. Sijawasikia mkilalamika. Sioni issue.

Hapa ndipo huwa nawashangaa sana hawa ndugu zangu wanaoamua kuchukua nafasi ya kutetea uhalifu eti tu kwa sababu ya mtu mwingine kuufanya. Swali langu la msingi ni hili kuna sababu gani sasa ya kubadilisha uongozi kama hawa tuliowaamini nao wako hivyo hivyo kama waliopo sasa au tunataka kubadilisha watu ili nao wale, waibe?
Nilisema hivi hivi kwenye tuhuma ya Lema na mpaka leo hajatoka hadharani kukanusha ila atakuja siku moja kutolea ufafauzi kama ilivyotokea kwa Dr. Slaa leo wakati hizi tuhuma ziliwekwa hapa miezi saba iliyopita. Alikuwa wapi wakati huo kutolea ufafanuzi huu?
 
Ndugu yangu ZeMarcopolo,
Unasahau kitu kimoja. Hata kabla hajaingia siasa Mbowe alikuwa ni mfanyibiashara mwenye mali zisizohamishika. Kwa hiyo anaweza kupata mkopo. Tungemuuliza Maalim Lipumba juu ya uzoefu wake kwa sababu huyu, kama Mzee Slaa, hana biashara. Kama Lipumba atasema kuwa ni rahisi kwake kupata mkopo, ingawa kazi yake ni full time mwanasiasa, basi tamko la Slaa litakuwa na mushkeli. Hata mwenye mshahara wa milioni saba hukopa. Labda kuna dharura ilitokea. Lakini the point is alishalipa.
Kama mtu anayelipwa sh. 7m anashindwa kukopesheka na taasisi za fedha vipi sisi walala hoi tunakesha barabarani na kutembea kwenye jua bila kipato cha uhakika tutapona?
 
Kama mtu anayelipwa sh. 7m anashindwa kukopesheka na taasisi za fedha vipi sisi walala hoi tunakesha barabarani na kutembea kwenye jua bila kipato cha uhakika tutapona?

Nimesemaje? Tumuulize Maalim Lipumba kama ni rahisi kwake kupata mkopo kama mwanasiasa? Sijui hapa issue ni nini. Mambo ya kuaminika yametoka wapi? Na wewe kama umeridhika na uongozi wa sasa endelea kuwaunga mkono. Hakuna mtu anayekushinikiza uunge mkono uongozi mbadala.
 
Options
Willibrod Slaa

Hoja ya kujikopesha kwa sura ya ufisadi ni "mfu" nimetamka nilikopa 20 kwa kuwa watumishi wa vyama hawawezi kukopa kwingine. Aidha siyo 140 Million. Zote 20 m zililipwa awamu ya mwisho June 2012. Hivyo hakuna deni la chama tena.
2. Josephine hajawahi kulipwa hata senti mmoja na chama kwa ziara za Mikoani, wala kwa shughuli yeyote ile isipokuwa wakati wa kesi Arusha alipokuwa na mtoto wa miezi 3 na tulihitaji yaya

hongera mama Josephin kwa kujitolea.
 
Huyu mzee mbona anataka kudanganya mchana kweupe!!! Watumishi wa chama hawawezi kukopa kwingine?????? Huyu mzee anadhani kila mtu anadanganyika kama nanihii...

Sijawahi changia thread za kijinga kama hii ila ngoja nifanye once and last. Kwani kama unafanya kazi sehemu ya kwanza kukopa ni kazini kwako au bank? Na je unapoishi utaanza kuulizia wakukukopesha jirani wa karibu au utatafuta mtaa wa tatu......Caritas peribus
 
Hukosi kua mtoto wa kambo aka wa haram, akili yako imeadhirika na kila mtu unahisi ni yule Babu ako alokulea.
Slaa ni Dr. ukishindwa kutaja jina taja nafasi yake kitaaluma Dr.,lakn utoto kambo hautokuacha.Pole masalia wee
 
Kama mtu anayelipwa sh. 7m anashindwa kukopesheka na taasisi za fedha vipi sisi walala hoi tunakesha barabarani na kutembea kwenye jua bila kipato cha uhakika tutapona?

Kwahiyo ulitaka riba iende taasisi ya fedha na wala tusiipate CDM. Haya basi mwenzio kaangalia penye riba nafuu akaona ni kazini kwake kwake kimeharibika nini?
 
Kwa hili kuna tatizo... Hoja inatakiwa ijibiwe vizuri maana kila kiongozi akikopa kwa ajili ya kujinufaisha na wakati chama kinazunguka kuomba watu wachangie wengine wanakopeshana. Je wakati wa kukopa waliangalia risk zinazoweza kutokea? Thanks God zimelipwa. Je aliyekopa aliweka dhamana? Kwa kweli inapaswa kutolea maelezo mazuri swala hili. Maana swala hili wakilochukua wapizani wenu litakuwa baya pia kwenu.
Asante
 
Utaratibu gani ulitumika kumkopesha? Je, viongozi wengine pia wanaruhusiwa kukopeshwa? kwa utaratibu upi?
Kwanini TUNTEMEKE alivyotoa tuhuma hizi kwa mara ya kwanza mwaka 2011 alipigwa ban wakati inaonekana kweli wakati huo deni lilikuwepo? - Tuntemeke aombwe radhi, to be fair...
Tuhuma zimeendelea kuwepo kwa sababu hazikujibiwa.

Mi hamna mwongozo wa suala kama ili kwenye vyama ila wakati flani kuna vitu vinafanyika kwa makubaliano.
Kwa hiyo Tuntemeke na wengine nazani wanaweza kutegemeana na mahusiano yao na chama.
 
Mkuu, issue ni kwamba swala hili lililetwa hapa JF kwa mara ya kwanza na TUNTEMEKE ambaye alipigwa ban kwa kosa la kuleta "taarifa ya uongo". More than 14 months later, ndio babu anajitokeza kukubali kuwa alichukua pesa za chama.
Mbaya zaidi, babu anakuja na porojo kuwa watumishi wa vyama vya siasa hawaruhusiwi kukopa. Halafu babu huyuhuyu anataka aaminiwe kuachiwa Ikulu. Bado huoni issue ilipo Jasusi?

Ni kweli Mtumishi wa chama haruhusiwi kukopa,kutumia ajira ya chama kama mdhamini wa bank,ila anaweza kukopa kama anabiashara yake binafsi ndo atumie kama dhamana bank.
 
Kwa hili kuna tatizo... Hoja inatakiwa ijibiwe vizuri maana kila kiongozi akikopa kwa ajili ya kujinufaisha na wakati chama kinazunguka kuomba watu wachangie wengine wanakopeshana. Je wakati wa kukopa waliangalia risk zinazoweza kutokea? Thanks God zimelipwa. Je aliyekopa aliweka dhamana? Kwa kweli inapaswa kutolea maelezo mazuri swala hili. Maana swala hili wakilochukua wapizani wenu litakuwa baya pia kwenu.
Asante
swala alikopeshwa na wala hajajikopesha,..alikubaliwa sababu alitimiza vigezo vya kukopa
swala la kujiuliza je mkopo ulikuwa na interest?kama ni kweli huoni kuwa hiyo interest inakwenda cdm?
 
Weka ushahidi kuonyesha kwamba sio 140 ni 20, na ushahidi kwamba zimelipwa zote...kwa hiyo yaya analipwa na chama?

Acha ushamba wewe katibu mkuu ana haki ya kupata msaidizi wa ndani, kama anavyowekewa vocha kwenye simu
 
Deni limeshalipwa, tena imepita miezi saba sasa. What is the issue? Sijui na siwezi kuhukumu madai kuwa watumishi wa vyama vya siasa hawaruhusiwi kukopa. Lakini nisingekurupuka na kusema ni uwongo kabla sijafanya utafiti. Let us give him the benefit of the doubt until proven otherwise. Lakini naona wenzangu mna haraka ya kutoa hukumu na kukimbilia conclusion kuwa asiaminiwe kupewa Ikulu. Leo ikulu inakaliwa na mwizi wa mali za umma. Sijawasikia mkilalamika. Sioni issue.
we mbona ujatuwekea ushahidi wa uyo unaesema anaiba mali za umma?!au babu tu ndio anatakiwa kusikilizwa wengine wanahukumiwa bila ushahidi ! Don't play double standard
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom