Dr Slaa ajibu tuhuma dhidi yake

Dr Slaa ajibu tuhuma dhidi yake

Status
Not open for further replies.
Kama utetezi huu ni kweli ameundika Dr.Slaa(siamini), basi utetezi wake ni wakifisadi.

1. Kusema kuwa watumishi wa vyama hawaruhusiwi kukopa ni uwongo mtupu na uzushi.Hakuna sheria inayomzuia mtu kukopa. Kukopa na kukopeshwa ni makubaliano ya kimkataba kati ya mtu na mtu au mtu na taasisi kadiri wanavyoaminiana. Unabisha wewe ni benki? Benki nyingi hazina utaratibu wa kukopesha wafanyakazi hasa wa private, kuwakopesha wafanyakazi wa vyama vya siasa ni risk sana na hivyo benki nyingi zinakwepa.
2. Je lengo msingi la fedha ya ruzuku ni kwaajili ya kukopeshana? Hata kama lengo kuu sio kukopesha lakini organisation nyingi hukopesha ili kuboresha maisha ya wafanyakazi wao, maana kwa kufanya hivyo wanakua wanawa-motivate kufanya kazi kwa bidii na kwa kujituma zaidi.
3. Yeye kama mtendaji mkuu wa chama, je haoni kujikopesha fedha za ruzuku kuna conflict of interests? Je haoni kwamba kitendo hiki kinajenga mashaka makubwa dhidi yake juu ya accountability, credibility,transparency? Chama sio Dr Slaa, hata kama yeye ndio mtendaji mkuu wa chama. Chama kina NEC, CC na baraza la wadhamini, hao wote ni zaidi ya Dr Slaa. Kungekua na tatizo, NEC, CC na baraza la wadhamini wangelishughulikia
4. Je haoni kuwa tendo hili la kujikopesha fedha za ruzuku ni tendo la kifisadi? Sio tendo la kifisadi, kukopeshwa ni kitendo halali na haivunji sheria ya nchi wala sheria za vyama vya siasa. Kumbuka mkopo sio wizi.
5. Je huku siyo kutumia vibaya madaraka? Mpaka Mwampamba akajua maana yake haikua SIRI, lilikua suala la wazi. Kama ni suala la wazi, maana yake utaratibu wa kupata mkopo huo ulifuatwa kikamilifu na hivyo hakuna matumizi mabaya ya madaraka.
6. Je haoni kuwa akiwa Ikulu kuna uwezekano mkubwa akajikopesha bajeti yote ya ikulu? Hilo ni swali la kitoto, kwa unataka kusema bajeti ya Chadema ni milioni 20 tu, kama ni zaidi mbona hakukopeshwa yote?

Tamko: Dr. Slaa hafai kuwa raisi.

Mkopo ulitolewa na ukarudishwa, tatizo lenu nini? Mbona mnawashwa pasipo sababu!!
 
Hii Nchi bwana mtu anaweza kuwa fundi wa kukosoa wengine, kumbe naye kakalia vya kukalia, usanii zaidi kuliko uhalisia je tutafika??
 
Hii hoja imekufa lakini sasa wanaolipwa lumumba wafanyeje? Wakikaa kimya maana yake hakuna perday, njaa inasumbua kwahyo hapa issue si mkopo wa dr slaa wala ufisadi wa aina yoyote chadema, wanajua hakuna na wanaelewa hivyo, isipokuwa wafanyeje? Wako kazini
 
Hii hoja imekufa lakini sasa wanaolipwa lumumba wafanyeje? Wakikaa kimya maana yake hakuna perday, njaa inasumbua kwahyo hapa issue si mkopo wa dr slaa wala ufisadi wa aina yoyote chadema, wanajua hakuna na wanaelewa hivyo, isipokuwa wafanyeje? Wako kazini

Unasema hoja hii imekufa, je ameiua nani? Hoja hii bado ipo mbele yetu. Tuna haki ya kuijadili kwa masilahi mapana ya nchi tetu. Hoja nyingi alizoziibua Moma2k dhidi ya Dr. Slaa hazijajibiwa. Slaa ajitokeze kuzijibu(au wafuasi wake).
 
WanaJF,
Nilidhani walioko humu ni great Thinkers. Nilisema hakuna hoja ya kujibiwa hivo sina muda wa kupoteza kujibu hoja za kufikkirika. Ni jukumu la mwenye kuleta hoja kutoa ushahidi si jukumu la mtuhumiwa. Ndio maana wakati wa EPA/B0T. Nilitoa account no, bank husika, majina ya wahusika, tarehe ya transaction na kadhalika. Kama ni kutamka anybody anaweza kutamka chochote hat a kichaa. Hivyo watanzania, nikikaa kimya maana yake nimepuuza kwa kuwa hakuna hoja ila wanaoleta wanadhamira tu ya kutuondoa kwenye hoja za msingi. Nagpenda kwa Mara ya mwisho niwahakikishie woe wenyewe mapenzi MEma Chadema iko makini, yote tunayofanya ni kwa mujibu wa taratibu zetu tulizojiwekea. Iwapo mwenye nia Njema anahitaji kufahamu jambo milango ya makao makuu yako wazi saa zote alimradi unafuata taratibu za kawaida za kiofisi.

Nafikili hii sentensi amepitiwa kwa sababu viongozi wetu wa siasa ni mahili wa gaffe. Lakini kama hakupitiwa, basi amejipiga risasi mwenyewe kwa sababu siyo yote aliyowahi kuyasema ameishatoa absolute evidence.
 
Viongozi wa vyama vya siasa wangekuwa hawawezi kukopa Mbowe angekuwa hadaiwi na NSSF. Yaani na wewe unadanganyika haraka na kirahisi namna hiyo?! au ndio ile mtu akipenda chongo huita kengeza? Mikopo ipo kwa watu wote wanaokopesheka.Kama hakopesheki basi tatizo ni lingine lakini siyo kwa kuwa ni mwanasiasa. By the way, Slaa na mshahara wa milioni 7 alikuwa na ulazima gani wa kuchukua tena milioni 20 za chama?

Wacha kukurupuka? unajua tofauti ya secured na unsecured Loans?
 
nimemchoka slaa na huyo sijui kimada wake. sina hamu nao. slaa aliwapa nini wanachama wa chdm hadi hawaoni madudu yake? mzee anakiua chama
 
Weka ushahidi kuonyesha kwamba sio 140 ni 20, na ushahidi kwamba zimelipwa zote...kwa hiyo yaya analipwa na chama?

Kabla ya kuweka vielelezo vya kulipwa kwa deni la 20 m, weka kwanza vielelezo vya deni la 140 m hapa!
 
Unasema hoja hii imekufa, je ameiua nani? Hoja hii bado ipo mbele yetu. Tuna haki ya kuijadili kwa masilahi mapana ya nchi tetu. Hoja nyingi alizoziibua Moma2k dhidi ya Dr. Slaa hazijajibiwa. Slaa ajitokeze kuzijibu(au wafuasi wake).
hata unapoandika naona kabisa unatetemeka maana hujui uandike nini, dr ameshajibu, alikopa mil 20 kwa kufuata taratibu za chama, na hatahivyo ameshazilipa zote na kwahyo hadaiwi..sasa niambie kipi cha kujadili? Nasema tena hoja imekufa mapema tu, wacha nikapalilie shamba langu
 
Mkopo ulitolewa na ukarudishwa, tatizo lenu nini? Mbona mnawashwa pasipo sababu!!

Tatizo siyo kurudishwa kwa mkopo tu, tatizo ni kanuni, mwongozo na taratibu zipi ndani ya chama zilitumika kumpatia huo mkopo na malipo ya nan wa girlfriend wake

Huoni kama kuna hoja ya kujibiwa ukizingatoa CHADEMA inataka kuudhihilishia uuma wa Watanzania kama ni chama makini katika utendaji wake
 
Hello Great Thinkers!!

Nimeanza na salamu ya kizungu kidogooo kuonyesha msisitizo! Hoja kweli imekuwa dhaifu hasa kutoka kwa wanachama wenzangu wa CCM. Sisemi hakuna mabaya Chadema yatakuwepo saana tu japo kwetu mabaya ni mengi zaidi ya mazuri. Kama kuna kitu wenzetu wa upinzani wanafanya ni suala la kumvua uanachama yeyote ambaye si mwadilifu au anaonekana sio mwadilifu labda kwa sababu hawana dola hivyo hawana mahala pa kumweka azidi kuishi..

Rejea issue ya NAPE MNAUYE na sakata la Jengo la CCm alipobaini ukweli wa mambo na ufisadi ambao alidai ulikuwa ukisimamiwa na kamati ya udhamini ikiongozwa na Mh. Lowasa. Makamba Senior ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu wa Chama alimsimanga sana kijana kwa kuongea nje ya vikao na pia akavuliwa uanachama wa UVCCM kama kukumbukumbu zangu ziko sawa. Baada ya hapo sasa NAPE akapewa ukuu wa Wlaya Masasii..kisa amesema ukweli akatimuliwa uanachama na kwa sababu labda ayajua mengi mkuu wa kaya akampa ukuu wa Wilaya. Lakini mwenye mamlaka ya uongozi wa Chama ni Mwenyekiti na Katibu pamoja na Kamati zao zilizochaguliwa kihalali. Hivyo CHADEMA kuwafukuza uanachama wale wenye kuvuruga taratibu za chama lawama zisiwe kwa Mbowe wala Dr. Tlaa (Slaa) kama wao bali kama viongozi kwa vyeo vyao. Yaani mwenyekiti na Katibu. Na kama CCM tungekuwa tunafanya hivii nadhani tungekuwa na watu wazuri sana wanaobakia Chamani.

Hivyo basi nahitimisha bila kukuchosha msomamaji wa waraka huu usio rasmi kuwa, kwa kurudia hivi..tutaiua CHADEMA kwa kumaliza ufisadi Tanzania na si kuanzisha hoja za kitoto kuwa mwenyekiti anakopa (SHAME!!) "ooh anakadi mbili hana Mke kaiba mke wa Mtu" Hapana WanaCCm tuungane na upinzani wa hoja sio kingine na hata kuwaunga mkono zile hoja zenye msingi tu..na maendeleo tutayaona. Sio kila lisemwalo ni baya ama zuri! Kuna mabaya tuyaache na kuyakosoa na mazuri tuyaendeleze.
 
Ukitaka kujua ukweli wa mtu ni kwenye Fedha.
 
Willibrod Slaa


"Hoja ya kujikopesha kwa sura ya ufisadi ni "mfu" nimetamka nilikopa 20 kwa kuwa watumishi wa vyama hawawezi kukopa kwingine. Aidha siyo 140 Million. Zote 20 m zililipwa awamu ya mwisho June 2012. Hivyo hakuna deni la chama tena.
2. Josephine hajawahi kulipwa hata senti mmoja na chama kwa ziara za Mikoani, wala kwa shughuli yeyote ile isipokuwa wakati wa kesi Arusha alipokuwa na mtoto wa miezi 3 na tulihitaji yaya"



Wewe Mzee hoja siyo kwamba umekopa na kurudisha, hoja hapa ni je kwa mujibu wa Katiba, Kanuni, Miongozo na Taratibu za Chama cha Chadema kuna utaratibu wa mwanachama au Kiongozi kukopo na kisha kurejesha? kama upo ni acha wanachama wa kawaida je ni Viongozi wangapi wameshawahi kukopesha na CHADEMA kisha wakarejesha? weka wazi hapa na siyo kulete hadithi za ni kweli nilikopa sasa nimerudisha hiyo siyo hoja. Hoja hapa umetumia Ibara ya ngapi ya Katiba ya CHADEMA kukopa? au umetumia Kanuni namba ngapi ya Kanuni za CHADEMA kukopa, au umetumia kipengele cha ngapi cha Taratibu au Miongozo ya CHADEMA kukopa?.

Lakini pili unaposemanimetamka nilikopa 20 kwa kuwa watumishi wa vyama hawawezi kukopa kwingine sikuelewi, hivi hakuna Taasisi za kukuwezesha wewe kukopa? Mbona Mwenyekiti wako Mbowe alikopa NSSF. Kuna Mabenki, kuna SACCOS n.k lakini hizo zote haziwezi kukukopesha ila umeona CHADEMA ndiyo inaweza kukukopesha eti?
Ni aibu kubwa sana kwa Kiongozi anayesema ni mtetezi wa kupiga ufusadi wewe ndo umekuwa mstari wa mbele kuchochea ufisadi. Ufisadi siyo kuiba pesa tu hata kuzitumia au kukopeshwa kinyume na Taratibu zozote hata kama umezirejesha.

NATAKA KUKUONA UNATOKA HADHARANI na kuwaambia wanachama wako kuwa umekiuka Katiba, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya CHADEMA.Ninaposema CHADEMA ni NGO unaweza kusimama na kusema siyo hivyo? kama siyo NGO au SACCOS unawezaje kwenda kukopa kwenye Chama cha Siasa. Hivi kumbe CHADEMA ni CHAMA CHA MAENDELEO NA DEMOKRASIA kwa maana ya kuweza kukopeshana?

Wanachama wa CDM amkeni hizi ni zile kidogo zilizojulikana hiyo mijihela ya M4C waulize inakwenda wapi?Tazama na hii unayomtetea Mzinifu mwenzako Josephine "isipokuwa wakati wa kesi Arusha alipokuwa na mtoto wa miezi 3 na tulihitaji yaya" haya ni mambo ya Kitoto ambayo hayatakiwi kufanywa na Kiongozi wa ngazi ya juu kama wewe. kwa hiyo Katiba au Taratibu za Malipo za CHADEMA zinasemaje kwa mtu ambaye siyo Kiongozi wa chama lakini mume au mkewe ni Kiongozi wa Chama. Kama mtu huyo siyo Kiongozi eti kwa sababu ana mtoto na kwa kuwa anahudhuria kesi basi alipwe pesa na CHADEMA kwa kuwa mumewe ni Kiongozi ili aweze kuhudhuria kesi? HUU NI UPUUZI MWINGINE wa matumizi mabaya ya Fedha za Chama.
 
Wacha kukurupuka? unajua tofauti ya secured na unsecured Loans?

Toka lini chama kikawa mkopeshaji wa unsecured loan. Kanuni, mwongozo na taratibu zipi za chama zinatoa uwezo wa maofisa wa fedha ndani ya chama kutoa unsecured loan kwa wanachama
 
nimemchoka slaa na huyo sijui kimada wake. sina hamu nao. slaa aliwapa nini wanachama wa chdm hadi hawaoni madudu yake? mzee anakiua chama
Kama ulikuwepo yaani mimi ndio sioni wala sisikii, hapa naomba uhai tu, kura yangu ya Urais 2015 ni kwa Dr Slaa na si vinginevyo, ila Tshirt na Kanga na pesa za Magamba kama kawaida nitachukuwa, pesa nitatafuna Tshirt na kanga na kopelo nitatowa msaada kijijini kwa wasio na nguo za kujistiri.
 
Options
Willibrod Slaa


Hoja ya kujikopesha kwa sura ya ufisadi ni "mfu" nimetamka nilikopa 20 kwa kuwa watumishi wa vyama hawawezi kukopa kwingine. Aidha siyo 140 Million. Zote 20 m zililipwa awamu ya mwisho June 2012. Hivyo hakuna deni la chama tena.
2. Josephine hajawahi kulipwa hata senti mmoja na chama kwa ziara za Mikoani, wala kwa shughuli yeyote ile isipokuwa wakati wa kesi Arusha alipokuwa na mtoto wa miezi 3 na tulihitaji yaya

haa! hii post wakiisoma wale wazee wa vijisenti watacheka sana...

Huyu ndiye rais ninayemtaka mimi, na akigombea uraisi 2015 lazima nimpe kura yangu, yaani kukopa hela ya chama ndio tuhuma nzito saaaaana aliyonayo??? hata kama ingekuwa bilioni 10...kukopa ni kukopa. Halafu inaelekea mambo ya viongozi wa juu kwenye chama chao yapo wazi...mpaka mwenyekiti msaidizi wa Bavicha kajua ha! hivi mwenyekiti msaidizi wa UVCCM taifa anajua nini kuhusu ufisadi wa viongozi wake?

viongozi wa CCM huwa hawajibu tuhuma hata za kama ni za kuuza nchi! wakielemewa sana wana "achia ngazi" kimya kimya.
 
...""Kama sio juhudi zake Shonza, haya yote tungepata wapi... kama sio, Kama sio juhudi zake TUNTEMEKE, haya yote angejua nani? x 3"" huu wimbo umebamba na ni mtamu ukisindikizwa na vigelegele vingiii vya masalia na miluzi. I looooove this song!!!!
Kitu ambacho nimegundua ni kuwa watu wanajaribu kujibu hoja zako bila kujua kuwa wewe ni mentally disorder.
Ulichoandika hapa ndicho kinadhihirisha hilo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom