Game Theory,
Naona nimeanza hii Chrismas break hapa JF vibaya. Umeshambulia post yangu haraka haraka sana.
Kwanza kama umesoma vizuri maandiko yangu, sikusema kuwa jamaa huyu siyo mtaalam wa Nuclear Physics, ila nilisema kuwa siyo kati ya world class Nuclear Physicists anayeweza kuchimba na kuibua jambo jipya la kisayansi. Ana Ph.D ya Nuclear Phyisics kama walivyo wengine wengi tu.
Ni kweli kabisa kuwa kuandika paper siyo kipimo cha uwezo wa mtu kitaalamu; kwa hiyo endapo mtu ana majukumu ambayo hayamhitaji kuandika papers za kitaalam ni dhahiri kuwa hataandika lolote. Ndiyo maana hao watu wawili uliowataja hapo juu hawakupublish lolote. Lakini huyu jamaa alifundisha pale UDSM huku akijua kuwa mojawapo ya majukumu yake ni ku-publish na alishindwa kufikiria na kupublish mawazo yake ya kisayansi ipasavyo kulingana na standard zilizokuwapo wakati huo. Kwa vyovyote vile hakuwa anaweza kufikiria kisayansi outside his box. Ndiyo maana naamini kabisa kuwa jamaa huyu hawezi kuongoza taasisi ya kisayansi kama COSTECH.
Kuhusu yeye kuwa consultant wa NSA kwanza sijui una maana gani unaposema NSA. Kama una maana ya "Nuclear Systems Associates;" basi ni lazima ufahamu kuwa hii ni kampuni ya watu binafsi na kati ya consultant wanaowatumia ni watu wenye Bachelor's degree tu. Hiyo inaonyesha kuwa kuwafanyia kazi siyo lazima uwe world class material.
NSA nyingine ni "Nuclear Safety Associates", ambayo nayo ni kampuni ya watu binafsi sawa kabisa na NSA ya hapo juu.
Inawezekana una maana ya ANS (American Nuclear Society). Hii ni society ambayo mtu yeyote mwenye interest na Nucrelar science anaweza kuwa member kuanzia na wanafunzi klwa hiyo siyo kipimo cha kumfanya mwanachama wake awe ni world class scientist.
Ingawa ni kweli kuwa Mzee Bilal ni mmoja wa watanzania wachache waliosomea Nuclear Physics, lakini tusiwe tunapiga ngoma sana kudai kuwa ni mtaalamu mkubwa sana katika field hiyo wanayetambulika duniani duniani kote.
Kurekebisha record yako moja, tambua kuwa A.Q Khan aliiba michoro yote ya nuclear reactors, accelerators na centrifuges kutoka Uholanzi na kuja kuzireproduce huko Pakistan; hakufanya jambo jipya la kumfanya awe world class scientist. Kitaalam, yeye ni Metallurgical Engineer, na wala siyo Nuclear Physicist. Kinachofanya ajulikane sana ni kwa vile alianza kusambaza michoro hiyo kwa nchi mbalimbali na hiyo kutishia usambazaji wa silaha na Nuclear.