Majuzi kumetokea tangazo kwa wafanyakazi wa TPA kuchagua kubaki TPA au kuhamia DP World. Hili ni jambo zuri lakini binafsi nina ushauri kwa wafanyakazi wa TPA. Kwanza uamuzi wa jambo hili lifanyike kwa umaakini mkubwa na ninashauri kama ifuatavyo:
(1) Kampuni yeyote inapofanya kazi nia kubwa ni kupata fada. Hilo halina mjadala na hivyo nia kubwa ya DP World ni kupata faida. Pindi DP World atakapoanza kazi atafanya maboresho makubwa katika shughuli zake kwa maana ya mashine za kisasa ili kurahisisha kazi na kazi iliyokuwa inafanyika mfano kwa watu 100 inaweza sasakufanyika na watu 10 na hivyo kupunguza watu 90. DP World watawaita wale watu 90 na kuwapunguza kazi. Nia yao ni faida kubwa.
(2) Wale watakaohamia DP World watawekewa sheria zisizo rafiki, sheria ambazo hawakuzizoea walipokuwa TPA na hivyo kuwafanya kujiondoa wenyewe.
(3) Kufanya kazi DP World hakutakuwa usalama wa kazi (Security) kama ilivyokuwa TPA hivyo wakati wowote mfanyakazi anaweza kufukuzwa bila kufuata utaratibu.
Pamoja na maelezo niliyoyatoa hapo juu pia nitatoa faida ya kuendelea kufanya kazi TPA.
(1) Kufanya kazi TPA kuna usalama mkubwa wa kazi. Una uhakika na mshahara wako japo unaweza kuwa ndogo lakini utaendelea nao mpaka utakapostaafu kazi.
(2) Pia kufanya TPA una uhakika wa malipo ya uzeeni yaani pensheni pindi utakapofika umri wa kustaafu.
(3) Inawezekana kuhamishwa mikoani kwenye bandari mbalimbali mfano Musoma, Mwanza, Kyela, Ukerewe, Bukoba, Mtwara, Tanga n.k. Hiyo isikutishe. Mikoani kuna fursa nyingi.
Kwa hitimisho nawashauri MSIHAMIE DP World na baadaye msije mkajuta ila kama DP World atamhitaji mtumishi mmoja mmoja basi mkae nao meza moja na kujadiliana nao kwa kufuata vipengele vyote vya kazi na baadaye mnaweza kukubaliana.