Mkuu nafikiri huu ni ushindi kwa RA na wenzake, kama wamewasha mitambo yake unategemea nini tena?
Hakuna ushindi Mkuu hapa, kwanza itabidi huo mkataba wa kuwashwa tena mitambo ya Dowans ujulikane ni nani aliyeuruhusu na details zote za mkataba ziwekwe hadharani. Pili kuwashwa mitambo hiyo hakuhusiani kabisa na malipo ya $95m.
Mhhhh! Ndiyo maana yule January Makamba alipiga debe sana hivi karibuni kwamba ni lazima mitambo iwashwe kumbe walikuwa wameshaamua hivyo maana hata wiki mbili hazijaisha tangu atoe kauli hiyo mitambo imewashwa. Uongozi wa nchi hii hovyo kabisa!
Mitambo iliyodaiwa kuuzwa nchi za nje kumbe ulikuwa ni UWONGO MTUPU!
~@@~@@~@@~@@~@@~@@~@@~@@~@@~@@~@@~@@~@@~@@~@@~@@~@@~@@~
JENERETA za kufufua umeme za kampuni ya Dowans Tanzania Ltd ambazo zinatumia gesi asilia na ambazo ziliibua mjadala mkubwa wakati serikali ilipotaka kuzinunua, zimeuzwa nje ya nchi kwa zaidi ya Sh101 bilioni.
Kampuni ya kufua umeme ya Cyprus, Independent Power Corporation (IPC) ndiyo iliyonunua mitambo hiyo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 112.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa nchini Uingereza na mkurugenzi mtendaji wa IPC, Peter Earl, kampuni yake imeshafikia makubaliano ya kununua mitambo hiyo na kampuni ya Dowans Tanzania.
Kwa mujibu wa habari za kuaminika kutoka Shirika la Umeme (Tanesco), mitambo hiyo imeuzwa kwa kampuni ya IPC kwa gharama ya dola 77 milioni za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh101 bilioni za Kitanzania).
Pamoja na kwamba Tanesco hawakuhusishwa katika uuzwaji wa mitambo ya Dowans, imeuzwa kwa zaidi ya dola milioni 77 za Kimarekani kwa kampuni ya IPC, kilisema chanzo chetu
Akizungumza na gazeti hili jana mbunge Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe aliitaka serikali isiruhusu mitambo hiyo kuondoka nchini.
Zitto, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alifafanua kwamba mitambo hiyo haipaswi kuruhusiwa kuondoka nchini kutokana na kuwepo kwa kesi baina ya Tanesco na Dowans pamoja na kampuni hiyo kudaiwa Sh12 bilioni na serikali.
Tunawezaje kuacha mitambo iondoke wakati hatuna umeme,alihoji Zitto na kuongeza: Serikali isiruhusu mitambo ya Dowans iondoke nchini kwa kuwa kampuni hiyo inadaiwa na serikali. Pia kuna kesi mahakamani.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo alipotafutwa na Mwananchi.
Kwa sasa siwezi kusema lolote kuhusu hizo taarifa za uuzwaji wa mitambo ya Dowans, alisema Ngeleja.
Taarifa za kuuzwa kwa mitambo hiyo ziliibuliwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam katika ofisi ndogo za Bunge, wakati wa kikao cha kujadili ripoti ya hesabu za Tanesco za mwaka 2008.
Ripoti hiyo ilikuwa imewasilishwa kwa kamati ya POAC.
Taarifa ya kuuzwa kwa Dowans ilibainishwa na Zitto katika kikao hicho.
Hata hivyo mwanasheria wa Tanesco, Subira Wandiba alisema mitambo hiyo imezuiwa na Tanesco ambayo iliomba amri ya mahakama ili kama shirika hilo la serikali litashinda, mitambo itumike kama fidia.
http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=19144