Nadhani huajielewa dahana ya soko huria. IMF ilisema serikali ijotoe katika kufanya biashara na iruhusu private sectort kufanya shughuli. IMF haimaanishi kuachia wezi wapore au mikataba ya hovyo, wanachosema ni serikali isimamie shughuli na isijishirikishe kama mfanyabiashara.
Marekani waliachia soko huru bila serikali kuingilia matokeo yake ni economical crisis tunayoiona. Obama ameingilia kati na sasa pale Wall street kuna rules and regulations.
Margreth Sacher alipobinafsisha kila kitu UK, ilifika mahali wananchi wake wakamwambia no! kaa pembeni, hawezi kubinafsisha Posta na Reli. Elewa kuwa soko huria si soko holela na serikali lazima iwajibike kuhakikisha wananchi wake wanatendewa haki na wenye pesa.
Hakuna tatizo la shirika binafsi kuuzi umeme TANESCO, tatizo ni kuwa akina RA hawafanyi biashara ni matapeli wanaotaka kulipwa kwa hila mabilioni ya fedha. Bado serikali ingeliweza kuwa ''BAIL OUT'' TANESCO wanunue mtambo kama wa Dowans, lakini kwa hila BoT wame bail out Richmond/Dowans kwa sababu tu kuna watu wachache wanafaidika na mgao wa RA. hapa ndipo hasira za wananchi zilipo, si privatisation! Kutokana na madudu ya RA/EL leo tunapandishiwa bei ya umeme ili tumlipe RA. Jiulize, hivi kama TANESCO haina pesa za kujiendesha, inapata wapi pesa billion 100 kumlipa Dowans! huu si upuuzi wa kutufanya matutusa.
Sasa, tunasikia umeme umewashwa, maana yake ni kuwa Dowans inatambuliwa na kama inatambuliwa Richmond inapata uhalali, na ni kwa uhalali huo Lowasa anakuwa safi, Zigo linakwenda kwa Mwakyembe na Sitta wazalendo wenye uchungu na nchi hii.
Kwa taarifa tu, hujuma za umeme zimeingia Mabwawani, Songas n.k ili kujenga mazingira ya Dowans kuzalisha umeme. Tulijua kuna jambo pale January alipoteuliwa kuwa mwenyekiti wa nishati, akaanza na safari mtera, akaja na wazo la mkataba w miezi 6, Ngeleja akasema kunnuua Dowans si tatizo na kama watauza umeme hakuan shida, jenerali kaingia kinyemela Dar, jenerata zinawashwa siku inayofuata!
Tukimruhusu RA aendelee hivi tujue kuwa tunamuandaa Jenerli Farah Aideed, naye alikuwa na power kama ya RA.
Bora tukae gizani kuliko kumhalalisha fisadi huyu. Tusimfundishe panya kula sufi ipo siku atatafuna vidole.
sad!