DOWANS wawasha Mitambo yao

Mkuu jana nilikupinga sana, samahani.... nimeuliza the same question, KUUNGUA SONGAS NA KUWASHWA DOWANS KUNATUAMBIA NINI??

INAKUAJE MTU MWENYE KESI NA SISI AND ALL SORTS OF TROUBLES AKUBALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SISI?? HOW COME MITAMBO ILIUZWA KWA KAMPUNI YA KIGENI IBAKI UBUNGO? ILIKUA INALINDWA KWA GHARAMA YA NANI?

Ladies and gents, grab yo popcorns take a laid-back stance and enjoy this DOWANS blocbuster! Sure u gwan feel like giving somebody a BLOODY NOSE at the end!
 
naomba kutofautiana na wachangiaji wengi wanaomlaumu ra kwa kumleta mwekezaji.

mimi nadhani tungepaswa kuilaumu aidha benki ya dunia au shirika la fedha la dunia (imf) ambao ndio walioshinikiza sera ya serikali kujitoa kwenye biashara. Nasema hivi kwa kuwa ni kutokana na sera hii serikali iliruhusu watu binafsi kuzalisha umeme na kuiuzia tanesco. Kama hii sera isingekuwepo sidhani kama tungekuwa na kina iptl, aggreko, songas badala yake kungekuwepo uwekezaji wa nguvu tanesco ili wamiliki hiyo mitambo

Nadhani huajielewa dahana ya soko huria. IMF ilisema serikali ijotoe katika kufanya biashara na iruhusu private sectort kufanya shughuli. IMF haimaanishi kuachia wezi wapore au mikataba ya hovyo, wanachosema ni serikali isimamie shughuli na isijishirikishe kama mfanyabiashara.
Marekani waliachia soko huru bila serikali kuingilia matokeo yake ni economical crisis tunayoiona. Obama ameingilia kati na sasa pale Wall street kuna rules and regulations.
Margreth Sacher alipobinafsisha kila kitu UK, ilifika mahali wananchi wake wakamwambia no! kaa pembeni, hawezi kubinafsisha Posta na Reli. Elewa kuwa soko huria si soko holela na serikali lazima iwajibike kuhakikisha wananchi wake wanatendewa haki na wenye pesa.
Hakuna tatizo la shirika binafsi kuuzi umeme TANESCO, tatizo ni kuwa akina RA hawafanyi biashara ni matapeli wanaotaka kulipwa kwa hila mabilioni ya fedha. Bado serikali ingeliweza kuwa ''BAIL OUT'' TANESCO wanunue mtambo kama wa Dowans, lakini kwa hila BoT wame bail out Richmond/Dowans kwa sababu tu kuna watu wachache wanafaidika na mgao wa RA. hapa ndipo hasira za wananchi zilipo, si privatisation! Kutokana na madudu ya RA/EL leo tunapandishiwa bei ya umeme ili tumlipe RA. Jiulize, hivi kama TANESCO haina pesa za kujiendesha, inapata wapi pesa billion 100 kumlipa Dowans! huu si upuuzi wa kutufanya matutusa.

Sasa, tunasikia umeme umewashwa, maana yake ni kuwa Dowans inatambuliwa na kama inatambuliwa Richmond inapata uhalali, na ni kwa uhalali huo Lowasa anakuwa safi, Zigo linakwenda kwa Mwakyembe na Sitta wazalendo wenye uchungu na nchi hii.
Kwa taarifa tu, hujuma za umeme zimeingia Mabwawani, Songas n.k ili kujenga mazingira ya Dowans kuzalisha umeme. Tulijua kuna jambo pale January alipoteuliwa kuwa mwenyekiti wa nishati, akaanza na safari mtera, akaja na wazo la mkataba w miezi 6, Ngeleja akasema kunnuua Dowans si tatizo na kama watauza umeme hakuan shida, jenerali kaingia kinyemela Dar, jenerata zinawashwa siku inayofuata!
Tukimruhusu RA aendelee hivi tujue kuwa tunamuandaa Jenerli Farah Aideed, naye alikuwa na power kama ya RA.
Bora tukae gizani kuliko kumhalalisha fisadi huyu. Tusimfundishe panya kula sufi ipo siku atatafuna vidole.

sad!
 
Hakuna wakati Jakaya Lowasa Rpstam watakapo liwa safi ,japo wao wanatuona mazuzu,majinga na majitu tusiolewa kitu lakini ukweli tunagahamu kwamba wao ni wezi na majambazi wanstahiki juchomwa motto ukweli wenyewe wezi na wadhulumaji wanafanana dunia nzima
 
Wakuu hivi ninavyoandika ni kuwa mtambo mmoja wa Dowans aina ya LM6000 PD 40MW uliopo site A nyuma ya ghorofa la Tanesco umewashwa na hadi sasa unazalisha 37MW.

Nitawaletea habari zaidi lakini nina uhakika kuwa hawataweza kutembeza mitambo yao yote kutokana na sababu ambazo nitazieleza hapo baadae. Kiufundi mtambo huo kwa sasa ume-substitute mtambo wa Songas ambao kwa sasa upo down kutokana na kupata ajali ya moto hapo jana.

Habari kamili baadae.

Ndugu Mkeshaji,

Hii ni habari nzuri sana. Jee ni lini watawasha hiyo mingine iliyobaki ili tuondokane kabisa na mgao huu. Wanaolalamikia hili mimi nawashangaa sana. Kwa nini tukae gizani na wakati uwezo upo hapa hapa nchini? Tena kwa bei nafuu?

Naona cheche za mwenyeiti Januari Makamba zimeanza kuzaa matunda.
 
MAFISADI MKOME HII SINEMA YA HIVI SASA JUU YA DOWANS LAASIVYO TUKAPOROMOSHE 'MI-WIKILEAKS' ZAKE HAPA MPAKA MJISIKIE KUFAKUFA HIVI!!!


ccm+evap.jpg

928 × 575 - Katuni husema vingi! Tazama hii. Kazi ya mchora katuni, ...
bwaya.blogspot.com

Hawa wamiliki wa Dowans wa KUKODI wala hatudanganyiki!! Lowassa na Rostam Azizi, kaundeni mpango mwingine; huu hapa tayari umeanguka kwa pua.

Na mkijaribu kubisha basi TUTAPOROMOSHA USHAHIDI KAMA MVUA HAPA kuliko hata ya Wikileaks mpaka mshangae wenyewe. Naona bora mkasimamishe hii sinema ya huyo Msaudia aliyeletwa nchini na Ridhiwani Kikwete tayari na makabrasha yote bandia, kabla hamjapata kuabika zaidi!!!!

Pindi mtakapomaliza uongo mzima basi mtuambie ili ndio mmanze kuumbuka rasmi mbele ya kandamnasi mnaofikiri hatuko-deep.
 
Mi huwa sijielewi yani!mambo ya nchi hii sometimes huwa naona kama naota au nilishakufa kitambo!!niambieni jamani nimekufa ama?nchi inaendaje?maana naona uoza kila siku na kila kukicha!nisaidieni jamani sijijui kama nipo naota au nimekufa!
 
Ndugu Mkeshaji,

Hii ni habari nzuri sana. Jee ni lini watawasha hiyo mingine iliyobaki ili tuondokane kabisa na mgao huu. Wanaolalamikia hili mimi nawashangaa sana. Kwa nini tukae gizani na wakati uwezo upo hapa hapa nchini? Tena kwa bei nafuu?

Naona cheche za mwenyeiti Januari Makamba zimeanza kuzaa matunda.

Mkuu hiyo mingine sidhani kama itawashwa na hata huo uliowashwa sidhani kama utatembea kwa muda mrefu. Sababu kubwa ni upungufu wa gesi ya kuendeshea mitambo. Hili nitalieleza baadae kwenye thread yake.
 
Kwa taarifa tu ni kwamba mtambo wa pili wa Dowans umewashwa leo asubuhi kuingiza umeme kwenye Grid ya Taifa ....
 
Kamati ya Nishati kupitia ilitaka kuishauri serikali iingie mkatapa na DOWNS. Nina maswali yafuatayo
1. Wmeingia lini?
2. Mkatabata ukoje?
3. Malipo yakoje?

Haya mambo yatajirudia tena , halafu huyu jamaa mmliki wa Downs kaja na makwara sana,
1. Hataki apigwe picha, (Mwananchi leo kaweka kapicha kadogo sana)
2. Hataki kukutana na Ngereja.

Jamani mimi naona kizunguzungu
 
Kilicho baki ni wananchi kuchoma moto mitambo yeyote ile ya Dowans na Rostam ndipo wataelewa hatuwataki Tanzania.
 
Dodoma washeni moto hiyo mitambo ya dowans tuache kuzungumzia hii story for good.
 
Dodoma washeni moto hiyo mitambo ya dowans tuache kuzungumzia hii story for good.

YES, Besides DOWANS ni mali ya Chama Tawala - CCM. ilianzishwa na secretarieti ya halmashauri/kamati kuu enzi hizo RA akiwa Mweka hazina mkuu wa chama, na ndiyo maana eti DOWANS costa rica ilimpa RA mamlaka ya kukusanya fedha na kutumia kama atakavyo na si kupeleka faida costa rica. Tatizo mwakyembe and Co were not informed. Huku kulumbanana ni janja ya Jk kupass time.

To me Costa Rica ni pale Mtaa wa Lumumba
 
Kwa taarifa tu ni kwamba mtambo wa pili wa Dowans umewashwa leo asubuhi kuingiza umeme kwenye Grid ya Taifa ....

DOWANS wameingilia mlango wa nyuma. Wameingia mkataba na SONGAS. Umeme wao wanawauzia SONGAS. Kisha SONGAS inaiuzia TANESCO. Tafakari.
 
Wakuu hivi ninavyoandika ni kuwa mtambo mmoja wa Dowans aina ya LM6000 PD 40MW uliopo site A nyuma ya ghorofa la Tanesco umewashwa na hadi sasa unazalisha 37MW.

Nitawaletea habari zaidi lakini nina uhakika kuwa hawataweza kutembeza mitambo yao yote kutokana na sababu ambazo nitazieleza hapo baadae. Kiufundi mtambo huo kwa sasa ume-substitute mtambo wa Songas ambao kwa sasa upo down kutokana na kupata ajali ya moto hapo jana.

Habari kamili baadae.

Ndiyo mkuu,

Hayo ni makubaliano yao na Songas, Tanesco wala Serikali haihusiki.
 
Ndugu Mkeshaji,

Hii ni habari nzuri sana. Jee ni lini watawasha hiyo mingine iliyobaki ili tuondokane kabisa na mgao huu. Wanaolalamikia hili mimi nawashangaa sana. Kwa nini tukae gizani na wakati uwezo upo hapa hapa nchini? Tena kwa bei nafuu?

Naona cheche za mwenyeiti Januari Makamba zimeanza kuzaa matunda.

Lakini wewe, Watanzania asilimia 88 hawana umeme mbona hawalamiki. Tuvumilie machungu kwa muda tutatue tatizo la ufisadi.
 
Back
Top Bottom