Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Sasa ndio kabisa si Raisi si waziri wasije wakamfuata na kumuulizia mbona umeme kidogo au mbona kuna mgawo ,jamaa atafanya juu chini ili aanzishe mgao kwa kasi na kishindo kikubwa na nafikiri jamaa hatachukua muda atajiuzulu ili akatafute kazi nchi zingine ambazo mtu kama yeye atathaminiwa kuliko hapa ambapo nchi imejaa viongozi wababaishaji chini ya Sultani CCM wanalindana.
 
Wakuu naomba kuklarify hili suala.... Kuna alot of confusion kutokana na either misunderstandings or personal opinions.

...kukitokea mafuriko, au uharibifu mkubwa wa ghafla wa mitambo iliyokuwa ikitumika....In less than three months you can get them from any corner in the world.

...Tulinunnua portable power plant from Caterpillar (KQ2000) ambazo ni containerized zinalingana lingana kama zile ze dowans (Fuel inaweza kuwa natural gas, diesel au HFO). Capacity yake ilikuwa ni 1.6MW per container ss tulinunua tano and therefore totaling 8MW. Bei ilikuwa ni USD 252,000.00per container kwa hiyo kwa tano = USD 1,260,000.00.

Sasa basi kutokana na mfano huo hapo juu. That means mara kumi yake kwa bei na capacity ni 80MW for 12,600,000.00. Na kwa 100MW = USD 15,750,000.00. Ukichukulia bei ya controls na transformers say USD 5,000,000.00 which is a very high estimate unapata total ya USD 20,750,000.00. Assume kodi ni 100% which is also very high estimate unapata ni USD41,500,000.00. Hii ni kwa mitambo mipya kabisaaaaaaa.... enzi zile tulikuwa tunasema unachana karatasi.... Kwa nini Tanesco isitafute mitambo mipya kama ni ya aina hiyo

...Hivi kwenye hiyo sheria ya manunuzi ya umma hakuna kipengele cha dharura. Kwa nini Tanesco isitumie hicho?

...Ni kwa Nini Dr. Idris atutishe watanzania woote...Jeuri hii anaitoa wapi Dr. Idris? wakati kukosekana kwa umeme ni kuonyesha kwamba ameshindwa kazi?

Politicized mathematics!

Nyambala, unasema mitambo yenu ilikuwa "inalingana lingana na ile ya dowans." Mitambo yenu ilikuwa ni ya 1.6MW kila mmoja. Ilibidi muunge unge mitambo mitano ili kupata 8MW. Dowans wanaweza kuzalisha 100MW. Kupata 100MW kama Dowans inabidi ku string along vimitambo vyenu 63 (100MW divide by 1.6MW = 62.5). Uwezo wa Dowans ni sawa na vimitambo venyu 63!! Sasa hiyo "inalingana lingana"?

Kingine, unasema hiyo mitambo inaweza kuingia chini ya miezi mitatu. Ina maana, kama ulivyosema, "kukitokea mafuriko, au uharibifu mkubwa wa ghafla wa mitambo ..." basi tusubiri miezi gizani, si ndio? Miezi mitatu ndio expedited delivery? Unataka kumpa Zitto msemo kwamba wengi tuko out of touch with reality on the ground!

Kuhusu hiyo sheria ya manunuzi na kipengele cha dharura ambacho unauliza kama kipo, nadhani ni vizuri unge establish kwanza kwamba kipo kabla ya ku wonder ni kwa nini TANESCO wasikitumie.

Kuhusu Dr. Rashid, unasema ameshindwa kazi, well, Dr. Rashid allegedly alishaomba ku quit wakamkatalia. Yuko huru kufanya atakavyo sasa hivi. Sio kosa lake!

Dowans imetoswa kisheria, na kwamba it is a tainted company, it is infected. Ila, mahesabu yako ni politicized.
 
Kuhani:

Umemalizia vizuri: Everything about Dowans seems to be correct in so far as maths is concerned, but it is simply politically dirty and incorrect to enter into a deal with them!!
 
Tanesco ni wapumbavu hasa huyo mkuu wao, Hawawezi kumtunishia Kikwete kufua hii ni aibu wanamwaibisha muungwana mbele yetu.
 
Kimaro ataka Ngeleja, Malima na Rashid wawajibishwe

2009-03-07 12:31:27
Na Simon Mhina

Mbunge wa Vunjo (CCM) mkoani Kilimanjaro Aloyce Kimaro, ametaka Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja, Naibu wake Adam Malima na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme (Tanesco) Dk. Idris Rashid wawajibishwe kwa kitendo chao cha kula njama za kufanya ufisadi wa kutaka kununua mitambo chakavu ya Dowans.

Akizungumza na Nipashe jana, Mbunge huyo alisema ipo haja kwa Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha watendaji hao na baadaye kuwachukulia hatua kali za kisheria, ili iwe fundisho kwa wengine.

Alisema kosa sio kuiba pekee, bali hata kufanya njama za wizi pia ni kosa la kisheria hivyo japokuwa maafisa hao hawakufanikisha njama zao, wanatakiwa wawajibishwe na kufikishwa mbele ya sheria.

``Ni jambo la kusikitisha sana, yaani nchi ipo kwenye vita kubwa ya ufisadi, vyombo vya dola vinafanya kazi ya kukomesha suala hilo, leo watu wanadiriki bila aibu kuturudisha nyuma,`` alisema.

Aliunga msimamo wa Spika Samuel Sitta kwamba kuanza mikakati ya kushirikiana na Dowans ilikuwa sawa na kuirudisha Richmond kwa mlango wa nyuma.

Mbunge huyo alisema amesikitishwa na hatua ya Dk. Rashid kupigana kufa na kupona ili ununuzi wa mitambo ya Dowans ufanyike, huku akidiriki kuwatishia Watanzania kwamba nchi itaingia gizani.

Kimaro alisema viongozi hao hawastahili kukalia ofisi zao kwa vile inaonekana wanatumia matatizo ya Watanzania kama ukosefu wa umeme wa kudumu, kujineemesha wao binafsi.

``Zile zama za kuchekeana sasa zimepita, inaonekana bado kuna watu hawaelei dhamira ya Rais Kikwete ya kukomesha ufisadi na wizi wa mali ya umma.


Hali inaonyesha kwamba viongozi wa Wizara na wale wa Tanesco, walikuwa na dhamira mbaya sana juu ya sakata la Dowans,``alisema Kimaro.

Alisema kutokana na mwenendo na hatua walizochukua viongozi hao, inaonekana wazi kwamba wanajua akina Richmond ni nani na wako wapi.

Alisema suala la kutumia mitambo ya Kiwira pia nalo halina budi kupuuzwa kwani serikali ina hisa asilimia 15 huku `Bwana fulani` akiwa anamiliki asilimia 85.

``Sasa tukitekeleza mpango huo maana yake ni kwamba atakayefaidi ni `Bwana fulani` anayemiliki hisa kubwa. Imefika wakati watu walitumikie taifa lao, badala ya taifa kuwatumikia watu wachache,`` alisema.


Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini William Shellukindo, amesema amemsamehe Zitto Kabwe, kwa vile hajui alitendalo.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Shellukindo alisema haelewi ni kwa vipi Zitto alipata ujasiri wa kuzungumza mambo yanayohusu kamati yake.

SOURCE: Nipashe
 
Haya, mambo yameanza, hapa wanaingia waliokuwamo na wasiokuwamo...maadamu 2010 inakaribia nadhani tutayaona mengi tu zaidi ya haya...the call kwa hawa jamaa waachie ngazi ni sawa kwa upande wangu
 
Wakuu suala la mitambo ya Dowans limejadiliwa mna na ktk threads mbali mbali humu jamvini. Personally nimeona ni vema tukawa na thread maalum kama mada isemavyo hapo juu. Hii ni kutokana kwamba Tanesco, Zito na kamat yake, na wale wote wanaotaka kutuaminisha kwamba ununuzi huo ni jambo la busara wanaegemea hapo.

1. Eti kuna mkaguzi kutoka ujerumani amekagua mitambo hiyo na kuiona ni ok na mingine ni mipya ikiwa imetembea for only 400 hrs.

2. Eti mitambo hii itaweza kutembea kwa miaka 13 bila kufanyiwa overhaul.

Ningependa kuanza na huyu the so called mkaguzi:

1. Anatoka kampuni gani?

2. Ana qualifications gani?

3. Ana uzoefu gani na kazi kama hii na amewahi kutumika wapi na kampuni zipi?

4. Ana bima yeyote inayotulinda iwapo ikigundulika alituingiza mkenge?

5. Anatambuliwa na Pratt and Whitney kama mkaguzi wa mitambo yao i.e is he a certified inspector?

6. Mtaalamu huyu aliletwa na Dowans au Tanesco na ni lini alianza kuwa contacted?

7. Kama ni Tanesco nini kilipelekea Tanesco kumuita mtaalamu huyu? Ina maana walikuwa na nia ya kununua mitambo hiyo kabla hata ya kuangalia taratibu zingine?

8. Alifanya kazi hiyo ya ukaguzi kwa muda gani?

9. Alitumia method gani kufanya uhakiki?

10. Tanesco ilimpataje mkaguzi huyu? Wangapi waliapply?

11. Je Tanesco ipo tayari kutoa ripoti ya mkaguzi huo?

12. Wakati wa ukaguzi Tanesco iliwakilishwa na nani? Na Dowans pia na nani?

13. Je mtaalamu huyo amewahi kuifanyia kazi yeyote Tanesco au Dowans before?

Well I know some of you might think we are now going in circles on this SAGA.
Lakini vijiswali hivi ni rahisi na vinaweza kujibiwa na Idris au mtaalam yeyote wa Tanesco aliyehusika na mchakato huu in just 10 mins tena bila hata kusoma mahali for any smart kiongozi. Cha msingi hapa na nia ya maswali haya ni kujiridhisha na kamchakatohaka kanakoonekana kujustfy ununuzi wa mitambo hii.

Pia kuna hili la mitambokuwa mipya na eti mingine imetembea masaa 400 tu. Ikumbukwe kuwa mitambo in this new tecnlogical era hauijaji kwa time based bali condition based. That applies kwenye hili la kwamba mitambo hii haitakuwa overhualed in 13 yrs. Nikiwa kama muhandisi hii sentensi naona imekaa kisiasa zaidi kwani overhauling pia ni condition based and not time based. How do you sell me an equipment and tell me it won't be overhauled in so many yrs? Nchofahamu hapa huyu jamaa atakuwa alikuwa nazungumzia PM (Preventive maintenance) ambayo inaweza kuwa say kuna za daily, monthly, yearly na labda hiyo ya say after every 5 or 10 or even 20 yrs fungua hiki au kile angalia pale na hapa. Hii ni staili ya zamani ya maintenance. You don't have to just overhaul a machine et kwa sababu imetembea masaa 100, 000. (Anyways anayehitaji ziada ya hii I am ready to debate ). Ninachoshangazwa hapa ni how huyu mkaguzi ali come up na hiyo miaka 13 -tena kwa mtambo iliyotumika?

Haya yote yanakuja just because historia ya kampuni hii formely known as Richmond ina utata. Tanesco pia ni watata, serikali ni watata. Hivyo basi kuna kila haja Tanesco itoe press release ya kuelezea mtaalam huyu namaswali hapo juu. Si mnakumbuka hata Richmond waliatuambia wamekubaliana na Pratt and Whitney kushirikiana kuzaisha zile 100 MW? of which they any written doc to support that. Sasa hili la mtaalamu mjerumani tunaaminije kirahisi rahisi? Tunamuaminije kirahisi rahisi Dr. Idris wakati ana questionable credibility? Tunaiaminije Tanesco kirahisi rahisi wakati imekuwa ikitudisapoint thousands of times?

Viongozi wanatakiwa wafundishwe adabu maana wamezidi kuichezea Nchi. Mbinu ni rahisi sana mkiteketeza familia hata tano tu! za viongozi wapumbavu huu ujinga utaisha hapo Tanzania hakuna kiongozi atakaeleta dharau.
 
Infact hata power rationing ikifanyika vizuri na kwa mipango sahihi, tunaweza kudunda vilevile bila karaha mpaka pale tutakapokuja na suluhisho la kudumu na si kila siku kuweka plasta mpya!

Mkuu Kishoka,

Wacha utani bwana! Matatizo ya Tanesco yameniongezee gharama ya zaidi ya 25% kwenye kamradi kangu.

Mimi ni mmoja tu na si ajabu kuna Wafanyabiashara zaidi ya milioni ambao ni real victims wa haya malumbano.

Halafu eti tunatakiwa tuzalishe ili tushindane na wenzetu wengine wa dunia? Sahau, kila tunachofanya Watanzania kitakuwa bei juu mno kuliko nchi nyingi.

Binafsi sina huruma yoyote na mafisadi ila ifike mahali tunaposhughulikia masuala ya kitaifa tuangalie faida ya nchi na wala sio hasara kwa mbaya wetu mmoja.

Ni sawa tumeachana na Dowans lakini pia tutafute njia nyingine za uhakika kwa haraka.

Mfano Kiwira inakufa kwasababu ya ufisadi wa Mkapa, mimi ningeona wabunge wetu wako serious kama wangeilazimisha serikali kuutaifisha huo mradi mara moja ili uongozwe na wananchi wasio na scandal na uweze kupata baraka za kuzalisha umeme kwa faida ya nchi.

Sasa mitambo inakufa, wanaoweza wanachota vyao na kuvunja vunja mali mbalimbali za mgodi. Sawa tumewakomoa MKapa na rafiki yake Yona, lakini je kwanini tuendelee kuwakomoa pia mamilioni ya Watanzania?

Kuna haja ya kuwapa Tanesco meno na hizo nafasi zote za uongozi hapo kutangazawa ili wenye sifa waombe na kupewa majukumu ambayo inatakiwa wayatekeleze. NI muhimu kufuata ushauri wa wataalamu wetu, wakichemsha wawajibike hapo hapo.

Hii ya wanasiasa kutuamulia kwenye mambo makubwa kama sera ya nishati naona itatuletea matatizo mengi sana.

Kwa mimi kama raia ninachotaka ni umeme, kwenye haya malumbano kuna real victims wengi sana ambao hata hatuna sauti kwenye sera ya nishati Tanzania.

Mimi siamini katika hii miradi mikubwa mikubwa ya nishati maana ina matatizo yake mengi sana. Tungegawa nishati yetu hata kwenye maeneno kama 100 madogo madogo na ambayo yanaungana pamoja. Tuna makaa ya mawe, tuna jua la kutosha, tuna bahari kuanzia kaskazini mpaka kusini, lakini bado tunataka generator moja lizalishe umeme wa robo nchi huku hata uwezo wa kutengeneza hizo generator hatuna?
 
Wafuasi wa Sultani CCM wawache kutubabaisha ,tunahitaji Katiba mpya ili uvunaji mnaoufanya wa nguvu za wananchi uondoke mikononi mwenu.

Mnaanza kuwaibia kura zao ,mnawaibia rasilimali za nchi yao ,mnawaibia hata maamuzi haya yote ni kule kulindana mliko kujenga na hakutakwisha ,ikiwa mnaogopana kufukuzana mnaogopana kuambiana kweli ,mfuasi mmoja mmoja hawezi kufua dafu kwa kundi ambalo lina mtandao ndani yenu ,mtabaki kutoleana mineno tu lakini hakuna lolote linalofanywa ,kunahitajika nguvu za kikatiba kuwabana wababaishaji ,sasa huyu bwana fulani kama si mfuasi nambari one wa Sultani CCM anatokea Chama gani ,je ni wafuasi wangapi wa Sultani CCM wenye nembo hiyo ambao wameshapita na ambao wapo kazini ,ikiwa huyo fulani ameshapita je juhudi gani zifanywe kuwabana wanaokuja ?

Jawabu ni katiba mpya ndio palipo bakia ,tushapiga makelele mengi tu hakuna linaloonekana zaidi ya kubadilishana nyadhifa na kupeana majukumu mengine au ulaji mwengine. Tunataka kuona nguvu za Katiba zinatumikaje kwa hawa waliohujumu uchumi sio mnakandiana kutokana na kukoseshana tonge au kuondoleana tonge mdomoni wakati WaTanzania walio wengi wanakosa mahitaji muhimu na kufa vichochoroni kutokana na uozo wa wafuasi wa Sultani CCM ,KATIBA YA TANZANIA inamlindaje MTANZANIA kwa haya mauza uza mnayotufanyia ? Uwozo wenu sasa hauna siri tena umechafua hali ya hewa Tanzania nzima , tunanuka ndani na nje ya Nchi ,nini Katiba inasema tunapofikia hali hii ? Weka kando vyama vyote vya siasa maana vinaonekana kushindwa kuiweka sawa hali iliyopo ,tuiangalie Katiba kama katika KATIBA hamna basi tunahitaji ukarabati ili tuendane na machafuko haya.

Haitochi kwa wafuasi wa Sultani CCM kuchafuliana majina kupashana kila mmoja kujiona yeye anajua zaidi ,haya hayatoshi kabisa ni kupotezeana muda tu na kutubabaisha wananchi ambao joto la yote haya ni hasira za wengine kutulaza giza bila ya umeme wala maji na kukosa huduma muhimu zinazotegemea vyanzo hivyo.

Sultani CCM na wafuasi wake wameshindwa kuiongoza nchi na sasa wanabaki kutupiana mipira kama vile watazuka na jingine jipya lakini hakuna ,kila siku wanazidi kukoromeana ,kuna umuhimu wa kurudi kwenye KAtiba na kuitengeneza upya.
 
Kuhani,
Mkuu swala sio kuunga unga isipokuwa ni uwezo wa kupatikana kiwango cha umeme kinachotakiwa... Mara nyingi ktk maswala ya mitambo kama hii inategemea na maamuzi ya wahusika.. unaweza kuwa na mtambo mmoja lakini ukiharibika ndio kila kitu kinasimamma pia unaweza kuwa na vipande kikiharibika kimoja vingine bado vinafanya kazi... zipo faida hasara kwa kila design ya mmitambo kama hii..Na zaidi ya hapo kila mtambo unaweza kuwa na kiwango tofauti ya turbines.. inategemea na muundo. au sio!

Mkuu nitaendelea kuuliza ikiwa Dowans wanatoa MW100 na leo hii bado zipo sehemu zinakosa umeme wa kutosha ni dharura gani hii inayozungumziwa ambayo bado haitoshelezi mahitaji ya dharura mjini kisha tunatishiwa nchi nzima..

Yes, tunahitaji mitambo haraka sana kufidia nafasi ya Dowans, nachotaka mimi kufahamu ni pale Tanesco walipovunja mkataba na Dowans walikuwa wamejiandaa vipi na dharura hii inayojitokeza leo kwani dharura hii sio matakwa ya Mungu, tumepanga na kuchagua wenyewe kuingia ktk matatizo haya..

Kama walikuwa wamepanga toka mwanzo kwamba watanunua mitambno ya Dowans watupe sababu za wao kufikia maamuzi hayo, wasitumie dharura kuwa ndio sababu.. Na ilikuwaje badala ya kuagiza mitambo mipya wakati wakivunja mkataba.. Tumeona bei ya mitambo hii chakavu ni sawa na mipya tena ukienda site ya Watsila utaona wakisema kwamba mitambo yao yenye uwezo sawa na Dowans inatosheleza asilimia 20 ya mahitaji ya mji wa Dar! hivyo Dowans hawana tofauti kwa kiwango...Zaidi ya yote haya ukisoma report ya Tanesco inaonyesha wazi kuwa Hydro power zetu zote zinatoa chini ya kiwango kwa asilimia 50 kwa zaidi ya miaka minne kufikia leo hii..Na toka hizi generators zimefungwa ndio kabisa ukarabati wa hydro umekwama kabisa kwa sababu sasa hivi nchi inategemea zaidi umeme wa dharura na mipango mingi inaanza kuingia bara wakitumia neno DHARURA..My read ni kwamba viongozi wetu wana hisa zao ktk mafuta IPTL na gas Songas, kiasi kwamba umeme wa dharura umekuwa ndio vyanzo vya uzalishaji..

Na mwisho nitarudia tena kuwalaumu Tanesco kwani ktk report yao kuhusiana na tatizo la umeme inasema hivi:-
The Government approved TANESCO's plans to implement short term generation projects to avoid severe energy shortages which had serious negative consequences in the national economy.


Hapa kazi ya Kikwete na serikali yake ilikwisha kuhusiana na swala la dharura! ilikuwaje Tanesco wakanunua mitambo ya Watsila kwa bei ya poa kisha wakakodisha (lease) mitambo mingine toka mashirika manne tofauti tena kwa kutugharimu zaidi, kwa nini wasinunue miatambo yote toka Watsila kwa kiwango cha watts zilizotakiwa!...Hii mikataba yote ilipitishwa wakati mmoja June to July 2006 hizi fikra za kuwaibia wananchi zimetoka wapi! na iweje leo iwe tofauti kwanza Tanesco haikubali kufanya makosa yale na wanafikiria wananchi hawana idea kilichoendelea..Pia mitambo wa Dowans ni sehemu tu ya dharura nzima iliyokuwepo mwaka 2006, acha mbali uwezo mdogo uliokuwepo toka mwanzo..

Unataka kunambia hayo mahesabu yameonekana tu baada ya kuanza kukodisha au ilijulikana toka mwanzo umuhimu wa Tanesco kumiliki vyanzo vya umeme!..

Tanesco wenyewe ni part of the problem na kibaya zaidi ni pale wanapofikiria kwamba sisi bado tumelala wanaweza kuiongiza mkenge mwingine...Mkuu ikiwa Tanesco wanshindwa kufanya maintanance ya mitambo yao waliyokuwa nayo toka zamani iweje kuongeza mtambo mwingne mchakavu iwe ndio solution ya matatizo ya leo..
 
Politicized mathematics!

Nyambala, unasema mitambo yenu ilikuwa "inalingana lingana na ile ya dowans." Mitambo yenu ilikuwa ni ya 1.6MW kila mmoja. Ilibidi muunge unge mitambo mitano ili kupata 8MW. Dowans wanaweza kuzalisha 100MW. Kupata 100MW kama Dowans inabidi ku string along vimitambo vyenu 63 (100MW divide by 1.6MW = 62.5). Uwezo wa Dowans ni sawa na vimitambo venyu 63!! Sasa hiyo "inalingana lingana"?


Kuhani,

Maelezo ya Nyambala yako sahihi kabisa. Kama mgodi wanaunganisha unganisha hizo 1.6 MW, kama nchi tunatakiwa tuunganishe unganishe 20-50MW. Hizi zisambazwe nchi nzima. Kwenye maji, upepo, makaa ya mawe, solar panel etc. Ili mradi hizi mashine kubwa za 50MW kwenda juu zisiwe za kutegemewa sana au ziwepo kwa tahadhali kuwa ikikwama basi kuna nyingine 5 za 50MW zinafanya au zinasubiri kufanya kazi. Ikibidi hata muda kwa muda zinapumzishwa na kufanyiwa ukaguzi.

Hii inafaida kubwa kuwa ukiharibika moja ya mtambo mdogo nchini, nchi haiteteleki. Ila sasa mkiwa na mtambo kama huu wanasema ujengwe Rufiji, na unaanza kutoa 300MW, loo ni poa sana. Ila siku ukisimama basi nusu ya nchi ni mgao.
Itakuwa vizuri nchi za East Africa tuunganishe line zetu na mara mmoja akikwama basi wengine wanampatia umeme palepale bila ya kuuliza mara mbili. Mwisho wa mwezi mnalipana tu bila shida.

Inasikitisha sana mradi wa umeme wa Upepo wa Singida umekufa. Hainiingii akilini kuwa eti umekufa. Sijui kama ulikuwa na 10%. Nafikiri kwa hali iliyopo Tanzania sasa tunahitaji PUTIN wetu. Kajamaa ni kadogo ila kababe. Kizuri ni kuwa kama walivyo Wakomunisti wengi "Hakachekicheki".
 
Babu Ataka Kusema,

Suala la kumlaumu Dr. Idrisa na TANESCO ni kukukwepesha lawama ambazo zinatakiwa zielekezwe serikalini.

Na hii ni namna nyingine ya Ufisadi.


Upungufu wa Umeme unasababisha na ucheleweshwaji wa ukamilikaji wa mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira.... ambao umeme huo ungekuwepo Dr. Idrisa asingethubutu kusema tununue mitambo ya DOWANS.


Dr. Idrisa na TANESCO niko pamoja nao!
 
Mtanzania,

According to Tanesco, umeme wanaozalisha unafikia only 11% ya Watanzania kwa takwimu za 2006.

Sasa jiulize, ikiwa ni resheni, itafanyikaje kwa ubora ili tuwe wazalishaji bora na tusisikie makali?

Kuna alternative nyingi, kubadilisha miundo ya uzalishaji kwa kupima efficiency na capacity zetu, hivyo kuweza kutumia umeme vizuri na kutosheleza mahitaji ya wote. Aidha tunaweza kutumia umeme wa jua, upepo lama alternatives.

Lakini kwenye hili unalosema la mahitaji yako ya umeme, will you approve the complete privatisation of energy sector especially on electricity?

We have EWURA, it can manage all the the Power Grid and lease the lines to Tanesco and other independent power companies to produce and distribute electricity hence ending teh monopoly of Tanesco (basically, privatise Tanesco to the full, without protection from URT)!
 
Politicized mathematics!

Nyambala, unasema mitambo yenu ilikuwa "inalingana lingana na ile ya dowans." Mitambo yenu ilikuwa ni ya 1.6MW kila mmoja. Ilibidi muunge unge mitambo mitano ili kupata 8MW. Dowans wanaweza kuzalisha 100MW. Kupata 100MW kama Dowans inabidi ku string along vimitambo vyenu 63 (100MW divide by 1.6MW = 62.5). Uwezo wa Dowans ni sawa na vimitambo venyu 63!! Sasa hiyo "inalingana lingana"?

Dowans wanauwezo wa kuzalisha hiyo 100MW kwa namna gani?
 
Nimesoma maelezo ya Rev.Kishoka na kuona hao seamens wanayo mitambo hadi ya 1200MW, mahitaji yetu kwa sasa ni 100MW then mwakani tutatakiwa kuongeza 75MW yaani itahitajika Dowans nyingine tena!

Kwani tukiachana na biashara ya vitambulisho dowans tanpower radar ATCL uchaguzi 2010, tutumie pesa hiyo kufunga mtambo wa 1200MW dar na 1200MW kiwira itakuwaje? kama kweli tanesco wanazalisha 575MW kwa sasa na hautoshi basi mapato yao yanatakiwa yawe 68bn kwa mwezi. sasa wanakusanya ngapi? isijekuwa tuna vi-ATCL vingi vingi humu nchini.

Nahuyu Dokta idrisa kasema tukipungukiwa 100MW wagonjwa watakufa, watoto hawataenda shule, kwamaana anatishia amani ya nchi yetu? kwamba tusiponunua mitambo ile nchi haitakalika, hao mongiki amewaandaa lini? yaani tuvunje nchi yetu tuliyoijenga kwa miaka 48 kisa ni 60bn, fedha isiyotosha hata dhamana ya Liyumba! kweli dokta unatuombea tufike hapo? kwa njaa gani hasa jamani? au kunaushirikina ndani yake?
 
Wakuu mnajua uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi haujafanyika mpaka sasa na tatizo ni pesa, ilikuwa Tanesco wanunue Dowas na baadaye uchaguzi ufanyike.
RA is very clever in fooling Tanzanians.
cjui EL angerudishwa kuwa PM tena ?kama Dowas ingenunuliwa na Tanesco? Du inashangaza sana nchi hii! cjui Hatuna Kiongozi wa nchi?
 
Kuhani,
Mkuu swala sio kuunga unga isipokuwa ni uwezo wa kupatikana kiwango cha umeme kinachotakiwa... Mara nyingi ktk maswala ya mitambo kama hii inategemea na maamuzi ya wahusika.. unaweza kuwa na mtambo mmoja lakini ukiharibika ndio kila kitu kinasimamma pia unaweza kuwa na vipande kikiharibika kimoja vingine bado vinafanya kazi... zipo faida hasara kwa kila design ya mmitambo kama hii..Na zaidi ya hapo kila mtambo unaweza kuwa na kiwango tofauti ya turbines.. inategemea na muundo. au sio!

Mkuu nitaendelea kuuliza ikiwa Dowans wanatoa MW100 na leo hii bado...

Mkandara, a.k.a Bob Mkandara, kama unavyoitwa na Sauti ya Umeme, halafu anasema heshima mbele!

Ni hivi. Ni kweli kabisa kuna faida na hasara za mitambo mikubwa na midogo na sijasema lolote ubaya wa mitambo ya power plant ya kampuni ya Nyambala. Ila nasema, hesabu alizotoa Nyambala zime misrepresent uwezo wa mashine zao kwamba "zinalingana lingana na za Dowans." Come to find out ili kuweza kufikia uwezo wa Dowans, inabidi uunge unge vi-mitambo vya Nyambala 63!

Kwa hiyo Nyambala asiseme, na wewe usitetee, upotofu kwamba vijimitambo vya power plant yao ni sawa na Dowans. Ubaya wa Dowans ni legacy ya ufisadi wa Richmond na kanuni zinazokataza kununua vifaa chakavu.

Kuhani,
Maelezo ya Nyambala yako sahihi kabisa. Kama mgodi wanaunganisha unganisha hizo 1.6 MW, kama nchi tunatakiwa tuunganishe unganishe 20-50MW. Hizi zisambazwe nchi nzima. Kwenye maji, upepo, makaa ya mawe, solar panel etc. Ili mradi hizi mashine kubwa za 50MW kwenda juu zisiwe za kutegemewa sana au ziwepo kwa tahadhali kuwa ikikwama basi kuna nyingine 5 za 50MW zinafanya au zinasubiri kufanya kazi. Ikibidi hata muda kwa muda zinapumzishwa na kufanyiwa ukaguzi.

Hii inafaida kubwa kuwa ukiharibika moja ya mtambo mdogo nchini, nchi haiteteleki. Ila sasa mkiwa na mtambo kama huu wanasema ujengwe Rufiji, na unaanza kutoa 300MW, loo ni poa sana. Ila siku ukisimama basi nusu ya nchi ni mgao.

Sikonge, hueleweki. Kwanza, fahamu kwamba Nyambala kasema tununue vimitambo vya 1.6MW, wewe unasema tununue mitambo ya 20-50MW. Kwa hiyo hata wewe unacho ki advocate hakiendani na alichosema Nyambala. Kwa kweli umeunga tela pointi kichwa kichwa wakati na wewe mwenyewe huonekani kui support. Pili, kuhusu faida na hasara za mitambao mikubwa na midogo, mimi sikusema ubaya na uzuri wake, ile nimesema Nyambala katoa mfano irrelevant, misrepresented, wa vi generator vya 1.6MW akasema vinafanana na nguvu ya Dowans. Si kweli!

Lakini tukiachana na mifano misreprented wa vijimitambo vya Nyambala, hata wewe umejichanganya. Umesema kuna faida ya kununua vijimitambo vidogo kama vya power plant ya Nyambala, halafu hapo hapo unasema utatoa 300MW na ni poa: "...Hii inafaida kubwa kuwa ukiharibika moja ya mtambo mdogo nchini, nchi haiteteleki. Ila sasa mkiwa na mtambo kama huu wanasema ujengwe Rufiji, na unaanza kutoa 300MW, loo ni poa ..." Una maana gani hapo, vimitambo hivi vitatoa 300MW? Hueleweki.
 
Nafikiri swala sio Rais wetu yuko upande upi,
Tazama aliwahi kuulizwa na mwandishi mmoja kule Paris juu ya umasikini wa afrika, akajibu namnukuu " hata mimi sijui kwanini mpaka leo sisi ni masikini" Hili ni jibu la mpumbavu haswa akiwa kiongozi wa nchi Aliye ingia madarakani na kukuta Gari mpya za aina ya benz mpya kwa ajili ya msafara wake zimenunuliwa punde tu kwa mapesa mengi lakini baada ya miaka mitatu ananunua gari nyingine aina ya BMW kwa mapesa mengi tu, bila hata ya kutueleza wananchi zile nyingine zina matatizo gani????? kwenye nchi maskini kama hii, inashangaza, tazama kama ukinunua gari mpya inaweza kutumika hata miaka ishirini kama inatunzwa vizuri, Haya kuna mradi wa vitambulisho vya Taifa utakaogharimu bilioni 200, hiki ni kichekesho kwenye nchi ambayo watu hufa kwa malaria na mama wajawazito kwa kujifungua, na albino na vikongwe kwa baadhi ya watu kukosa elimu kwa sababu tu eti hakuna pesa za kutosha kuweka zahanati na shule ili watu waondokane na ujinga, inashangaza priorities zetu ni zipi????? hivyo vitambulisho ni muhimu kuliko elimu na uhai wetu?????????, Tazama ziara yake ya bandarini ndio iliyo nitia kishefushefu kabisaaaaa, aliwauliza kuhusu idadi ya container ( makasha ) yaliyopo na yaliyokwishatolewa akajibiwa bado wanafanyia kazi eti kwa sababu bado wanatumia manual hawana computer, jibu lili tolewa na waziri mwenye dhamana yeye akacheka tu, huu ni upuuzi kwanini hatimui waziri na watendaji wa bandari kama bandari inanunua vogue ya mamilioni kila baada ya miaka miwili kwa ajilia ya mkurugenzi mkuu kutembelea hivi hawaoni kwamba wakiacha kununua mwaka mmoja tu hiyo pesa inatosha kuweka mtandao wa computer ili kazi ifanyike kwa ufanisi faida ikue mara dufu hapo wataweza kununua hata gari kama analotembelea obama?????, yapo mengi siwezi kuandika yote yanatia hasira sana,

Rais anaweza kumfukuza kazi waziri wa Nishati na kuihamishia wizara nzima ikulu ili ashughulikie mwenyewe suala la nishati.
Ni kweli kwamba suala la umeme halimsumbui Rais hata kidogo, aidha hajui umuhimu wa nishati ya uhakika kwa maendeleo ya nchi.
Yeye akienda nje ya nchi kuongea na wawekezaji siku zote anatakiwa kujua wakija watakuwa na nishati ya uhakika, vinginevyo nakubali maneno ya watu kadhaa kwamba shule aliiacha pale Mlimani akaja uraiani mtupu.
 
Dowans wanauwezo wa kuzalisha hiyo 100MW kwa namna gani?

Mwanakijiji, kwenye hili swala la Dowans, mkuu una spin spin tu.

Mwanzoni ulisema tumwachie huru Gire nunue mitambo, na kwamba Rostam ameshatushinda and what not.

Baadae ukamtetea Zitto, japo ukasema hukubaliani na mahitimisho yake.

Ulipoulizwa mahitimisho yako wewe ni yapi ukasema tukasome Cheche.

Kwenye Cheche kuna mahitimisho ya Jessica Fundi na Fred Katunzi.

Sasa basi, kwa sababu kwenye hili swala wewe kama Mwanakijiji unaogopa kuchukua msimamo mimi nadhani sio busara kujadili kitu na ghosti Jessica na ghosti Fredi!
 
Back
Top Bottom