Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

==========

Ni kweli kauzoefu kanapungua kwa kijana huyu. Lakini tufanyeje, in the absence of ... hata mwenye jicho moja tunamshangilia.

Kaumaarufu ndio kanapungua lakini naamini changamoto hii inampa uzoefu zaidi kama KIONGOZI na pia kama Mwanasiasa.

omarilyas
 
Jamani zitto sio fisadi ila napata wasiwasi, kakaa bungeni mwaka mmoja kaja na Hammar, then sijui mhindi au mmatumbi kafika bei, sasa ana VX Lexus. keshavuta za malikia yuro 200,000 ati anapeleka maendeleo pemba, duh! namna hii ushirikina hautaisha, hivi lile prado la marehemu CCM walishalikomboa gereji? Mzazi anasema hana hela linakunywa wese kama airbus.
 
KGM,
Una ushahidi gani wa hiyo accusation yako? I disagree with Zitto kwa jinsi alivyolishughulikia hili suala la TANESCO-DOWANS, lakini ku-conclude kuwa yeye ni fisadi kwa vile tu amesema ambacho Rostam anataka kusikia, ni kuonyesha kuwa ulikuwa una nia ya kumpa hiyo branding no matter what na ulikuwa unatafuta tu nafasi ya kufanya hivyo kwani hakuna ushahidi wowote wa ufisadi wa Zittto.

Na wewe nawe unataka ushahidi gani ndugu yangu?.
Unataka nikwambie nimemshudia akipewa Burungutu la wekundu wa msimbazi.????. He He He He He He He.

Hata Ubunge amekwambia hana haja nao tena unafikiri ni BURE+Maneno yanayomtoka utafikiri mgonjwa wa maleria iliyopanda kichwani.
 
Wakuu,

Hivi kelele zote hizi bado hakuna anayesema mtambo mpya wa kununua huu hapa?

Angalau Zitto ameonyesha hafuati upepo na yuko tayari kukosa umaarufu wa kisiasa kwa kitu anachokiamini.

Wanasiasa wote wamehamia Dar kupiga kelele za mtambo, hakuna uamuzi unachukuliwa, nchi giza totoro baada ya muda tunajiuliza eti kwanini hatuendelei?

Haya makundi yanayopingana yangeliweza kukaa pamoja na kujadiliana kwa wiki na kisha kuamua cha kufanya sio kama sasa wanasiasa wamegeuka watalaamu wa umeme.

Wacha wengine tuwajibike!

Mtanzania,

Kuna mtu anaitwa Kokolo alishaweka jibu ya swali lako...angalia posts za nyuma utaikuta hiyo unayoulizia
 
Mitambo tayari ipo ni $39million for 100MW mipya pamoja na warranty ya miaka 7 from the world biggest company of manufacturing Turbine and Jet engine ni kwenda kuchukua na kuwasha, hakuna kununua second hand kwa $60million.

ooopps kumbe alishakujibu hapo juu......haya sasa Mtanzania washauri hao wakulu basi
 
Zitto, huyo anaeitwa Omary Ambaye kila saa anajitia kukusafisha ama kukutetea hafai hata kidogo kuwa mshauri wako kwani ni kama wale ambao wanaweza kumwambia mfalme umependeza kumbe yuko uchi.

Huyu jamaa anapaswa kuwashauri watu wapenda sifa kama Mzee wa kiraracha pamoja na Mtikila ambao wanapenda kusifiwa kila wanalolifanya ila ukimwendekeza atakupotezea mbali sana .

Huyu jamaa anajifanya kujua kuwa wewe unamsimamo gani ,na anafika mbali zaidi kuwaona wengine ambao wanajaribu kukuonyesha upande wa pili wa shilingi kuwa hawajui wanalolifanya , jiepushe na washauri wa aina hiyo kwani ni watu hatari na hata siku moja ukikosea hawatakuwa tayari kukueleza ukweli wa mambo.

Sijawahi kujiunga humu Jf ila tangu mjadala huu uanze , nimekuwa nikisoma na nimemwona kuanzi thread za mwanzo kabisa akimshambulia kila mtu ambaye anajaribu ama kukuonyesha feeling za jamii na haswa watanzania wengi ambao walikuamini.

Anafika mahali anaandika eti wewe uko tayari kuchukua maamuzi magumu , na anaita hilo unpopular decisions , kwenye ulimwengu huu anayechukua maamuzi magumu sharti awe na uwezo wa kuyatekeleza , wewe unauwezo gani wa kuamua kununuliwa kwa hiyo mitambo kama huo ndio uamuzi mgumu?

Bush alichukua unpopular decisions , na alikuwa na mamlaka ya kufanya yatekelezeke, wewe hizo mamlaka huna mpaka sasa , sasa hao wanaokushauri hivyo jua kuwa ni watu ambao hawakutakii mema , jitahidi sana kuwa msikivu,mpole ila mwerevu kama nyoka .

Nimejiunga humu leo ili niweze kuandika ujumbe huu, niko mbali sana na huko nyumbani ila leo niliongea na watanzania walioko huko na wamenieleza kusononeshwa sana na msimamo wako huo, tafuta njia ya kutoka kwenye mtego.

Namshukuru aliyeanzisha mtandao huu kwani ni wa afya pamoja na wengine kujiandikia tuu kwa sababu wanajua kuwa majina yao sio halisi hivyo hawako responsible kwa chochote watakachoandika.
 
===============
Breaking News: 100% verified.

Tayari keshapata taarifa kwamba mitambo mipya ipo tayari kutoka kwa biggest manufacture of Gas turbine na bei yake ni $39million for 100MW ndo maana hakupenda kusema uongo mbele ya waandishi wa habari maana angejimaliza moja kwa moja. Mitambo hipo tayari ni kwenda kuchukua tu na kuwasha. Warranty ni 7 years with commissioning for 30 years. hiyo mitambo Serikali watakaa nayo kwa miaka 40-50. hiyo mipya toka kwa huyo manufacture . Mtambo mpya kwa hali ya kawaida ni $35-46million na siyo $90million labda kama inatengenezwa mbinguni.

kama mambo ni hivi basi kuna kundi la watu linahitaji kujiuzulu haraka iwezekanavyo. Angalia PM yako.
 
Ahsante Mkuu. Huyo Omary ni mmoja wa makuwadi wa Rostam, hivyo lazima amtetee Zitto pale ambapo Mbunge huyo kijana anamwekea kifua "ndugu" yake Rostam. Tumeshasema awali kuwa Zitto ni rafiki mkubwa wa Rostam na diyo maana Zitto yuko tayari kumcriticise mtu yeyote awe Kikwete au Sitta laki hwezi hata kidogo kumgusa Rostam.
 
Hapa JF kwa mtu ambaye si mzoefu anaweza akajikuta anapakimbia siku ya pili. Wakati mwingine najiuliza nifananishe na kikaangio cha samaki au tanuru ya matofali ya kuchoma..?
 
===============
Breaking News: 100% verified.

Tayari keshapata taarifa kwamba mitambo mipya ipo tayari kutoka kwa biggest manufacture of Gas turbine na bei yake ni $39million for 100MW ndo maana hakupenda kusema uongo mbele ya waandishi wa habari maana angejimaliza moja kwa moja. Mitambo hipo tayari ni kwenda kuchukua tu na kuwasha. Warranty ni 7 years with commissioning for 30 years. hiyo mitambo Serikali watakaa nayo kwa miaka 40-50. hiyo mipya toka kwa huyo manufacture . Mtambo mpya kwa hali ya kawaida ni $35-46million na siyo $90million labda kama inatengenezwa mbinguni.

Kokolo,
Nina wasiwasi na hiyo Breaking News yako yenye 100% proof.
  1. Mitambo ya 100MW tubine kwa U$39mil??? Tuambieni mtengenezaji ili tuijadili maana hii mitambo sio siri, habari zake zote zipo kwenye ripoti mbali mbali mitandaoni.
  2. Hii mitambo hasa inapokuwa mikubwa zaidi (in this case 100MW), haipatikati off-the-shelf, unless iwe used. Kwa kawaida inatengenezwa tu pale order inapotolewa.
 
Zitto, huyo anaeitwa Omary Ambaye kila saa anajitia kukusafisha ama kukutetea hafai hata kidogo kuwa mshauri wako kwani ni kama wale ambao wanaweza kumwambia mfalme umependeza kumbe yuko uchi.

Huyu jamaa anapaswa kuwashauri watu wapenda sifa kama Mzee wa kiraracha pamoja na Mtikila ambao wanapenda kusifiwa kila wanalolifanya ila ukimwendekeza atakupotezea mbali sana .

.

U need to know me better than that but thanks kwa maneno yako makali inawezekana unayosema ni kweli haswa mfano wako wa Bush na msimamo wake ambao ukweli hata kama umesaidia kulinda Marekani lakini pia ilimuumiza kisiasa.

Hata hivyo kama umesoma vizuri tatizo langu ni wale wanakimbilia kuhukumu kuwa Zitto amekuwa na msimamo aliochukuwa jeti kwa sababu amehongwa. Hilo nitalisimamia hadi mwisho labda nipate ushahidi unaosema tofauti na nimjuavyo Zitto.

Kuhusu USHAURI wa kununua mitambo ya DOWANS kama umenifuatilia vizuri basi utajua kuwa mimi sijaunga mkono hoja hiyo asilimia 100 but nalichukulia suala zima kama nafasi ya Zitto kukomaa kiuongozi. Natambua kuwa kusimamia msimamo wa KAMATI, narudia tena msimamo wa KAMATI YA MAHESABU YA MASHIRIKA YA UMMA kunamuweka vulnerable for political attacks lakini pia kunamsaidia kukua kiuongozi na pia kushape style ya uongozi na siasa katika nchi yetu.

Omarilyas
 
ooopps kumbe alishakujibu hapo juu......haya sasa Mtanzania washauri hao wakulu basi

Mkuu Ogah,

Hiyo ndio taarifa ya kutumia kununua mtambo wa dola 30m? Kumbe ndio maana Richmond walituzidi speed.

Kamati ya bunge walisema kuna mitambo ni bei rahisi, si watoe data kamili? Pia waeleze hiyo ya DOWANS ni pesa ngapi?

Longo longo za sisi watanzania zimezidi. Watu wanaingia hasara kwa kukosa umeme, sisi bado ni yale yale habari za nusu nusu.
Itafika mpaka budget bado hakuna kitu zaidi ya mabishano ya siasa.
 
Na wewe nawe unataka ushahidi gani ndugu yangu?.
Unataka nikwambie nimemshudia akipewa Burungutu
la wekundu wa msimbazi.????. He He He He He He He.

Hata Ubunge amekwambia hana haja nao tena unafikiri ni BURE+Maneno yanayomtoka utafikiri mgonjwa wa maleria iliyopanda kichwani.

Kwa mtu ambaye siku zote amekuwa mbele kulitetea taifa, ili umfanye awe fisadi ni lazima uwe na proof zaidi ya kuunganisha sentensi mbili tatu.

Naamini Zitto amekosea na ninamshauri hili suala likikamilika aweke wazi kuwa alikosea lakini tusimkatishe tamaa kwa vile tu tuna key board. Hakuna jemadari asiyekosea, muhimu kwetu ni kumkosoa kila anapoyumba.
 
Ahsante Mkuu. Huyo Omary ni mmoja wa makuwadi wa Rostam, hivyo lazima amtetee Zitto pale ambapo Mbunge huyo kijana anamwekea kifua "ndugu" yake Rostam. Tumeshasema awali kuwa Zitto ni rafiki mkubwa wa Rostam na diyo maana Zitto yuko tayari kumcriticise mtu yeyote awe Kikwete au Sitta laki hwezi hata kidogo kumgusa Rostam.

Sawa wewe MZALENDO uliokubuhu. Mwenyewe najijua na thats what matters. Mnataka mpige kampeni zenu chafu halafu mnyamaziwe. Hapanaaaaaaaaaa

Omarilyas
 
Ahsante Mkuu. Huyo Omary ni mmoja wa makuwadi wa Rostam, hivyo lazima amtetee Zitto pale ambapo Mbunge huyo kijana anamwekea kifua "ndugu" yake Rostam. Tumeshasema awali kuwa Zitto ni rafiki mkubwa wa Rostam na diyo maana Zitto yuko tayari kumcriticise mtu yeyote awe Kikwete au Sitta laki hwezi hata kidogo kumgusa Rostam.

Acheni hizo za kuleta umbea.

Kila mtu anahaki ya kuwa na muelekeo tofauti ndani ya JF. Tusianze kupakana matope kwa vile tu wengine wana fikara tofauti na za kwetu.

Anayesema Zitto ni shoga wa Rostam alete data, o/w huo umbea afanyie nyumbani sio JF.
 
Naona huyo Mama anawachezesha mdumange anapiga filimbi na nyie mnacheza kweli kweli.

Duh, kama vile mko kwenye mbio za rilei washkaji, poleni sana.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,
MakaayaMawe na wengineo, tafadhali tusitoke nje ya Mjadala...
Ikiwa wapo watu wamekosa imani na Zitto sio dhambi kabisa kwanai hata rais wetu popularity yake inapungua na kupanda kutokana na watu wale wale..Leo Zitto kateleza kesho atajikusanya na kurudisha imani za watu..

Binafsi nina imani kubwa sana na Zitto, ni mtu ambaye namkubali sana ktk mambo mengi isipokuwa ktk hili nadhani nilikuwa wazi toka siku ya kwanza. Tatizo laker kama binadamu aliyekanyaga miwaya hakutaka kuelewa wala kusikia na pengine lugha yake mwenyewe ilikuwa nzito kiasi kwamba watu kama KGM na Moelex23 (including me) tulishtuka sana..Kuna tofauti kubwa sana kati ya kufanya makosa ukakubali kufanya makosa yakarekebishwa, kuyarudi maneno (kauli) yako na mtu kuwa mkali usieleweke ktk issue ambayo ni tata Kisiasa na Kiuchumi..

Kifupi mapishi ya deal hili, tuliyasikia kabla Zitto hajajitokeza na tulifahamishwa kupoteza baadhi ya watu muhimu sana ktk mapambano ya Ufisadi..Bahati mbaya mtu mwenyewe ndio kawa Zitto!..na hii ikanirusidha nyuma kuanza kufikiria siku ambayo Kikwete alipomchagua Zitto ktk kamati hizi, viongozi wengi wa Chadema walipinga uchaguzi huo na kumkanya Zitto asijiunge, lakini yeye alichukua msimamo wake ambao wengine tulimuunga mkono.. leo hii ni ktk mlolongo wa kamati hizo alipokuja na somo pinzani na mtazamo wa wananchi wengi (JF).. tena basi akiwa kamati ya mahesabu, kamati ambayo ilitakiwa kuwa na hesabu zote za gharama na matumizi toka pande mbili (Tanesco na Mitambo) kabla ya kutoa maamuzi (Mahitaji ya mtambo) yanayohusiana na kamati ya nishati..
Ni lazima watu wataweka mashaka wakuu zangu.. sio kwamba hatuna imani tena na Zitto, huyu wetu tutakwenda naye sambamba kuliko kumwachia akazama..Tukimpoteza mtu kama Zitto ni pigo kubwa sana kwa Upinzani, hivyo maneno yetu ayachukulie kama ni hasira zetu zinazoweza kusameheka iwe yeye kutusamehe au sisi kumsamehe lakini kikubwa ni kwamba ameelewa msimamo wetu kuliko kukaa vijiweni na kuanza kumteta!
 
Mama,
Duh ama kweli mwanamke wewe hunitaki!..nachelea kusema kwamba unafikiri kuna fumbo hapa lakini sivyo wala sivyo kabisa unavyofiiria.. ni lugha tu ya mtaani mama yangu tunapozungumzia issue kama hizi..Msome, Moelex23 utaelewa!
 
Back
Top Bottom