Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Sasa hivi Zitto kazama kisiasa na kimaadili vile vile. Zitto hawezi kuandikwa vizuri kwenye RAI ya sasa na bado ukaamini kuwa ni Zitto yule yule. Hivi rai ilinunuliwa na nani vile? Sasa nilipoona tu positive news za Zitto ndani ya RAI nikajua kumekucha. Inawezekana CHADEMA bado wanaangalia upepo. Lakini naibu katibu mkuu wa CHADEMA akiandikwa vizuri kwenye RAI hatuhitaji kuuliza maswali mengi. RAI si Tanzania Daima na kwa siku za nyuma tulikuwa tukiona. Tusubiri kuona makala za Mbowe tena kwenye rai? Let's wait and see...... Pengine ni mawazo tu!

Kuandikwa na RAI = kazama kisiasa na kimaadili vile vile

Hii conclusion kali sana na labda ndio zinahitajika kuwaongoza watanzania wa aina yako ndugu yangu.

Nadhani umesahau kuwa RAI kumekuwa na uasi wa aina fulani lakini pia kuna uwezekano kuwa walioandika taarifa/makala hiyo wanalenga hukohuko ulikofikia na pia ni sehemu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe ya CCM. Ni kweli kuwa msimamo wa Zitto unamweka katika hali ngumu KISIASA na hata kuwapa nafasi MAFISADI wa makundi yote ndani ya CCM kumtumia kuendeleza mapambano yao lakini kamwe hatuwezi kufikia cheap conclusion just because "ametetewa" na RAI.

omarilyas
 
Mag3.

Tunashindwa kumuunga mkono Zitto si kwa sababu ya kufurahia kuanguka kwake. Ni kwa sababu ya logic rahisi. Zitto sasa hivi ana positive coverage RAI, unataka tuamini kuwa RAI iko balanced katika reporting yake? Imebadilika? May be.

Lakini logic rahisi ni hii. Zitto anaungana na TANESCO pamoja na Wizara ya madini na Nishati kuunga mkono ununuzi wa mitambo ya Dowans, na kwa maneno yake mwenyewe issue siyo tunanunua wapi. Issue ni kuwa tupate solution. Nakubaliana na huu msimamo ikiwa tungekuwa tunanunua bidhaa rahisi. Hiki tunachonunua ni MITAMBO!!! Reputation ya muuzaji kwenye bidhaa kama hizi ni muhimu kuliko kitu kingine chochote. Kununua mitambo ni kufungua mahusiano ya muda mrefu, kwani mitambo ina vitu vingi ambavyo hata ukimleta mtaalam gani hawezi kuona vyote na kujiridhisha kuwa kinachosemwa na muuzaji ni sahihi. Ndo maaana tunahitaji kujua reputation ya muuzaji, ili ikitokea tatizo huko mbeleni turudi kwake. Na kwa issue kama ya mitambo tatizo lazima litatokea dogo au kubwa!!!!

Sasa ikiwa unanunua kutoka kwa mtu ambaye humjui vizuri ni kama kununua CD kwa machinga barabarani. Unabeba ukifika nyumbani, ukiweka kwenye DVD player yako ile CD ikagoma basi unatulia na kujiridhisha kuwa "after all nimenunua shilling elfu tatu tu". Je unataka tufike hapo? Mitambo ile hatuinunui kwa elfu tatu wala milioni tatu.

Zitto anayajua yote hayo. Atueleze kwa nini sasa hivi yuko tayari kununua relationship (kununua mitambo ni kununua relationship) ya muda mrefu, bila kuwa na uhakika wa unayenunua hiyo relationship kutoka kwake? Au Zitto anajua zaidi kuhusu huyu Dowans ni nani na ana uhakika naye. Mbona hatuambii wengine wote ili tukaondoa wasiwasi???

Tunategemea consistency kutoka kwa mtu tunayeamini kuwa ni kiongozi mzuri. Tungetarajia kuwa Zitto, Kabla ya kutoa support yake angeuliza maswali ambayo wote tungeyaona na kujua. Viongozi wazuri hawako predictable, ila wako consistent. Kama ni republican atakuwa conservative always. Suala la kutokuwa predictable lisichanganywe na consistency. Nyerere was somehow not predictable, lakini he was consitent mpaka anakufa. Kwa suala kama hili wala usingejiuliza nyerere angekuwa upande gani!!!

Zitto????? Let's wait and see. Lakini so far utetezi alioutoa ni shameful. Ndo maana KGM and other well wishers wa Zitto wanakuwa concerned. What has gone wrong?

Ni kweli kuna a lot of well wishers katika mjadala huu lakini KGM na moelex23 sio miongini mwao. Wao kwao hii ni nafasi ya "kummaliza Zitto" wanasahau kuwa tofauti na vijiwe vingine Jamboforum kuna watu makini wasiokubali kubabaishwa na cheap spinning kama zao. Mchango kama wako ndio tunaweza kusema kuwa una nia njema na Zitto pamoja na Tanzania yetu kwa ujumla. Keep it up

omarilyas
 
Ukweli tangu Dr. Idrisa aingie tanesco kunamabadiliko fulani mita za luku zimekuwa za kumwaga, kuunganishwa sasa ni chap chap, longolongo za wasoma mita hakuna tena. Hawa wanaonyonya mafuta ya transforma tumeshajiundia sungusungu wenyewe, mtaani kwetu tumeajiri korokoroni pamoja na kulinda mtaa wanalinda na transforma. Ila hili la kukiuka maamuzi ya bodi linataka kufanana na kesi ya liyumba vile! nadhani takukuru wanaliona hili, watamchukua maelezo sio muda mrefu.

Nadhani Dr. anatakiwa aajiri Strategic planning manager pia.

Nisaidie ndugu yangu mita ya Luku. Na huko kuunganishiwa chap ni muda gani, maana wengine twasubiri na vibanda vyetu vya madongo kuinama.
 
Wabunge wa ulaya wananguvu sana huyo rais angekua ulaya angekua ameshafanya press conf. Kama kumi kuhusiana na dowans
 
Ni kweli kuna a lot of well wishers katika mjadala huu lakini KGM na moelex23 sio miongini mwao. Wao kwao hii ni nafasi ya "kummaliza Zitto" wanasahau kuwa tofauti na vijiwe vingine Jamboforum kuna watu makini wasiokubali kubabaishwa na cheap spinning kama zao. Mchango kama wako ndio tunaweza kusema kuwa una nia njema na Zitto pamoja na Tanzania yetu kwa ujumla. Keep it up

omarilyas

Wewe acha maneno mingi bwana, unataka kuniambia ZITO hajui anachokifanya?. Hivi unajua humu janvini Zito alifikia hatua ya kutukana watu? Hakujua alichokuwa anafanya?. Tulishaamua kupambana na MAFISADI basi hatua haja kumwangalia mtu usoni.

Zito ni Fisadi kama MAFISADI wengine hivyo hatuna urafiki naye maadamu tumeshaamua kupambana na mafisadi. Ukweli nikuwa tunasikitika lakini hatuna Jinsi. Mimi nimeshaandika huko nyuma kwamba Wapenda mageuzi tumepata pigo sana. Mimi sina umaarufu wowote lakini napenda mageuzi sana. Tuliyemweka mbele tukamwamini ametusaliti sasa unataka tucheke naye.

Fisadi ni Fisadi 2.
 
Kubali au usikubali mitambo ya Dowans ikinunuliwa haitafanya kazi zaidi ya miaka mitatu bila kwenda chini na kuhitaji major repair itakayogharimu si chini ya Dola milion 10. Halafu baada tu ya kununuliwa Dowans itayeyuka majini na mtengenezaji wa mitambo ndo atasema ukweli.

Let's go out tutangaze tenda mapema (ilikuwa possible since july last year tulipovunja mkataba na Dowans). Shetani na mungu wote wanajua kuwa tulipovunja mkataba na Dowans tulikuwa na mahitaji ya umeme. Ingetangazwa tenda sasa hivi tungekuwa tuko kwenye final touches za kupata mitambo mipya. Wakati mkataba wa Dowans unavunjwa watu ndani na nje ya TANESCO walikuwa buzy kuandaa mazingira yatakayosababisha kununuliwa mitambo ya Dowans iwe kama kusukuma mlevi.

Muda huo ndo sasa na wamepata new and unexpected supporters. Sasa ni wakati wa kula. Dr. I may go ahead and buy the Machines. He knows what he will be buying. But he know also that in Tanzania it is easy to get away especially when you are well connected. He has important people who trust him. What he fears is to blow-up their trust. This will happens if he buys Dowans. I bet he doesn't.

And Zitto, the staunch supporter of Dowans? Well let's wait and see him join Kaburu, his homeboy. Keep your eyes open, it will happen men/women!!!!!

Mitambo haijatengenezwa na DOWANS ila DOWANS walinunua kutoka katika kampuni inayotengeneza mitambo hiyo. Katika hili naamini ni muhimu kufuatilia zaidi na kujua jinsi gani Tanzania itaathirika ama kufaidika itakapotokea matatizo yanayohitaji uhusika wa waliotengeneza mitambo hiyo na kujua mikataba kati ya DOWANS na hiyo kampuni inasemaje na kampuni yenyewe ina hali gani kwa sasa tukichukulia hali ya kiuchimu duniani.

Vilevile ni vizuri kujua kama KAMATI MASHIRIKA YA UMMA ambayo ndio iliyoamua kuishauri serikali kuangalia uwezekano wa TANESCO kununua mitambo hiyo ilishauri inunuliwe mitambo yote ikihusisha na ile iliyoletwa na RICHMOND ama ile tu iliyoletwa na DOWANS.

Vilevile ni muhimu kujua endapo Tanesco watanunua mitambo hiyo nini itakuwa mustkalbali wa madai ya Tanesco dhidi ya DOWANS na kama fedha ambazo Tanesco inadai DOWANS zitakuwa sehemu ya manunuzi hayo kama yekiwezekana.

Mimi kama mtanzania wa kawaida msimamo wangu ni Serikali kutaifisha mitambo hiyo lakini pia nahofia zoezi hilo lisije likatufikisha katika halia kama ya VALAMBHIA na manunuzi ya silaha ambayo mwisho wake ni hasara kubwa kwa taifa na ulaji usiokwisha wa wanasheria ukiacha athari kubwa kwa nadharia nzima ya utawala wa sheria ambayo serikali inapswa kuwa mfano wa kuigwa hata katika kulinda maslahi ya Taifa.

Again kaka ingawa una tone kali katika huu mjadala lakini wazi kuwa upo genuine katika nia na mawazo yako.

omarilyas
 
Wakuu,

Hivi kelele zote hizi bado hakuna anayesema mtambo mpya wa kununua huu hapa?

Angalau Zitto ameonyesha hafuati upepo na yuko tayari kukosa umaarufu wa kisiasa kwa kitu anachokiamini.

Wanasiasa wote wamehamia Dar kupiga kelele za mtambo, hakuna uamuzi unachukuliwa, nchi giza totoro baada ya muda tunajiuliza eti kwanini hatuendelei?

Haya makundi yanayopingana yangeliweza kukaa pamoja na kujadiliana kwa wiki na kisha kuamua cha kufanya sio kama sasa wanasiasa wamegeuka watalaamu wa umeme.

Wacha wengine tuwajibike!

Mitambo tayari ipo ni $39million for 100MW mipya pamoja na warranty ya miaka 7 from the world biggest company of manufacturing Turbine and Jet engine ni kwenda kuchukua na kuwasha, hakuna kununua second hand kwa $60million.
 
PM hakuna kitu kuhusu ZITTO, ameshaingia mkenge na mimi binafsi ile blank support niliyokuwa natoa kwa Dr. Slaa na kina Zitto naiamishia kuanzia leo kwa Dr. Mwakyembe, Mama Kilango na Seleli.

Zitto tulikuwa naye hapa for almost 4 days tukimpa mambo ya jikoni na mikorogo itakayotokea, lakini katupuuza na kututukana.

Sasa kweli ukimpa hayo mahojiano mtu ambaye hajui Tanzania, ukamuambia guess yupi ni kutoka chama cha upinzani, si atapick Dr. mwakyembe??

Dr. Mwakyembe hapa anatetea maslahi ya nchi na sisi wananchi, na Zitto anatetea maslahi ya Dowans, simple as BLACK and WHITE.

Halafu Mh. Zitto usipende kuchanganya mambo kwa kumention tu vitu unavyoambiwa eti serikali inakosa bilioni 58 watu wa migodi kwenye mafuta wanayotumia kwenye private generator zao, je kisa ni sababu hatujanunua mitambo ya Dowans au kisa ni misamaha ya kijinga serikali inayotoa na jie bunge kuridhia??? Unafikiri hata kukiwa na umeme, watu wa migodi watatupa generator zao au watatumia hiyo loophole ya tax refund kwenye mafuta ya hizo generator??? Give me a break!!!

Moelex23;
Usimpe mtu yeyote a blank check iwe Dr. Mwakyembe, Seleli, Mama Malecela, Zitto, Slaa etc.
  1. Zitto inaelekea (a) Ana-kaulevi ka madaraka aliyopewa kwenye kamati, (b) Ana-ukosefu wa uzoefu wa mambo ya uongozi na biashara (c) Ameonyesha kuwa ni mgumu kukubali hard criticism. Lakini at least he has a record behind him ya kupigania wananchi. Tusimuweke pembeni bali tuendelee kumdadisi na kumsaidia ikibidi.
  2. Lakini mtu kama Mama Malecela sio wa kuamini kabisa, she is a populist na sijaona matendo yake yakafanana na anayopigiaga kelele. Ameifanyia nini nchi hadi hivi sasa badala ya kujipandishia tu chati kwa kelele bungeni?
  3. Dr. Mwakyembe na Seleli wana maneno mazuri tunayotaka sikia, lakini hawajawahi kusimamia kidedea issues ambazo wanazijua kwa undani kuliko watu wengine na zina utata hadi leo (Richmond-Dowans). Baada ya kuandika ripoti, Dr. Mwakyembe akiwa ni mwanasheria, je wamefanya nini zaidi kuhakikisha kuwa Richmond-Dowans inakuwa dealt with once and for all?
Dont give anyone a blank check, they all need to qualify for one.
 
Wewe acha maneno mingi bwana, unataka kuniambia ZITO hajui anachokifanya?. Hivi unajua humu janvini Zito alifikia hatua ya kutukana watu? Hakujua alichokuwa anafanya?. Tulishaamua kupambana na MAFISADI basi hatua haja kumwangalia mtu usoni.

Zito ni Fisadi kama MAFISADI wengine hivyo hatuna urafiki naye maadamu tumeshaamua kupambana na mafisadi. Ukweli nikuwa tunasikitika lakini hatuna Jinsi. Mimi nimeshaandika huko nyuma kwamba Wapenda mageuzi tumepata pigo sana. Mimi sina umaarufu wowote lakini napenda mageuzi sana. Tuliyemweka mbele tukamwamini ametusaliti sasa unataka tucheke naye.

Fisadi ni Fisadi 2.

Kwa hiyo unadhani kuwa ni wewe tu mwenye haki ya kutukana watu. Sasa kwa kuwa Zitto ni mheshimiwa basi asikwambie kama ni mpuuzi hata kama madai yako ni ya kipuuzi?

Tatizo umezoea viongozi wanaowadanganya na kuwapamba kila wakati kwa minajili ya kura hata kama unakosea. Msimamo wa Zitto na ujasiri wake wa kutokunyenyekea wakati ukimtuhumu kipuuzi ndio uongozi tunaautaka ili tuendelee na sio siasa za matumbo ambazo wewe umezizoea....

omarilyas
 
Moelex23;
Usimpe mtu yeyote a blank check iwe Dr. Mwakyembe, Seleli, Mama Malecela, Zitto, Slaa etc.
  1. Zitto inaelekea (a) Ana-kaulevi ka madaraka aliyopewa kwenye kamati, (b) Ana-ukosefu wa uzoefu wa mambo ya uongozi na biashara (c) Ameonyesha kuwa ni mgumu kukubali hard criticism. Lakini at least he has a record behind him ya kupigania wananchi. Tusimuweke pembeni bali tuendelee kumdadisi na kumsaidia ikibidi.
  2. Lakini mtu kama Mama Malecela sio wa kuamini kabisa, she is a populist na sijaona matendo yake yakafanana na anayopigiaga kelele. Ameifanyia nini nchi hadi hivi sasa badala ya kujipandishia tu chati kwa kelele bungeni?
  3. Dr. Mwakyembe na Seleli wana maneno mazuri tunayotaka sikia, lakini hawajawahi kusimamia kidedea issues ambazo wanazijua kwa undani kuliko watu wengine na zina utata hadi leo (Richmond-Dowans). Baada ya kuandika ripoti, Dr. Mwakyembe akiwa ni mwanasheria, je wamefanya nini zaidi kuhakikisha kuwa Richmond-Dowans inakuwa dealt with once and for all?
Dont give anyone a blank check, they all need to qualify for one.

Kaka Dr Mwakyembe hakuandika ile ripoti kama mwanasheria bali MAMLUKI WA KISIASA. Na hapa ndio tatizo langu na MWAKYEMBE hata kama alisaidia kuangusha KINARA WA UFISADI WA ENZI MPYA.....

Ripoti ilikuwa na mikogo ya kisiasa mno kiasi ya kwamba ikashindwa hata kujumuisha/kukusanya taarifa kuhimu ambazo kama zingekuwepo zingelisaidia sana kumaliza huu utata wa RICHMOND?DOWANS.

Kingine ni lazima tutambue kuwa kuna ushindani mkubwa kati ya kamati ya mahesabu ya mashirika ya umma(POC) na kamati zingine kamati ya nishati na madini. Hizi kamati zingine zimekuwa zikijaribu kuinyang'anya kamati ya mahesabu ya mashirika ya umma baadhi ya majukumu yake ama kwa nia njema lakini pia kutaka kujipatia ulaji. No wonder Mwakyembe alispin suala la posho wakati akijua wazi msimamo wa Zitto kupinga suala la posho kutoka katika asasi za umma katika suala hilo tangia alipopewa madaraka ya uenyekiti wa hiyo. Kitu ambcho kilipeleka hata kuanza kwa uhasama na baadhi wanakamati wake ambao wanaamini posho hizo ni haki yao.

omarilyas
 
Last edited:
Kaka, huku kwetu ukituma maombi ya Luku unapewa 21 days baada ya kukamilisha malipo watakuwa wameshafunga ila sanasana wanachukua 14 days tayari stima imeshapatikana, na mgao haupo tena, labda kama kunamatengenezo kama kuondoa matawi ya miti kwenye nyaya.

Juzi niliumwa sikio na mtu wa tanesco kuwa mita zimejaa tele stoo. Lugha chafu pale reception sasa hakuna nasikia wanafundishwa customer care.
 
Mitambo haijatengenezwa na DOWANS ila DOWANS walinunua kutoka katika kampuni inayotengeneza mitambo hiyo. Katika hili naamini ni muhimu kufuatilia zaidi na kujua jinsi gani Tanzania itaathirika ama kufaidika itakapotokea matatizo yanayohitaji uhusika wa waliotengeneza mitambo hiyo na kujua mikataba kati ya DOWANS na hiyo kampuni inasemaje na kampuni yenyewe ina hali gani kwa sasa tukichukulia hali ya kiuchimu duniani.

Again kaka ingawa una tone kali katika huu mjadala lakini wazi kuwa upo genuine katika nia na mawazo yako.

omarilyas

Kwani Hawa DOWANS haswa ni nani? Na wali-urithi makataba wa Serikali na Richmond katika mazingira gani. Je kulikuwa na Tenda ya wazi?

Huyu Idris Rashid, alikuwa wapi wakati Richmond inapewa mkataba. Hivi wakuu ni lini aliingia Tanesco?
 
Kwa karibu masaa sita ka nzi kalikuwa kametulia kwenye ukumbi makao makuu ya Tanesco ambapo Mkurugenzi wa Shirika hilo Dr. Idris Rashid alikuwa aje kuzungumza na waandishi hususan suala kununua majenereta ya kufulia umeme ambayo yanamilikiwa na kampuni yenye utata wa umiliki wake na yenye kuhusishwa na kampuni ya kifisadi ya Richmond, Dowans.

Hata hivyo, muda si mrefu uliopita mtumishi wa Tanesco aliingia ukumbini na kuwaambia waandishi waliokuwa wanasubiri kwa muda mrefu kuwa Bw. Idris hatozungumzia nao na kuwaomba radhi.

Hata hivyo, vyanzo vyetu vyenye uwezo wa kupenya kuta na madari vinadokeza kuwa suala la Dowans limefikia mahali pagumu ambapo sasa Tanesco wako tayari kuachana na wazo hili ili kutafuta vyanzo vingine vya umeme wa dharura na ya kuwa wametilia maanani "kelele" za wadau mbalimbali. Hili linakuja baada ya sauti za Spika wa Bunge la Muungano Mhe. Samuel Sitta na Mbunge wa Kyela Mhe. Harrison Mwakyembe kupaza sauti zao kupinga mpango huo. Ujumbe ambao umepokelewa toka kwa watunga sheria hao ni kuwa yeyote atakayenunua majenereta ya Dowans ajiandae kuwajibika Dodoma kama walivyowajibishwa wengine!

Tishio hilo ambalo limepokelewa kwa hisia ya kunyong'onyea limetuma ujumbe ulio wazi kuwa endapo serikali itatekeleza au kutoa baraka kwa Tanesco kufanya kitu ambacho wanajua hawapaswi kufanya basi patakuwa hapakaliki. Hadi hivi sasa kundi kubwa la wabunge waliosimama upande wa ripoti ya Kamati Teule kuhusu Richmond, limeshajipanga tayari kuanzisha "kasheshe" jingine ambalo linaweza kabisa kuitikisa serikali.

Hata hivyo, Dr. Idris inaonekana bado amekuwa na 'kichwa ngumu' hasa baada ya serikali na kamati za Bunge zote kuiachia uamuzi wa mwisho kuhusu suala la mitambo. Hata hivyo, kuna imani kuwa alichofanyiwa Dr. Idris ni kupewa kisu ashike, tatizo ni kuwa amepewa upande wa makali huku mpingi ukiwa umeshikwa na wengine ambao wako tayari kuuvuta.

Kutokana na hili, kuna kila dalili Dr. Idris anaweza kutangaza kujiuzulu wadhifa huo kitu ambacho alijaribu kukifanya muda si mrefu uliopita kuhusiana na suala la kampuni ya saruji ya huko Tanga. "Hayuko tayari kujitundika mwenyewe kitanzini kwa kamba yake mwenyewe!" amedokeza mmoja wa watu wanaojua suala hilo.

Sasa hivi kinachosubiriwa ni muda tu kuona Dr. Idris atafanya nini huku akijua kuwa tayari anahusishwa na kashfa ya rada suala ambalo nalo hajalitolea maelezo yoyote. Hadi hivi sasa uchunguzi wetu unaonesha kuwa asilimia 90 ya uamuzi uliofikiwa hadi sasa ni kutoendelea na suala la Dowans.

Hata hivyo upande mwingine bado unadokeza kuwa endapo serikali haitanunua mitambo ya Dowans na hivyo kuwasababishia hasara "wawekezaji" hao ambao walikuwa na uhakika kuwa serikali itanunua mitambo hiyo basi Watanzania "watakiona" kwani upungufu mkubwa wa umeme ambao tulidokeza unakuja mwezi wa nne, utaifanya serikali iipigie magoti Dowans na hata kununua majenereta yale yale katika bei ya juu!!

"Watanzania hawawezi kuvumilia kukaa gizani muda mrefu hasa huku mjini, kwa hiyo usishangae hao hao wanaopinga sasa wakaja baadaye kutaka serikali inunue mitambo hiyo aidha kutoka kwa dowans au kwa mtu atakayekuw ameinunua" alisema mdokezaji huyo.

Uwezekano wa kutokea yote mawili ni mkubwa zaidi. Hata hivyo, kama dhamira ya kuwalipa Dowans kwa gharama yoyote itatekelezwa basi kuna dalili Dr. Idris na timu yake watacheza bahati nasibu na kuendelea na mradi huo wakijua kuwa huko Bungeni tayari wana kura za kutosha kuzuia mapigo ya kina "mwakyembe".

===============
Breaking News: 100% verified.

Tayari keshapata taarifa kwamba mitambo mipya ipo tayari kutoka kwa biggest manufacture of Gas turbine na bei yake ni $39million for 100MW ndo maana hakupenda kusema uongo mbele ya waandishi wa habari maana angejimaliza moja kwa moja. Mitambo hipo tayari ni kwenda kuchukua tu na kuwasha. Warranty ni 7 years with commissioning for 30 years. hiyo mitambo Serikali watakaa nayo kwa miaka 40-50. hiyo mipya toka kwa huyo manufacture . Mtambo mpya kwa hali ya kawaida ni $35-46million na siyo $90million labda kama inatengenezwa mbinguni.
 
Zito ni Fisadi kama MAFISADI wengine hivyo hatuna urafiki naye maadamu tumeshaamua kupambana na mafisadi. Ukweli nikuwa tunasikitika lakini hatuna Jinsi. Mimi nimeshaandika huko nyuma kwamba Wapenda mageuzi tumepata pigo sana. Mimi sina umaarufu wowote lakini napenda mageuzi sana. Tuliyemweka mbele tukamwamini ametusaliti sasa unataka tucheke naye.

Fisadi ni Fisadi 2.

KGM,
Una ushahidi gani wa hiyo accusation yako? I disagree with Zitto kwa jinsi alivyolishughulikia hili suala la TANESCO-DOWANS, lakini ku-conclude kuwa yeye ni fisadi kwa vile tu amesema ambacho Rostam anataka kusikia, ni kuonyesha kuwa ulikuwa una nia ya kumpa hiyo branding no matter what na ulikuwa unatafuta tu nafasi ya kufanya hivyo kwani hakuna ushahidi wowote wa ufisadi wa Zittto.
 
Omari kaka, sio "spin" sasa makampuni makubwa yanaajiri Strategic Managers/Directors, kwa ajiri ya kuandaa Long term objectives na strategic missions. Kuna pia "Strategic Business" ambayo inatakiwa iwe directed na huyu Strategic Manager.
 
Kuhusu ajira sina uhakika lakini naamini wanayo master plan tatizo inakingana na sera na maamuzi ya kisiasa hivyo huwa inabidi kuwekwa viraka kila wakati kutimiza matakwa ya wakati uliopo na kukingana na matakwa ya muda mrefu...

omarilyas
 
Kwa majibu hayo machache tu inaonyesha kuwa kwa msimamo wa Serikali, Dr. Mwakyembe na kundi lake wameanguka na Mh. Zitto na kundi lake wameibuka kidedea.

Lakini tusubiri filimbi ya mwisho..

Mkuu, sidhani hapa ni suala la kuanguka kwa Mwakyembe and his so-called "kundi lake", ni kuanguka kwa Watanzania wote mikononi mwa mafisadi! Ngeleja na Idris Rashid ni kundi moja na Rostam Aziz lenye historia kutokea VODACOM ambalo Rostam analitumia kama atakavyo, mithili ya toilet paper. Wenye nchi tutahakikisha Ngeleja anafuata mkumbo wa akina Karamagi. Akina Zitto na utumwa wao wa fedha wataishia kudhalilika tu.
 
Moelex23;
Usimpe mtu yeyote a blank check iwe Dr. Mwakyembe, Seleli, Mama Malecela, Zitto, Slaa etc.
  1. Zitto inaelekea (a) Ana-kaulevi ka madaraka aliyopewa kwenye kamati, (b) Ana-ukosefu wa uzoefu wa mambo ya uongozi na biashara (c) Ameonyesha kuwa ni mgumu kukubali hard criticism. Lakini at least he has a record behind him ya kupigania wananchi. Tusimuweke pembeni bali tuendelee kumdadisi na kumsaidia ikibidi.
  2. Lakini mtu kama Mama Malecela sio wa kuamini kabisa, she is a populist na sijaona matendo yake yakafanana na anayopigiaga kelele. Ameifanyia nini nchi hadi hivi sasa badala ya kujipandishia tu chati kwa kelele bungeni?
  3. Dr. Mwakyembe na Seleli wana maneno mazuri tunayotaka sikia, lakini hawajawahi kusimamia kidedea issues ambazo wanazijua kwa undani kuliko watu wengine na zina utata hadi leo (Richmond-Dowans). Baada ya kuandika ripoti, Dr. Mwakyembe akiwa ni mwanasheria, je wamefanya nini zaidi kuhakikisha kuwa Richmond-Dowans inakuwa dealt with once and for all?
Dont give anyone a blank check, they all need to qualify for one.
==========

Well said. Binafsi niko tayari kumpa another chance and benefit of doubt ikiwa atarudi jamvini na kushughulikia hii hard ball.
Ni kweli kauzoefu kanapungua kwa kijana huyu. Lakini tufanyeje, in the absence of ... hata mwenye jicho moja tunamshangilia.
 
Hakuna anayezuia kununua mitambo bali ni sheria.Pia wabunge wanaingizwa "choo cha kike" kwani Tanesco yenyewe inaogopa kununua mitambo hiyo ndio maana wanataka kuwauzia wabunge ili lolote litakapo jitokeza lilaumiwe bunge.
 
Back
Top Bottom