Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,080
- 136,553
Unamaanisha nini hapo brother?
kipi usichokielewa hapo?
Unamaanisha nini hapo brother?
Kibaya alichokifanya MWAKYEMBE ni kipi? Huo MSIMAMO wenu ndio tusiotaka kusikia kabisa. Sasa ZITO sio swala la msimamo, ni SWALA la KITU KIDOGO TU, hakuna cha msimamo wala nini, kala/kaahidiwa hela ya ukuwadi, basi ndio anayoendelea nayo. Mwisho wake ndio huo. Alipewa ushauri toka mapema, rudisha hela ya mafisadi bado tunakutaka, yeye akaja na matusi hapa. Anyway si haba, nasikia kala fungu la kutosha. >10%
Kwa karibu masaa sita ka nzi kalikuwa kametulia kwenye ukumbi makao makuu ya Tanesco ambapo Mkurugenzi wa Shirika hilo Dr. Idris Rashid alikuwa aje kuzungumza na waandishi hususan suala kununua majenereta ya kufulia umeme ambayo yanamilikiwa na kampuni yenye utata wa umiliki wake na yenye kuhusishwa na kampuni ya kifisadi ya Richmond, Dowans.
Hata hivyo, muda si mrefu uliopita mtumishi wa Tanesco aliingia ukumbini na kuwaambia waandishi waliokuwa wanasubiri kwa muda mrefu kuwa Bw. Idris hatozungumzia nao na kuwaomba radhi.
Hata hivyo, vyanzo vyetu vyenye uwezo wa kupenya kuta na madari vinadokeza kuwa suala la Dowans limefikia mahali pagumu ambapo sasa Tanesco wako tayari kuachana na wazo hili ili kutafuta vyanzo vingine vya umeme wa dharura na ya kuwa wametilia maanani "kelele" za wadau mbalimbali. Hili linakuja baada ya sauti za Spika wa Bunge la Muungano Mhe. Samuel Sitta na Mbunge wa Kyela Mhe. Harrison Mwakyembe kupaza sauti zao kupinga mpango huo. Ujumbe ambao umepokelewa toka kwa watunga sheria hao ni kuwa yeyote atakayenunua majenereta ya Dowans ajiandae kuwajibika Dodoma kama walivyowajibishwa wengine!
Tishio hilo ambalo limepokelewa kwa hisia ya kunyong'onyea limetuma ujumbe ulio wazi kuwa endapo serikali itatekeleza au kutoa baraka kwa Tanesco kufanya kitu ambacho wanajua hawapaswi kufanya basi patakuwa hapakaliki. Hadi hivi sasa kundi kubwa la wabunge waliosimama upande wa ripoti ya Kamati Teule kuhusu Richmond, limeshajipanga tayari kuanzisha "kasheshe" jingine ambalo linaweza kabisa kuitikisa serikali.
Hata hivyo, Dr. Idris inaonekana bado amekuwa na 'kichwa ngumu' hasa baada ya serikali na kamati za Bunge zote kuiachia uamuzi wa mwisho kuhusu suala la mitambo. Hata hivyo, kuna imani kuwa alichofanyiwa Dr. Idris ni kupewa kisu ashike, tatizo ni kuwa amepewa upande wa makali huku mpingi ukiwa umeshikwa na wengine ambao wako tayari kuuvuta.
Kutokana na hili, kuna kila dalili Dr. Idris anaweza kutangaza kujiuzulu wadhifa huo kitu ambacho alijaribu kukifanya muda si mrefu uliopita kuhusiana na suala la kampuni ya saruji ya huko Tanga. "Hayuko tayari kujitundika mwenyewe kitanzini kwa kamba yake mwenyewe!" amedokeza mmoja wa watu wanaojua suala hilo.
Sasa hivi kinachosubiriwa ni muda tu kuona Dr. Idris atafanya nini huku akijua kuwa tayari anahusishwa na kashfa ya rada suala ambalo nalo hajalitolea maelezo yoyote. Hadi hivi sasa uchunguzi wetu unaonesha kuwa asilimia 90 ya uamuzi uliofikiwa hadi sasa ni kutoendelea na suala la Dowans.
Hata hivyo upande mwingine bado unadokeza kuwa endapo serikali haitanunua mitambo ya Dowans na hivyo kuwasababishia hasara "wawekezaji" hao ambao walikuwa na uhakika kuwa serikali itanunua mitambo hiyo basi Watanzania "watakiona" kwani upungufu mkubwa wa umeme ambao tulidokeza unakuja mwezi wa nne, utaifanya serikali iipigie magoti Dowans na hata kununua majenereta yale yale katika bei ya juu!!
"Watanzania hawawezi kuvumilia kukaa gizani muda mrefu hasa huku mjini, kwa hiyo usishangae hao hao wanaopinga sasa wakaja baadaye kutaka serikali inunue mitambo hiyo aidha kutoka kwa dowans au kwa mtu atakayekuw ameinunua" alisema mdokezaji huyo.
Uwezekano wa kutokea yote mawili ni mkubwa zaidi.
Tatizo ni kuwa kwa kuwa wewe unajiona ni rahisi kununulika basi kila mtu yuko kama wewe. Wenzako wengi wanadiscuss issue lakini wewe kwa kuwa kwako rushwa ni sehemu ya maisha basi kila mtu anafanya maamuzi kwa msukumo wa rushwa.
Hata hivyo sishangai sana maana hali hii ya kutokuaminiana ni zao la MFUMO FISADI ulioanza tangia 1977 kwa kuanzishwa hili zimwi linaloitwa CCM na kubarikiwa rasmi na AZIMIO LA ZANZIBAR....
omarilyas
Unataka chanzo kwa Takwimu zipi?
Maana kuna takwimu za Idrisa, za Mawaziri na Takwimu halisia , kwani zilizopo sasa zinzonyesha kuwa wanaotumia umeme ni asilimia 12 tuu ya watanzania .
Hiii 12% ni kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa mkukuta.
Napenda kujua mahitaji ya umeme nchini (tunahitaji megawatts ngapi kwa siku- matumizi yote kwa ujumla, majumbani, viwandani na maofisini).
Na kiasi gani cha umeme (megawatts) kinachozalishwa ni ngapi kwa ujumla? Na kiasi hicho kinakidhi asilimia ngapi ya mahitaji ya nchi?
Kama unazo zote sio mbaya (yaani takwimu ya Idris, Mawaziri na hata halisia).
Natanguliza shukrani.
Itanichukua muda kidogo kupekua sehesehemu hapa , ntajitahidi kuweka
Mwiba , neno Sultan inaonyesha limekukaa sana yakhe, ila njoo kaweke vizuri kuhusu gazeti lako la alasiri kufutika.
Napenda kujua mahitaji ya umeme nchini (tunahitaji megawatts ngapi kwa siku- matumizi yote kwa ujumla, majumbani, viwandani na maofisini).
Na kiasi gani cha umeme (megawatts) kinachozalishwa ni ngapi kwa ujumla? Na kiasi hicho kinakidhi asilimia ngapi ya mahitaji ya nchi?
Kama unazo zote sio mbaya (yaani takwimu ya Idris, Mawaziri na hata halisia).
Natanguliza shukrani.
si ufanye utafiti, taarifa zote hizo ziko kwenye mtandao. Mahali pa kuanzia ni Tanesco.com sidhani kama hili ni gumu hadi umuombe mtu mwingine.
si ufanye utafiti, taarifa zote hizo ziko kwenye mtandao. Mahali pa kuanzia ni Tanesco.com sidhani kama hili ni gumu hadi umuombe mtu mwingine.