Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

KGM;

Ngoja niwe devil's advocate hapa. Toka mada hii inaanza hakuna aliyekuja na bei ya mitambo mbadala mpaka inakuwa installed. Tungemnyooshea Zitto kidole kama tungesema kuwa mitambo kutoka US au Malaysia yaneye ubora uleule au zaidi ni Billion 40 na ya Dowans ni Bilion 60. Ila mitambo ya kutoka nje itachukua miaka miwili. Kimahesabu Billions 20 ni nyingi. Tuagize kutaka nje.

Huo ndo uchambuzi niliokuwa nikiisubiri hapa.

Tatizo lingine ni kuwa sehemu kubwa ya umeme wetu unatokana na Maji. Je tumefanya analysis kujua kama mvua hazitanyesha mwaka huu?.

Suala zima mi naona ni siasa tupu.

Wezi watupu wote huko Sirikalini na Tanesco!

Mbona humu ndani bei zimeshatolewa sana tu. wewe pitia pitia tu utaona.
Tena bei zimetoka kwa wenyewe sio wababishaji kama DOWNS ambayo hata inakotokea hakujulikani au mwenzetu unajua Downs walitokea wapi na walifahamianaje/walipasianaje Dili lao la kuihujumu nchi na RICHMOND

Hata hivyo sijakuelewa kama uko upande gani. Uko upande wa Sita+Mwakiembe+Shelukindo+Wananchi au Uko na Zito+RA+IDIRSA RASHID+MAFISADI bila kumsahau OMalys
 
Kwa hiyo unadhani kuwa ni wewe tu mwenye haki ya kutukana watu. Sasa kwa kuwa Zitto ni mheshimiwa basi asikwambie kama ni mpuuzi hata kama madai yako ni ya kipuuzi?

omarilyas

'Haki ya kutukana'? Hili linashtua na kuhuzunisha sana!
 
Mzee unaweza ukatupa reference, ili tuzimwage hapa zikae kwa ajili ya vizazi vijavyo, ili vione ni kwa jinsi gani tunavyokosa busara?

Mheshimiwa reference ni kampuni nilizo zitaja kama unataka kuhakiki developommunication nao watakupa details zote bei installation na usafiri na warrant. vilele vilevile wapo wapo wabongo kibao ni maenginia kwenye hizo kampuni na wapo wengi wametoa maombi ya kutoa huduma hizo kupitia kampuni zao kusaidia taifa ila kina ngeleja na rostam wanaweka mizengwe hivyo ama giza ama kulizwa tatukula vyao kwa bei yeyote.
 
Awali ya yote: HII MITAMBO MWANZONI KABISA SI TULIAMBIWA SERIKALI INAKODI TU NA SI VYINGINEVYO??

Mambo yanavyokwenda ama kweli inaonekana kuna mtu ambaye anaongoza idara / wizara kwa remote.

Of all the people we appended hope to (kwamba ni mtetezi wa maslahi ya Taifa) Zitto has let his calibre slide down.
 
Mbona humu ndani bei zimeshatolewa sana tu. wewe pitia pitia tu utaona.
Tena bei zimetoka kwa wenyewe sio wababishaji kama DOWNS ambayo hata inakotokea hakujulikani au mwenzetu unajua Downs walitokea wapi na walifahamianaje/walipasianaje Dili lao la kuihujumu nchi na RICHMOND

Hata hivyo sijakuelewa kama uko upande gani. Uko upande wa Sita+Mwakiembe+Shelukindo+Wananchi au Uko na Zito+RA+IDIRSA RASHID+MAFISADI bila kumsahau OMalys

Ndugu yangu.

Sipo upande wowote bado. Mimi ni positive thinker. Nimeona bei ila kuna utata kidogo.

Hizo ni bei za huko zilipo. ACHENI KULINGANISHA MAEMBE NA MAPAPAI.

Nipe bei ikiwa imeshafungwa hapa Tanzania.

Labda nitoe kashule jinsi gani unapata bei ya kulinganisha chungwa na chungwa.

Bei ya marekani (mtambo wa kununuliwa nje) + Freight + Insurance + Duties and VAT(if any)+Installation costs +commisioning costs =<> bei ya mitambo ya Dowans hapo Dar.

Hiyo ya bei ni Usd 39 Million ni CRAP!. Tupe analysis ya gharama zote zinazofuatia.

Hope nimeeleweka.
 
Jamani hebu niwaulizeni:
Ni wapi Zitto amekosea? Mbona tunaharakisha kumhukumu kuwa ni fisadi, ni rafiki ya Rostum, ameshapokea hongo etc.etc? Nimesoma threads zake zote hakuna mahali Zitto amesema kuwa Tanesco LAZIMA wanunue mitambo ya Dowans. Au mimi ndiye mbumbumbu?

Katika maelezo yake kuna sehemu amepinga kununua mitambo hii? Mashabiki wake walitegemea angekuwa wa mwanzo kupinga bila kuuma maneno! Kamati ya Shelukindo ilikuwa wazi juu ya msimamo wao. Kamati ya Zitto wao wanataka mjadala!
 
B + Duties and VAT(if any)+commisioning costs =

Hiyo ya bei ni Usd 39 Million ni CRAP!. Tupe analysis ya gharama zote zinazofuatia.

Hope nimeeleweka.

Nilidhani zigo la serikali linakuwa tax exempted na kwamba unalipa commission kama utatumia agent. Isn't it?
 
Wakuu kumhukumu zito eti kanunuliwa na rostam hapo tumeenda mbali sana, hoja za zito na kamati yake ziko wazi. Wa tz tunasahau kuwa siasa chafu ndio iliyotufikisha hapa tulipo na si vinginevyo, hatukuwa wakweli tangu uhuru na tunaendelea na utamaduni huu na kuwajengea watu wakweli majungu na kuwapa wasifu potofu, tunataka mitambo iliyoingizwa tz 2006-7 leo inaitwa mitumba, ninyi tanesco ndio mlioianza kuitumia sasa muendelezo wake unaitwa tayari mtumba, ufisadi n.k tuache ushabiki usio na tija.

Dr. Rashid alipoichukua tanesco alifanya deal na makampuni yanayotajwatajwa kwa commitment ya dr rashid, jamaa wakatoa mapesa $300m kama mkopo wa kuifanya tanesco ijiendeshe na kuwapa assurance wadau hao huduma.

Dr.rashid anasimamia ukweli halis na siyo siasa zetu chafu.

Watz tuwe wakweli tu jamani kuwa shelukindo na mwakyembe hawasukumwi na uzalendo bali agenda yao ndani ya ccm. Spika huyo tushamjua ni mropokaji na dikteta tunamwacha hukohuko.

Tufanye kazi kwa dhati ya mioyo yetu na siyo chuki na majungu
 
Tukio likitokea linazua maswali mengi sana Hapo chini ni maoni ya mdau mmoja kutoka Tanzania Daima.

"ZITTO KABWE ALIANZA KUSEMA KUWA MKAPA ASIVULIWE KINGA ILI ASISHITAKIWE.

ALICHOKUWA AKIKIFANYA ZITTO NI KUKUZA JINA ILI CCM WAMNUNUE KWA BEI KUBWA. SASA AMECHUKUA CHAKE KWENYE DOWANS.

NA ZITTO ALISEMA MUDA MREFU KUWA YEYE 2010 HATAGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA, JIBU MNALO NYINYI WENYEWE.
KATUMIA CHADEMA KAMA PLATFORM YA SAFARI YAKE KISIASA.

HAKUNA BINADAMU ANAYEWEZA KUSHINDANA NA NJAA ANAWEZA KUJICHELEWESHA KULA TU SIO KUISHI NA NJAA.

MAMA YAKE ZITTO KABWE NI MSANII WA MJINI MNATEGEMEA MTOTO WAKE ATAKUWAJE? MTOTO WA NYOKA NI NYOKA.

SAFI SANA ZITTO UMETOKA FAMILIA DUNI NA BINGO IMEKUFUATA MIKONONI USILAZE DAMU.WATASEMA WATANYAMAZA SIO WEWE WA KWANZA.MBOWE MWENYEWE ANAKULA RUZUKU WEWE UKALE WAPI? UMEWABWAGA WACHAGGA.
CHADEMA MWAKANI MUWEKENI MWANAKIJIJI NA KITILA MKUMBO NAO WAKIPATA UBUNGE WANA WAMWAGA."

Hata mimi ikanikumbusha ujasiri wa KIjana wetu kumutetea FISADI MKAPA, hivi kweli mnasema huyu kijana bado yuko kundi letu. Amekuwa na maneno yenye utata mno. BP inapanda,BP inashuka.

Na mimi naongezea, Isije ikawa yeye ndiye aliyempotosha Shitambala Kule Mbeya. Tusizidi kuangalia yaliyotangulia isije ikawa kijana anatafuna upinzani Taratibuuuuuuuu Tujadili.
 
Wakuu kumhukumu zito eti kanunuliwa na rostam hapo tumeenda mbali sana, hoja za zito na kamati yake ziko wazi. Wa tz tunasahau kuwa siasa chafu ndio iliyotufikisha hapa tulipo na si vinginevyo, hatukuwa wakweli tangu uhuru na tunaendelea na utamaduni huu na kuwajengea watu wakweli majungu na kuwapa wasifu potofu, tunataka mitambo iliyoingizwa tz 2006-7 leo inaitwa mitumba, ninyi tanesco ndio mlioianza kuitumia sasa muendelezo wake unaitwa tayari mtumba, ufisadi n.k tuache ushabiki usio na tija.

Dr. Rashid alipoichukua tanesco alifanya deal na makampuni yanayotajwatajwa kwa commitment ya dr rashid, jamaa wakatoa mapesa $300m kama mkopo wa kuifanya tanesco ijiendeshe na kuwapa assurance wadau hao huduma.

Dr.rashid anasimamia ukweli halis na siyo siasa zetu chafu.

Watz tuwe wakweli tu jamani kuwa shelukindo na mwakyembe hawasukumwi na uzalendo bali agenda yao ndani ya ccm. Spika huyo tushamjua ni mropokaji na dikteta tunamwacha hukohuko.

Tufanye kazi kwa dhati ya mioyo yetu na siyo chuki na majungu
FDR mitambo ilikuja haikuwa mipyaa, ni mmoja tuu wa 35mw ndio ulikuwa mpyaa, watu wanachouliza ni kwamba kwa nini isinunuliwe mipyaa kabisa na yenye warranty kuliko hiyo mitumba, na ukiangalia bei ya hiyo mitumba ya dowans inauzwa bei kubwa zaidi ya mpyaa, ndio maana hata mimi najiuliza kwani Mhe Zitto kaona yaani solution ni kununua mitambo ya Dowans tuu, na wakati huwa anakuja kusoma hapa na kuna mahali wameweka hata bei ya mitambo mipya na yenye warranty. Kwani anashindwa kuuliza na wakaweka hii tenda kwenye uwazi na watu wagombanie tenda na waone nani atatoa huduma nzuri ya uhakika kwa bei nzuri? Mhe Zitto anang'ang'ania hii ya Dowans tuu kuna nini? kalipwa? yaani theres no alternative in his mind? kwa sababu kuna mahali kaandika kwamba hawezi aku-back down kwenye hili! ya kweli hayaa!
 
Nilidhani zigo la serikali linakuwa tax exempted na kwamba unalipa commission kama utatumia agent. Isn't it?

Commision sio sawa na commisioning costs. ni kuwa baada ya Installations kuna kujaribu mtambo na kuhakikisha unafanya kazi vizuri, Pale wataalamu wanaofanya hiyo kazi wanatoka kampuni iliyoifunga na wanalipwa na kuna vitu vinatumika kutest mitambo.

Uwiano maalum,
Hili suala ni pana. Humu JF ni kama tunaropoka. So far hakuna analysis yoyote ya maana iliyofanyika humu!.

Ndo maana nikasema sipo upande wowote. Mimi ni positive thinker!

Regards

FP
 
Wakuu kumhukumu zito eti kanunuliwa na rostam hapo tumeenda mbali sana, hoja za zito na kamati yake ziko wazi. Wa tz tunasahau kuwa siasa chafu ndio iliyotufikisha hapa tulipo na si vinginevyo, hatukuwa wakweli tangu uhuru na tunaendelea na utamaduni huu na kuwajengea watu wakweli majungu na kuwapa wasifu potofu, tunataka mitambo iliyoingizwa tz 2006-7 leo inaitwa mitumba, ninyi tanesco ndio mlioianza kuitumia sasa muendelezo wake unaitwa tayari mtumba, ufisadi n.k tuache ushabiki usio na tija.

Dr. Rashid alipoichukua tanesco alifanya deal na makampuni yanayotajwatajwa kwa commitment ya dr rashid, jamaa wakatoa mapesa $300m kama mkopo wa kuifanya tanesco ijiendeshe na kuwapa assurance wadau hao huduma.

Dr.rashid anasimamia ukweli halis na siyo siasa zetu chafu.

Watz tuwe wakweli tu jamani kuwa shelukindo na mwakyembe hawasukumwi na uzalendo bali agenda yao ndani ya ccm. Spika huyo tushamjua ni mropokaji na dikteta tunamwacha hukohuko.

Tufanye kazi kwa dhati ya mioyo yetu na siyo chuki na majungu

Mzee hizi unazotuletea ni non-issues.

Sisi tungependelea ututhibitishie, wewe au huyo Zitto unayemtetea, kwa maelezo ya kitaalamu, kuwa anachokikazania kinunuliwe ni bora na ni cost-effective. Na hakuna best deal beyond that.

Thats what we are asking.
 
Commision sio sawa na commisioning costs. ni kuwa baada ya Installations kuna kujaribu mtambo na kuhakikisha unafanya kazi vizuri, Pale wataalamu wanaofanya hiyo kazi wanatoka kampuni iliyoifunga na wanalipwa na kuna vitu vinatumika kutest mitambo.

Uwiano maalum,
Hili suala ni pana. Humu JF ni kama tunaropoka. So far hakuna analysis yoyote ya maana iliyofanyika humu!.

Ndo maana nikasema sipo upande wowote. Mimi ni positive thinker!

Regards

FP

Vipi mzigo wa serikali nao hulipwa tax?

Halafu kama huna upande na unasema hili suala ni pana, na kwamba humu JF tunaropoka, upositive thinker wako una walakini.
 
Mkuu FDR Zito hakuna mtu anayemhukumu ila anatakiwa kutoa maelezo nini kamati yake imekisukuma kutaka tununue mitamba yenye tag price ya 170billion shilingi wakati mitambo hiyohiyo tunaweza kupata kwa chini ya 50billion shillings.
Atuambia je kamati yake imehakiki kwamba jeneretor zile zilikuwa mpya zilipo litwa tanzania. na je ile sababu ya jenerator haziwezi kuwaka zimekwisha lini na kama jenerator zote zilikuwa nzima mbona zilishindwa kufanyakazi wakati tunahitaji nini haswa kilikuwa sababu ya hayo yote??

Je tuelezwe wazi matatatizo ya richmond yalikuwa yapi na haya ya downs ni yapi.

Atoe kamati yake kwanini ione jenerator hizi zinamanufaa kwa watanzania wakati tutanunua kwa bei mbaya sana.
Na kama ni kweli dowans ina kesi na serikali ni kitu gani kinaifanya kamati ya zito kutaka kununua mitambo ambayo tunakesi na mwenye mitambo.
najua kamati ina info nying kuliko mimi ila tunataka tukijue.

Kitu pekee ambacho ninauhakika nacho ni bei ya hiyo mitamba sio bei halisi kutoka inapouzwa ikiwa mipya kwa 100 megawatt. Huwezi nunua kwa 170 billioni badala ya chini ya 50 billion sh.
Je kamati ya zito iliwahi kutana na rostam ama mmiliki yeyote wa dowans???

Zito nampenda sana na ninamuunga mkono kwa mengi ila asipofafanua hili kwa kweli itakuwa ngumu.
 
Mie naungana na kauli ya Dr. Mwakyembe kuwa hivi huyu Zitto ni yule tunayemfahamu au ni mwingine? Iweje leo ashauri Tanesco inunue mitambo ya Dowans haraka wakati akijua kwamba Dowans wametushtaki ufaransa na serikali inawadai pesa? Kwa hili Zitto umeniangusha saaana! Na lazima jamii ielewe kuwa kuna 'foul' imefanyika, kwani kamati husika ilishatoa mapendekezo yake kwa Tanesco. Nakuomba sana ujisafishe, kwani jamii imekosa imani na wewe.

Hivi jamani kama Tanesco wanasema wana pesa $59m kwa nini wasiagize mitambo mipya? Kwa kweli nchi hii usanii umezidi. Tuache mijadala isiyo na faida na nawaomba watanzania wenzangu tufanye kazi kwa bidii na tuwe na moyo wa kizalendo. Hizi 10% zitatumaliza kabisa na hapana shaka enzi za 'Mwalimu' haya mambo yasingetokea na wahusika wangewajibishwa kwa maslahi ya taifa bila kuangalia sura na ukaribu wa mtu.
 
Mchakato wa Richmond mpaka upatikanaji wa Mitambo hiyo ulikuwa na matatizo kwa Mujibu wa Ripoti ya Mwakyembe, mpaka sasa Mkurugenzi wa Richmond Naimu Gile anakabiliwa na kesi Mahakama ya Kisutu, ikiwa wale walanguzi wa mafuta ya Transit wakikamatwa na TRA, hutaifishwa, kwa nini hii mitambo isitaifishwe? au kuna ubaguzi kwenye mapambano dhidi ya wahujumu uchumi?
 
Nakubaliana na mawazo yenu pamoja na spika au kuna mkono wa serikali kupunguza wapinzani nguvu kwa kuwasababishia maamuzi finyu,basi kama anakana basi afanye kama alivyo anzisha hoja hii ya utetezi.
 
Wakuu,

Hivi kelele zote hizi bado hakuna anayesema mtambo mpya wa kununua huu hapa?

Angalau Zitto ameonyesha hafuati upepo na yuko tayari kukosa umaarufu wa kisiasa kwa kitu anachokiamini.

Wanasiasa wote wamehamia Dar kupiga kelele za mtambo, hakuna uamuzi unachukuliwa, nchi giza totoro baada ya muda tunajiuliza eti kwanini hatuendelei?

Haya makundi yanayopingana yangeliweza kukaa pamoja na kujadiliana kwa wiki na kisha kuamua cha kufanya sio kama sasa wanasiasa wamegeuka watalaamu wa umeme.

Wacha wengine tuwajibike!

Mkuu Mtanzania, nadhani hujaelewa.

Hakuna kati ya wote wanaozungumzia mitambo ya DOWANS hadi sasa (zaidi ya TANESCO na Serikali) mwenye mamlaka ya kutafuta mitambo ya kuzalisha umeme, si wanansiasa wala wana JF.

Wanasiasa wanatakiwa kuonyesha political will ya kununua au kutonunua mitambo, bila kuingilia mchakato (process) ya manunuzi ya mitambo hiyo.

Mh. Zitto hana uwezo pia wa kuonyesha njia ya nini kifanyike. Sababu ni nyingi, ila kubwa ni kwa kuwa sio wajibu wake. Analaumiwa kwa kushauri wadau kuridhia manunuzi ya mitambo ya DOWANS tu. Wengi hapa na nje ya JF hawaamini kuwa hiyo ndio njia nzuri ya kufuata (sababu zimetolewa nyingi).

Makundi yanayopingana hayana haja ya kukaa mahali popote na kuzungumzia suala hili (Zaidi ya Bungeni). Hawana haja kwasababu sio wajibu wao kuamua kununua au kutonunua mitambo hiyo. Kazi ya Kamati hizi ni kuishauri serikali kulingana na sheria za nchi na taratibu za Bunge. Serikali ina wajibu wa kufuata ushauri huo au kuukataa. Serikali ikikataa ushauri wa Kamati hizi, watakutana Bungeni na kujadiliana kuona nini kilichofanyika na kwa sababu gani na hatua gani zichukuliwe. Ama sio Mkuu?
 
Wakurugenzi wakuu wa MASHIRIKA na TAASISI za UMMA wanajua sana kuwa-handle wanasiasa wetu kwa NJAA na TAMAA zao zisizo na kikomo. Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma inaongoza katika hili. Bahati mbaya kabisa "shujaa" wetu Zitto naye ameangukia kwenye mitego ya Wakurugenzi hawa wala sio pesa ya Rostam. Alianza na yule wa DAWASA na kaja kumaliziwa na huyu wa TANESCO.
 
Back
Top Bottom