Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Kibaya alichokifanya MWAKYEMBE ni kipi? Huo MSIMAMO wenu ndio tusiotaka kusikia kabisa. Sasa ZITO sio swala la msimamo, ni SWALA la KITU KIDOGO TU, hakuna cha msimamo wala nini, kala/kaahidiwa hela ya ukuwadi, basi ndio anayoendelea nayo. Mwisho wake ndio huo. Alipewa ushauri toka mapema, rudisha hela ya mafisadi bado tunakutaka, yeye akaja na matusi hapa. Anyway si hapa nasikia kala fungu la kutosha. >10%

Punguza jazba ndugu yangu - the world is full of surprises and Tanzania tops the list !! Do not rule out anything. Kuna watu wamebobea katika usanii - yes, ndiyo jadi yao. Inawezekana Zitto amechukua msimamo ambao wengi hawakuutegemea, lakini hebu jiulize jambo moja. Kweli katika wakati huu ambao watu wamekuwa na mwamko mkubwa kama huu, Zitto, of all the people, atakuwa mjinga kiasi gani kujimaliza kirahisi hivyo ? Mnachosema ni kuwa Zitto amenunuliwa - na nani ? Kweli jibu linaweza kuwa rahisi namna hiyo ?

Wengi tunamlaumu lakini nachelea kusema tusitoe hukumu ya haraka haraka. Kuna wanaoshabikia hili kwa kuwa Zitto, kwa matendo na matamshi yake, amekuwa kero kubwa kwao - wengi wa hawa sasa hivi wanajichana na kujipongeza na kutupa maneno ya kejeli. Kwa nini tusiwaangalie hawa ambao kuanguka kwa Zitto kutawapa ahueni ni akina nani hasa ? Je ni wenzetu wale wale tulio nao vitani kupinga ufisadi au mafisadi wenyewe kwa kupata angalu mwanya wa kupumua kwa kuwa mawe sasa yanaelekezwa kwa Zitto.

Simtetei Zitto mpaka sasa lakini siko tayari kumhukumu. Niliwahi kusema katika hii vita dhidi ya hawa wezi na wahujumu uchumi, kila aina ya silaha itatumika. Wenzetu wamejitayarisha miaka mingi kulinda matumbo yao na tukilegeza kibano tu wataweza kujipanga tena upya. Hii ni lifetime opportunity ya kuiumbua mzimu wa Richmond na shemeji yake Dowans. Mwakyembe aliyewasilisha ripoti nusu nusu kuinusuru serikali, bila shaka atapata nafasi ya kufunua aliloficha kwa sababu safari hii hana tena namna ya kukwepa - daggers are drawn, twende kazini.
 
hivi kwanini watendaji wasiaminiwe? mpaka Bunge ndio liamue? to me bunge is just a bunch of political ****** who wants to be re-elected. Can you guys imagine when other countries have long done away with power rations, and these countries are a way poor than us?Maswala ya utendaji tunaleta siasa, sasa spika amekuwa na uwezo kuliko rais? JK you are too soft.

Hawa watu wanalindana ndugu , spika kachaguliwa na nani ? Raisi kachaguliwa na nani ? Usultani wa CCM umepatikana kwa njia za kukimbia na masanduku ya kura ,sasa wakianza kubamizana na kuonekana wanavunjiana heshima ,wanapingana kwa maelezo yao wengine watakuwa hawana adabu ,natumai Mwakiyembe kama sikosei alisema kumkosoa kiongozi ni kukosa heshima na ni utovu au ni kukosa adabu. Spika anaheshimika ,Raisi anaheshimika na kila mmoja ni mkubwa katika anga zake ,hivyo hakuna wa kumkemea mwenziwe maana adabu itakosekana ,we wacha wabanane hivyo hivyo kama kuna upinzani wa kweli basi ni kuwawacha na mazambi yao ,au kwa lugha nyingine waachwe wabebe misalaba yao wao wenyewe na upinzani utafute jino lingine haraka waanze kulitingisha na jino ambalo linafaa kutingishwa ni Katiba ambayo haiendani na mfumo wa Vyama vingi ,katiba ambayo haimsaidii mwananchi wa kawaida wala asie wa kawaida ila inawasaidia wafuasi na mafisadi wa Sultani CCM.
 
Kubali au usikubali mitambo ya Dowans ikinunuliwa haitafanya kazi zaidi ya miaka mitatu bila kwenda chini na kuhitaji major repair itakayogharimu si chini ya Dola milion 10. Halafu baada tu ya kununuliwa Dowans itayeyuka majini na mtengenezaji wa mitambo ndo atasema ukweli.

Let's go out tutangaze tenda mapema (ilikuwa possible since july last year tulipovunja mkataba na Dowans). Shetani na mungu wote wanajua kuwa tulipovunja mkataba na Dowans tulikuwa na mahitaji ya umeme. Ingetangazwa tenda sasa hivi tungekuwa tuko kwenye final touches za kupata mitambo mipya. Wakati mkataba wa Dowans unavunjwa watu ndani na nje ya TANESCO walikuwa buzy kuandaa mazingira yatakayosababisha kununuliwa mitambo ya Dowans iwe kama kusukuma mlevi.

Muda huo ndo sasa na wamepata new and unexpected supporters. Sasa ni wakati wa kula. Dr. I may go ahead and buy the Machines. He knows what he will be buying. But he know also that in Tanzania it is easy to get away especially when you are well connected. He has important people who trust him. What he fears is to blow-up their trust. This will happens if he buys Dowans. I bet he doesn't.

And Zitto, the staunch supporter of Dowans? Well let's wait and see him join Kaburu, his homeboy. Keep your eyes open, it will happen men/women!!!!!
 
Zitto Kabwe awanasa CCM katika nyavu zao

:: Atumia ndoano ya PPRA kuwachota wenye msigano CCM
:: Ahoji upya wa mashine za IPTL, uzee wa mashine za Dowans
:: Maslahi ya makundi yazidi kujidhihirisha, kila mtu na lake

Na Innocent Munyuku
...

Source: RAI

If RAI Owner = Dowans Owner then Dowans = ?
 
Kwa taarifa tu Mtwara wanatumia umeme wa gesi ,ni majuzi tu nilitokea huko na wapo njiani kuupeleka lindi nafikiri kumetokea matatizo ya 10% na ile kampuni imeondoka sasa wanaendesha wenyewe huku wakidokoa fedha kidogo kidogo .
 
Mama,
Nimeitoa hii kule Tanesco nadhani inaweza kusaidia pamoja na kwamba mahitaji yetu yanaweza kabisa kuwa mara mbili ya kiwango kilichoelezewa..


Asante kaka.

Hizo Takwimu are as for 31.12.2006.Though they have mentioned that their challenge is to provide electric power to 89 % of the population (11% electrified).

Ningependa kujua power demand ya nchi yetu, au current power deficit.

Hii ni muhimu in relation na kununua mtambo wa kuzalisha umeme (je mtambo huo utakuwa kwa ajili ya emergency tu au utacontribute kwenye daily power supply na utacontribute kiasi gani).
 
Inaonekana kuwa TANESCO itajitoa katika mchakato baada ya mkwara mzito wa Bunge. Suala la kujiuliza, ni je hao mafisadi watarudi kinamna gani?
 
hivi kwanini watendaji wasiaminiwe? mpaka Bunge ndio liamue? to me bunge is just a bunch of political ****** who wants to be re-elected. Can you guys imagine when other countries have long done away with power rations, and these countries are a way poor than us?Maswala ya utendaji tunaleta siasa, sasa spika amekuwa na uwezo kuliko rais? JK you are too soft.
======

Iwe Mujuni

Umeme kwa Kiingereza ni "Power". Wanasiasa kazi yao ni kutafuta "Power". Kwa issue ya umeme, wanagombania "power".
Usishangae maana ukiona msamiati unaotumika katika mjadala huu wa umeme ni "Mabilioni" siyo maelfu. Kwa mtaji huu, hakuna aliye tayari kukaa ofisini kusubiri mhimili fulani ufanye kazi yake. Wote ni jikoni, na atakayezubaa dinning ataliwa, maana chakula hakitakaa kije huko.

The end game ndugu zangu ni kuwa Dowans belongs to Mtandao asilia.
 
Asante kaka.

Hizo Takwimu are as for 31.12.2006.Though they have mentioned that their challenge is to provide electric power to 89 % of the population (11% electrified).

Ningependa kujua power demand ya nchi yetu, au current power deficit.

Hii ni muhimu in relation na kununua mtambo wa kuzalisha umeme (je mtambo huo utakuwa kwa ajili ya emergency tu au utacontibute kwa daily power supply na utacontribute kiasi gani).

acha uvivu! piga simu Tanesco au muulize waziri wa Nishati.. au tafuta hotuba za bajeti ya Madini na Nishati za miaka unayoiulizia.. Yaani unataka ulimiwe, uvuniwe, upikiwe mpaka utafuniwe wewe ubakie kumeza tu na kushiba halafu useme "chakula gani hiki hata siyo kitamu"! Fanya homework uje utuhabarishe uchunguzi wako na wengine tufaidike na kujituma kwako. Hili dogo namna hii linakushinda?
 
IPTL ni tofauti kabisa na Dowans.

IPTL tuko liable kuwalipa millions of dollars mpaka I beleive 2020. Sasa kama capacity charges ni dola $100 million lazima tuzilipe mpaka 2020 wakati hata hatuown mitambo, tukifanikiwa kununua kwa say $80 million si tunasave HELA??

Zitto acha kabisa gia zako zote zinaeleweka na huwezi kumsafisha Rostam
 
Last edited:
Mama,
Navyofahamu mimi vyanzo vya umeme toka mwaka 2006 havijaongezeka wala kubadilika na kama umesoma vizuri utaona kwamba karibia asilimia 80 ya vyanzo hivi vilikuwepo toka Mwalimu..why wala sielewi!..
Sasa tukianza kurudi ktk swala la mahitaji yetu nadhani tutakuwa tunajidanganya zaidi ya guess work kama vile hesabu ya wananchi, wakazi wa nchi nzima..nina hakika hata idadi ya nyumba Tanzania haipo acha mbali hesabu ya viwanda na maendeleo kwa miaka 10 au 20 ijayo.. Maisha yetu tunakwenda kwa siku kama mlo wa mlalahoi..

Kifupi tu ni kwamba tunahitaji mara mbili ya jumla zote za nguvu za umeme uliopo sasa hivi kwa sababu asilimia kubwa ya nchi/wananchi hawana umeme..
Kinachoniudhi mimi ni pale hawa wanasiasa wanapojaribu kutumia mitambo hii ya Dowans kuwa sababu kubwa ya ukosekanaji umeme na kutumia neno KIZA kama vile nchi nzima inategemea Dowans tena wakitumia mikoa kama Mwanza ambayo taarifa yao wenyewe inawashutumu..

Hapo juu wamesema hivi:- There are several diesel generating stations connected to the national grid in Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Dodoma, Musoma and Mbeya. These have installed capacity of 80 MW but they effectively contribute about 35 MW due to running problems.

Unaona habari hiyo?... sasa kama sii ujuha ni kitu gani!
Kama mimi kiongozi ningekuwa much concerned na sababu zinazofanya mitambo hiyo kutoa 35MW badala ya uwezo wake wa 80MW, wala sio hapo tu Mama karibu kila mitambo ya uzalishaji Umeme nchini inatoa chini ya kiwango chake kutokana na utamaduni tusiokuwa nao (Maintenance)..Hii dhahiri inaonyesha wazi kwamba ni UJINGA mkubwa kukimbilia kununua mitambo iliyochakaa wakati tunashindwa ku maintain mitambo tuliyokuwa nayo tayari kwa fikra za Kisiasa..
 
Mag3.

Tunashindwa kumuunga mkono Zitto si kwa sababu ya kufurahia kuanguka kwake. Ni kwa sababu ya logic rahisi. Zitto sasa hivi ana positive coverage RAI, unataka tuamini kuwa RAI iko balanced katika reporting yake? Imebadilika? May be.

Lakini logic rahisi ni hii. Zitto anaungana na TANESCO pamoja na Wizara ya madini na Nishati kuunga mkono ununuzi wa mitambo ya Dowans, na kwa maneno yake mwenyewe issue siyo tunanunua wapi. Issue ni kuwa tupate solution. Nakubaliana na huu msimamo ikiwa tungekuwa tunanunua bidhaa rahisi. Hiki tunachonunua ni MITAMBO!!! Reputation ya muuzaji kwenye bidhaa kama hizi ni muhimu kuliko kitu kingine chochote. Kununua mitambo ni kufungua mahusiano ya muda mrefu, kwani mitambo ina vitu vingi ambavyo hata ukimleta mtaalam gani hawezi kuona vyote na kujiridhisha kuwa kinachosemwa na muuzaji ni sahihi. Ndo maaana tunahitaji kujua reputation ya muuzaji, ili ikitokea tatizo huko mbeleni turudi kwake. Na kwa issue kama ya mitambo tatizo lazima litatokea dogo au kubwa!!!!

Sasa ikiwa unanunua kutoka kwa mtu ambaye humjui vizuri ni kama kununua CD kwa machinga barabarani. Unabeba ukifika nyumbani, ukiweka kwenye DVD player yako ile CD ikagoma basi unatulia na kujiridhisha kuwa "after all nimenunua shilling elfu tatu tu". Je unataka tufike hapo? Mitambo ile hatuinunui kwa elfu tatu wala milioni tatu.

Zitto anayajua yote hayo. Atueleze kwa nini sasa hivi yuko tayari kununua relationship (kununua mitambo ni kununua relationship) ya muda mrefu, bila kuwa na uhakika wa unayenunua hiyo relationship kutoka kwake? Au Zitto anajua zaidi kuhusu huyu Dowans ni nani na ana uhakika naye. Mbona hatuambii wengine wote ili tukaondoa wasiwasi???

Tunategemea consistency kutoka kwa mtu tunayeamini kuwa ni kiongozi mzuri. Tungetarajia kuwa Zitto, Kabla ya kutoa support yake angeuliza maswali ambayo wote tungeyaona na kujua. Viongozi wazuri hawako predictable, ila wako consistent. Kama ni republican atakuwa conservative always. Suala la kutokuwa predictable lisichanganywe na consistency. Nyerere was somehow not predictable, lakini he was consitent mpaka anakufa. Kwa suala kama hili wala usingejiuliza nyerere angekuwa upande gani!!!

Zitto????? Let's wait and see. Lakini so far utetezi alioutoa ni shameful. Ndo maana KGM and other well wishers wa Zitto wanakuwa concerned. What has gone wrong?
 
Mama, navyofahamu mimi vyanzo vya umeme tokqa mwaka 2006 havijaongezeka wala kubadilika na kama umesoma vizuri utaona kwamba karibia asilimia 80 ya vyanzo hivi vilikuwepo toka mwalimu..

Wasikusikie!!!
Sasa tukianza kurudi ktk swala la mahitaji yetu nadhani tutakuwa tunajidanganya zaidi ya guess work kama vile hesabu ya wananchi, wakazi wa nchi nzima..nina hakika hata idadi ya nyumba Tanzania haipo acha mbali hesabu ya viwanda na maendeleo kwa miaka 10 au 20 ijayo.. Maisha yetu tunakwenda kwa siku kama mlo wa mlalahoi..

Kifupi tu ni kwamba tunahitaji mara mbili ya jumla zote za nguvu za umeme uliopo sasa hivi kwa sababu asilimia kubwa ya nchi/wananchi hawana umeme..
Kinachoniudhi mimi ni pale hawa wanasiasa wanapojaribu kutumia mitambo hii ya Dowans kuwa sababu kubwa ya ukosekanaji umeme na kutumia neno KIZA kama vile nchi nzima inategemea Dowans tena wakitumia mikoa kama Mwanza ambayo taarifa yao wenyewe inawashutumu..

true!

Hapo juu wamesema hivi:- There are several diesel generating stations connected to the national grid in Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Dodoma, Musoma and Mbeya. These have installed capacity of 80 MW but they effectively contribute about 35 MW due to running problems.

Unaona habari hiyo?... sasa kama sii ujuha ni kitu gani!
Kama mimi kiongozi ningekuwa much concerned na sababu zinazofanya mitambo hiyo ya huko mikoani kutoa 35MW badala ya uwezo wake wa 80MW, wala sio hapo tu Mama karibu kila mitambo ya uzalishaji Umeme nchini inatoa chini ya kiwango chake kutokana na utamaduni tusiokuwa nao (Maintenance)..Hii dhahiri inaonyesha wazi kwamba ni UJINGA mkubwa kukimbilia kununua kitambo iliyochakaa wakati tunashindwa ku maintain mitambo tuliyokuwa nayo tayari kwa fikra za Kisiasa..[/QUOTE]


Ukiambia inagharimu kiasi gani kuikarabati mitambo yote hiyo hautarudi JF!!
 
acha uvivu! piga simu Tanesco au muulize waziri wa Nishati.. au tafuta hotuba za bajeti ya Madini na Nishati za miaka unayoiulizia..

Hivi mbona unakiherehere namna hii, ombi langu halikuwa kwa mwanaJF yeyote yule awaye, nimelielekeza kwa mtu specific. Alijua na akaelewa na akanijibu apropriately. Sasa wewe kinachokuwasha nini!?

Yaani unataka ulimiwe, uvuniwe, upikiwe mpaka utafuniwe wewe ubakie kumeza tu na kushiba halafu useme "chakula gani hiki hata siyo kitamu"!

Wewe hii inakuhusu nini? acha kimbelembele, kisebusebu na kiroho papo!

Fanya homework uje utuhabarishe uchunguzi wako na wengine tufaidike na kujituma kwako. Hili dogo namna hii linakushinda?


Homework yangu ni kwenda sokoni, kupika, kuogesha watoto na kusafisha nyumba. Nimeifanya hiyo homework, hivyo nakuhabarisha, faidika na habari toka kwa homework yangu.
 
Hivi mbona unakiherehere namna hii, ombi langu halikuwa kwa mwanajF yeyote, nimelielekeza kwa mtu specific. Alijua na akaelewa na akanijibu apropriately. Sasa wewe kinachokuwasha nini!?



Inahusu nini? acha kimbelembele, kisebusebu na kiroho papo!




Homework yangu ni kwenda sokoni, kupika, kuogesha watoto na kusafisha nyumba. Nimeifanya hiyo homework, hivyo nakuhabarisha, faidika na habari toka kwa homework yangu.

Hizi zote ni dalili za uvivu! uko kwenye mtandao, tafuta habari kwenye mtandao kuhusiana na energy sector. Maswali yako yote unaweza wewe mwenyewe kuyatafutia majibu endapo tu utaamua kufanya kazi kidogo kuliko kukaa na kusubiri mwingine akufanyie kazi. Kwa kadiri watu wanakupatia majibu ambayo wewe mwenyewe ungeweza kupata wanaendelea kukubariki katika uvivu huu.

Kuna vitu ambavyo unaweza kuomba mtu mwingine afanye lakini kuna vingine ni bora kufanya wewe mwenyewe. Hili la kutafuta takwimu hizi rahisi ni jambo ambalo hata wewe unaweza kulifanya.

Vinginevyo, kuna mtu anapenda kudekezwa humu!
 
Tanesco kupasua jipu
Mwandishi Wetu
Daily News; Thursday,March 05, 2009 @19:40

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) leo linatarajiwa kupasua jipu juu ya mjadala ulioibuka hivi karibuni, ukihusu ununuzi wa mitambo ya umeme ya Kampuni ya Dowans.

Ingawa shirika hilo halikueleza wazi kuwa lengo ni kuzungumzia suala hilo, lakini waandishi wa habari waliokuwa wameitwa leo ofisini hapo kwa ajili ya mkutano, waliambiwa kuwa leo ndipo Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco atazungumzia kile kilichoelezwa kuwa ni taarifa nyeti ambazo wananchi inafaa ziwafikie kwa usahihi.

Tanesco kupitia kwa maofisa wake haikufafanua taarifa zinazokusudiwa kuwekwa hadharani leo kwa waandishi, lakini mazingira yanaonyesha kuwa inahusu mjadala ulioibuka hivi karibuni kuhusu ununuzi wa mitambo ya umeme ya Kampuni ya Dowans, hususan kauli ya juzi ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta.

Alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Sitta aliitahadharisha serikali juu ya athari zinazoweza kujitokeza iwapo itapuuza ushauri wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ya kuamua kuendelea na mchakato wa kununua mitambo hiyo.

Baada ya taarifa kuhusu kauli ya Spika kujitokeza katika vyombo vya habari, leo Tanesco ilitoa taarifa katika vyombo vya habari kuwa Mkurugenzi Mkuu, Dk Idris Rashid angefanya mkutano na waandishi wa habari. Hata hivyo, waandishi walikaa katika ofisi za makao makuu ya shirika hilo kuanzia saa 9 alasiri hadi saa moja kasoro jioni jana bila kufanyika mkutano wowote zaidi ya maofisa habari kuwataka radhi kuwa mkutano huo ungefanyika leo.

Ofisa Mawasiliano, Ray Naruyaga aliwaambia: "Mkurugenzi anaomba radhi kwa kuwaweka muda mrefu. Ameahirisha hadi kesho(leo). Wamefanya hivyo kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika,” alisema. Aliongeza, “siyo kwamba hawaheshimu habari, taarifa ziwafikie wananchi kwa usahihi,” alisema Naruyaga bila kutaja taarifa husika lakini akisema ni nyeti.

Awali, mmoja maofisa wa Huduma kwa Wateja wa Tanesco, Fatuma Mruma, aliwasihi waandishi wa habari kusubiri kutokana na kile alichosema Mkurugenzi alikuwa akipata simu nyingi kutoka kwa waandishi zikihitaji ufafanuzi wa Tanesco. Kulingana na taarifa zilizopatikana, Dk Idris alikutana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima katika ofisi hizo za shirika, katika mkutano ambao hata hivyo haikufahamika ulihusu nini.

Hivi karibuni, ulijitokeza mjadala mzito baina ya wanasiasa juu ya ununuzi wa mitambo hiyo. Mjadala huo ulitokana na kitendo cha kamati mbili za kudumu za Bunge, (Kamati ya Nishati na Madini na ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma) kukinzana katika uamuzi huo. Wakati Kamati ya Madini ikiongozwa na William Shellukindo ilishauri serikali isiiruhusu Tanesco kununua mtambo huo kutokana na kile kilichoelezwa kwamba Sheria ya Manunuzi inakataza kununua vitu vilivyotumika, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma chini ya Zitto Kabwe iliunga mkono ununuzi.
 
Wakuu,

Hivi kelele zote hizi bado hakuna anayesema mtambo mpya wa kununua huu hapa?

Angalau Zitto ameonyesha hafuati upepo na yuko tayari kukosa umaarufu wa kisiasa kwa kitu anachokiamini.

Wanasiasa wote wamehamia Dar kupiga kelele za mtambo, hakuna uamuzi unachukuliwa, nchi giza totoro baada ya muda tunajiuliza eti kwanini hatuendelei?

Haya makundi yanayopingana yangeliweza kukaa pamoja na kujadiliana kwa wiki na kisha kuamua cha kufanya sio kama sasa wanasiasa wamegeuka watalaamu wa umeme.

Wacha wengine tuwajibike!
 
Nimeisoma post ya Mpaka Kieleweke, naona kuna maswali mengi! Iwapo Richmond alipata mkataba wa us$ 88.7m kwa miaka miwili kwa 100MW, kwa hiyo tanesco walilipa tshs 60.754/KW kwa saa ambayo sawa na unit moja ya umeme ninayotumia kibandani kwangu. Nimechukua bili yangu ya 2007 na kuona nilikuwa nalipa tanesco tshs 126 vat exclusive. Inamaana tanesco walipata tshs 65.246 profit before tax. Nisaidieni mie hata kuchomeka bulb sijui !

Dowans angejitokeza tungewauliza gharama za ges, vipuri, kodi, depreciation, capital investment allowance, long term interest, administration fees zilikua kiasi gani? Isijekuwa walikuwa fair! Kama gesi na vipuri tulimpa bure basi utakuwa ujinga mwingine.
 
Ukweli tangu Dr. Idrisa aingie tanesco kunamabadiliko fulani mita za luku zimekuwa za kumwaga, kuunganishwa sasa ni chap chap, longolongo za wasoma mita hakuna tena. Hawa wanaonyonya mafuta ya transforma tumeshajiundia sungusungu wenyewe, mtaani kwetu tumeajiri korokoroni pamoja na kulinda mtaa wanalinda na transforma. Ila hili la kukiuka maamuzi ya bodi linataka kufanana na kesi ya liyumba vile! nadhani takukuru wanaliona hili, watamchukua maelezo sio muda mrefu.

Nadhani Dr. anatakiwa aajiri Strategic planning manager pia.
 
Back
Top Bottom