Tumezingatia sheria za nchi na Mahitaji ya nishati ya Umeme kwa Taifa
Maslahi gani ya taifa umesimamia?
Sheria ya manunuzi inayosimamia maslahi ya taifa ili kuzuia vitu mitumba visinunuliwe hujaisimamia utasemaje umesimamia maslahi ya taifa?
Ili taifa lipate vitu kwa bei nzuri huhitaji tenda ziitishwe kampuni nyingi zishindanishwe kwa uwazi kila kampuni ilete bids zao ndipo ujue uchague yupi mwenye maslahi kwa taifa wewe Zitto umeshupalia Dowans tu kuna nini na Dowans?
Ungesimamia maslahi ya Taifa ungezungumzia kuitisha tenda ambapo Dowans naye angetaka ange bid lakini kuishupalia Dowans tu inaonyesha una maslahi na Dowans na si Taifa.Kwa nini usishupalie tender bids ziitishwe unashupalia tu Dowans,Namini zingeitishwa Tender Bids Dowans wasinge bid kabisa wao kama Dowans maana wanajua sheria ya manunuzi inavyosema kuwa hairuhusu mitumba.Wasingekubali ku bid na kupoteza ile tender bid fee kienyeji.
Nadhani Dowans kuna wajanja wenye akili wakaona zikiitishwa tenda bids watakwama wakaona watafute watu wasio na uchungu na hela za wananchi wawatumie kama vikaragosi UCHWARA wa ku-twist mambo ili tender bids zisiitishwe ila wao wafanyiwe single sourcing. Ni bahati mbaya kuwa Zitto umenaswa kwenye huo mtego na huyo mkurugenzi wa Tanesco naye akaingia mkenge na usomi wake.Mngekuwa na uchungu kwa maslahi ya taifa wewe na huyo Idrisa mngewaambia Dowans kuwa walete bids zao na mkatangaza Tender bids za ku-supply mitambo haraka mkazisambaza kwa vyombo mbalimbali vya habari na kutoa deadline hata ya muda mfupi muone nini kingetokea kabla ya kumshupalia Dowans kama mshindi pekee.
Sijui aliwapa nini Dowans mkamhakikishia kuwa akae atulie hakuna cha Tendering process wala nini wewe na Idrisa mkajivika ujemadari wa kumkingia kifua kuhakikisha tendering process isiwepo bali uimbwe wimbo tu wa Dowans.Kwani Dowans ni nani kwenu?
Mumeshupalia Dowans wanauza mitambo wanauza mitambo.Wao si wauzaji pekee wa mitambo wauzaji wako wengi.Zito na mwenzio kwa nini hamkushupalia Tendering process mkashupalia Dowans tu kuwa ndiye mwenyewe huyo mhhhhhh Zitto Kabwe nasikia kaharufu ka ufisadi.
Kwa nini hamkupenda katenda kaitishwe na kipenzi chenu Dowans a-bid ashindane na wengine hata kama si wauza mitambo mipya basi ashindane hata na wauza mitambo mitumba wengine walioko ndani au nje ya nchi? Kwani wanaozalisha umeme kwa kutumia mitambo mitumba na kuiuzia umeme Tanesco si Dowans tu si wapo na wengine pia? Hata kama mitambo mitumba haiko hapa unajuaje kama hawana sehemu nyingine.Naamini ingetangazwa tender ya mitumba tungepata suppliers kibao tena wenye mitumba mizuri na ya kisasa zaidi na bei poa kuliko Dowans. After all nani anahitaji mitumba tungeipata kwa throw away price kama tungeitisha tender na kusema tunahitaji masharti yetu tunahitaji mitambo mitumba.
Wewe kama mbunge unashindwa hata kulinda na kutetea sheria ya manunuzi iliyotungwa na bunge lenyewe hivi kama huwezi tetea hata kilichotungwa na bunge lenyewe hivi wewe ni mbunge au afisa masoko wa Dowans?
Unasema sheria ya Manunuzi si msahafu yaweza badilishwa unajua unachosema? Mimi mpagani ninavyojua sheria ni kubwa kuliko msahafu sababu misahafu Tanzania ni kwa ajili ya kundi la watu wachache mfano Kurani si kwa ajili ya watu wote ni kwa ajili ya waislamu,na Biblia ni kwa wachache wakristo lakini sheria ni kwa ajili ya watu wote.Kimatumizi sheria ni pana zaidi kuliko misahafu ya dini.
.Huwezi tu kuibuka ukiwa umelewa ulevi wa Dowans na kuanza kuiponda sheria tu kirahisi hivyo.Wewe kama mbunge ilipaswa ujue kuwa sheria ni kitu kikubwa haitungwi siku moja na huwezi kuibadilisha kwa siku moja kuna process ndefu sana ya kutunga na kubadilisha sheria.Na taratibu za kubadilsha sheria hazifanywi na kamati yako ya bunge ya mahebu wala ya Mwakyembe ile ya madini wala na Tanesco bali hufanywa na bunge baada ya mchakato mrefu.Sasa unaposema kamati ya akina Mwakyembe wakaonane na Tanesco ili iwe nini.
Ungekuwa kweli unajali maslahi ya Taifa ungeiomba tume ya kurekebisha sheria iangalie uwezekano wa kupeleka mswada bungeni wa kubadili sheria ya manunuzi kama huridhiki nayo au ungewakilisha hoja zako bungeni ukajenga hoja zako kule.Taratibu za kubadili sheria unazijua au huzijui au umepofushwa na Dowans kiasi kuwa hukumbuki na huoni?
Na huyo mkurugenzi wa Tanesco mbumbumbu mwenzio naye anasema sheria ya manunuzi ni kikwazo anatoa kwenye press release. Msomi mzima hajui kama sheria ina utata ukitaka ibadilishwe hajui kuwa mtu anatakiwa apeleke hiyo hoja wapi? Kama anataka sheria ibadilshwe msomi yule hajui kweli pa kuanzia? Hivi press release na usomi wake ndiyo kaona njia ya maana ya kulalamikia sheria ya manunuzi? Matangazo yale pesa kibao zimetumika kuwalipia kufaidisha magazeti yakiwemo yanayomilikiwa na Rostam Azizi mtuhumiwa kwenye Richmond na Dowans.Ufisadi mwingine.Napendekeza pesa ambazo zimetumiwa na Tanesco kwa ajili ya ile press release zikatwe kwenye mshahara wa mkurugenzi mkuu wa Tanesco zirudi kwenye akaunti ya shirika.Aliyewaambia mnaanzia Dowans,Tanesco,au kwenye kamati za bunge za hesabu na madini kubadili sheria ni nani.Nashukuru Mwakyembe na kamati yake kuukataa wito wako feki wa kuwataka wakaongee na Tanesco kuhusu ununuzi wa mitambo mitumba ya Dowans kinyume na sheria ya Bunge.
Mwalimu Julius Nyerere alipokuwa Uingereza aliwahi siku moja kuulizwa ni kitu gani anakiona kigumu kama mwanasiasa akasema kitu kigumu ni kujaribu kutunga uongo na kujaribu kuufikisha kwa wananchi na kuwafanya wananchi waukubali huo uongo.Inavyoonyesha Zitto umefikia mahali pagumu pa namna hiyo.Unapata shida ya kutunga uongo na unapata shida zaidi kuufikisha uongo huo kwa wananchi.
Kumbuka siku zote kuwa kutunga uongo ni kazi kubwa na kuufanya uongo ukubalike ni kazi kubwa zaidi.Pole.
Mwisho nashauri hata kama sheria ya manunuzi itabadilishwa tukasema tunahitaji mitambo mitumba kama ya Dowans Lazima tender process ifanyike na wauza mitumba wengi wa bid.Siyo kuwa ikibadilishwa basi Dowans wapewe hapana.Lazima waingie kwenye tender.Kama wakishinda washindie kwenye tender lakini sio mezani kwenye meza ya Zitto kabwe au Idrisa Rashid mkurugenzi wa Tanesco.