WanaJF,
Sikuwa katika mazingira ya kupita humu jamvini na kushiriki katika mjadala. Nimerudi safari na nilipopita nimekuta masuala mengi ya kujibu kwa upendo wangu kuhusiana na mjadala huu wa Mitambo ya kuzalisha Umeme. Ni mjadala mkali na wenye kubeba uchungu wa Taifa letu. Nimeona mumemuweka kiti moto kweli Dr. Slaa. Nadhani ni mwafaka mimi mwenyewe kujibu baadhi ya hoja na kama kuna maswali, basi niweze kujibu kadiri nitakavyoweza.
Kwanza Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (Public Investments Committee) haina mamlaka ya kikanuni au ya kikatiba kuiamrisha Serikali au Shirika la Umma kufanya au kutofanya manunuzi. Kamati kazi yake ni oversight (kusimamia). Kwa kweli hii ndio kazi ya Bunge na Kamati zake. Hata Kamati ya Nishati na Madini haina mamlaka ya kuingilia suala la utendaji wa kila siku wa Serikali. Ukishaifanya kamati ifanye kazi hiyo maana yake ni kuwa siku mhimili wa utendaji ukiboronga, Bunge halitaweza kusimamia kwani litakuwa ni sehemu ya uborongaji huo.
Pili, Kamati yangu imepewa mandate ya kufuatilia ufanisi wa mashirika ya Umma. Baada ya kuangalia income statement, na balance sheet, ambazo ndizo nguzo kuu zetu kufuatia taarifa ya CAG huwa tunaangalia je, Shirika linaendana na Corporate Plan yake? Melengo yanafikiwa? Huduma kwa wananchi ni bora, etc.
Kamati ilikutana na TANESCO mwezi Januari mwaka 2009 ili kutizama hesabu zao zinazoishia Disemba 2007. Tuligundua masuala yafuatayo:
- TANESCO katika mwaka unaoishia Disemba 2006 walipata 'Disclaimer Audit Opinion' kutoka kwa mkaguzi. Hesabu zao zilikuwa chafu sana kiasi cha Mkaguzi kuzikataa na kushindwa kutoa Opinion.
- TANESCO katika mwaka unaoishia Disemba 2007 walipata 'Unqualified Audit Opinion' kutoka kwa mkaguzi. Walifanikiwa kuruka hatua kadhaa (hati chafu, hati yenye mashaka) na kufikia hati safi. Hili lilikuwa jambo la kupongeza sana. Hasa ukizingatia kuwa wakati Kampuni ikiwa chini ya menejiment ya wageni (Net Group solutions) tulipata hati 'disclaimer' na ndani ya mwaka mmoja wa menejimenti ya Watanzania, tukapata hati safi na kusafisha madudu yote.
Hata hivyo, tulikuta matatizo kadhaa ndani ya TANESCO. Moja ya tatizo kubwa sana tulilolikuta ni kwamba gharama za kununua umeme kutoka kwa wauzaji (kama IPTL na Songas) zilikuwa zinachota fedha nyingi sana wakati umeme wanaozalisha ni kidogo sana ukilinganisha na umeme unaozalishwa na TANESCO wenyewe. Hebu fikiria: TANESCO inanunua kutoka kwa wawekezaji 42% ya umeme wote wanaouza. Hivyo TANESCO yenyewe inazalisha asilimia 58 ya umeme wote. Hata hivyo asilimia 84 ya mauzo yote ya umeme yanalipia umeme unaonunuliwa kutoka kwa wawekezaji (cost of sales) - yaani katika kila sh 100 ambayo TANESCO inakusanya kutoka kwa wateja wake, sh 84 zinatumika kununua 42% ya umeme ambao TANESCO inauza kwa wateja. Hivyo TANESCO inabakia na sh 16 kwa ajili ya kujiendesha ikiwemo kusambaza umeme zaidi kwa wananchi (kumbuka 12% ya watanzania ndio wenye umeme, na kwa Dar 50% ya wakazi hawana umeme - Household Budget survey 2007 iliyotoka November 2008). Kamati yangu ikasema, he, hili mbona halikubaliki?
Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kamati ikaagiza TANESCO waje kujieleza mbele ya Kamati juu ya hatua wanazochukua ili kupunguza gharama (cost of sales) na kuongeza mapato. (Kamati yangu imejiwekea lengo la kuhakikisha kuwa mpaka itakapokuwa inamaliza muda wake mwaka 2010 Agosti, mashirika yote muhimu ya Nchi yawe ama yana-break-even au yanapata faida. Ndio maana huwa hatupitishi hesabu mpaka tupate commitment za ma-CEO).
TANESCO wakaja katika kamati tarehe 21 Februari an kuwasilisha hatua mbalimbali wanazochukua. Katika hatua hizo ni pamoja na kutaka kununua mitambo ya DOWANS. Wakatueleza sababu zao zote. Tukawauliza maswali yetu. Ilikuwa ni mjadala sober sana katika Kamati. Kamati ikaona kuwa hoja za TANESCO zina mantiki.
Tukawauliza TANESCO, haya mnayotuambia mliiambia kamati ya Nishati na Madini? Kama ndio, mbona wao wamewakatalia? TANESCO, wakatujibu na kusema kamati haijawahi kutoa nafasi kwao kuelezea hoja zao. Tukasema, kama ndio hivyo basi, tunataka haya mnayotueleza sisi mwende mkayaseme tukiwa ni kamati mbili kwa pamoja kwani sisi hatupendi tupingane na wenzetu. Kamati ikaazimia hivyo.
Tukawauliza, Kamati ya Richmond walituambia DOWANS hawazalishi umeme. Iweje leo mitambo yao iwe inafaa ilhali wao walishindwa kuzalisha? TANESCO wakasema sio kweli, kwa mwaka mzima na tulikuwa tunanunua umeme wao MW 100 na hata wakati Dr. Mwakyembe anasoma taarifa ile, tulikuwa tunatumia mitambo ya Dowans. Wakaongeza kuwa ndio maana kipindi kama hiki (ambacho uzalishaji viwandani hukua na kutumia umeme mwingi) mwaka jana hatukuwa na mgawo kwani tulikuwa na 100MW kutoka Dowans mpaka tulipovunja mkataba mwezi Agosti. Pia kulikuwa na AGGREKO ambayo ilikuwa na 40MW. Hivi sasa kuna deficit ya 150MW ya umeme katika gridi.
Tukawauliza, hawa jamaa tunawadai. Wakasema ni kweli. Wamelipa deni lote ambalo tulikuwa tunawadai Richmond (35% of the value of the contract advanced to Richmond) na mpaka tunavunja mkataba tulikuwa tunawadai dola 8m tu maana walikuwa wanakatwa katika malipo yao. Hivyo tukiwanunua pia tunakata na pesa yetu.
Tukawauliza, sheria ya manunuzi inakataza. Wakasema ni kweli inakataza. Ilikuwa inakataza hata mitambo ya IPTL ambayo ni mikuukuu zaidi lakini sheria zina waiver kulingana na mahitaji ya nchi. Hata Ugiriki wakati wa Olimpiki walinunua mitambo iliyotumika nk. Ndio maana huwa tunanunua ndege zilizotumika. Mitambo ya miundombinu mara nyingi huwa ina special cases kisheria na ni nchi zote duniani.
Kamati ikasema sawa. Tutakutana Kamati mbili, Serikali na PPRA ili tuangalie suala hili. Nikafunga kikao
Haya jamani niambieni kosa langu lipo wapi?
Tatizo Watanzania mmezoea viongozi wanaowaambia mnayoyapenda tu. Hamjazoea na kwa mtindo huu hamtazoea viongozi ambao wanathubutu kuingia hata kwenye maeneo msiyoyapenda kusikia. Ndio maana maamuzi hayafanywi serikalini kwa sababu ya midomo.
Hapa JF kila mwanachama kawa leo mtaalamu wa Umeme, wengine wataalamu wa kanuni za Bunge, wengine wataalamu wa manunuzi lakini hata hawawezi kusema kifungu gani cha sheria ya manunuzi kinazungumzia suala la kununua mpya au hapana na kwa mazingira gani. Siasa tuuuuuu. Wengine mnahoji credibility yangu. Bila hata soni mnadhani mimi ni mpumbavu sana wa kuweza kujiwekea bei, at my age!
I am proud to what i have done for my country. I can die today smiling for my achievements. Wengine mdomo tuuuuuuuuuuu.
Wengine mnasema twende gizani. Mpo Ulaya na Marekani. Mnajua giza nyinyi? Mnajua madhara kwenye uchumi kwa umeme kukatika saa moja? Mwaka 2006 this sector grew at -2.5 kwa sababu ya giza and costed 2 points growth to our economy (read my speech bungeni katika mjadala wa richmond and economic survey 2006). Today the sector grow at 8% na mnataka twende nose diving again. Someni EIU survey feb 2009, kale kamgao ka Januari kalisababishwa na nini mnajua? Socket breaker tu iliungua na nchi ikaingia gizani kwani hakukuwa na reserve energy. Grid yetu ipo over done.
Mnajifanya mnajua, si lolote si chochote. Sisi ndio wawakilishi wenu. Tuulizeni. Tutawajibu. Tuulizeni tena. Tutawajibu. Tena na tena. Dont call us names.
This stupidity kills the courage of some of us to question myths of our society.
Lakini ninaelewa. Nchi imekuwa na wanasiasa wezi na waongo kwa muda mrefu sana. Hivyo trust to political class hakuna tena. Mpo paranoid. Kila mwanasiasa mnamwogopa masikini. Mnapata viongozi aina yenu Watanzania, kwani wengi ambao wanahoji humu pia hata ukimpa kijiji atakula mpaka bata wa kijiji (78% of Tanzanians dont trust each other - PHDR 2007).