Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,890
Kwa nini hao wahandisi wasiamzishe kampuni zao za kuunda hiyo mitambo?
Sijui. Mie sio mhandisi. Wamo humu, watajibu
Kwa nini hao wahandisi wasiamzishe kampuni zao za kuunda hiyo mitambo?
Ndugu yangu sikwepi kukujibu hata kidogo. Mie sifichi kitu na ndio maana nipo hapa ninajibu kila ninaloona naweza kujibu au kujieleza licha ya watu kufanya judgements zao (which is very unfair).
Kwa sasa siwezi kujibu moja kwa moja msimamo wangu binafsi kwa sababu nitaweza kusababisha tatizo la kikanuni maana ni vigumu watu kutofautisha na msimamo wa Kamati ya Bunge ninayoongoza.
So far ninasimamia msimamo wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma. Tumeandika kwa Spika na pia kwa Waziri wa Nishati na Madini kwa mujibu wa kanuni za Bunge. Tumezingatia sheria za nchi na Mahitaji ya nishati ya Umeme kwa Taifa. Tumezingatia umuhimu wa Shirika la Umeme la Taifa kujiendesha kibiashara na kuanza kupata faida.
Is being pragmatic means kununua zigo lililiopatikana kifisadi? Kwa hiyo kamati yenu inakubaliana na ufisadi? Kisheria inakuwaje?
Sijui. Mie sio mhandisi. Wamo humu, watajibu
maana ya kuwa pragmatic ni nini? labda mheshimiwa atumie neno la kiswahili naona limekuchanganya.
Ok, I will reserve my judgement.
Pamoja na hayo, nadhani MKJJ hukuweza kumuuliza kuwa hiyo Dowans ni ya nani kwani si mahali pake hapo, ila pia tujiulize:
Iweje DOWANS (ambayo haijulikani ni kampuni ya nani wala ya wapi Dubai, Costa Rica, South Africa au Mauritius) iliyorithi mkataba HARAMU toka kwa kampuni HARAMU ya ki-tapeli Richmond (TANESCO na serikali waliuvunja huo mkataba kuwa ni batili, kwa maana pia hata Dowans walirithi mkataba batili), leo hii iwe HALALI kumiliki na kuuza mitambo yake kwa gharama takribani mara 2?
?Katika kuuza na kununua, kuna mmoja humfuata mwenzie. Ama muuzaji humfuata mnunuzi au mnunuzi humfuata muuzaji. Hapa ni nani kamfuata nani
Ama kweli kichwa cha mwendawazimu!
Na ndugu yangu Zitto naye, au basi nitasema zaidi baada ya Cheche ........
Wahandisi wapo lakini hakuna kampuni ya kuunda.
Kaka sijui kiswahili chake. Nimetoa mfano wa Mwalimu Nyerere na utaifishaji baada ya Azimio la Arusha. Williamson Diamond haikutaifishwa kwa sababu ya pragmatism ya Mwalimu. Au Mwalimu alipoamua kuita askari wa UK kumsaidia wanajeshi walipoasi badala ya kuita kutoka Ghana au Nigeria na hivyo kulaumiwa sana na wenzake wa Afrika kwa kuita jeshi la imperialists. Alikuwa Pragmatic. Tunapataje kiswahili chake?
==========Kaka sijui kiswahili chake. Nimetoa mfano wa Mwalimu Nyerere na utaifishaji baada ya Azimio la Arusha. Williamson Diamond haikutaifishwa kwa sababu ya pragmatism ya Mwalimu. Au Mwalimu alipoamua kuita askari wa UK kumsaidia wanajeshi walipoasi badala ya kuita kutoka Ghana au Nigeria na hivyo kulaumiwa sana na wenzake wa Afrika kwa kuita jeshi la imperialists. Alikuwa Pragmatic. Tunapataje kiswahili chake?
Zitto,Kaka sijui kiswahili chake. Nimetoa mfano wa Mwalimu Nyerere na utaifishaji baada ya Azimio la Arusha. Williamson Diamond haikutaifishwa kwa sababu ya pragmatism ya Mwalimu. Au Mwalimu alipoamua kuita askari wa UK kumsaidia wanajeshi walipoasi badala ya kuita kutoka Ghana au Nigeria na hivyo kulaumiwa sana na wenzake wa Afrika kwa kuita jeshi la imperialists. Alikuwa Pragmatic. Tunapataje kiswahili chake?
==========
Mwalimu alikuwa pragmatic na kiswahili chake ni kigumu. Hii ya kamati ya Zitto siyo pragmatism, na kiswahili chake ni "kukosa msimamo" au kuwa na "ujasiri wa kifisadi".
Hivi Zitto are you serious unaturushia changa machoni?
Zitto uliyejipatia umaarufu ambao wanasiasa wengi waliokaa madarakani miaka mingi hawana na wanautamani, leo unaamua kuupoteza kwa ajili ya Dowans (siyo taifa). Tanesco wameunda mgawo wa lazima ili kutulazimisha kununua mtando wa Rostam. Ndugu yangu Zitto nakusihi kwa kutumia kifungo cha Buzwagi achana na mpango huu.
Sema wewe kiazi, mitambo ya Dowans lazima inunuliwe kwani mwezi April kutakuwana shida ya umeme. Unaona bana, hivyo basi lazima hiyo kamati ya mheshimiwa Zitto iwe pragmatic, halafu na wadandiaji utawaona wakiuliza dola kumi. Hawana comment zaidi ya kwenda personal, so wary.
Sitetei Dowans maana hata kuwajua siwajui. Sijui kuanzia mmiliki mpaka hata mlinzi wa Dowans.
Nataka Umeme. Sitaki uchumi utetereke tena kwa kukosa umeme. Tunaumia kwenye Utalii, Pamba na Maua hivi sasa. Makampuni makubwa yameanza kupunguza wafanyakazi na hata kwenye sekta madini. Mwezi Januari, circuit breaker iliharibika pale Kidatu na kusababisha mgawo. Circuit breaker tu - kisa hatuna reserve ya umeme bali tuna nakisi ya 150MW.
Madhara ya kukosa umeme ni makubwa mno na ndio yananitisha na hasa kwenye sekta ya viwanda (manufacturing) ambayo ndio pekee imebakia kutoumizwa na economic meltdown. Tunaposema giza watu wanafikiri ni giza la nyumbani. Hapana industrial production etc.
Ninapoyaona haya na sioni leadership being provided, ni bora umaarufu wangu ufutike wote lakini nchi yangu ibaki imara. Its a risk worth taking and i will triumph.
Kuhusu hili mimi nimenawa mikono, na sitacomment tena ila nitaendelea kuiombea Tanzania na Mungu akipenda tutasonga mbele tu ingawaje power ya maadui imeongezeka sababu wanatumia njia za kila namna kuwarubuni watu wapende wasipende, kwa kutumia hata mbinu chafu.
Personally sasa hivi nitaweka matumaini zaidi kwa wabunge wa CCM kama kina Mwakyembe, Seleli, Mama Kilango sababu wao wako kwenye firing lane kutoka mafisadi which them implies wanatutetea watanzania.
Hawa wapinzani nakuwa forced kuconclude kuwa ni opportunistic na walevi wa madaraka ambayo hata hawajayapata.
Upinzani wakweli utatoka CCM, kwa hiyo hata kama nafanya makosa kwenye hii conclusion potelea mbali, nitajua mbele kwa mbele, maana hawa wapinzani nimegundua kuwa wana misimamo yao wenyewe na hawatusikilizi sisi wananchi.
Kama wajanja wa humu JF tunaburuzwa hivi, wale ndugu zangu kule milimani si watatukanwa mchana kweupe.
Mzee ES naomba mkuu ufikishe ujumbe huko kwa hao wana CCM kina Mwakyembe, Mama Kilango na wengine kuwa sasa tutabase support zaidi kwao na mategemeo yetu yako kwao sababu wakitutupa na wao tutakuwa hatuna pa kwenda.
May God Almighty Bless Tanzania.