Mkandara,Mh. Dr. Slaa,
Mkuu nimekusikia sana tatizo bado unatumia siasa ktk ku solve tatizo hili..Mimi Mbongo na nimeishi miaka yote ya ujana wangu Bongo.. naelewa harufu mbaya ya mnyama hatari kama Simba bila hata kumwona..
Mimi sina haja ya kusoma hadidu za Zitto kwa sababu alivyoanza tu kasema alimwomba ruksa Spika..hapo tu tayari anaingilia kazi isiyokuwa yake kisha swala hili la Dowans ni swala ambalo yeye alitakiwa kukaa mbali kabisa nalo hasa upende huo!...Trust me, sioni tofauti yake na Masha ktk swala la vitambulisho hata kama kuna tofauti za miradi hii.
Sasa tuzungumze kama watu wazima. wewe kama kiongozi na pongine unayeunga mkono kamati ya Zitto nambie sababu ambazo wewe zimekuvutia ktk maamuzi hayo!..Kwa sababu mimi sioni kabisa argument yenye malengo mazuri.. nipe points zako wewe kutokana na hadidu hiyo maanake mimi sikuoina la maana kabisa kufikia maamuzi ya kuunga mkono ununuzi wa mitambo iliyochakaa..
...hoja kubwa hapa ni kuwa hatuna majibu kwa vile hatujui yaliyojadiliwa na Kamati ya Zitto na wala yaliyojadiliwa na Kamati ya Shellukindo. Ukitafakari sana, kuna majibu mengi yanahitajika hivyo, namna pekee ya kupata maelezo ya kina ni kukubali kwa Kamati hizi mbili zikae zikajadili kwa kina na Taifa tujulishwe. Vinginevyo hatuna namna ya kujua ukweli kuhusiana na suala hili zima.
4. Kwanini Bunge linataka kuingia mkenge? Hoja ya kuzikutanisha kamati za Bunge pamoja na Tanesco na serikali, ili kupata muafaka ninapata mashaka kwamba tunaweza kuwa tunatengeneza upenyo wa Bwana Ngeleja kuja kukwepa kusulubiwa iwapo mitambo hiyo itakuja kugundulika kuwa bomu. Bunge litakuwa halina nguvu ya kuihoji serikali kwamba kuna ufisadi umefanyika maana Bunge lilishiriki kutoa baraka na kuruhusu kuvunja sheria kwa kununua mitambo chakavu.
Hoja ya kamati mbili kukutana ni hoja ya kamati ya Mashirika ya Umma, sio hoja ya Serikali. Hoja hii imekuja baada ya kukataa kuingana na Kamati ya Nishati na Madini ambayo ilikwishasema kuwa serikali isinunue mitambo. Kamati ya Hesabu inasema hapana, tuwasikilize TANESCO ili kuona hoja yao na tusijikite kwa mitambo ya Dowans tu. Hakuna mbadala?
Nakubaliana nawe kuwa iwapo kamati za Bunge zitajiingiza katika mjadala wa tununue au tusinunue, likiharibika kwa uamuzi wowote, Bunge ndio litalaumiwa na serikali kutua mzigo. Kazi yetu ni Oversight
5. Mwaka juzi wakati wa semina ya mswada wa umeme ambao ilikuwa uwasilishwe na Mh. Karamagi wabunge walitaka kupata master plan ya umeme, na nilitarajia ndani ya hiyo master plan kungekuwa na hizi issues ambazo leo wanazileta na kuzifanya kuwa ni dharura. Hivi kwanini kamati haikumkumbusha Dr Rashid hilo?
Kamati ilizungumza kuhusu MasterPlan. Kimsingi hoja ya Masterplan ndio imeleta hoja zote hizi kwani miradi yote iliyopo kwenye masterplan iliyopangwa kumalizika mwaka huu haiwezi kumalizika.
- Kiwira walitakiwa waingize MW50 mwezi March, hawataingiza na 150MW mwezi Oktoba hawataingiza.
- Kinyerezi 240 MW haitaingia
- Upepo Singida mazungumzo bado yanaendelea na hayaishi na hivyo 50MW hazitaingia.
- Mtwara 300 MW Barrick wamejitoa due to global financial crisis
Net Group Solution wametoka miaka karibu 3 iliyopita, hakuna excuse kwamba eti TANESCO hawakuwa na mipango ya muda mrefu kwa kuwa walikuwa wanasubiri kubinafsishwa. Hapa naona wanatafuta excuse kila kona ili mradi hiyo mitambo iweze kununuliwa.
Mkandara,
Lakini hoja kubwa hapa ni kuwa hatuna majibu kwa vile hatujui yaliyojadiliwa na Kamati ya Zitto na wala yaliyojadiliwa na Kamati ya Shellukindo. Ukitafakari sana, kuna majibu mengi yanahitajika hivyo, namna pekee ya kupata maelezo ya kina ni kukubali kwa Kamati hizi mbili zikae zikajadili kwa kina na Taifa tujulishwe. Vinginevyo hatuna namna ya kujua ukweli kuhusiana na suala hili zima.
Kamati yangu haijalazimisha Dowans hata kidogo. Mjadala huu ndio umejikita huko. Maelezo yako ni mazuri na tuendelee na mjadala. Kuna maeneo haupo sahihi sana kwani unahitaji maelezo zaidi. Nilisema katika moja ya vikao vya kamati kuwa, ingekuwa wakati wa Mwalimu suala hili lingekuwa rahisi sana kwani tungetaifisha tu. Kwa sasa neno taifisha linaonekana sio zuri masikioni mwa 'investors' lakini ndivyo ingepaswa. Kamati yangu haikujikita hata kidogo kwa Dowans. Hiyo ni option mojawapo ambayo TANESCO wameitoa. Kamati ilijadili options kadhaa
- Kufast track Kinyerezi project (240MW)
- Kufast track Umeme wa Upepo Singida (50MW)
- Kuokoa Umeme wa Mtwara (300MW)
Na haya ndio masuala tulioomba kamati mbili zikutane na kujadili kwa pamoja na kuona ipi itaokoa mambo kwa haraka.
TANESCO wametaka kuongeza uwezo wao wa kuzalisha umeme hizo 100MW kwa haraka kwani tayari mitambo hiyo imeunganishwa katika gridi. Mitambo mipya kutoka GE etc tulijadili kuambiwa kuwa ni sawa lakini itachukua muda mrefu sana mpaka kufungwa na kwamba wanataka kuchukua mtabo wa 60MW kuupeleka Mwanza ili kukabili tatizo lililopo kule sasa hivi. Hivyo suluhisho la muda mrefu ni lazima liwepo na hapo ndio umuhimu wa kikao cha kamati mbili.
Ni muhimu tukumbuke kuwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita TANESCO lilikuwa specified company (shirika linalosubiri kubinafsishwa). Hivyo hapakuwa na uwekezaji wowote uliiofanywa. Hivyo sehemu kubwa ya matatizo tunayoyapata sasa yanatokana na maamuzi yetu kama nchi ya kisera.
Kuhusiana na IPTL. Mimi silinganishi bali ninaonesha kuwa kigezo cha sheria ya manunuzi (ambayo haitajwi ni kifungu gani hapa) itakwamisha pia mpango wa kununua IPTL na kuigeuza kuwa gesi. Ninaamini Two wrongs never make it a right. Kununua IPTL kutazuiwa na sheria hii ya manunuzi ijapokuwa uamuzi huo wa kununua mitambo chakavu itasaidia sana TANESCO kutatua tatizo lake la cash flow (tutaokoa $9m altogether kila mwezi kwa uamuzi huo wa kununua IPTL na kugeuza mitambo kuwa ya gesi).
Suala la nishati ya Umeme, kwa mwono wangu, ni suala linalohitaji mjadala uliotulia na wenye kuona picha kubwa (broader picture). Ndio maana Kamati yangu iliamua ilivyoamua.
Huyo mtalam aliyekuja kutathimini mitambo ya Dowans tuna uhakika gani kwamba alifanya kazi yake jinsi inavyopaswa? Tuna mifano mingi ya kununua vitu used ambavyo vimekuja kuwa mzigo kwa taifa, mfano ni ndege ya rais ambayo hata JK haitumii tena. Tusidanganyane kwamba mitambo ikikaguliwa tutaweza kuepuka kuingia mkenge.
Wakuu naomba nieleweshwe kidogo hapa hii inayoitwa mitambo ni majenereta tu au ni pamoja na switch gears, transformers, capacitor banks etc.??????
Dr.Slaa,
Mheshimiwa kwanza heshima mbele... nakusikia mkuuu na ningependa sana kujadili swala hili kwa fikra huru zaidi hasa pale napoona kiongozi wangu (Zitto) anajiingiza ktk mkenge ambao mimi nafahamu kuwa umepikwa..Nahofu kufikiria nje ya sanduku.. trust me.
Sina haja ya kusema mengi sana isipokuwa tu inanishangaza pale mtu kama Zitto anapokuja kwa jazba kwa sababu tu kuna mtu/watu wametumia vigezo au mifano ambayo hakuipenda kisha naye anarudia makosa yaleyale..
Kifupi Ununuzi wa mitambo ta Dowans ni kosa kubwa sana kisiasa na hata kufikiria tu kwamba hatuna njia isipokuwa wao.. kwa sababu ukisoma mwanzo wa mkataba mitambo hii iliagizwa kwa mkataba wa muda mfupi yaani miezi 24 kama sikosei..Na viongozi waliokuwepo madarakani walituambia kuwa hili ni tatizo la muda tu.. wananchi hatukutaka kabisa habari ya Richmond from day one na kama unakumbuka hapa JF tulianza kupiga kelele zetu..vijana wa Houston waliweka hadi picha za ofisi za Richmond na kadhalika, hao Richmond walikuwa hawana site wakaunda ya harakaharaka na kujihusisha na Boieng ili kutuzuga zaidi bahati vijana wetu waliendelea kufuatilia hadi ukweli ukawa wazi kabisa kuwa hili lilikuwa kanyaboya..
Sasa pamoja na yote hayo, matumizi ya mitambo hii ilikuwa ni ya muda mfupi tu, ajabu serikali (Tanesco) haikuweza kufanya lolote pamoja na jipu zima kupasuka kuiandaa nje ya mkataba feki..badala yake wakaingia ktk mkataba mwingine na Dorwans jambo ambalo nina hakika Tanesco walisukumwa na wanasiasa tena kama mwanzo.. Kuna taarifa kamili zinazoonyesha Lowassa akishauri mkataba uhamishiwe Dorwans.. badala ya kushauri tender mpya ifanyike.. Wapi hao Dorwans wametokea hatufahamu.. leo hii tujiingize katika kununua mitambo yao huku tumefukia vichwa vyetu mchangani kama mbuni kuficha ukweli kwamba mitambo hiyo ni ya Richmond sio Dorwans..Aliyenunua mitambo ni Richmond na ku sub contract kwa Dorwans hivyo mchezo bado upo palepale kwani mmiliki ni yule yule...
Hakuna kati yetu anayefahamu mkataba kati ya Richmond na Dowans, hakuna anayefahamu tofauti ya mmiliki wa Richmond na Dorwans.. ni jambo la kawaida kabisa hapa Ulaya kuuwa kampuni moja ukaunda nyingine..
Nakubaliana na maneno ya Zitto anaposema kwamba Tanesco wanahitaji hizo 100Kwt za umeme, well kama tunawadai basi tuendelee na contract yetu hadi fedha zetu zitakapo kwisha wakati huo huo tukiagiza mitambo yetu...ni jambo ambalo lilitakiwa kufanyika toka zamani na nadhani lilikuwepo ktk mpango wa serikali auTanesco wenyewe walipoweka makataba na Richmond kwa kuhitaji mitambo hiyo kwa miezi 24, kama haikufanyika basi ifanyike leo..Na kama Zitto anataka vijana hapa waende mbio kutafuta generators zenye uwezo zaidi ya hiyo ya Dorwans atupe kazi hiyo aone kama kweli mitambo hiyo itafika nchini baada ya mwaka 2009 kama wanavyodai wao.. Siemen wapo Tanzania, nakuombeni nendani ofisini kwao kamwone kijana mmoja anaitwa Alaf muulizeni kuhusiana upatikana wa mitambo hii kama kweli inaweza chukua miezi sita toka leo hii tunavyozungumza..
Kinachonipa shida mimi ni pale tunapotaka kununua mitambo hii kwa sababu tuna shida.. Ni sawa na kuposa mke kwa sababu una kiu (nyege) na hicho kiu ndicho kinatazamwa kama kigezo cha manunuzi badala ya kufikiria ni mke gani unayemhitaji na kwa sababu gani..
Nina hakika kabisa hakuna uchunguzi wa kina umefanyika kuziangalia hizo generators za dorwans (mke) badala yake tumefikira zaidi nyege za Tanesco hata kama kweli wanahitaji mke mwenye kizazi..
Kama nilivyosema hapo awali siwezi kununua mali yoyote ya mwizi hata kama naihitaji kiasi gani...nitakwenda kununua dukani..
Mkuu, Dr. W. Slaa, heshima mbele.
Kwanza niseme, kama siku zote, ahsante kwa kuja kujadili mambo nasi hapa, ukiwa mmoja wa viongozi wachache nchini, pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ambao wanajitolea kuhojiana moja kwa moja na wananchi. Binafsi nadhani kuna kujitoa muhanga fulani kwenye hadhi yako unapokuja kwenye jamvi la kila mtu hapa. Rais Kikwete jana Ikulu amegomba kwamba maoni juu ya serikali yake yatolewe kama anavyofanya Mzee Kawawa, ndani vyumba vya viyoyozi, maji ya chupa na usiri mkuu, na sio kwenye "vijiwe." Tafadhali usinunue maneno ya Rais, ukakitupa kijiwe chetu. Ahsante kwa hilo.
Sasa, Mkuu, mimi siamini wewe Dr. Slaa hujui yaliyoendelea ndani ya Kamati ya Kudumu ya Zitto Kabwe.
Kwanza, Kamati ya Kabwe imemaliza kazi ya kutathmini swala la TANESCO na mitambo ya Dowans, imetoa ushauri wake. Wajumbe nadhani hawafungwi na kanuni inayokataza kujadili mambo ya Kamati kabla haijamaliza kazi, kipengele 50 ( 4 ), na ndio mana hata Shelukindo, wa Kamati ya Kudumu ya madini anaongea wazi wazi. Mh. Kabwe nadhani anaweza kujadili haya mambo na wewe, kama ungetaka, na najua unataka, kujua.
Kabwe pia, kama wewe, ni kiongozi mwandamizi wa chama chako, CHADEMA, nyote mna kila sababu ya kushirikiana kisiasa, na la chini kuliko yote mnaloweza kufanya ni kuwasiliana. Lenu moja. Sasa ukisema Katibu Mkuu wa CHADEMA na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA hawaongei kuhusu siri walizonazo kuhusu shughuli au udhoofu wa serikali ya CCM, hususan yahusuyo Bunge ambalo nyote ni wajumbe, mimi sielewi, nataka kukataa.
Hilo la pili, lakini la tatu, zaidi ya ukaribu wa kichama ulionao na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ni kwamba ni watu wachache Tanzania, kama wapo, ambao wanapata nyeti na siri za serikali, mpaka "siri za kijeshi," achilia mbali za mabenki na ma akaunti ya mafisadi na nyeti nyingine za nchi zaidi yako wewe Dr. Slaa. Sasa leo utanambia eti hujui yanayoendelea kwenye Kamati ya Zitto? Umejua ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya "siri za kijeshi" utashindwa ya Kamati ya CHADEMA mwenzio? Wamarekani wanasema give me break Mr. Politician. Acha kumsafisha mwenzio kwa kukunjakunja mada eti hatujui yaliyotokea ndani ya Kamati ya Kabwe, tusubiri. Baada ya kupigana na "siri za kijeshi na madini" sasa na wewe umeanza kulea "siri za kamati na umeme"?
Isitoshe mna ukaribu wa binafsi. Wa kusafishana. Kama jana ulivyokuja kumsafisha hapa kabla hajaja kututukana mchana mchana kwamba wananchi hatujui chochote wala lolote, tusubiri atuambie. Amempiku Samuel Malecela wa CCM katika vitabu ya historia ya maneno fidhuli kwa wananchi. Kwamba tuna "stupidity," tuko Marekani na Ulaya tuna neema ya kutokatiwa umeme! Zitto wako huyo huyo ambae mwaka jana alitamka akiwa Detroit Marekani kwamba Watanzania waishio nchi moja tu ya ng'ambo wameiingizia nchi hela (dola milioni 450) mara sita zaidi ya faida iliyopatikana kwenye sekta ya madini kuanzia 2007 kwenda nyuma miaka 10 ( dola millioni 73 )! Leo aja kututukana? Uko tayari kumsafisha mwanasiasa mfurahisha halaiki kama huyo ndio utashindwa kuongea nae kuhusu ya serikali, na CCM , na Bunge na CHADEMA kweli?
Dr. Slaa, mmepata pata mafanikio upande wa upinzani miaka ya karibuni sasa msianze kuharibu kwa kutufanya - mpaka kutuita - stupid. Mnahitaji kuungwa mkono na wananchi ambao ndio kwaaaanza wanaanza kuelewa dhana nzima ya upinzani. Msianze kuwapoteza kwa siasa za usanii na kulindana na kusafishana; hiyo karata siku hizi hata CCM wameona inawalostisha, ndio maana hata Kikwete anawatema maswahiba na kuwatosa jela siku hizi. Sasa Dr. Slaa, si itakuwa matusi nikikwambia wapinzani muende kuangalia, kujifunza CCM?
Nyani ngabu,
Mkuu swala la miafrika ndivyo tulivyo ni ukweli unaokubalika, sisi ni WAJINGA (hatuna elimu) lakini sio wajinga hivyo mkuu wangu..Kweli tumeshindwa kutengeneza vitu hivyo basi iwe hata kuchagua kitu kizuri?..
Mbona ndio sifa kubwa ya Miafrika ktk kuchagua!..