Tatu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2006
- 1,143
- 375
Majuzi nilimsikia Dr. Mwakyembe akizungumza katika TBC kuwa Tanesco wasinunue mitambo ya Dowans. Hoja yake kuu ni kuwa wakinunua mitambo ya Dowans watakuwa wamekiuka taratibu za ununuzi. Hakutoa sababu nyingine yeyote ya kiuchumi.
Leo nimeskiliza Mh. Zitto Kabwe katika TBC hiyo hiyo. Yeye ameunga mkono ununuzi wa mitambo hiyo kwa sababu kuu tano za kiuchumi na kiutendaji:-
1. Mitambo hiyo ipo nchini na inazalisha umeme bila matatizo. Pia moja ya mtambo huo ni mpya kabisa.
2. Tanesco inaendeshwa kwa hasara kutokana na high capacity charges. Zaidi ya 80% ya mapato yake hutumika kununulia umeme toka kwa wazalishaji binafsi unaofikia 42% tu ya umeme wote unao gawiwa.
3. Hivi sasa Tanesco inaendeshwa kwa hasara. Ununuzi wa mitambo hiyo pamoja na mingine ya IPTL etc utaisadia Tanesco kuendeshwa kwa faida. Serikali/Tanesco imo katika mazungumzo na wazalishaji wote hao binafsi. Kwa hiyo, inaonyesha kuwa, zoezi hilo si la Dowans peke yake bali ndio sera ya serikali/Taneso hivi sasa.
4. Mitambo hiyo ikinunuliwa sasa itaepusha sokomoko la mgao wa umume baadae mwaka huu.
5. Katika sheria za manunuzi kuna kipengele cha waiver ikiwa kuna umuhimu wa kununua mitambo ambayo si mipya.
Sasa mimi najiuliza:-
1. Hivi kung'ang'nia kikataza Tanesco kununua mitambo hiyo kwa sababu tu ya kukiuka taratibu ambapo Mr. Zitto kisha eleza hapo kuwa kuna uwezekano wa waiver, ni kwa maslahi ya nchi au ni kwa maslahi ya kulinda heshima za kisiasa? Yaani kuonekana tu kama kichwa cha thread hii kuwa Dowans wataonekana wameshinda?
2. Surely katika jambo nyeti kama hili ni lazima mtu atoe hoja nzito za kiuchumi, kama alivyotoa Mr. Zitto. Sasa kweli hoja moja tu ya kukiuka taratibu ndio inatosha kuzuia project ya muhimu kwa taifa kama hii?
Jamani lazima tuwe serious. Tuachane na ubinafsi, chuki na kujijenga kisiasa na tuzingatie zaidi maslahi ya taifa na huduma kwa umma. I for one, hakuna kitu kinacho nikera na kunikasirisha kama kukatika kwa umeme.
tk,
I think all FISADI's like your last sentence. They will keep this argument about urgency and demand growth so that they can go ahead with the purchase.
So what's their plan for next year, 3yrs, 5yrs, 10yrs from now?
What was their forecast plan on 2006? Did they see demand growth at that time or this was an overnight spike?
We don't want to be fooled anymore.