Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
Je, amerejea CHADEMA? Tusubiri tuone




Aliyewahi kuwa Katibu wa CHADEMA Taifa na baadaye Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbrod Slaa kwa mara ya kwanza jana Jumapili amehudhuria mkutano wa Chadema Wilaya ya Karatu na kuahidi atashirikiana na chama hicho kudai Katiba mpya.

Dkt. Slaa aliondoka CHADEMA akiwa Katibu Mkuu wakati wa mchakato wa uchaguzi Mkuu mwaka 2015 baada ya chama hicho, kumteua Edward Lowassa kugombea urais kupitia chama hicho.

Dkt. Willibrod Peter Slaa anasema:
“Mimi sina chama, nawaambia CCM ili kuwasaidia, kuna sababu gani ya kuchagua kama hawajirekebishi, lakini kwa sasa twende na chama ambacho angalau kinaonesha kina wafikiria na kuwajali Watanzania hiyo ni katika uchaguzi unaoakuja, maandalizi yaanza ndani ya chama

“Hatua ya pili twende katika mikutano ya Katiba, CCM wanasema Katiba itakuletea Uji, Wali au chakula kingine chochote nyumbani kwako? Niwaambie Katiba ni kila kitu.

“Ugali unaoupata maamuzi ya huo bei ya ugali na chakula kingine unachopata inatokana na Katiba.

“Katiba ya sasa imetoa mamlaka yote kwa Rais, simlaumu Rais peke yake bali nalaumu mfumo uliotengeneza Katiba.”

SLAA NI PROFESA
Mimi ni Profesa wa Siasa, kazi yangu ni kutoa ushauri na nitawaelekeza, Profesa amepita mengi na magumu ana uzoefu

Ndio maana naongea kwa uhuru kabisa katika Nchi yangu najua Sheria najua haki zangu na hakuna wa kuniuliza kwanini nazungumza na CHADEMA, nitasema bila kumung’unya maneno

Bei ya Mchele inapanda licha ya kuwa tunalima hapahapa Nchini, bei ya nyama ya ng’ombe nayo inazidi kupanda
 
Je amerejea Chadema? Tusubiri tuone

View attachment 2531118
Kama ni kweli basi mbowe na wahuni wenzie wamekubali kuwa chadema ipo shimoni sasa wanatafuta mtu wa kukitoa chama shimoni.

Wakumbuke huyo jamaa alikuwa mfuasi wa siasa za magufuli tuliwaambia chadema siku nyingi kuwa kumpinga mzalendo ni kujichimbia shimo wenyewe wakabisha.

Chadema washukuru kuwa sasa hivi hakuna chama chochote cha upinzani chenye kubeba legasi ya nyerere wala magufuli vinginevyo wangebaki mdomo wazi maana kifo cha hicho chama kinge vunja rekodi ya vifo vyote
 
Back
Top Bottom