Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,856
- 12,096
Fuatilia kinachojiri kwenye ufunguzi wa maneno ya nanenane Mkoani Mbeya, leo Agosti 1, 2023 ambapo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ni mgeni Rasmi.
===
Tulia Ackson
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema Bunge litaendelea kufanya kazi na Serikali katika kuishauri na kuisimamia katika matumizi yake.
Amewatoa hofu watanzania kuhusu uwekezaji unaofanywa na Serikali kwenye maeneo mbalimbali.
Wananchi wanapaswa kuiamini Serikali kwani Rais Samia ana nia njema na watanzania. Anapaswa kutiwa moyo anapobezwa na baadhi ya watu.
Aidha, CCM ndicho chama chenye ilani inayoongoza Serikali, wanaobeza waachwe maana hawana walichoahidi wananchi. Hatuwezi wote kuwa walalamikaji, na wengine wanaleta hoja mufilisi za kibaguzi, tusikubali kugawanywa.
Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais
Mhe. Waziri hapa (Bashe) Mhe. Rais ameonesha uvumilivu wa hali ya juu sana, ameonesha ukomavu wa hali ya juu kabisa. Sasa alifungua uwanja wa siasa katika taifa letu ili tufanye siasa za kistaarabu.
Matusi sio utamaduni wa Mtanzania. Sasa, wale ambao wanatumia fursa waliyopewa badala ya kujadili hoja, badala ya kujadili maendeleo ya mama Tanzania wanaishia kutumia lugha za hovyo, tena dhidi ya kiongozi mkuu wa nchi nawasihi kiungwana waache.
Nawasihi tena, wengine wanasema makamu kanyamaza, inahitaji busara kubwa. Kwa hiyo wasitupeleke huko, watu wanaona yanayoendelea katika nchi jirani, vurugu barabarani kila siku badala ya kuhangaika na maendeleo ya wananchi. Hatutaki kwenda huko.
Nadhani salamu zao zimefika.