Dkt. Mpango: Wanaotumia lugha za ovyo dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Nchi nawasihi kiungwana waache. Yanayoendelea nchi jirani watu wanayaona

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Fuatilia kinachojiri kwenye ufunguzi wa maneno ya nanenane Mkoani Mbeya, leo Agosti 1, 2023 ambapo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ni mgeni Rasmi.

===

Tulia Ackson
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema Bunge litaendelea kufanya kazi na Serikali katika kuishauri na kuisimamia katika matumizi yake.

Amewatoa hofu watanzania kuhusu uwekezaji unaofanywa na Serikali kwenye maeneo mbalimbali.

Wananchi wanapaswa kuiamini Serikali kwani Rais Samia ana nia njema na watanzania. Anapaswa kutiwa moyo anapobezwa na baadhi ya watu.

Aidha, CCM ndicho chama chenye ilani inayoongoza Serikali, wanaobeza waachwe maana hawana walichoahidi wananchi. Hatuwezi wote kuwa walalamikaji, na wengine wanaleta hoja mufilisi za kibaguzi, tusikubali kugawanywa.

Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais
Mhe. Waziri hapa (Bashe) Mhe. Rais ameonesha uvumilivu wa hali ya juu sana, ameonesha ukomavu wa hali ya juu kabisa. Sasa alifungua uwanja wa siasa katika taifa letu ili tufanye siasa za kistaarabu.

Matusi sio utamaduni wa Mtanzania. Sasa, wale ambao wanatumia fursa waliyopewa badala ya kujadili hoja, badala ya kujadili maendeleo ya mama Tanzania wanaishia kutumia lugha za hovyo, tena dhidi ya kiongozi mkuu wa nchi nawasihi kiungwana waache.

Nawasihi tena, wengine wanasema makamu kanyamaza, inahitaji busara kubwa. Kwa hiyo wasitupeleke huko, watu wanaona yanayoendelea katika nchi jirani, vurugu barabarani kila siku badala ya kuhangaika na maendeleo ya wananchi. Hatutaki kwenda huko.

Nadhani salamu zao zimefika.
 
Fuatilia kinachojiri kwenye ufunguzi wa maneno ya nanenane Mkoani Mbeya, leo Agosti 1, 2023 ambapo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ni mgeni Rasmi.

===

Tulia Ackson
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema Bunge litaendelea kufanya kazi na Serikali katika kuishauri na kuisimamia katika matumizi yake.

Amewatoa hofu watanzania kuhusu uwekezaji unaofanywa na Serikali kwenye maeneo mbalimbali.

Wananchi wanapaswa kuiamini Serikali kwani Rais Samia ana nia njema na watanzania. Anapaswa kutiwa moyo anapobezwa na baadhi ya watu.

Aidha, CCM ndicho chama chenye ilani inayoongoza Serikali, wanaobeza waachwe maana hawana walichoahidi wananchi. Hatuwezi wote kuwa walalamikaji, na wengine wanaleta hoja mufilisi za kibaguzi, tusikubali kugawanywa.

Wazanzibari wanaita muhali!
Tulia usipofanya kazi yako ipasavyo, usilaumu wanaochukua kazi yako!

Nia ni nchi iwe moja bila makando kando yoyote, ila siungi mkono abisa wanaomtukana Rais wetu aliyeleta utengamano baada ya mwendazake.

Kateleza, lakini ni kwa sababu ya kuendekeza uchawa.
 
Jibuni hoja kenge maji nyie..

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Yeye mwenyewe hajausoma huo mkataba zaidi ya usanii
 
Duh

Ova
 
Nchi jirani kuna nini?? Imekuaje tumekua na diplomasia ya chokochoko kila kitu nchi jirani, viongozi jitafakarini mnaleta mpasuko wa kidiplomasia
 
Back
Top Bottom