Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Vitambulisho vya Machinga sio lazima, acheni uongo

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Mgombea Urais kupitia CCM Dkt John Magufuli amesema, watu wanazusha kwamba Machinga wanalazimishwa kuwa na vitambulisho, sio kweli. Vitambulisho sio lazima.

''Vitambulisho havilazimishwi ni lazima itolewe elimu kwa wanaoshiriki kwenye vitambulisho ili wakafanye bishara mahali popote, tunataoa vitambulisho ili wanananchi hawa wenye biashara ndogondogo wasisumbuliwe''. Dkt John Magufuli, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

Aidha amewataka wasaidizi wake wakiwamo wakuu wa wilaya kuendelea kuzingatia maelekezo yake ni wafanyabiashara wa aina gani wanaohitajika kuwa na vitambulisho vya machinga.

Vitambulisho hivyo humwezesha mjasiriamali kufanya baishara bila kutozwa kodi na halmashauri kwa kipindi cha mwaka mzima jambo ambalo hutajwa kuwa linalenga kuwainua wafanyabiashara wa mitaji midogo.

''Tulianzisha vitambulisho hivi kwaajili ya kuwalinda wafanyabiashara wadogo wadogo baada ya kuona wanasumbuliwa na halmashauri, ukiwa na kitambulisho chako utafanya biashara mahali popote Tanzania, vitambulisho haviwezi vikatafutwa kwa bunduki, vitambulisho mtu anakata mwenyewe ni Sh 20000'' Dkt John Magufuli, Mgombea urais kwa tiketi ya CCM.
 
Yeah, ameyasema hayo muda mfupi uliopita huku akisisitiza elimu itolewe juu ya suala hilo.

Ni katika mfululizo wa kujibu Tundu Lissu.

Nakumbuka kina Ally Hapi walijiapiza kuwa hawajajiandaa kushindwa kumaliza vitambulisho walivyopewa wawakabidhi wafanya biashara ndogo ndogo kwa malipo ya fedha halali shilingi elfu ishirini tu za kitanzania kwa mwaka.

My take!
Wakuu, kama tutakuwa serious kweli basi hili suala la vitambulisho vinavyolopiwa Tshs. 20000 ni wizi mtupu maana hiyo kodi haina draft yoyote kisheria! Yani hata ukienda mahakamani au bungeni hayo malipo hayatambuliki kisheria! Huu ni wizi wa mchana kweupe.

Mbaya zaidi wala haijuilikani inakoenda, mahesabu yake, ukaguzi wa matumizi yake. Yani ni mambo ya hovyo hovyo tu ya uongozi wa ufalme.

Sijui Bunge la Ndugai tulililipa ili liifanyie nini nchi. Huyu Spika Mungu atakuja kumpa funzo maana hakuwahi kulinda hadhi ya bunge lake!
 
Hahahhh nacheka utafikiri mazuri. Jiwe umeona umekusanya pesa za maskini kwa ajili ya kampeni zoezi umekamilisha ndio unakuja na hadithi za alfu ulelaulela.

Acha kuwafanya watu wajinga, Umeona Tundu Lissu anawafumbua watu macho ndio unakuja na gear hizi
Muwe na soni kidogo khaaaa!
Hela yote wamezitumia kusambaza mapicha yao kila kona.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Yeah, ameyasema hayo muda mfupi uliopita huku akisisitiza elimu itolewe juu ya suala hilo.

Ni katika mfululizo wa kujibu Tundu Lissu.

Nakumbuka kina Ally Hapi walijiapiza kuwa hawajajiandaa kushindwa kumaliza vitambulisho walivyopewa wawakabidhi wafanya biashara ndogo ndogo kwa malipo ya fedha halali shilingi elfu ishirini tu za kitanzania KWA MWAKA.
Kweli umebanwa Magu! Ulisema ukawatishia kuwa RCs, DCs wasipouza vitambulisho watafukuzwa kazi! Nao ili wasifukuzwe, wanawabana wamachinga... hiyo imeshakuwa lazima
KWELI JIWE UMESHIKWA PABAYA johnthebaptist
 
Yeah, ameyasema hayo muda mfupi uliopita huku akisisitiza elimu itolewe juu ya suala hilo..
It is more than too late. Yaani mtu alishafanya "overwhelming demage" kwa walalahoi waliokuwa wengi, halafu leo ndio anakuja na kauli nyepesi namna hiyo! One term president, inatosha kwa maumivu uliyokwisha yaleta kwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom