Dkt. Leonard Akwilipo: Wanafunzi waliopata mimba Tanzania kurejea masomoni kupitia vyuo vya maendeleo ya wananchi

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
834
1,000
Serikali ya Tanzania imetangaza kuwaruhusu wanafunzi waliokatiza masomo yao kwa kwasababu ya kupata mimba kurejea masomoni kupitia vyuo vya maendeleo ya wananchi.

Akizungumza na wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi nchini humo, Katibu mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk Leonard Akwilapo amewataka wakuu hao wa vyuo kuhakikisha kuwa wanafunzi wa kike walioshindwa kuendelea na masomo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba wanarudi na kuendelea na masomo. Amewataka wakuu hao wa vyuo kutekeleza agizo hilo la kudahili wanafunzi hao kupitia mpango wa elimu haina mwisho ifikapo mwaka 2022.

Pamoja na kutaka vyuo vyote vya maendeo ya wananachi viwe vimesajiliwa kama vituo vya kufanyia mitihani ya kidato cha pili na kidato cha nne, amesema hatua hiyo ya kurejesha wanafunzi wa kike waliokatiza masomo yao yanatokana na majadiliano ya muda mrefu ya wizara hiyo na benki ya dunia.

Elimu

Katibu mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk Leonard Akwilapo

'Tulikuwa na mabishano mazungumzo marefu kwenye mpango wa kuimarisha na kuboresha elimu ya sekondari hapa nchini, moja ya makubaliano , ilikuwa ni kutoa fursa kwa wasichana ambao wamekatiza masomo kwa njia yoyote ile, wapate fursa ya kurudi na kuendelea na masomo, na tukasema tutatumia vyuo vya maendeleo ya wananchi, lazima tuanze hatuna uwanja, sio suala la kujadiliana, mambo mengine ya walimu mtatuachia sisi', alisema Dk. Akwilapo.

Kwa mujibu wa maelezo hayo, wanafunzi hao watarejea darasani katika vyuo 54 kuanzia mwakani, ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano ya kuboresha elimu ya sekondari pamoja na kuwapa fursa wasichana waliokatiza masomo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba kupata haki ya elimu.

Aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli alipiga marufuku wanafunzi wanaopata mimba mashuleni kuendelea na masomo ya shule ya msingi na sekondari hali iliyozua mijadala na makelele kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu nchini na nje ya nchi hiyo.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania Zitto Kabwe aliwahi kuiandikia Benki ya Dunia kusitisha kuikopesha Tanzania dola milioni 500 za elimu kabla ya mabadiliko ya kisera kufanyika.

Vyama vya upinzani nchini Tanzania na wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo na wa kimataifa wamekuwa wakitishia shinikizo la kutotolewa kwa mkopo huo mpaka pale Tanzania itakaporuhusu wanafunzi wanaopata ujauzito waruhusiwe kuendelea na mfumo rasmi wa elimu.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
9,970
2,000
Hivyo vyuo viko wapi, viko mikoa gani, mwanafunzi wa kijijini huko ndanindani atavifikiaje, atanufaikaje na elimu bure, watoto wakiwa mbali na nyumbani nani atagharamia malazi yao?

Hawa watoto inabidi warudi shule zilezile zilizoko karibu yao. Mimba si ugonjwa. Tuonee aibu tendo lakini tusionee aibu mimba wala kumchukia mtoto aliyeko tumboni
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,547
2,000
Hivyo vyuo viko wapi, viko mikoa gani, mwanafunzi wa kijijini huko ndanindani atavifikiaje, atanufaikaje na elimu bure, watoto wakiwa mbali na nyumbani nani atagharamia malazi yao...
Si vyuo kitu. Na hii ina maana msichana yeyote atakaesoma kwenye "vyuo" hivyo siku zote atatambulika kama ni mmoja wa wale waliopata mimba wakiwa wanafunzi. Hii ni fig leaf tu.

Binti aliyekuwa akiongoza darasani na ambae kweli ni potential ataishia kujifunza ufundi cherehani! Na frustration hizo ndio zitawapelekea kuongeza watoto maana wanajua jamii haiwataki!

Amandla...
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,547
2,000
Hivyo vyuo viko wapi, viko mikoa gani, mwanafunzi wa kijijini huko ndanindani atavifikiaje, atanufaikaje na elimu bure, watoto wakiwa mbali na nyumbani nani atagharamia malazi ...
Watakaoenda huko ni watoto wa wananchi wa kawaida tu. Watoto wa wenye nazo wataendelea na masomo katika shule nzuri tu.

Amandla...
 

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
3,886
2,000
Si vyuo kitu. Na hii ina maana msichana yeyote atakaesoma kwenye "vyuo" hivyo siku zote atatambulika kama ni mmoja wa wale waliopata mimba wakiwa wanafunzi. Hii ni fig leaf tu. Binti aliyekuwa akiongoza darasani na ambae kweli ni potential ataishia kujifunza ufundi cherehani! Na frustration hizo ndio zitawapelekea kuongeza watoto maana wanajua jamii haiwataki!

Amandla...
Kwani hivi so PM alitoa amri Ile elimu ya watu wazima irudishwe na mkazo uwepo kwa hawa mabinti watakaopata ujauzito pindi watakapojifungua wapate fursa ya kusoma kawaida na kuendelea kimasomo?
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,734
2,000
Si vyuo kitu. Na hii ina maana msichana yeyote atakaesoma kwenye "vyuo" hivyo siku zote atatambulika kama ni mmoja wa wale waliopata mimba wakiwa wanafunzi. Hii ni fig leaf tu. Binti aliyekuwa akiongoza darasani na ambae kweli ni potential ataishia kujifunza ufundi cherehani! Na frustration hizo ndio zitawapelekea kuongeza watoto maana wanajua jamii haiwataki!

Amandla...
Mimba ina stigma kiasi hicho?
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,547
2,000
Kwani hivi so PM alitoa amri Ile elimu ya watu wazima irudishwe na mkazo uwepo kwa hawa mabinti watakaopata ujauzito pindi watakapojifungua wapate fursa ya kusoma kawaida na kuendelea kimasomo?
Sidhani kama ni hivyo Mkuu. Nia hapa ni kuwatenga ili wasiwaharibu binti zao ambao wanajidanganya kuwa ni malaika.

Amandla...
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
117,686
2,000
UPUUZI MTUPU! Watoto wa waheshimiwa watakaopata mimba hawatatia mguu kwenye vyuo hivi vya hovyo. Watalipiwa na wazazi wao kufanya abortion na kuendelea na masomo yao katika shule walizokuwepo.
 

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
3,886
2,000
Sidhani kama ni hivyo Mkuu. Nia hapa ni kuwatenga ili wasiwaharibu binti zao ambao wanajidanganya kuwa ni malaika.

Amandla...
Hao mabinti zao wanaoshinda kwenye ma-bar makubwa wanalewa kila siku kushinda hata baba zao? Wanajidanganya tu. Mtoto ni mtoto tu, ukishakuwa mzazi unakuja kuelewa haya mambo hayahitaji stigmatism.
 

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,788
2,000
Huyo Mzee ukimtazama sura anaonekana anatangaza tu lakini hajalipenda kabisa Hilo jambo kama mzazi.

Mzazi anayelishabikia hili swala kwakweli hajali future ya mwanae wa kike.
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,547
2,000
Wamewanyenyepaa watakaopata mimba, utaskia kile chuo cha waliopata mimba wakiwa shuleni.
Kabisa Mkuu. Na jamaa wataenda kujizolea tu kwa sababu tayari wameharibika. Hapo ni pamoja na walimu wao.

Tunasahau wengi wa watoto hawa wanapata mimba baada ya kubakwa ( kutembea na mtoto alie na umri chini ya umri wa consent ni kumbaka hata kama alikubali) kwa hiyo wataadhibiwa mara mbili.

Amandla...
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,580
2,000
UPUUZI MTUPU! Watoto wa waheshimiwa watakaopata mimba hawatatia mguu kwenye vyuo hivi vya hovyo. Watalipiwa na wazazi wao kufanya abortion na kuendelea na masomo yao katika shule walizokuwepo.
Sio abortion tu, hata kama wakizaa watafanyiwa mipango warudi shule hizi hizi walikopatia mimba.
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,547
2,000
Hao mabinti zao wanaoshinda kwenye ma-bar makubwa wanalewa kila siku kushinda hata baba zao? Wanajidanganya tu. Mtoto ni mtoto tu, ukishakuwa mzazi unakuja kuelewa haya mambo hayahitaji stigmatism.
Wale wana access ya contraceptives na mambo yakiharibika wanaitoa fasta bila madhara yeyote. Ikishindikana na akazaa basi mtoto atachukuliwa na bibi yake na yeye atapelekwa Kenya au Uganda kuendelea na shule.

Amandla...
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,580
2,000
Hawa jamaa wanaenda kutengeneza tatizo jingine juu ya tatizo, hiki wanachotaka kufanya kitakuwa kibaya sana kwenye psychology ya hawa watoto, wengi wao wanaweza hata wasimalize hivyo vyuo, watanyooshewa vidole kote watakapopita.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom