Wanafunzi wa Tanzania 13 waliopata ufadhili wa Masomo nchini Poland wanyimwa Visa na Ubalozi

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Naomba kuiambia serikali kupitia Wizara ya Elimu na Wizara ya mambo ya nje ,kuingilia kati suala hili la wanafunzi wetu waliopata ufadhili wa Elimu (Master's Degree ) nchini Poland.

Serikali ya Poland ina Program inaitwa NAWA- Stefan Banach Scholarship. (The Polish National Agency for Academic Exchange) tangu 2018 ambapo huwa inatoa ufadhili wa Elimu ya Juu kutoka nchi mbalimbali.

Nchini kwetu Tanzania Mwaka huu 2024 vijana wetu 13 wamepata ufadhili huu kwenda kusoma Poland chuo cha Warsaw "University Of Technology " ngazi ya Uzamili (Master's degree). Ambapo wanatarajiwa kuanza Masomo tarehe 19/Februari/2024.

Changamoto iliyopo hadi sasa ni ubalozi wa Poland nchini Tanzania kuzuia kutoa Visa kwa vijana hawa ikiwa tayari walifanikiwa kufanya Interview ya visa tangu tarehe 19 Januari 2024 na Ubalozi wakaahidi Visa zao zitatoka ndani ya siku 14 tu.

Jambo la kushangaza hadi leo hii ni siku takribani ya 25 wanazungushwa na Ubalozi wa Poland na hawatoi majibu yeyote ya kueleweka. Mara ya Mwisho Ubalozi wa Poland waliwaambia vijana wakate tiketi kabisa za ndege ili kuondoka tarehe 18 Februari 2024 yaani siku ya kesho ,Vijana hawa 13 walikata tiketi kabisa wakambiwa waende Jana Ijumaa tarehe 16 Februari kuchukua Visa ila walienda na hawakupewa.Na hivyo leo siku ya J.Mosi Ofisi hazifunguliwi hadi J.tatu na Safari ya walipaswa kuondoka kesho tarehe 18.

Vijana wote wa nchi Jirani waliopata ufadhili huu tayari wameondoka ila vijana wa Kitanzania wanazungushwa kwanini ? . Naomba Wizara ya Elimu ,Wizara ya Mambo ya ndani muingilie suala hili ili vijana hawa wapewe Visa wawahi masomo haraka yanayoanza tarehe 19 Februari 2024 . Lakini hasara ya tiketi kwa hawa vijana inapaswa ilipwe na Ubalozi wa Poland au Serikali yetu iwasaidie kulipa gharama za tiketi.

Natarajia serikali itafanyia kazi suala hili .

Abdul Omary Nondo.
 
Mwafrika kashindwa kujenga nchi yake sasa analilia kwenda kwa Mzungu aliyepambana kujenga nchi yake kwa akili mingi.

Waafrika tuna uwezo mdogo wa akili ndio maana kitu cha maana kwetu ni kupata madaraka, kuua yeyote anayetishia nafasi yetu, kujipendekeza na wizi.

Hao watoto watulie home kwani Poland nao wanalilia kuja Tanzania?
 
kuna watu nchi hii ni wajinga hadi aibu, viza siyo haki bali ni hiari ya nchi husika, kama wamewanyima viza ya poland maana yake ni kwamba hawawataki huko, sasa unataka raisi aingilie nini? hakuna sheria inayolazimisha upewe viza ya kwenda nchi nyingine …
 
Iliwa ufadhili umetolewa na Poland na Ubalozi wa Poland ndo wamekataa kutoa visa hili siyo suala la kuleta mtandaoni, hata serikali unayoililia tayari itakuwa inajua sababu, hivo kuweni Wapole na kuwa hili suala limeletwa Abdul nina wasiwasi wote kumi na tatu ni kina Abdul, Hamis, Huisen, Faudhia, Makame nk.

Hivo sababu zipo
 
Iliwa ufadhili umetolewa na Poland na Ubalozi wa Poland ndo wamekataa kutoa visa hili siyo suala la kuleta mtandaoni, hata serikali unayoililia tayari itakuwa inajua sababu, hivo kuweni Wapole na kuwa hili suala limeletwa Abdul nina wasiwasi wote kumi na tatu ni kina Abdul, Hamis,Huisen, Faudhia, Makame nk. Hivo sababu zipo
Wamewashtukia uenda wakawa magaidi! Wavaa makubasi sio watu wa kuwaamini!
 
Wana haki ya kuiomba serikali ishughulikie tatizo hilo mara moja, ili vijana wetu waifuate Elimu huko Poland!
Pili, kama hawana nia ya kuwapa viza, warudishiwe nauli zao kama muda wa Departure utakuwa umepita!
 
Mwafrika kashindwa kujenga nchi yake sasa analilia kwenda kwa Mzungu aliyepambana kujenga nchi yake kwa akili mingi.

Waafrika tuna uwezo mdogo wa akili ndio maana kitu cha maana kwetu ni kupata madaraka, kuua yeyote anayetishia nafasi yetu, kujipendekeza na wizi.

Hao watoto watulie home kwani Poland nao wanalilia kuja Tanzania?
Naona mwafrika katype hapa kwa keyboard iliyotengenezwa na mzungu..!!

Tuna safari ndefu sana yaani..!! Mwamfrika anamcheka mwenzake kuwa analilia kwenda kwa wazungu, lakini kicheko hicho anakifikisha kwa huyo mwenzake kwa kutumia vitu vya mzungu..!!
 
Back
Top Bottom