Serikali Kutenga Fedha Ujenzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Kwenye Mikoa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
"Je, ni lini Serikali itakipandisha hadhi Chuo cha Maendeleo ya Jamii Musoma ili kiweze kutoa Shahada" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum (Vijana Taifa)

"Ili Chuo kiweze kufikia elimu kwa ngazi ya Shahada kinatakiwa kiwe na ithibati kamili n vigezo stahiki ikiwemo miundombinu ya kutosha, kutoa kozi husika, rasilimali watu ya kutosha na yenye sifa stahiki na bodi ya uendeshaji" - Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

"Wizara itaendelea kushirikiana na wadau kufanya tathmini ya kina kuhusu lini kozi hiyo ianze hasa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya soko la ajira kwa wahitimu wa Shahada" - Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

"Katika Chuo, wanafunzi wanapata tabu sana maeneo ya kuishi ili kupata taaluma pale. Ni upi mpango wa Serikali kuhakikisha inajenga mabweni ili wanafunzi wapate sehemu ya kukaa?" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum (Vijana Taifa)

"Katika Kanda ya Kaskazini, mikoa yote hakuna Chuo cha Maendeleo ya Jamii. Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Chuo cha Maendeleo ya Jamii katika Jimbo la Hai ambapo tayari tumeshapanga eneo la kujenga?" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai.

"Tunatambua kuwa umuhimu wa miundombinu endelevu katika kujenga mabweni ya wanafunzi katika Vyuo. Serikali itaendelea kutenga rasilimali fedha ili kuendelea kujenga mabweni katika kila sehemu ya Vyuo ili wanafunzi wapate mahali pa kuwa na Maendeleo mazuri na kuishi maeneo ya karibu na Shule" - Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

"Ushauri wake tumeupokea na tunawapongeza wana Jimbo la Hai kuwa na kiwanja cha kujenga Chuo cha Maendeleo ya Jamii. Wameona umuhimu wa Vyuo hivi. Wizara itaendelea kutenga fedha katika mwaka wa fedha 2024-2025 kuona vipi tunajenga Chuo ili wananchi wawe na Chuo katika Mkoa wao" - Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

 
Back
Top Bottom