Diva aomba kurejea Clouds Media, apewa sharti la kwenda kufanya kazi Wasafi FM. Kutambulishwa hivi karibuni

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,635
2,000
Wasalaam wana jamvi.

Baada ya Mtangazaji Diva kuacha kazi kwa mwaka sasa ni rasmi kurejea tena.

Baada ya kukaa muda mrefu bila kufanya kazi na uku hakuna media iliyomfata kutaka kufanya nae kazi baada ya kukaaa muda mrefu nje ya utangazaji.

Mtangazaji Diva aliandika barua kwa kusaga kuomba kurejea kazini na aliomba arejeshwe na kukiri kuna sehemu alikosea na kuahidi kujirekebisha.

Hivi karibuni Msanii Diva alijibiwa barua yake na kutakiwa kwenda kufanya kazi kwenye kituo cha Wasafi FM ambacho nacho kinamilikiwa na Joseph Kusaga.

Ni uamuzi ambao ulifikiwa baada ya kuambiwa kuwa nafsi yake amepewa mwingine kule lakini akapewa task ya kwenda kukuza kipindi kama cha ala za roho kule Wasafi FM kwani media zote ni za baba mmoja.

Hivi karibu Diva alikutanishwa na Diamond na kutambulishwa na wakakubaliana kuandaa kipindi na kuambiwa wafanye kazi wao ni vijana wasisikilize maneno ya watu, hivyo Diva alisha andaa kipindi kitakachoanza kurushwa Wasafi FM ambayo inamilikiwa na Joseph Kusaga.

Hongera Diva and welcome back.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom