Wasafi Media Mtegoni. Diamond, Kusaga wavurugana

Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
31,530
65,290
IMG_5080.jpeg

Wakurugenzi wa Wasafi Media, Joseph Kusaga na Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ wanaripotiwa kukosa maelewano kati yao juu ya uendeshaji wa media hiyo inayomilikiwa na wawili hao.

Chanzo ni TRA
Diamond ambaye amekuwa akitafutwa na maafisa kodi kwa muda mrefu, huku yeye akitumia 'janja janja' kuwakwepa, maafisa kodi hao wamehamishia majeshi kwa Joseph Kusaga.

Joseph Kusaga ambaye majukumu ya uendeshaji amemwachia Diamond, amekuwa akimpigia simu mara nyingi bila mafanikio.
Hivyo Diamond anawakwepa maafisa kodi, na huku simu za Kusaga pia hapokei.

Kusaga achoshwa na mabifu ya Diamond!
Inaarifiwa kuwa Kusaga amekuwa akilalamika mara nyingi juu ya mabifu ya Diamond na watu wengi ambayo yanaikwamisha Wasafi Media kukua.

Wakati anaanzisha media hiyo 2016, alikuwa na malengo makubwa ya kuikuza kuwa kubwa pengine kuizidi Clouds Media ambayo ni mali ya familia yao. Hivyo kupitia umaarufu wa Diamond alitegemea kuvuna wasikilizaji kutoka kila pembe ya nchi jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limefanikiwa ila kikwazo kikiwa ugomvi wa Diamond na watu wengi ambao wengi hutumia mabifu hayo kama fursa ya kuikwamisha Wasafi Media.

Kusaga amgeukia Ali Kiba…
Habari za uhakika ni kwamba mastermind huyo wa biashara za vyombo vya habari na nyinginezo lukuki, ameelekeza nguvu zake kwa hasimu wa Diamond, Ali Kiba.

Wawili hao (Kusaga na Ali) wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha masuala muhimu likiwemo jina rasmi la kutumika kuitambulisha Media hiyo.

Kupitia chanzo changu makini nimefanikiwa kunasa jina linalopewa kipaumbele, Kings Media (Kings TV & Kings FM).

Pia watangazaji ambao tayari wameshawekwa kwenye list ni Abdallah Ambua ‘Dullah Planet’ aliyeng’oka EATV na EA Radio hivi karibuni, pamoja na Khalid Mohamed ‘TID’.

Kusaga na utajiri wa frequencies!
Kwa wafuatiliaji wa masuala ya media hasa radio, watakuwa wanafahamu ya kwamba hivi sasa hakuna frequency mpya hapa jijini Dar Es Salaam.

Yaani kwamba ukitaka kuanzisha redio huwezi kupata mawimbi ya kukuwezesha kusikilizwa Dar, labda ununue (frequency) ambayo inamilikiwa na wengine kisha uibadilishe kuwa redio yako.

Wajanja wa mjini wamezihodhi, akiwemo Joseph Kusaga ambaye anaarifiwa kuwa nazo kwa idadi ambayo haifahamiki.

Kupitia chanzo changu nyeti,

Nifah.
 
View attachment 2929146Wakurugenzi wa Wasafi Media, Joseph Kusaga na Nassib Abdul ‘Diamond Platinumz’ wanaripotiwa kukosa maelewano kati yao juu ya uendeshaji wa media hiyo inayomilikiwa na wawili hao...
Hiyo Paragraph ya mwisho uwongo,Frequency ni mali ya TCRA yy ndiye anaye panga na kuengineer na ukitaka nenda pale TCRA Frequency bado wanazo na ukimzingua anakunyang'anya Frequency zake.
 
Walugaluga kama wewe hamjawahi kukosekana. Frequency ni bidhaa adimu Dar, nenda wewe huko TCRA leo ukaulizie.
Dada yangu hilo eneo ni field yangu japo sasa nafanya kitu kingine, ila ninacho kizungumza na kijua theoretical mpaka mathematical.

Wewe kama unakubali kudanganywa ni ww, ila Frequency moja haziwezi kuisha wala kuwa mali ya mtu,anaye zimiplan,kuzicontrol,kuzimonitor,kuzimiliki na kuengineer ni TCRA.
 
Back
Top Bottom