DID GIANTS EXIST? Historia ya Majitu ya Kale

Ndugu naomba unitofautishie kati ya roho kuvaa mwili na mwili kupagawa na roho.
Maana naona kama hivi viwili tunavichanganya.
 
Kuna Henoko wawili, baadhi ya machapishi yanawatofautisha kama Henoko na Enoko.
Henoko ni bloodline ya Kaini na Enoko ni wa bloodline ya Seth.
 
Ndugu naomba unitofautishie kati ya roho kuvaa mwili na mwili kupagawa na roho.

Maana naona kama hivi viwili tunavichanganya.

Mkuu kwa uelewa wangu MWILI hauwezi kuishi bila ROHO hivyo ROHO kuvaa mwili ni pale ambapo mwili unaingizwa ROHO either ikiwa bado tumboni kwa mama au hata maiti ikiingiliwa na ROHO iwe pepo jini malaika n.k basi mwili huo unakuwa UMEVALIWA na ROHO


Kuhusu kupagawa ni pale mwili una ROHO tayari ila ROHO nyingine inataka kuuvaa mwili huo..... Hapo tunasema amepagawa sababu ana ROHO ila ROHO nyingine iwe jini au pepo inataka kuuvaa mwili huo huo wa mhusika.


Ila kwenye maoni yangu nlisema ROHO hawezi kuzalisha mwili mpaka ROHO awe amevaa MWILI sio KUUPAGAA mwili...... Either ajibadilishe kuwa mwili (which is possible maana malaika wana uwezo wa kujibadilisha) ila AKIUPAGAA mwili hatoweza kuzalisha ila ataweza kufanya ngono kupitia mwili wa mwanamdamu aliouvaa na mtoto atakayezaliwa atakuwa binadamu tu maana mbegu zilizotoka ni za mwili wa kibinadam kabisa


Cjui kwa maoni yangu tofauti umeiona kidogo??
 
Kwanza naelewa kwamba viumbe wa kiroho nao wana miili.
.
1 Wakorintho 15
39 Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki.

40 Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.

41 Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota.
Hata hivyo miili hii hutofautiani kifahari. Miili waliyokua nayo malaika waliomtembelea Abraham ilikua ni ya fahari tofauti na ule wa Yesu uliozaliwa kwa bikira. Miili ile ya malaika ni teofania au logos ambayo haiwezi kufa. Na ndio maana ili kufa Yesu ilibidi kuwa na miili ya nyama na damu kama sisi iliyotokana na Anguko la Adamu.
.
Hakuna ushahidi wa kiumbe wa kiroho kua na uzao kwa kiumbe wa kimwili na ndio maana tunaona shetani kiumbe wa kiroho hana uzao kwa binadamu zaidi ya kumpagaa nyoka mnyama aliyejipatia uzao kwa binadamu kabla ya kubadilishwa maumbile.
Pia nataka tufahamu kuwa Yesu Kristo hakuwa malaika bali yeye alikua na malaika wake. Yeye Yesu alikuwa mwana na hata wa leo wana wa Mungu sii malaika ila wana malaika wanaowahudumia.
.
Mathayo 18
10 Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.
.
Waebrania 1
13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Niseme kwamba viumbe wote hai kuanzia mimia, wanyama hadi watu wana roho ya uhai ila sii wote wenye nafsi.
Mfano mzuri wa uharibifu katika maumbile ni haya mapandikizi tunayoyashuhudia leo. Kuna kupandikiza genes za tofauti ya wanyama kama mbwa na nyati au na fisi nk au mti wa mlimao kwa mchungwa nk. Matokeo ya huu mchanganyo ni chotara lililo dubwana la ajabu.
Ndicho kitu kilichofanyika kule nyuma yaani kuifanyia vurugu asili.
.
Mathayo 13
24 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;

25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.

27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?

28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?

29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing'oa ngano pamoja nayo.

30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
 
Mkuu Kiby nimependa maelezo yako yana mashiko sana ila nlitaka nizungumzie vitu viwili tu kwenye post yako

hiyo wakorinto 15 haizungumzii malaika ila inazungumzia wanadamu embu tuanzie nyuma kidogo

35 Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani?
36 Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa;
37 nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo;
38 lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake.
39 Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki.
40 Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.


Hivyo hapa mwandishi anajaribu kutuelezea kuwa mwili wa mwanadamu duniani hautokuwa sawa na ule wa mbinguni siku ya ufufuo yaani mwisho wa dunia

2. Hoja ya pili ni kweli hakuna ushahidi wa viumbe kuzaa na binadamu KWENYE biblia maana kulingana na biblia malaika hawakuumbwa kwa kazi hiyo ila ni binadamu pekee waliopewa agizo la kuzaliana hivyo nakubaliana na wewe ila nje ya biblia kuna nadharia nyingi kuhusu uzao wa binadam na nyoka (malaika walioasi) ndio maana nikajaribu kuelezea kidogo kuwa malaika hawezi kuzaa na mwanadamu mpaka awe ameupagaa/kuvaa mwili wa mwanadamu na hata mtoto atazaliwa akiwa mwanadamu 100% however kuna kitu kinaitwa EPIGENETICS naomba uchukue dakika chache kukitafiti

Ila kwa ufupi epigenetics ni pale tabia za mzazi zinavyoweza kuathiri tabia za mtoto mfano kma baba ni malaya basi kunakuwepo na element za umalaya kwa yule mtoto!!! It's scientifically proven hivyo malaika hta kma atampagaa mtu mtoto anaweza gusiwa x-tics za host parent kma anapossesion za mapepo basi kuna uwezekano mtoto akawa na some characteristic za hayo mapepo au majini au vitendo ambavyo baba yake anafanya kwa influence ya hayo mapepo/majini

Hivyo malaika wanaweza wasitunge mimba ila wanauwezo wa kumbadilisha huyo mtoto kuwa kitu wanachotaka kupitia EPIGENETICS..... However kma wachawi wanaweza kumuiba mtoto na kumfanya apotee apae aue mtu kwa kuangalia je kwanni hao malaika washindwe kumfanya huyo mtoto kuwa wa mazingara hata kma hajazaliwa kwa mbegu zao!!!!

3. Hoja ya tatu malaika wanaweza shape shifting Yaani anaweza kuwa ndege anaweza kujibadilisha kuwa jiwe na anaweza kujibadilisha kuwa mwili ndio maana hata waliomtembelea abraham waliskia njaa,walinawa,walichoka na waliongea kma binadamu hivyo kma waliweza kujibadilisha na kuwa wanadamu 100% unafkiri je hawatoweza kulala na mwanamke (sio kuzalisha)???
 
Mkuu nakubaliana na wewe kwa njia moja ya ushawishi wa kiroho kwamba nafsi ya mtu sii mwili wa huyo mtu hapana! Ni tabia ya roho maana tunaposema tumekufa na maisha yetu kufichwa kwa Mungu kwa njia ya Kristo sii kwamba ni mwili na roho yako iliyokufa la! Ni tabia ya roho yako ndio iliyokufa yaani tabia. Kwa maana hiyo kuna muunganiko wa ulimwengu wa kiroho na wa kimwili.
Kwenye hoja yangu ya wakorento 15 nilichokua natafuta pale zaidi ni miili kwamba viumbe wa kiroho nao wana miili ya kiroho kama vile viumbe wa kimwili(flesh) walivyo na miili. Watu tuna dhana kwamba roho ni kitu kama upepo au mvuke hapana wana miili.
Tukirudi sasa kwenye main topic ya mleta mada mimi nilijaribu kutafuta chimbuko la asili ya majitu na kwa mtizamo wa kibiblia ninaona kwamba asili ya hiki kitu ni cross bleeding kati ya mnyama na binadamu yaani mnyama nyoka na binadamu Eva.
Hili tokeo ndilo lililosababisha vurugu katika uumbaji. Ni sawa na msemo huu kwamba uki iharibu asili tarajia kuvuna uharibufu.
Wewe unaliona je hili?
 
Mkuu hapa naona ukakasi labda tujaribu kufikiri hivi.
Mungu aliwaangamiza kidogokidogo ili hata vizazi vingine vipate kujua habari zao maana kama angewaangamiza wote katika garika ya nuhu Leo tusingeona hata mabaki ya mifupa yao mifupa ya mabaki ingekuwa baharini ili kuujua ukweli aliwaacha waishe taratibu ili tujifunze na kupata ushahidi wa wao kuishi.
 
Kuna nyayo nilizikuta Ruangwa sehemu inaitwa machang'anja katika majabari ya miamba mpaka sasa najiuliza aliyekanyaga pale ni mtu wa aina gani maana unyayo mmoja una centimetres 51 na upana wa centimetres 22 na alikuwa akipiga hatua za centimetres 380 katika jabari hilo kuna nyayo 11 hizi kubwa ni 4 na ndogo 7 na hizi ndogo ni centimetres 28.4 na upana wa centimetre 13 na alikuwa akipiga hatua za centimetres 185 kuna vitu vingi tukiweza kuvitaftia majibu itatusaidia kuujua ukweli.
 
Naksubiri mkuu kama kawa nategemea uje na ESSAY nzima kuhusu mada husika
Nakumbuka miaka ya 1989 nikiwa mdogo kuna jitu liliitwa Ndindiyeahaga lilikuwa nene sana na refu kupita mtu yeyote pale kijijini na lilikuwa na nguvu nyingi sana na kila mtu aliliogopa uzuri halikuwa na akili watu walilitumikisha kulibebesha kuni na maji kuna Pombe inaitwa Ndimasi na rubisi lilikuwa linakunywa ndoo tatu.
Lilikuwa linabeba chungu (ndoo ya kiasili ya udongo) kubwa na kujitua ambayo wanaume wa 5 hawawezi kubeba na miaka hiyo lilikuwa zee likafariki alibebwa na watu 10 na kaburini walitumia miti kuviringisha tangu hapo mpaka nimekuwa mtu mzima sijawahi kuona jitu kama lile tena nadhani alikuwa Mnefili.

Alizikwa katika kijiji kiliitwa Mkiyonga Mbuba Mkoani kagera nadhani Leo hii likifukuliwa lile kaburi ikapimwa DNA ya jitu lile inaweza kutupa majibu ya haya majitu.

Na kama jitu lile lingekuwa na akili likaamua kuasi lingeweza hata kuua kijiji kizima maana nilishawahi kuambiwa na Babu kuwa miaka ya 1945 Simba walikuwa wakivamia mifugo linawakamata kwa mikono na kuwaua na lilikuwa likibeba ngombe kama kuku hakika ni moja ya majitu ya kutisha yaliyotokea ktk inchi yetu tatizo ni kuwa hatuoni umuhimu wa vitu hivi tungeweza kujifunza mengi.
 
Sasa kama ni vigumi kuwatambua wewe umejuaje kama wapo?
naamini wapo ila sijui unawatambuaje

Nilitumia sentesi hii ya "vigumu kuwatambua" nikimaanisha kwamba kwa Baadhi ya watu hawa majini hujidhihirisha lakini asipo penda kujionyesha kwa mtu husika hawezi mjua kamwe.
 
Duh story yako imenisisimua kwa kweli...... Naona kuna haja ya watanzania tuanze kuenzi mambo kama haya ili tuweze kuwaachia historia vizazi vijavyo kuhusiana na historia ya nchi yetu.

Ilibidi vitabu viandikwe.... Makumbusho yawekwe yangeweza kuwa hata vituo vya utalii vikubwa vikatuingizia mapato makubwa tu
 
Zitto junior hebu kwenye hili naomba tuwasiliane... Nina idea lakini inakosa support
 
M

MADA NZURI SANA HIII
 
Nikiwa mtoto nilikua napewa story na Bibi yangu kuhusu mtu aliekwenda kwa jina la Ibhamba Ngulu huko usukumani aliekua JITU kubwa na inasemekana aliacha nyayo zake kwenye mapango ya mawe na alama ya mkuki wake aliouchomeka kwenye jiwe.
 
Vipi hakuwahi kukusimulia kuhusu asili (wazazi au ndugu na jamaa) ya huyo giant?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…