Historia ya UJ ni pana sana tena sana na katika historia hiyo huwezi amini imeanzia Tanzania na ndipo ilipoanza kuonekana lakini kwa sababu tusizozijua historia hii imefichwa na hivyo wengi kuona Uj hakuna anaejua alikotokea.
Uj inaaminika kwamba fuvu lake lipo mexico kwa sababu ni fuvu la mtu mweusi na lilionekana sio la mtu wa kawaida (Giant)
Kwa kuwa ni historia pana juu ya mtu huyu basi kifupi naomba upitie hapa chini nawe waeza kuja nisaidia pale nilipokwama kuhusu mtu huyo ila ukweli ndio huu kwamba historia yake imeanzia hapa Tanzania
Unju bin Unuq (pia:
Unju bin Unuku,
Unzi Bin Ununuk) ni
jina la
jitu katika masimulizi ya wakazi wa
pwani ya
Tanzania.
Hadithi zake zasimuliwa kuanzia
Bagamoyo hadi
Kilwa.
Historia yake inapatikana katika makumbusho ya
Kaole huko Bagamoyo.
Moja ya mambo ya ajabu ya mtu huyu ni
urefu wake yaani
kimo, inasadikiwa alikuwa na urefu mkubwa ulioweza kumfanya atembee
baharini na
miguu yake kugusa chini.
Pia alikuwa akitembea kutoka nchi hadi nchi kutokana na urefu wake. Inasimuliwa kuwa moja kati ya nyayo zake inapatikana kwenye
jiwe alilokanyaga huko
Tabora, Tanzania,
wayo wa mguu wa kushoto wakati wayo wa mguu wa kulia ulionekana kwenye jiwe alilokanyaga huko
Kongo.
Inasimuliwa pia akitaka kula alikuwa akichukua
samaki baharini kwa mkono na kuchoma katika
jua kisha anakula.
Kuhusu
maisha yake inasimuliwa kuwa Unju bin Unuk hakuoa wala kuolewa kutokana na
umbo lake.
Sehemu nyingine ya hadithi yake ni alipokufa Unju bin Unuq, aligawanyika vipandevipande kutokana na urefu wake na inasemekana
kidole chake chenye urefu wa
kilometa moja kasoro ndicho kilichopatikana na kuzikwa pale Bagamoyo, lakini hakuna simulizi
mwili wake uliobaki uliangukia wapi.
Unju bin Unuq alikuwa na ndugu yake aliyejulikana kama Geofrey bin Unuk, huyu alipatikana maeneo ya
Dodoma. Au kwamba Unuq baada ya kupotea kwa muda wa miaka mingi ndugu zake wa mbali sana wameonekana katika
mkoa wa Dodoma.
Asili ya jina la Unju bin Unuq katika Uarabuni na BibliaEdit
Jina lake linatokana na
Kiarabu cUdj bin Unuq / ‘Anaq عوج بن عنق anayejulikana katika visa vya nchi nyingi za
Uislamu kama jitu kubwa sana. Waislamu walipokea
hadithi kutoka kwa
Wayahudi anakojulikana kwa jina la Og עוֹג.
Asili kabisa ni taarifa za Biblia kuhusu mapigano kati ya
Wanaisraeli waliotoka
Misri na
Ogu mfalme wa
Bashani (
Hesabu 21,33)
[1]; Wanaisraeli walimshinda wakiongozwa na
Musa.
Ogu alisemekana kuwa mtu mrefu;
Kumbukumbu la Torati 3,11 kinamtaja hivi: "aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama,
kitanda chake kilikuwa kitanda cha
chuma; kitanda hicho je! Hakiko
Raba kwa wana wa
Amoni? Urefu wake ulikuwa ni
mikono kenda, na
upana wake mikono minne, kwa mfano wa mkono wa mtu".
Katika masimulizi ya Wayahudi tabia hii iliendelea kuongezeka; katika
Kitabu cha Amosi 2,9 anatajwa (bila kusema jina) kama "Mwamori" "nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa
mierezi, tena alikuwa na
nguvu kama
mialoni".
Wataalamu Wayahudi wa baadaye waliona ya kwamba
vipimo vya Kumb. 3 kuhusu kitanda chake chenye urefu wa mikono yaani
dhiraa 10, sawa na
mita 4-5, vilihusu mkono wa hilo jitu lenyewe, hivyo walimwona mkubwa zaidi tena.
Kwenye
kitabu Berakhot cha
Talmudi Ogu anasimuliwa ya kwamba aliweza kuinua
mlima aliotaka kurusha dhidi ya Wanaisraeli, lakini
Mungu alimzuia
[2]. Katika kitabu cha Nidah katika Talmudi Ogu anasemekana ni mtu aliyeishi kabla ya
gharika ya
Nuhu akiwa ni mmoja wa hao ambao walitunzwa.
[3]
Katika UislamuEdit
Masimulizi ya Kiyahudi yalipokewa na
Waislamu na kupanuliwa tena. Ushahidi uko kwa
Al Tabari aliyeandika ya kwamba
maiti ya cUdj ilikuwa kama
daraja juu ya
mto Naili.
Al-Thaclabi aliandika ya kwamba cUdj alikuwa na urefu wa
dhiraa 23,333 akiweza kunywa kwenye
mawingu, kushika ngumi baharini na kuichoma kwenye
Jua. Alitembea mbele ya Nuhu wakati wa gharika kuu lakini
maji yalifikia
magoti yake tu. Aliishi miaka 36,000. Alipoona kambi la Wanaisraeli na
Musa alivunja
mlima akashika kipande cha kuangamiza kambi lote kwa pigo moja, lakini
Mungu alituma
ndege waliokula shimo katikati ya mlima uliomuangukia na kumfunga katikati. Hivi Musa aliweza kumshinda kirahisi
Hii ni picha iliopigwa huko Mexico miongo kadhaa nyuma
Asalaam kudo