DID GIANTS EXIST? Historia ya Majitu ya Kale

DID GIANTS EXIST? Historia ya Majitu ya Kale

Mkuu mvyosema malaika hawawezi kuzaa na mtu sababu ni roho mpaka wawe na mwili wa kibinadamu,
Vipi kuhusu majini mahaba wanaoingilia watu ndotoni? Tena inasemekana wengine wanazaa kabisa watoto na binadamu..
Majini nao si roho?
Mmmh hii elimu ya majini labda Mshana Jr au MziziMkavu ndio wanaweza kutudadavulia

Ila kwa uelewa wangu mdogo kwenye elimu ya demonology.... Ni ngumu sana kwa roho kuzaa na mwili hadi pale ROHO inapovaa mwili ni sawa na mwanadamu pia huwezi kupambana na ROHO hadi uwe unatumia ROHO sio mwili yaani mfano kupitia meditation,maombi n.k ila sio kwa mapanga na marungu!!

Vivo hivyo kma hao majini wamelala na mwanamke KIROHO zaidi yaani ndoto au njozi basi hata huyo mtoto anakuwa sio wa kimwili ila anakuwa wa kimazingara either anaibwa kutoka kwenye uzazi wa mwanamke mwingine n.k maana as far as nmesoma sijaona popote ambapo malaika/mashetani wanaweza kuzaliana na kuongezeka!!!

However vitabu vinasema malaika waliumbwa kwa MWANGA na majini waliumbwa kwa MOTO...... Hivyo huenda tabia zao zinatofautiana wajuzi wa elimu ya kiroho watusaidie hapa
 
tunaambiwa walikua watoto wa MUNGU, kwa kipindi hicho wakizubgumzia watoto wa MUNGU walikua wanamaanisha malaika.

Na malaika wanauwezo wa kuuvaa mwili wakawaida kabisa wa kibinadamu, tunaona wale walio mtokea Ibrahimu wakati wa hali huko karibu na mialoni ya mamre alipoluwa ameketi malangoni mwa hema yake .

Ukisoma ule mstari wa 16 sura ya 18 kitabu cha mwanzo, biblia inatuambia "kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao sodoma "

Lakini ukiendelea kusoma unagundua kwamba hawakua watu walikua malaika ila walioamua kumtembelea Ibrahim kwa maumbo ya kibimadamu.


Hivyo kumbe hata hayo majitu yaliweza kuja kwa wanadamu kikawaida kabisa yakiwa umbo la kibinadamu la kawaida sawa na wanadamu wa enzi hizo.

Na inawezekana kabisa ukuaji wa mimba na kuzaliwa watoto ilikua kawaida tu, ila huenda mabadiliko ya maumbo ya watoto wa (MAJITU) yalianza tu mara baada ya watoto hao kuzaliwa.
Umejibu vizuri asee safi sana,lakini humu kuna watu wanaamini kuwa wao pia ni wana wa mungu,japo huyo mungu hawamfaamu wala hawajapata kuuona uwepo wake,...embu siku tujaribu kumsaka mungu yuko wapi unawezajikuta mungu ni ww mwenyewe.
 
Historia ya Uj ni pana kuliko unavyodhania ila hapa nimejaribu tu kuweka sawa kuhusu huyo huyo Uj kwenye vitabu vya dini na wanavyomzungumzia humo ili nisitoke nje ya msatari wa mtoa Mada

Lakini kuhusu baadhi ya sehemu kufichwa inaeza kuwa ni sehemu ndogo sana ilifichwa lakini imetupotezea uhalali wa stori nzima kumhusu huyu jamaa yani ni kama vile ile fomula ya maji kisayansi ukitoa kale ka mbili ikabaki HO utakuwa umepteza maana kabisa.

So huyu jamaa yaezekana haijwahi kuwapo mtu kama huyo tena na yaezekana bila yeye ile safina isingekuwa na ubora ule hivyo ukianzia hapo tu utaona huyu mtu mweusi kuna haja ya kuficha historia yake kwa maslahi fulani

Au walishindwa kuitambua maana hawakufahamu alikotokea na kifo chake kilikuwa vipi
So yote yawezekana lakini ukiichambua zaidi historia hiyo unaeza leta mkanganyiko wa mambo flani kuhusu dini na baadhi ya maandiko yake kuhusu huyo mtu

So inatosha kwa hapo palipoelezwa Chief mengine tafuta na wew utapaata jambo
pitia hii comment""

alibakari
 
Queen of Sheba ni kweli nae historia yake inawekewa kigiza hivi lakini waethopia wanaijua vizur sana na huwadanganyi hapo

Lakini ndio maana nilikwambia hakuna kitabu cha dini kilicho straight katika mambo flanflan lakini kweli ni ipi kila mtu atakwambia kitabu chake cha dini kipo sawa lakini ukitizama vitabu vyote vinaeleza vizuri sana kuhusu watu weupe ila kunapokuwepo na kuonekana kwa mtu mweusi tu basi utaona historia yake inaisha bila kuelewa ilikuwaje

Ila tukiyaacha yote ni wakati wetu sasa kutafuta historia zetu wenyewe zile historia zilizopo zina jambo flani tata yaeza kuwa ni makusudi au walishindwa tu kupata ushirikiano kwa sababu walitoka mbali kuja kwetu au vinginevyo wanajua lakini wanataka tuwaamini zaidi wao yaani ni kama lile fumbo la ustarabu wa binadamu ulikoanzia kila siku hawataki kuamini ulianzia Afrika wanataka tuamini ulianzia kwao

Tuyaache yote na sisi ni wakati wetu kuweka historia zetu wenyewe na wao wasome kutuhusu lakini mtafanya wanagapi ili mganikiwe? Ikiwa hata serikali inaeza kushindwa kukupa ushirikiano pale inapohitajika.

Mfano.

Pale itigi wilayani Manyoni mkoa wa singida kuna njia ipo chini ya ardhi njia ndefu sana lakini njia hii inasemekana ilikuwa ni handaki la moja wa machifu alikuwa akijificha huko wakati wa vita na pia kunaaminika kuna sehemu alijenga kama madhabahu ya kufanya sala ya kimila huko chini lakini nilipoenda kuomba kibali cha kuingia huko nikakataliwa kwa nguvu zote lakini njia ya kuingilia ipo na inaonekana na watu kadhaa wamewahi kupita huko kiusalama ni popo tu waliopo huko na hata nilipoomba basi wanipe ulinzi walikataa ikabidi utafiti wangu uishie pale

Huo ni mfan mdogo sana kati ya mingieniliokutana nayo

Tukibadilika hata Mabomu tutatengeneza wenyewe


pitia hii essay"" alibakari
 
Ni kweli malaika kama malaika au ROHO yeyote hawezi kuzalisha sababu haikuumbwa kwa sababu hiyo ila mwili unaweza kuzalisha sababu uliumbwa kwa kazi hiyo na ndipo mjadala unapoaanza.

kutokana na ushahidi wa kibiblia (sijui imani yako utaniradhi) tunaweza kuona mwandishi wa kitabu cha Yuda ambaye alikuwa kaka yake Yesu anaongelea kisa hiki cha malaika kuwaingilia wanadamu,twende pamoja

Waraka wa YUDA
6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele
.

Hapa tukisoma tunaona wazi mwandishi anafananisha dhambi waliofanya watu wa sodom ya uzinzi kma walivyofanya wale malaika.... Neno JINSI MOJA NA HAWA.... Linaweza kusummarise kuwa iliwezekana malaika kuwaingilia wanadamu na kuwazalisha viumbe na watafiti wengine wanadai ndio moja ya sababu Mungu aliamua kufuta uzao huo kwa gharika ila Yuda hapa anaelezea kuwa malaika hao kwa sasa wamefungwa kuzimu hivyo kuna uwezekano kwa sasa hawana uwezo huo wa kuhamisha asili yao kwa mwili kama walivyofanya kwa WANEFILI

2. Nadharia ya pili malaika kuvaa mwili wa binadamu ili aweze kuzalisha however swali lako linahoji kivpi anaweza hamisha genes zake

Kwa maoni yangu binafsi nachoona kuna uwezekani mtoto asiwe na gene yoyote ya kimapepo/kimalaika sababu mwili umezaa na mwili ila MAKUZI yanaweza kumbadilisha huyo mtoto kuwa wa mazingara..... Mfano mtoto aliyezaliwa kibinadamu akachukuliwa na wachawi lazima atakua tofauti na mtoto wa kawaida maana atapandikizwa matambiko ya ajabu yanayomuwezesha kupaa...kuyeyuka....kuua....nguvu za ajabu n.k

Hivyo kwa nadharia hii ya pili hao wanefili wanaweza kuwa walizaliwa kwa malaika kuvaa miili ya binadamu wengine na watoto walizaliwa kma wanadamu tu ila makuzi mfano waliwafanyia matambiko.... Walihamishia mapepo yao mengine humo..... Waliwapa nguvu zao n.k mwisho wa siku miili yao ikabadilika ikawa ya kimazingara maana mfano kma leo hii mchawi anaweza akakuotesha busha...tumbo n.k kwa nni tusiamini hao MALAIKA walikuwa na uwezo wa kuwapa urefu wa ajabu... Nguvu za ajabu nyingine kma leo hii tu wachawi wakawaida wanavyoweza kuotesha viungo flani vya mwili

Sijui it makes sense now ila all in all nakubaliana na ww malaika HAWEZI kumzalisha mwanadamu ila inawezekana kwa exception nlizotaja hapo juu

Ni hayo tu labda tuwaite na wajuvi wengine watusaidie

Cc : SALA NA KAZI @Malcom Lumumba [USER=113939]Palantir hearly Eiyer Kudo900 Mshana Jr[/USER]
Zitto nipo sana ila nimejikuta nakuwa mwanafunzi zaidi... Kuna vitu vipya najifunza hapa vingine ni kujikumbusha.... Ila nipo kama mwanafunzi mtiifu
 
Zitto nipo sana ila nimejikuta nakuwa mwanafunzi zaidi... Kuna vitu vipya najifunza hapa vingine ni kujikumbusha.... Ila nipo kama mwanafunzi mtiifu
Hahahhaa mwanafunzi tena!!! Itabidi utupe elimu kidogo kuna mmoja hapo kauliza kma jini linaweza kumpa mtu mimba na akazaa kabisa

Embu tutoe tongotongo maana ww ndio mtaalam wa mambo hayo
 
Kwa mtizamo ninaouona kupitia biblia uzao wa giants/nafeli umepatika kwa njia ya uzao wa myama kuchanganyikana na uzao wa mtu.
Nyoka alikuwa mnyamwe mwerevu kushinda wanyama wote aliowaumba Bwana Mungu. Huyu nyoka mnyama ndie shetani aliyepitia kwake kumwangusha hawa hata ikawa kukawa na zao mbili tofauti yaani mzao wa nyoka na mzao wa mwanamke na kuanzia hapo ndipo kuliwekwa uadui kati ya hizi zao mbili.
Ndipo sasa unakuta biblia inasema wanadamu walipo ongezeka, wana wa Mungu walijitwalia wake kwao.
.
Mwanzo 6
4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.
.
Uzao wa Adamu kadri ulipoongezeka ni kwamba uzao wa nyoka kupitia kaini nao uliongezeka na kadri walioongezeka walioana wao kwa wao na hivyo kukawa na hybrid ya kuchanganya uzao wa Adam kwa Eva na ule wa nyoka mnyama kwa Eva.
Hata hivyo baada ya tendo hili kutokea Mungu hakumwacha nyoka katika asili yake bali alimbadili maumbile ili hali ile isijirudie tena.
.
Mwanzo 3
14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;
 
Tafuta jibu kwanza sio unaquote, roh zinapuliziwa kwenye mwili, kinachozaliwa ni mwili na ndio maana mwili hufa ila roho baada ya mwili kufa hurudi kwa muumba.
Jiulize vizuri usije ukaniuliza nini kufa
Kinachozurura huwa nini
 
Back
Top Bottom