Mgonga Like
JF-Expert Member
- Mar 30, 2015
- 1,256
- 1,661
Sasa kama ni vigumi kuwatambua wewe umejuaje kama wapo?Mkuu nikikwambia unawatambuaje hao, nitakua mwongo kwa maana ni vigum pia kuwatambua,
Ila wapo tunaishi nao.
Sasa kama ni vigumi kuwatambua wewe umejuaje kama wapo?Mkuu nikikwambia unawatambuaje hao, nitakua mwongo kwa maana ni vigum pia kuwatambua,
Ila wapo tunaishi nao.
Ndugu naomba unitofautishie kati ya roho kuvaa mwili na mwili kupagawa na roho.Roho haizaliwi ila inazaliwa kwa mwanadamu kama ikiwa ndani ya mfumo wa mwili kwa hiyo Yesu ni Roho kweli ila kwakuwa alipokuja duniani hakuja kma MZIMU ila MWANADAMU hivyo aliweza kuzaliwa sababu alikuwa kwenye form ya MWILI
Hata wewe una Roho ndani ya mwili na siku ukifa Roho inatoka na mwili unabaki hivyo kabla hujazaliwa unakuwa roho ila ili uingie duniani unavaa mwili same case kwa Yesu
Pia Yesu si malaika ila wote ni ROHO/DIVINE BEINGS so wana tabia zinazofanana
Moja kauliza kama malaika wana sex?? Wakiwa kwenye form ya malaika hawawezi ila wakivaa mwili kma wwe ulivyovaa mwili basi wanaweza kusex na mwanamke au mwanaume
Hata kwenye biblia tunaona malaika wakimtembelea Abraham walikula,waliomba maji,walipumzika,walinawa n.k hivyo wakishavaa miili ya kibinadam wana uwezo wa kufanya kila kitu ambacho unaweza kufanya
Hope nmeeleweka
Kuna Henoko wawili, baadhi ya machapishi yanawatofautisha kama Henoko na Enoko.Hapana Henoko aliishi miaka mia tatu na sitini na mitano tu (365) halafu Mungu akamtwaa
Soma Mwanzo 5 : 21 - 24.
Aliyeishi miaka mingi kutokana na Biblia ni Methusela mtoto wa Henoko, yeye aliishi miaka mia tisa sitini na tisa (969)
Mwanzo 5 : 25 - 27.
Ndugu naomba unitofautishie kati ya roho kuvaa mwili na mwili kupagawa na roho.
Maana naona kama hivi viwili tunavichanganya.
Kwanza naelewa kwamba viumbe wa kiroho nao wana miili.Mkuu kwa uelewa wangu MWILI hauwezi kuishi bila ROHO hivyo ROHO kuvaa mwili ni pale ambapo mwili unaingizwa ROHO either ikiwa bado tumboni kwa mama au hata maiti ikiingiliwa na ROHO iwe pepo jini malaika n.k basi mwili huo unakuwa UMEVALIWA na ROHO
Kuhusu kupagawa ni pale mwili una ROHO tayari ila ROHO nyingine inataka kuuvaa mwili huo..... Hapo tunasema amepagawa sababu ana ROHO ila ROHO nyingine iwe jini au pepo inataka kuuvaa mwili huo huo wa mhusika.
Ila kwenye maoni yangu nlisema ROHO hawezi kuzalisha mwili mpaka ROHO awe amevaa MWILI sio KUUPAGAA mwili...... Either ajibadilishe kuwa mwili (which is possible maana malaika wana uwezo wa kujibadilisha) ila AKIUPAGAA mwili hatoweza kuzalisha ila ataweza kufanya ngono kupitia mwili wa mwanamdamu aliouvaa na mtoto atakayezaliwa atakuwa binadamu tu maana mbegu zilizotoka ni za mwili wa kibinadam kabisa
Cjui kwa maoni yangu tofauti umeiona kidogo??
Mkuu nakubaliana na wewe kwa njia moja ya ushawishi wa kiroho kwamba nafsi ya mtu sii mwili wa huyo mtu hapana! Ni tabia ya roho maana tunaposema tumekufa na maisha yetu kufichwa kwa Mungu kwa njia ya Kristo sii kwamba ni mwili na roho yako iliyokufa la! Ni tabia ya roho yako ndio iliyokufa yaani tabia. Kwa maana hiyo kuna muunganiko wa ulimwengu wa kiroho na wa kimwili.Mkuu Kiby nimependa maelezo yako yana mashiko sana ila nlitaka nizungumzie vitu viwili tu kwenye post yako
hiyo wakorinto 15 haizungumzii malaika ila inazungumzia wanadamu embu tuanzie nyuma kidogo
35 Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani?
36 Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa;
37 nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo;
38 lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake.
39 Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki.
40 Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.
Hivyo hapa mwandishi anajaribu kutuelezea kuwa mwili wa mwanadamu duniani hautokuwa sawa na ule wa mbinguni siku ya ufufuo yaani mwisho wa dunia
2. Hoja ya pili ni kweli hakuna ushahidi wa viumbe kuzaa na binadamu KWENYE biblia maana kulingana na biblia malaika hawakuumbwa kwa kazi hiyo ila ni binadamu pekee waliopewa agizo la kuzaliana hivyo nakubaliana na wewe ila nje ya biblia kuna nadharia nyingi kuhusu uzao wa binadam na nyoka (malaika walioasi) ndio maana nikajaribu kuelezea kidogo kuwa malaika hawezi kuzaa na mwanadamu mpaka awe ameupagaa/kuvaa mwili wa mwanadamu na hata mtoto atazaliwa akiwa mwanadamu 100% however kuna kitu kinaitwa EPIGENETICS naomba uchukue dakika chache kukitafiti
Ila kwa ufupi epigenetics ni pale tabia za mzazi zinavyoweza kuathiri tabia za mtoto mfano kma baba ni malaya basi kunakuwepo na element za umalaya kwa yule mtoto!!! It's scientifically proven hivyo malaika hta kma atampagaa mtu mtoto anaweza gusiwa x-tics za host parent kma anapossesion za mapepo basi kuna uwezekano mtoto akawa na some characteristic za hayo mapepo au majini au vitendo ambavyo baba yake anafanya kwa influence ya hayo mapepo/majini
Hivyo malaika wanaweza wasitunge mimba ila wanauwezo wa kumbadilisha huyo mtoto kuwa kitu wanachotaka kupitia EPIGENETICS..... However kma wachawi wanaweza kumuiba mtoto na kumfanya apotee apae aue mtu kwa kuangalia je kwanni hao malaika washindwe kumfanya huyo mtoto kuwa wa mazingara hata kma hajazaliwa kwa mbegu zao!!!!
3. Hoja ya tatu malaika wanaweza shape shifting Yaani anaweza kuwa ndege anaweza kujibadilisha kuwa jiwe na anaweza kujibadilisha kuwa mwili ndio maana hata waliomtembelea abraham waliskia njaa,walinawa,walichoka na waliongea kma binadamu hivyo kma waliweza kujibadilisha na kuwa wanadamu 100% unafkiri je hawatoweza kulala na mwanamke (sio kuzalisha)???
Mkuu hapa naona ukakasi labda tujaribu kufikiri hivi.Ahsante kwa mchango wako lakini hapa bado inaniacha na maswali kidogo labda uniweke sawa
1. Kama waliangamizwa na gharika je hao 'MAJITU' yaliyokuja baada ya gharika mfano Goliath au Mfalme Ogu walitokea wapi??
2. Kama walitokana na malaika ina maana malaika walizaa upya na wanadamu baada ya gharika??
3. Kama walikuwepo baada ya gharika je kizazi chao kimeishia wapi kiasi leo hatunao tena duniani??
Tutoe tongotongo kidogo
Kuna nyayo nilizikuta Ruangwa sehemu inaitwa machang'anja katika majabari ya miamba mpaka sasa najiuliza aliyekanyaga pale ni mtu wa aina gani maana unyayo mmoja una centimetres 51 na upana wa centimetres 22 na alikuwa akipiga hatua za centimetres 380 katika jabari hilo kuna nyayo 11 hizi kubwa ni 4 na ndogo 7 na hizi ndogo ni centimetres 28.4 na upana wa centimetre 13 na alikuwa akipiga hatua za centimetres 185 kuna vitu vingi tukiweza kuvitaftia majibu itatusaidia kuujua ukweli.Dah mada tamu sana japo nimekuja kwa kuchelewa.... Ithibati kadha zipo na hawa majitu hawakuwa pekeyao bali mpaka na wanyama na mimea yao.. Hakukuwa na mbilikimo hizo enzi
Ushahidi wa wazi kwenye hili unaonekana Arusha kwenye ule unyayo kwenye mwamba na Tanga Lushoto sehemu inaitwa Irente kuna mwamba mkubwa usiofikika kirahisi una unyayo mkubwa sana.. Ithibati ziko lukuki
Lakini vile vile kwenye Bible takatifu tunaambiwa kuhusu habari za Goliath... Jitu kubwa lenye nguvu nyingi... Tunaambiwa kuhusu watu wale wa zamani kuishi miaka 800... Kwa vimwili vyetu hivi vya leo kuishi miaka mia tu ni kasheshe
Tuendelee na mjadala nimeweka kikao
Nakumbuka miaka ya 1989 nikiwa mdogo kuna jitu liliitwa Ndindiyeahaga lilikuwa nene sana na refu kupita mtu yeyote pale kijijini na lilikuwa na nguvu nyingi sana na kila mtu aliliogopa uzuri halikuwa na akili watu walilitumikisha kulibebesha kuni na maji kuna Pombe inaitwa Ndimasi na rubisi lilikuwa linakunywa ndoo tatu.Naksubiri mkuu kama kawa nategemea uje na ESSAY nzima kuhusu mada husika
naamini wapo ila sijui unawatambuajeSasa kama ni vigumi kuwatambua wewe umejuaje kama wapo?
Duh story yako imenisisimua kwa kweli...... Naona kuna haja ya watanzania tuanze kuenzi mambo kama haya ili tuweze kuwaachia historia vizazi vijavyo kuhusiana na historia ya nchi yetu.Nakumbuka miaka ya 1989 nikiwa mdogo kuna jitu liliitwa Ndindiyeahaga lilikuwa nene sana na refu kupita mtu yeyote pale kijijini na lilikuwa na nguvu nyingi sana na kila mtu aliliogopa uzuri halikuwa na akili watu walilitumikisha kulibebesha kuni na maji kuna Pombe inaitwa Ndimasi na rubisi lilikuwa linakunywa ndoo tatu.
Lilikuwa linabeba chungu (ndoo ya kiasili ya udongo) kubwa na kujitua ambayo wanaume wa 5 hawawezi kubeba na miaka hiyo lilikuwa zee likafariki alibebwa na watu 10 na kaburini walitumia miti kuviringisha tangu hapo mpaka nimekuwa mtu mzima sijawahi kuona jitu kama lile tena nadhani alikuwa Mnefili.
Alizikwa katika kijiji kiliitwa Mkiyonga Mbuba Mkoani kagera nadhani Leo hii likifukuliwa lile kaburi ikapimwa DNA ya jitu lile inaweza kutupa majibu ya haya majitu.
Na kama jitu lile lingekuwa na akili likaamua kuasi lingeweza hata kuua kijiji kizima maana nilishawahi kuambiwa na Babu kuwa miaka ya 1945 Simba walikuwa wakivamia mifugo linawakamata kwa mikono na kuwaua na lilikuwa likibeba ngombe kama kuku hakika ni moja ya majitu ya kutisha yaliyotokea ktk inchi yetu tatizo ni kuwa hatuoni umuhimu wa vitu hivi tungeweza kujifunza mengi.
Zitto junior hebu kwenye hili naomba tuwasiliane... Nina idea lakini inakosa supportDuh story yako imenisisimua kwa kweli...... Naona kuna haja ya watanzania tuanze kuenzi mambo kama haya ili tuweze kuwaachia historia vizazi vijavyo kuhusiana na historia ya nchi yetu.
Ilibidi vitabu viandikwe.... Makumbusho yawekwe yangeweza kuwa hata vituo vya utalii vikubwa vikatuingizia mapato makubwa tu
Habari za asbuhi wana jukwaa, niende moja kwa moja kwenye mada kama kichwa cha habari kinavyosema je Giants/Majitu makubwa yanayoelezwa kufika hadi futi 45 waliwahi kuishi hapa duniani?? na kama waliwahi kuishi walitoweka wapi?? Na kwanini siku hizi hawazaliwi tena??
Hadithi za uwepo wa hawa watu zipo karibu katika kila kabila na jamii hapa duniani kwa mfano wahispania wana historia ya Giant (basajaun) ubelgiji alikuwepo antigoon, indonesia (Buto), waebrania (Goliath), Irimu wa wakikuyu na Yalmavuz wa uturuki nikitaja kwa uchache.
Hata vitabu vya kidini na kihistoria zimewaongelea hawa watu embu tuone mifano kidogo
WANEFILI
Mwanzao 6:4
4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa
Kwa tafsiri ya kiingereza
Genesis 6:4
4There were giants in the earth in those days; and also after that, when the sons of God came in unto the daughters of men, and they bare children to them, the same became mighty men which were of old, men of renown.
Inaelezwa watu hawa walikuwa ni majitu makubwa yenye nguvu yanaongelewa pia kwenye vitabu vya kihistoria kma Book of giants tunaona watoto wa Semyaza kina ohyah na hahyah walikuwa ni majitu makubwa sana yanazidi futi 100!!!..... Pia kitabu cha Enoko (book of watchers) anaongelea watu hawa ambao walikuwa ni wakubwa sana na walikuwa wakitesa wanadamu maana walidai vyakula kuliko viwango vyao vya uzalishaji na wakaanza hadi kuwala wanadamu wenyewe.... So dunia ilijaa vurugu tupu kipindi cha kabla ya gharika sababu ya hawa WANEFILI
2. WANA WA ANAKI (ANNUNAKI)
Kwenye vitabu vya dini hawa pia wanaongelewa kama WANEFILI ambao ni majitu marefu yenye nguvu sana
Hesabu 13:33
32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.
33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
Walisema haya baada ya waisraeli kutuma wapelelezi kwenda kukagua nchi ya kanaan iliyokaliwa na wana wa Canaan mtoto wa Ham wakiwemo Waamori,waamaleki,wayebusi,wahiti,Hivitites,Gilgashites n.k ambao kwenye biblia wanaelezwa kma majitu makubwa na marefu yaliyoishi Canaan kipindi waisraeli wanataka kurudi kwenye nchi yao ya ahadi
Amos 2:9
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini
NB:Mierezi ni miti mirefu sana sasa iliopatikana huko lebanon
QURAN TAKATIFU
Mfano ambao upo ndani ya Quran ni Mfalme Og wa Bashan au kwa kiarabu alifahamika kma Uj ibn Anaq huyu alikuwa mfalme wa kale ambaye alikuwa ni mrefu sana na ana mwili mkubwa tunaambiwa alikuwa na futi 13 na alikuwa na nguvu sana,pia kwenye Quran anatajwa Jitu linaitwa Jalut ambalo nalo linaelezwa alikuwa mtu mkubwa mwenye maguvu sana kuliko umbo la kawaida la mwanadamu.
GILGAMESH
Huyu ametajwa na Enocko kwenye book of giants kwamba alikuwa ni JITU kubwa sana lenye manguvu kiasi kwamba lilitangaza vita na Mbingu..... Inadaiwa alitawala ufalme wa sumeria (Uruk) enzi za kale na alitawala kwa miaka 126... Ana stori ndefu kidogo itabidi afunguliwe uzi siku moja (Epic of gilgamesh) ila kwa leo nimemtaja tu kma mmoja ya GIANTS
USHAHIDI WA KISAYANSI
Hii ni baadhi ya mifano tu ili twende pamoja... Na baadhi ya tafiti zimefanyika wamepata ushahidi wa miji walioishi hawa wanefili ambayo majengo yao tofali moja tu haliwezi bebwa na kifaa chochote cha sasa hivyo wameconclude ulijengwa na MAJITU haya ndio pekee yana uwezo wa kubeba tofali kma zile miji hii mfano ya maeneo hayo ni magharibi wa mto yordani, Pia Hebron, mesopotamia na maeneo ya mashariki ya kati. Kwa maeneo zaidi angalia kiambatanisho cha video hapo chini kuhusu majengo hayo afu uniambie kma mwanadamu wa kawaida angeweza kujenga kulingana na technologia ya kipindi kile!
Pia ushahidi mwingine ulipatikana na mtafiti Georges Vacher de Lapouge na mifupa akiita Giant of castelnau... Mifupa hiyo kwa picha inaonekana ni ya kibidanadam ila ni mikubwa kuliko ya mwanadamu wa kawaida maana estimation ilifika futi 12 hivi ya urefu kwa kutumia mifupa hiyo ya miguu
WALIISHIA WAPI HAWA MAJITU??
1.Kwenye vitabu vya kihistoria na dini wanadai kwamba wanefili walikufa kwenye gharika la Nuhu ila cha kujiuliza kma kweli walikufa kwenye gharika walirudije baadae mfano hao waamori au wayebusi walikuwa ni wanefili (wajuzi mtusaidie hapa)
2. Kuendana na kitabu cha Joshua tunasoma kwamba alidhamiria awaangamize wote ili waweze kuiteka Canaan na kuiweka mikononi mwao..... Ila tunaona HAKUUA wote sababu wengine walikimbia hivyo waliachwa wakaishi miji ya kusini (Gaza ya sasa)
Maswali ya kujiuliza
Je asili yao ni nini mpaka wakawa wakubwa hivyo??
Je uzao wao uliishia wapi??
Je watu hao walikuwepo kweli??
Je kwanini siku hizi hawazaliwi tena??
Ahsanteni kwa kusoma,karibuni kwa michango View attachment 748594 View attachment 748595 View attachment 748596 View attachment 748597
CC wanajukwaa wote bila kuwasahau
Malcom Lumumba, hearly Da'Vinci ,Te Lavista,Kiranga Elungata ,nyabhingi ,Mchawi Mkuu,Eiyer ,Mshana Jr n.k
Vipi hakuwahi kukusimulia kuhusu asili (wazazi au ndugu na jamaa) ya huyo giant?HAWA WATU inaonekana walibaki.bibi yangu alyefariki 1986 akiwa na umri miaka 100 au pungufu kidogo alinisimulia juu ya mtu mkubwa. Alikuwa anabeba mti mzima uliojauka kwa ajili ya kuni kwa familia. ujira wake ulikuwa unamchomea mikungu 3 ya ndizi na maziwa ya mgando. bibi alikuwa ni msichana wakati wa vita ya kwanza ya dunia. baba alizaliwa 1923 kwa rekodi za misheni
Huyu naye alikuwa giant?!Kuna jamaa Alikua anapigana mieleka anaitwa UMAGAAAAAAA