Ushahidi wa kihistoria unathibitisha uwepo wa majitu japo historia inashindwa kututhibitishia asili yao.
Mpaka sasa hatujui haya majitu yalikuwa ni Uzao wa binadamu (Adam) au Ilikuwa ni jamii nyingine tofauti kabisa na jamii ya Binadamu. Hivyo kwenye huu mjadala tungesema: GIANTS DID EXIST, BUT WHERE DID THEY COME FROM AND WHERE ARE THEY NOW ???? Hapa sasa ndipo tungeanza kuja na nadharia za kidini ambazo zinatoka kwenye Biblia, Kurani na hadithi za kidini (Mythologies) au Utafiti wa kisayansi ambao unazungumzua mabadiliko kutokana na muda na mzaingira (Evolution)
Mkuu heshima kwako....
Nafurahi kukuona tena hapa kwa mara nyingine.Tumshukuru Mungu kwa pamoja mkuu na tuendelee kumuomba uzima zaidi na zaidi....
Nina machache ninayotaka kuongezea kwenye maelezo yako...
Hapo juu umeonesha hoja au swali tata kwamba historia inatuthibitishia kuwa hawa majitu walikuwepo lakini haisemi asili yao.Hoja hii ni nzito kweli kweli na huwezi kuamini naandika hapa nikiwa nasikia baridi kutokana na uzito wake.Nasikia baridi kwasababu inanisisimua na inaogopesha na kufurahisha kwa wakati mmoja....
Kuna mambo mengi sana hayapo sawa hasa haya ambayo mimi na wewe tunayaelewa.Sijajuwa kwa hakika ni kwanini hayako sawa ila nina asilimia kadhaa za uhakika kutokana na "dhana"kuwa kuna waliosababisha haya kwasababu mbali mbali....
Historia ikiwa ni moja ya haya "mambo" yasiyo sawa ndio sababu kuu ni kwanini haisemi asili ya hawa majitu ya enzi hizo.Lakini kingine cha kujiuliza ni kwamba,ni kwasababu ipi "wakubwa" wa dunia hawakiri hadharani kuwa kulikuwa na hawa majitu? Nasema hivi kwasababu sijapata kuona mahali wanakiri uwepo wake hadharani.Kama kuna mahali wamekiri basi itakuwa siyo mbaya ukanionesha mkuu...
Katika "pita pita" zangu naweza kusema kwamba zinaweza kuelezea kiduchu sana sababu ya historia kutosema asili ya hawa majitu...
Kwanza suala la wakubwa wa dunia kutokiri hadharani kuwa hapa duniani waliwahi kuwepo majitu linahusiana [kwa mtazamo wangu] moja kwa moja na historia kutosema asili yao.Ninavyoona wakubwa hawa watakapokiri hadharani kuwa majitu walikuwepo moja kwa moja swali litakalofuata ni asili yao na hili ndilo ambalo ni gumu zaidi na nina sababu za kuliona hivi hili...
Kutokana na "maendeleo" ya kiteknologia yaliyopo leo siyo kweli tumeshindwa kufahamu asili yao bali hawataki/hatutaki kusema asili yao kama vile ambavyo hawataki/hatutaki kukiri kuwa waliwahi kuwepo hawa majitu...
Ni ukweli [kwa mujibu wa pita pita zangu] kuwa duniani paliwahi kutembelewa na na viumbe ambao hawakuwa binadamu.Viumbe hawa inadaiwa walikuwepo hapa kabla ya binadam KUWEPO duniani na ujio wa binadamu hapa duniani ulionekana kama kikwazo kwao,naomba hapa nisiende ndani zaidi maana nitakuwa napotelea machakani kwenye ninachotaka kukisema...
Ushahidi wa kutembelewa kwa viumbe hawa nao ni tatizo kama vile ilivyo kuwa tatizo kuelezea asili ya majitu na kwa maana ile ile tunajikuta tunazunguka pale pale.Kwa nukta hii pia naomba nisijikite zaidi hapa maana tutaleta mada nyingine zaidi na ngumu zaidi...
Viumbe hawa ndiyo chanzo kikubwa sana cha tech tunayoiona leo [mtafute Phill Schneider utanielewa kidoogo kwenye hili].Viumbe hawa wameelezwa kwa namna tofauti tofauti kabisa katika masimulizi mbali mbali. Viumbe hawa ndio sababu ya jambo hili tunalolisema leo hii hapa,Majitu.....
Zipo nadharia mbali mbali za kuelezea jambo hili na nadharia ya Alien ni mojawapo na ndiyo sababu nadharia hiyo inapingwa vikali na hao hao wakubwa wa dunia.Uhusika wa viumbe hawa kwenye maarifa ya binadamu imepelekea usiri mkubwa kutokana na kile wanachokihitaji viumbe hao...
Kile wanachokihitaji ndicho kinafanya swali lako lisijibike leo au kesho maana likijibika ukweli utajulikana na kufanya "mission" yao kushindikanika....
Inategemea umesoma nini ili kujuwa wanachokihitaji viumbe hawa lakini niseme tu kuwa kinachofanya swali lako kushindikana ni MAHITAJI ya hawa viumbe kwetu na ikijulikana tu inakuwa tatizo na ndio maana wanaficha kweli kweli na kwa nguvu zote isijulikane...
Kule kisiwani Sardinia,kwa mfano,mafuvu na mifupa yote ya majitu iliyokuwa inafukuliwa na wenyeji wa maeneo yale ilizuiwa na serikali na baadaye kupelekwa Vatican na haikueleweka imeenda wapi baada ya hapo...
Kwenye milima yote ambapo iligundulika mashimo na mahandaki makubwa ambayo ndani yake kulikutwa mafuvu makubwa sana ya majitu haya,kule America ya Kusini [Latin America] milima hiyo yote ilichukuliwa na kanisa Katoliki na baadaye kujengwa kanisa juu ya milima hiyo [siyo mmoja ni mingi sana] na baadaye milango ya mahandaki hiyo kufungwa na kulindwa 24/7....
Maeneo yote ya "ajabu" au mabaki ya viumbe vya "ajabu" yamekuwa yakifungwa na serikali za nchi husika.Mkuu ni nini wanazuia kisijulikane? Kule Sardinia kuna Choppa maalum zinazurula kwenye maeneo "maalum" ambayo yanadaiwa yana mafuvu ya haya majitu...
Kuna eneo moja kuna maziko ya hawa majitu na kuna ngazi za kuingia kwenye jengo kubwa sana la ardhini ambalo ndilo lilitumika kuwazikia hawa majitu.Mzee mmoja anasema kuwa huwa wanashuka huko chini kwenda kufanya ibada zao na wanaamini mafuvu ya majitu hayo yatakuja kurudiwa na uhai tena.Mzee huyu anasema kwamba majitu yae yamezikwa kwa kusimama.....
Jengo hili ambao kwa juu hwezi kulifahamu lina eneo kubwa sana kwa chini na linalindwa hatari na huruhusiwi kuingia huko labda uwe mwenyeji na unafuailiwa unachoenda kufanya kule. Wanaruhusiwa wenyeji tu kuingia humo kwasababu wanakwenda kufanya ibada zao za kijadi hivyo hawawezi kuwa threat sana....
Kama mambo yapo hivi na zaidi ya hivi,unatarajia jibu la swali lako litapatikana kweli?
Viumbe waliosababisha mabadiliko haya ya kizazi ni viumbe gani na wanataka nini?
Sitaki kujibu swali hili japokuwa kuna aina ya majibu tayari wakuu wanayajadili kwenye huu uzi na nyuzi nyingine lakini,kama ulivyosema,umakini na tahadhari ni muhimu katika kuyafuatilia haya na kuamua kipi cha kuamini...
Kwa mtu mwingine haya yanaweza kuwa kama maneno ya mlevi na yasiyokuwa na maana lakini tuwe makini kweli kweli....
Sijaweza kuwa wazi sana na inaonekana kama nimeeleza nusu nusu,nimefanya hivi kwa sababu maalum.Lakini angalau tumepata "dhana" nyingine kuwa kuna wanachohitaji viumbe ambao nao ni kazi kubwa kuwatafutia uthibitisho wa uwepo wao au kujuwa kama kweli waliwahi kuwepo. Naomba tuendelee kutafakari mkuu na ninaamini kuna tutakachopata hapa...