T11
JF-Expert Member
- Oct 11, 2017
- 5,096
- 4,574
920Mkuu kwenye biblia mtu alieishi miaka mingi ni Enoko, na umri wake unakadiriwa ulifika miaka 900 na zaidi kidogo. ila haikufika elfu moja
920Mkuu kwenye biblia mtu alieishi miaka mingi ni Enoko, na umri wake unakadiriwa ulifika miaka 900 na zaidi kidogo. ila haikufika elfu moja
kituko, Kwanza watu/binadamu wa kale walikua na maumbo makubwa sana, ukiachilia mbali hao jamii ya (MAJITU) pia wanadamu wa kawaida tu, wa enzi izo walikua na miili na maumbo makubwa hivyo ilikua rahisi pengine kufanya mapenz na hiyo mijitu.Kaka hapo mbona Pagumu kidogo, maana kama hao ni magiant basi hata uume wao pia ni mkubwa kuendana na size ya miiki yao, waliwezaje kuwaingilia wanawake wa kawaida na kuwapa mimba?
We jamaa muongo sana.Hizo story nimezikuta hapa zakhemu kibonde Maji Jamaa aliemda kuoa akachukua mshenga MTU mbili Tu. Mkwe kawauliza wenzenu wako wapi? Tumepika chakula kingi.jamaa akasema sisi wawili tunatosha.Jamaa akaletewa sinia akafuta akanywa na togwa ndoo lita kumi.kulikua na gogo la mnazi limeanguka uwanjali kalibeba amamuuliza mkwe niliweke wapi? Mkwe macho yamemtoka gogo la kubeba watu watano,baada ya kuondoka mahari ilirudishwa. Kuna jamaaa huyu nilimshuhudia anaitwa wa mmongo.jamaa alikua naguvu hatali kwa madreva wa matipa ya mchanga miaka ya 2000 lazima umjue. Askari maturubai walikuwa wanamuogopa sikumoja nami nipo kawajambisha askali saba wakatulia mwanaume anakatiza zake njia ya kibulugwa.alikua anadhulumu wapakiaji wenzake ukitoka mgao hella yote anachukua yeye. Aliwahi kumpiga bondi japo si bondia laundi ya tatu mtu kazima.muda wote koti kubwa na buti anatroti kama mbwa. Mpaka raia walipo mchoka ikaaandaliwa mechi timu mmoja ikachukua kama baunsa majoe huko.dk za mwisho mechi ikaanza twimbili timu zote mashabiki wakachenjia piga sana na kumuacha uwanjani wakijua kavuta.kaja kuokotwa na wanajeshi baada ya kujivuta hadi kwenye vichaka anavidonda mwilimzima kaenda kuvutia temeke baada ya siku tatu. Huyo ndo mbabe was zakhem wamongo
kituko, Kwanza watu/binadamu wa kale walikua na maumbo makubwa sana, ukiachilia mbali hao jamii ya (MAJITU) pia wanadamu wa kawaida tu, wa enzi izo walikua na miili na maumbo makubwa hivyo ilikua rahisi pengine kufanya mapenz na hiyo mijitu.
Lakini pia hao giant ni miroho ambayo pia ingeweza kuwaungilia binadamu kwa njia tofauti tofauti, kwani majini yanauwezo wa kujigeuza kivyovyote kwaiyo hata kama walikua na maumbo ya kutisha pia wangeweza kujigeuza kuwa mfano wa binadamu kama hao waliyokuwepo enzi hizo, kwahiyo inawezekana kabisa.
Kwani Malaika wana hisia za kufanya mapenzi mkuu?
Dinosaurs walikuwepo kweli...hata ushahidi wa fuvu lao lipo china na AfrikaNi kweli mkuu hii hoja yako hata mafuvu ya wanyama wa zamani sio kma ya hawa wa sasa sielewi kwanni
Mfano kwenye bible Ayubu anamuongelea mnyama anaitwa BEHEMOTH ambao wengine wanadai ni dinosaur.....huyo kiumbe kwa maelezo yake anasema ndio mnyama mkubwa duniani na alikuwa na mifupa kama CHUMA na anatema cheche!!! Hao wanyama sahvi hawapo sijui wametoweka wapi.... Ipo Ayubu 40 sura nzima anamsifia mnyama huyo
Ukijuliza sana mwanadamu kuishi miaka 1000 kweli sio jambo la kitoto lazima mwili wake uwe ''umejibeba'' haswaa ili aweze kuhimili magonjwa na mabadiliko ya hali ya hewa kwa miaka yote hiyo
Mkuu naongelea BEHEMOTH sio dinosaurs..... Huyo mnyama ameongelewa kwenye AYUBU 40....kwamba ana mbavu za chuma na mkubwa kma mnazi na anatema cheche!!! Huenda ni tofauti na dinosaurs maana sio kwa maelezo yale ya job!!Dinosaurs walikuwepo kweli...hata ushahidi wa fuvu lao lipo china na Afrika
Lakini Donosaurs sio wanyama ila wapo kwenye jamii ya Ndege na wanaruka.
Dinosaurs kamwe hawatemi moto...waliokuwa wakitema moto ni Dragons.
Mkuu Tanzania 80% wanaamini vitabu vya dini ndio shida ukiwaletea mada ya asili za wanadamu bila reference kwenye vitabu vya dini wanaishia kukupinga tu kisa mahaba ya kiimani!!Mkiamini bible mtapotea tafuteni vitabu vizito vilivyofichwa,tatizo hamjishughulishi kuvitafuta,wale walojiunga na forum ya quora kuna nondo kule za maana mtajua haya vizr.
tunaambiwa walikua watoto wa MUNGU, kwa kipindi hicho wakizubgumzia watoto wa MUNGU walikua wanamaanisha malaika.1. Hata kama unasema hao Binadamu wa Zamani walikuwa ni wakubwa bado hawakuwa wakubwa kuliko hao majitu, na ndio maana tofauti ilionekana kati ya hao Binadamu wa kawaida (Wanawa watu) na hiyo mijitu
2. Kumbe hao Majitu yalikuwa ni Miroho, so walijigeuza na kuwa size ya kawaida ya watu waliokiwepo na kifanya nao tendo la ndoa
Kwahyo unataka useme watu wanaoingiliwaga na mapepo wakifanya mapenzi wanazaa wanadamu wa ajabu au mapepo!
Maana kusema roho imemuingilia mtu aliyepo katika mwili inabidi uelezee hiyo roho inabadilishaje vitu kama mbegu za mwanaume hadi kuwa mbegu za hao mapepo(sijui umenipata)..
Maana kusema tuu pepo limemuingilia mtu afanye mapenzi na mwanadamu ndio kiumbe cha ajabu kikazaliwa bado hakijibu swali la msingi kuwa mbegu zilizotoka ni za mwanadamu au za huyo pepo sijui malaika
poa tuu haina kwere na noma. Yani hata mimi kunitag tuu.Habari za asbuhi wana jukwaa, niende moja kwa moja kwenye mada kama kichwa cha habari kinavyosema je Giants/Majitu makubwa yanayoelezwa kufika hadi futi 45 waliwahi kuishi hapa duniani?? na kama waliwahi kuishi walitoweka wapi?? Na kwanini siku hizi hawazaliwi tena??
Hadithi za uwepo wa hawa watu zipo karibu katika kila kabila na jamii hapa duniani kwa mfano wahispania wana historia ya Giant (basajaun) ubelgiji alikuwepo antigoon, indonesia (Buto), waebrania (Goliath), Irimu wa wakikuyu na Yalmavuz wa uturuki nikitaja kwa uchache.
Hata vitabu vya kidini na kihistoria zimewaongelea hawa watu embu tuone mifano kidogo
WANEFILI
Mwanzao 6:4
4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa
Kwa tafsiri ya kiingereza
Genesis 6:4
4There were giants in the earth in those days; and also after that, when the sons of God came in unto the daughters of men, and they bare children to them, the same became mighty men which were of old, men of renown.
Inaelezwa watu hawa walikuwa ni majitu makubwa yenye nguvu yanaongelewa pia kwenye vitabu vya kihistoria kma Book of giants tunaona watoto wa Semyaza kina ohyah na hahyah walikuwa ni majitu makubwa sana yanazidi futi 100!!!..... Pia kitabu cha Enoko (book of watchers) anaongelea watu hawa ambao walikuwa ni wakubwa sana na walikuwa wakitesa wanadamu maana walidai vyakula kuliko viwango vyao vya uzalishaji na wakaanza hadi kuwala wanadamu wenyewe.... So dunia ilijaa vurugu tupu kipindi cha kabla ya gharika sababu ya hawa WANEFILI
2. WANA WA ANAKI (ANNUNAKI)
Kwenye vitabu vya dini hawa pia wanaongelewa kama WANEFILI ambao ni majitu marefu yenye nguvu sana
Hesabu 13:33
32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.
33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
Walisema haya baada ya waisraeli kutuma wapelelezi kwenda kukagua nchi ya kanaan iliyokaliwa na wana wa Canaan mtoto wa Ham wakiwemo Waamori,waamaleki,wayebusi,wahiti,Hivitites,Gilgashites n.k ambao kwenye biblia wanaelezwa kma majitu makubwa na marefu yaliyoishi Canaan kipindi waisraeli wanataka kurudi kwenye nchi yao ya ahadi
Amos 2:9
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini
NB:Mierezi ni miti mirefu sana sasa iliopatikana huko lebanon
QURAN TAKATIFU
Mfano ambao upo ndani ya Quran ni Mfalme Og wa Bashan au kwa kiarabu alifahamika kma Uj ibn Anaq huyu alikuwa mfalme wa kale ambaye alikuwa ni mrefu sana na ana mwili mkubwa tunaambiwa alikuwa na futi 13 na alikuwa na nguvu sana,pia kwenye Quran anatajwa Jitu linaitwa Jalut ambalo nalo linaelezwa alikuwa mtu mkubwa mwenye maguvu sana kuliko umbo la kawaida la mwanadamu.
GILGAMESH
Huyu ametajwa na Enocko kwenye book of giants kwamba alikuwa ni JITU kubwa sana lenye manguvu kiasi kwamba lilitangaza vita na Mbingu..... Inadaiwa alitawala ufalme wa sumeria (Uruk) enzi za kale na alitawala kwa miaka 126... Ana stori ndefu kidogo itabidi afunguliwe uzi siku moja (Epic of gilgamesh) ila kwa leo nimemtaja tu kma mmoja ya GIANTS
USHAHIDI WA KISAYANSI
Hii ni baadhi ya mifano tu ili twende pamoja... Na baadhi ya tafiti zimefanyika wamepata ushahidi wa miji walioishi hawa wanefili ambayo majengo yao tofali moja tu haliwezi bebwa na kifaa chochote cha sasa hivyo wameconclude ulijengwa na MAJITU haya ndio pekee yana uwezo wa kubeba tofali kma zile miji hii mfano ya maeneo hayo ni magharibi wa mto yordani, Pia Hebron, mesopotamia na maeneo ya mashariki ya kati. Kwa maeneo zaidi angalia kiambatanisho cha video hapo chini kuhusu majengo hayo afu uniambie kma mwanadamu wa kawaida angeweza kujenga kulingana na technologia ya kipindi kile!
Pia ushahidi mwingine ulipatikana na mtafiti Georges Vacher de Lapouge na mifupa akiita Giant of castelnau... Mifupa hiyo kwa picha inaonekana ni ya kibidanadam ila ni mikubwa kuliko ya mwanadamu wa kawaida maana estimation ilifika futi 12 hivi ya urefu kwa kutumia mifupa hiyo ya miguu
WALIISHIA WAPI HAWA MAJITU??
1.Kwenye vitabu vya kihistoria na dini wanadai kwamba wanefili walikufa kwenye gharika la Nuhu ila cha kujiuliza kma kweli walikufa kwenye gharika walirudije baadae mfano hao waamori au wayebusi walikuwa ni wanefili (wajuzi mtusaidie hapa)
2. Kuendana na kitabu cha Joshua tunasoma kwamba alidhamiria awaangamize wote ili waweze kuiteka Canaan na kuiweka mikononi mwao..... Ila tunaona HAKUUA wote sababu wengine walikimbia hivyo waliachwa wakaishi miji ya kusini (Gaza ya sasa)
Maswali ya kujiuliza
Je asili yao ni nini mpaka wakawa wakubwa hivyo??
Je uzao wao uliishia wapi??
Je watu hao walikuwepo kweli??
Je kwanini siku hizi hawazaliwi tena??
Ahsanteni kwa kusoma,karibuni kwa michango View attachment 748594 View attachment 748595 View attachment 748596 View attachment 748597
CC wanajukwaa wote bila kuwasahau
Malcom Lumumba, hearly Da'Vinci ,Te Lavista,Kiranga Elungata ,nyabhingi ,Mchawi Mkuu,Eiyer ,Mshana Jr n.k
Mkuu mvyosema malaika hawawezi kuzaa na mtu sababu ni roho mpaka wawe na mwili wa kibinadamu,Ni kweli malaika kama malaika au ROHO yeyote hawezi kuzalisha sababu haikuumbwa kwa sababu hiyo ila mwili unaweza kuzalisha sababu uliumbwa kwa kazi hiyo na ndipo mjadala unapoaanza.
kutokana na ushahidi wa kibiblia (sijui imani yako utaniradhi) tunaweza kuona mwandishi wa kitabu cha Yuda ambaye alikuwa kaka yake Yesu anaongelea kisa hiki cha malaika kuwaingilia wanadamu,twende pamoja
Waraka wa YUDA
6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.
Hapa tukisoma tunaona wazi mwandishi anafananisha dhambi waliofanya watu wa sodom ya uzinzi kma walivyofanya wale malaika.... Neno JINSI MOJA NA HAWA.... Linaweza kusummarise kuwa iliwezekana malaika kuwaingilia wanadamu na kuwazalisha viumbe na watafiti wengine wanadai ndio moja ya sababu Mungu aliamua kufuta uzao huo kwa gharika ila Yuda hapa anaelezea kuwa malaika hao kwa sasa wamefungwa kuzimu hivyo kuna uwezekano kwa sasa hawana uwezo huo wa kuhamisha asili yao kwa mwili kama walivyofanya kwa WANEFILI
2. Nadharia ya pili malaika kuvaa mwili wa binadamu ili aweze kuzalisha however swali lako linahoji kivpi anaweza hamisha genes zake
Kwa maoni yangu binafsi nachoona kuna uwezekani mtoto asiwe na gene yoyote ya kimapepo/kimalaika sababu mwili umezaa na mwili ila MAKUZI yanaweza kumbadilisha huyo mtoto kuwa wa mazingara..... Mfano mtoto aliyezaliwa kibinadamu akachukuliwa na wachawi lazima atakua tofauti na mtoto wa kawaida maana atapandikizwa matambiko ya ajabu yanayomuwezesha kupaa...kuyeyuka....kuua....nguvu za ajabu n.k
Hivyo kwa nadharia hii ya pili hao wanefili wanaweza kuwa walizaliwa kwa malaika kuvaa miili ya binadamu wengine na watoto walizaliwa kma wanadamu tu ila makuzi mfano waliwafanyia matambiko.... Walihamishia mapepo yao mengine humo..... Waliwapa nguvu zao n.k mwisho wa siku miili yao ikabadilika ikawa ya kimazingara maana mfano kma leo hii mchawi anaweza akakuotesha busha...tumbo n.k kwa nni tusiamini hao MALAIKA walikuwa na uwezo wa kuwapa urefu wa ajabu... Nguvu za ajabu nyingine kma leo hii tu wachawi wakawaida wanavyoweza kuotesha viungo flani vya mwili
Sijui it makes sense now ila all in all nakubaliana na ww malaika HAWEZI kumzalisha mwanadamu ila inawezekana kwa exception nlizotaja hapo juu
Ni hayo tu labda tuwaite na wajuvi wengine watusaidie
Cc : SALA NA KAZI @Malcom Lumumba [USER=113939]Palantir hearly Eiyer Kudo900 Mshana Jr[/USER]