Diamond Platnumz: Mdee ni Mzigo Jimbo la Kawe

Diamond Platnumz: Mdee ni Mzigo Jimbo la Kawe

Diamond si anasema kwamba JK ni rafiki yake sana kiasi kwamba, majuzi JK amempigia simu akiwa Marekani na kumwuliza anavaa saizi gani ya koti, ili amletee zawadi ya koti!!!???? Kama JK ni rafiki yake kihivyo, kwa nini JK asimtafutie kiwanja sehemu zenye barabara za lami kama Oyster Bay, au akamjengea barabara ya lami kwenda Madale? Urafiki au unafiki ??????
 
yeye asubiri kukata kiuno majukwaani...., siasa haijui.
 
Kama wewe ni mbunge na katika jimbo lako kero hazitatuliwi, ujue tu hauna ushawishi.

Katika hali hiyo ya kukosa ushawishi, basi hufai kuwa mwakilishi wa wananchi husika. It's simple as that.

Halima, time to go!

Kwa hiyo mnataka kutudhihirishia ccm nchi imewashinda manake hata sikupeleki mbali hapo kinondoni manzese nenda temeke wanafunzi wanakaa chini hamna madawati nikienda kwenye huduma ya vyoo ndio mama utazimia sasa huko mikoani ndio wanasomea chini ya.mwembe mwaka wa 53 huu ndani ya utawala wa makoloni ccm back Tanganyika.
 
Michango ya aibu kabisa wikendi hii kutoka kwa Great Thinkers. Kauli za Amina hii hutoka kwenye vinywaji Vya wanywa gongo .

Sio aibu ndio hazina ccm iliyo nayo kwa sasa ni sheeeda.
 
Mbona alipokuwa Mbagala hakuongea huo upiuzi
CCM wamekaa hapo miaka 50 sembuse huyu wa miaka 4? Apelek uccm wake huko mbagala jalalani
 
Mzinzi yeyote hutokwa na aibu,sasa teja wa uzinzi ndo mnaweza chukua ksuli yake na kuanza kuisema cdm,yapo makubwa cdm imesukuma yakawa mbona hamyasemi,atuelize hbr za kikongwe wake,hiyo ndo level yavufahsmu wake
 
Kama wewe ni mbunge na katika jimbo lako kero hazitatuliwi, ujue tu hauna ushawishi.

Katika hali hiyo ya kukosa ushawishi, basi hufai kuwa mwakilishi wa wananchi husika. It's simple as that.

Halima, time to go!

Kwa hiyo hata kero ambazo nchi nzima inapitia toka uhuru ndo kusema ccm imekosa ushawishi hvo instakiwa itoke?,
its simple as that
Ccm,time to go
 
Dont ask what America have done to you! Ask what have you done to America. J F K

Mhh!! haya ndiyo majibu ya wanasiasa na washabiki wapuuzi wasiofaa kuigwa kwani hata penye hoja wao ni siasa tu na kulinda wachoiita maslahi ya chama kwa kuficha ukweli.
 
Sasa halima mdee ajenge barabara kwa hela ipi kama sio kupitia kodi za wananchi?
Sehemu nyingi sana ambamo ni majimbo ya upinzani,wananchi wamecheleweshewa sana huduma za kijamii Zikiwemo huduma za maji safi mf
ubungo,barabara mf kawe,umeme,afya nk nk.
Tuache kuwalaumu wawakilishi wetu kwani wamefanya makubwa nje na barabara..serikali ilaumiwe kwa hili na si mdee.

Nataka kujua kiukweli mbunge anapotoa ahadi kwamba atahakikisha matatizo yote ya wananchi yanatatuliwa, hivi ni mbinu gani anatarajia kutumia iwapo yeye si serikali! So anapotoa ahadi means anajua fika ni njia gani atakayoitumia ku accomplish yote yanayowatatiza wananchi! Vinginevyo kama nayeye atakuja tu kukaa kusubiri utekelezaji wa serikali basi nadhani hakuna umuhimu wa hiki cheo, yeye hatakuwa na msaada wowote basi kwa wananchi, ndii hapo tunasema sasa ni kwamba amegombea kupata nafasi au fursa binafsi!
 
Mbona alipokuwa Mbagala hakuongea huo upiuzi
CCM wamekaa hapo miaka 50 sembuse huyu wa miaka 4? Apelek uccm wake huko mbagala jalalani

Mwenye majibu kama yako ni yule tu mwenye zaidi ya miaka hamsini lakini kwa diamond yuko sahihi kumwambia mbuge wake kwani hana hiyo miaka hamsini
 
Mzinzi yeyote hutokwa na aibu,sasa teja wa uzinzi ndo mnaweza chukua ksuli yake na kuanza kuisema cdm,yapo makubwa cdm imesukuma yakawa mbona hamyasemi,atuelize hbr za kikongwe wake,hiyo ndo level yavufahsmu wake

kusukuma ukimaanisha nini!! kuwa wazi kwa kuanisha cdm tumefanya 1,2 nk
 
Diamond si anasema kwamba JK ni rafiki yake sana kiasi kwamba, majuzi JK amempigia simu akiwa Marekani na kumwuliza anavaa saizi gani ya koti, ili amletee zawadi ya koti!!!???? Kama JK ni rafiki yake kihivyo, kwa nini JK asimtafutie kiwanja sehemu zenye barabara za lami kama Oyster Bay, au akamjengea barabara ya lami kwenda Madale? Urafiki au unafiki ??????

Jinga sana jibu hoja acha viroja
 
Afadhali hata wasanii wanaliona hilo.

Manispaa ya Kinondoni imekazana kuweka lami mitaa yote ya Oysterbay waliko wanene.

Huku kwetu Kawe hakuna kabisa barabara za kwenye mitaa.

Ndio maana niliwahi kusema heri Mtemvu kule Temeke anafanya mambo yanayoonekana kuliko huyu kipeperushi cha CHADEMA.

Lakini mbaya zaidi, kwa hasira za wananchi bado wataichagua CHADEMA kwa vile huku KAWE CCM haipo kusikiliza kero za wananchi na kuzishughulikia.
Watu mkiwa Dar-es-salaam hamzijui shida zinazowakabili wakazi wa japo hapo Mkuranga tu kutokana na ubovu wa barabara na huku mbunge wa jimbo hilo ni naibu waziri wa fedha. Yaani hii nchi nyie acheni tu, na tumuombe sana Mungu huyu Kikwete aondoke salama. Miaka yake kumi imekuwa ni michungu mno kiasi cha kwamba waliokuwa wanamshabikia hivi leo wanajuta. Yaani barabara hata ambazo angalau zilikuwa na Changalawe wakati wa Mkapa, na changalawe zimeondoka limebaki vumbi mashimo na madimbwi ya maji tu. Naongea kwa uchungu sana, kutokana na adha ninayoiona huko. Nyie wa daresalamu hata hampaswi kusema kabisa.
 
Hivi majukumu ya mbunge kwa serikali ni yapi? Wewe kama mbunge wakati unakuja kuomba kura ulituahidi nini; na yale ambayo ulituahidi yasipotekelezwa nani wa kwanza napaswa kwenda kumshika shati?

Hebu tuanze nahuyu alietuahidi maisha bora kwanza mana na barabara nzuri ziko humo humo!!
 
kusukuma ukimaanisha nini!! kuwa wazi kwa kuanisha cdm tumefanya 1,2 nk

Tuanze na hawa tuliowapa dhamana kwanza ya kukusanya kodi yetu na kugawana kwa masalfeti na masandalusi kisha ndo turudi kwa cdm!!
 
Back
Top Bottom