Ila afahamu kwenye tatizo wilaya ya kinondoni sio huko madale tu, pia Halima mdee hana kampuni ya ujenzi yeye anategema mipango thabiti ya halmashauri ya kinondoni ambayo ndiyo ina vipaumbele vyote vya barabara mezani, badala ya kumlaumu moja kwa moja aende kwanza kwenye Ofisi ya mtendaji kata wa eneo lenye tatizo aelezwe tatizo ni nani? pamoja na hayo kwa kuwa yeye amefanikiwa sana kwenye medan ya music basi aeleze kama mwananchi aliyeguswa na kero hiyo anasaidiaje japo vifusi tu?Wana Ukumbi,
Msanii maarufu nchini mwenye mafanikio makubwa katika sanaa ya mziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz, amevunja ukimya wake juu ya ubovu wa barabara iendayo Madale ambayo ipo kwenye jimbo la Kawe chini ya Halima Mdee.
Msanii huyo ameelekeza lawama zake kwa mbunge huyo wa kupitia tiketi ya CHADEMA kwa kuwa Halima Mdee aliahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa katika kipindi chake cha ubunge atahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami, lakini hadi hii leo barabara imejaa tope tu!
Diamond alieleza masikitiko yake huyo kupitia katika kituo cha Clouds TV pale alipoulizwa swali kuhusu makazi yake mapya yaliyopo katika jimbo la Kawe na ndipo hapo akafunguka kuhusu suala hilo la kero ya barabara ambalo lina muda mrefu alijashughulikiwa na mbunge Halima Mdee.