Diamond Platnumz: Mdee ni Mzigo Jimbo la Kawe

Diamond Platnumz: Mdee ni Mzigo Jimbo la Kawe

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,830
Wana Ukumbi,

Msanii maarufu nchini mwenye mafanikio makubwa katika sanaa ya mziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz, amevunja ukimya wake juu ya ubovu wa barabara iendayo Madale ambayo ipo kwenye jimbo la Kawe chini ya Halima Mdee.

Msanii huyo ameelekeza lawama zake kwa mbunge huyo wa kupitia tiketi ya CHADEMA kwa kuwa Halima Mdee aliahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa katika kipindi chake cha ubunge atahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami, lakini hadi hii leo barabara imejaa tope tu!

Diamond alieleza masikitiko yake huyo kupitia katika kituo cha Clouds TV pale alipoulizwa swali kuhusu makazi yake mapya yaliyopo katika jimbo la Kawe na ndipo hapo akafunguka kuhusu suala hilo la kero ya barabara ambalo lina muda mrefu alijashughulikiwa na mbunge Halima Mdee.
 
Afadhali hata wasanii wanaliona hilo.

Manispaa ya Kinondoni imekazana kuweka lami mitaa yote ya Oysterbay waliko wanene.

Huku kwetu Kawe hakuna kabisa barabara za kwenye mitaa.

Ndio maana niliwahi kusema heri Mtemvu kule Temeke anafanya mambo yanayoonekana kuliko huyu kipeperushi cha CHADEMA.

Lakini mbaya zaidi, kwa hasira za wananchi bado wataichagua CHADEMA kwa vile huku KAWE CCM haipo kusikiliza kero za wananchi na kuzishughulikia.
 
Kwani Halima Mdee anakusanya kodi kutoka kwa wananchi au ameskia wapi kuwa mbunge ndio mwenye maamuzi ya barabara gani ijengwe? Acha Umbulula wewe

Kama wewe ni mbunge na katika jimbo lako kero hazitatuliwi, ujue tu hauna ushawishi.

Katika hali hiyo ya kukosa ushawishi, basi hufai kuwa mwakilishi wa wananchi husika. It's simple as that.

Halima, time to go!
 
Matokeo ya kufikiri kwa masaburi. Halima anawaahidi kuwajengea barabara yeye ni serikali? Tangu lini wabunge wakajenga barabara. Serikali ndiyo ya kulaumiwa na si HM.

Kwanini alitoa ahadi kwa wananchi kuwa katika ubunge wake huu atahakikisha barabara inajengwa? Ikiwa alijua yeye sio serikali in the first place!
 
Hivi cdm ndio wanakusanya kodi? avumilie tu hayo ndiyo maisha bora aliyoahidiwa na kikwete
 
Back
Top Bottom