Kwa sasa mmepoteza vitu vifuatavyo;
1,integrity
2,ownership
3,credibility
4, Honesty
Integrity( Uadilifu)
Sasa chadema hakuna uadilifu tena , mmebaki kupuyanga tu na kukosa jambo la kuwafanya muwe waadilifu machoni pa watanzania na wanachama wenu , na hii ndio imewagawa mpaka sasa kubalini mkatae kuna kundi la waadilifu bado ni watiifu kwa Dr slaa aliyeweka misingi mizuri ya uadilifu na kuisimamia ndani ya chadema , e.g humu jukwaani wamo kina IDAWA, MTAZAMO n.k ambao hawaipendi ccm lakini wako chadema ila si wanachama hai wana subiri kuhuishwa upya kwa chadema sijui itakuwa lini? Badilikeni
2, Ownership ( umilikaji)
Kwa sasa wapenzi na wanachama wa chadema hawana umiliki wa chadema tena , kimebaki chama cha wachache wenye pesa , ndio maana hata Leo ukianzisha harambee hawachangii maana umilikaji sio wa wanachama tena Bali kundi dogo, hawa wamebaki yatima , mmekopi ya ccm mmepeleka chadema , hvyo lazima mbinu za kiccm zitumike ambazo wao wanaanza kuachana nazo
3, Credibility
Chadema kwa sasa ile credibility na upokelewaji wake umepungua ndani ya jamii na hii heshima inapungua siku baada ya siku msipikuwa makini mtakuwa kama nccr , kinachowabeba ni kutaka kushindana tu ccm ili mtajwe tajwe lakini kiuhalsia mmepoteza sana heshima nzuri mliyokuwa mmejijengea toka 2007, situkeni
4, Honesty ( Uongofu/ uaminifu)
Kwa hili ndilo limezidi kuwapotezea sifa kwa wanachama wenu , moja suala la UKUTA mlilipigia debe japo halikuwa na maana yoyote yaani kama ni silaa ni risasi 1 iliyobaki kwenu either ujiue au umuue adui , mwisho wa siku imewaua ninyi , maana kauli za viongozi, wenu kama msigwa , nanukuu " anayeogopa polisi hafai , lazima totafautishe Men na Boys" hii kauli sijui ataificha wapi ?
Maana ni kauli tata tata tu mfano ile ya kipindi kile nanukuu " atakayemuunga mkono lowasa akapimwe akili"
Kauli tata kabla ya kuhairishwa ukuta za mnyika, mbowe ,tundu lisu n.k zimewaondolea uaminifu kwa wanachama wenu
Pia imewaondolea uaminifu kwa vyama vingine vya upinzani , maana kuanzisha UKUTA ilikuwa ni kuua UKAWA bila makubaliano , hvyo ukawa imekufa kibudu , UKUTA imekufa kibudu sasa ni mmeanzisha internal strife katika vyama vya upunzani maana hakuna wa kuwaamini tena
Ushauri , mkubali mmekosea sana na kosa lenu ni Kumkaribisha Lowasa na kingine zaidi hamuaminiki katika kile mnachosimamia
" Kiongozi Mzuri ni yule anayelinda kauli zake na kuzisimamia hata kama kawekewa mtutu wa bunduki like kina Che Guevara na the like ". Sio nyie wajasiliamali wa siasa
Nimeshauri nasubiri Matusi