Baada ya jana kuahirishwa maandamano ya UKUTA kwa mwezi mmoja zimefumuka post za kukejeli hiki kitendo
Kila mtu kasema lake, lakini wengi wakijikita kwenye kusema kuwa eti
-CHADEMA ni vigeugeu
-CHADEMA ni mabingwa wa kubadili gia angani
-CHADEMA inapoteza mwelekeo chini ya Lowassa (utafikiri ndio mwenyekiti)
Kejeli ni nyingi kweli na hili halina tatizo kwakuwa wale waliokuwa wamejiandaa kuumiza wananchi wasio na hatia hawataweza tena kufanya hivyo! Maandalizi yalikuwa mengi na kabambe mno ya kukipaka damu chadema kama maandamano haya yangefanyika
Kichekesho na dhikaha ya kukera sana ni wale wanaojifanya kutaka kuihama CHADEMA eti tu kwakuwa wameahirisha maandamano! Hilo tu likufanye uhame chama? Maandamano yangefanyika wewe ungeenda? Uhame Chadema uende chama gani? CCM? kama kuhama chama kungekuwa rahisi hivyo Lipumba asingeng'ang'ania cuf....unazi wetu uko nyuma ya keyboard tuu lakini waandamanaji wa kweli wasioogopa chochote iwe virungu iwe maji ya kuwasha ile jela, hawapo hapa na hawa wamekubaliana na maamuzi! Hakuna haja ya kutishia kuhama FANYA SASA
Dhima ya CHADEMA haikuwa kuandamana!maandamano huwa silaha ya mwisho kabisa kwenye nchi ya kidemokrasia kama njia zote zikishindikana
CHADEMA kwenye hili wamefanikiwa sana tena sana, harakati za ukuta zimeleta matunda mengi
Maamuzi mengi ya kibabe yamepungua ama kubatilishwa
Kupayuka payuka kumepungua
Utawala wa sheria unaanza kurejewa
Utawala ulioanza kujisahau umekuwa makini zaidi sasa
Viongozi wengi wameamua kuingia kwenye mazungumzo
CHADEMA SASA IMEANZA KUSIKILIZWA NA ITASILIKOLIZWA..hii ndio ilikuwa dhima ya yao KUSIKILIZWA
CHADEMA itasikilizwa bila kusababisha madhara kwa wananchi bila uharibifu wa mali na kwa gharama bei chee kabisa
CHADEMA imepiga hatua kumi zaidi mbele waliokamatwa kwa mashtaka ya kutunga na kunjuka ni viongozi tuu raia hawafiki watano! Huu ni ushindi mkubwa sana
Kama unahama CHADEMA Salam zao huko uendako
1.CHADEMA ni vigeugeu
2.CHADEMA ni mabingwa wa kubadili gia angani
3.CHADEMA inapoteza mwelekeo chini ya Lowassa
Hakuna ubishi juu ya hayo matatu nyie ndo tabia zenu hizo kila mtu anajua
4. kama kuhama chama kungekuwa rahisi hivyo Lipumba asingeng'ang'ania cuf
Ata Nyerere alisema chama sio baba yangu wala mama yangu kuhama chama ni rahisi tu kama kunywa maji.Zito Lowasa wote wamehama chama
5 Waandamanaji wa kweli wasioogopa chochote iwe virungu iwe maji ya kuwasha ile jela, hawapo hapa.
Unawakana wenzako wa hapa jamii forum kweli nyie usaliti uko damuni, wenzio leo unawatenga kisa wanaongea ukweli.
6. Dhima ya CHADEMA haikuwa kuandamana.
Hapa umechekesha kama hamkutaka kuandamana mlikua mnalialia nini?
7. Maamuzi mengi ya kibabe yamepungua ama kubatilishwa
Kupayuka payuka kumepungua
Utawala wa sheria unaanza kurejewa
Utawala ulioanza kujisahau umekuwa makini zaidi sasa
Viongozi wengi wameamua kuingia kwenye mazungumzo
CHADEMA SASA IMEANZA KUSIKILIZWA NA ITASILIKOLIZWA
Uache Uongo hakujawahi tokea maamuzi ya kibabe nchi hii wala kupayuka wala utwala ambao hawafuati sheria. Utawala huu uko makini toka uanze ndomana mnabaki kulialia tu njiani.
Hakuna mtu wakuja kuwasikiliza nyie wahuni jifarijini tu Ikulu mtaisikia kwenye magazeti unafikiri ni utawala wa JK HUU. Endeleeni kuisoma namba.