Dhihaka ya karne: Eti wanataka kuhama CHADEMA

Dhihaka ya karne: Eti wanataka kuhama CHADEMA

Baada ya jana kuahirishwa maandamano ya UKUTA kwa mwezi mmoja zimefumuka post za kukejeli hiki kitendo

Kila mtu kasema lake, lakini wengi wakijikita kwenye kusema kuwa eti

-CHADEMA ni vigeugeu
-CHADEMA ni mabingwa wa kubadili gia angani
-CHADEMA inapoteza mwelekeo chini ya Lowassa (utafikiri ndio mwenyekiti)

Kejeli ni nyingi kweli na hili halina tatizo kwakuwa wale waliokuwa wamejiandaa kuumiza wananchi wasio na hatia hawataweza tena kufanya hivyo! Maandalizi yalikuwa mengi na kabambe mno ya kukipaka damu chadema kama maandamano haya yangefanyika
Kichekesho na dhikaha ya kukera sana ni wale wanaojifanya kutaka kuihama CHADEMA eti tu kwakuwa wameahirisha maandamano! Hilo tu likufanye uhame chama? Maandamano yangefanyika wewe ungeenda? Uhame Chadema uende chama gani? CCM? kama kuhama chama kungekuwa rahisi hivyo Lipumba asingeng'ang'ania cuf....unazi wetu uko nyuma ya keyboard tuu lakini waandamanaji wa kweli wasioogopa chochote iwe virungu iwe maji ya kuwasha ile jela, hawapo hapa na hawa wamekubaliana na maamuzi! Hakuna haja ya kutishia kuhama FANYA SASA

Dhima ya CHADEMA haikuwa kuandamana!maandamano huwa silaha ya mwisho kabisa kwenye nchi ya kidemokrasia kama njia zote zikishindikana

CHADEMA kwenye hili wamefanikiwa sana tena sana, harakati za ukuta zimeleta matunda mengi

Maamuzi mengi ya kibabe yamepungua ama kubatilishwa

Kupayuka payuka kumepungua

Utawala wa sheria unaanza kurejewa

Utawala ulioanza kujisahau umekuwa makini zaidi sasa

Viongozi wengi wameamua kuingia kwenye mazungumzo

CHADEMA SASA IMEANZA KUSIKILIZWA NA ITASILIKOLIZWA..hii ndio ilikuwa dhima ya yao KUSIKILIZWA

CHADEMA itasikilizwa bila kusababisha madhara kwa wananchi bila uharibifu wa mali na kwa gharama bei chee kabisa

CHADEMA imepiga hatua kumi zaidi mbele waliokamatwa kwa mashtaka ya kutunga na kunjuka ni viongozi tuu raia hawafiki watano! Huu ni ushindi mkubwa sana
Kama unahama CHADEMA Salam zao huko uendako
Mimi hasira yangu kutumia viongozi wa dini kujitafutia umaarufu. Nahisi hao ni wale viongozi wa dini njaa tuliyowaona wkt mchakato wa urais ndani ya ccm
 
umenena mkuu wengi humu wana ushabiki mandazi wengi walitaka kuona majeraha ya watu
 
Hivi nyie watu mnawafikiliaje watu wenzenu. Mnawafikiria kuwa ni mambumbu kiasi cha kuwaongopea namna hiyo?
Kwani ni nani alisema atafanya maandamano na mikutano tena isiyo na kikomo kuanzia tarehe mosi september?
Kama ilijuwa kuwa maandamano si kitu kizuri kitamwaga damu kwanini hawKughairisha tangia zamamni au kwanini waliamua kutumia njia hoyo wakati njia za amani zipo kutatua mogogoro?
Makamanda wenu wangapi wako Rumande hadi sasa?
Utawala upi wa sheria ulioanza kutumika ambao zamani haukutumia?
Chedema gani imeanza kusikilizwa, tena imeanza kusikilizwa na nani? Wakati mtaalamu wako wa kubadili gia angani jana kasema kanpbisaaa wazi kuwa Raisi alishakataaga kuongea na chadema...
We unayemuona kuwa ni mbumbu kama wewe ni nani hasa?
Acha kupenda sana kijana. Usipokubali kumshauri kiongozi wako na ukawa ni mjumbe ndiyooooo hautakuwa na tofautii sana na ccm.
Mlishasema tatzo la wanzania ni kusherehekea kila kitu kinachosemwa na kufanywa na Magufuri, na ndio maana anafanya mambo pasipo kushauriwa... Sasa na wewe na wenzio msipomshauri kiongozi wenu ( mataalamu wa gia) naye ataendelea kufanya mambo ya kijinga na kukurupuka kama mkuu wa kaya na hatimaye chama kitakosa watu na wafiasi kila uchwao...
Amka wewe zuzu....
Sawa mwerevu ila hebu tulia uandike vizuri post yako ina typing errors nyingi sana
Kuwa na typing errors nyingi kiasi hicho ni dalili za kuwa hata huko kichwani hakuko vizuri
Hapa sio whatsapp kwamba uwahi kujibu kabla ya mwingine jibu lako litakuwepo tu kwa mlengwa
 
Watanzania wengi ni wanafiki kiliko unafiki wenyewe, Leo wanajifanya kuimiss chadema ya Dr. Slaa wakati enzi za uongozi wake walikuwa wanamwita mvunja sheria kwa kulazimisha maandamo. Na kweli chadema chini ya Dr. Slaa ilisababisha matatizo makubwa sana ikiwamo vifo ambayo ambavyo vingeweza kuepukika. Leo hii chadema wanasitisha maandamano baada ya kuona kuna watu wamejiandaa kupiga na kuuwa RAIA, wanasema eti CDM kimepoteza mwelekeo. Kifupi ni ujinga mtupu.
Kuna msemo unasema

"ADUI MUOMBEE NJAA".....
Eti kwanini CDM mmehairisha maandamano!
 
Kusikilizwa kupi?? ni lini wameomba kuonana na mkulu wakapuuzwa???? Tatzo sio maandamano wala hekima tatzo iweje waje wahairishe siku moja kabla ya tukio?? kwn hvyo vikao inamaana havikupatiwa suluhu muda wote huo hadi jana asimame na kutoa tamko?? Mbona kipindi cha Jk walikuwa wanaenda kuonana nae na kuweka mambo sawa kwa mustakabali wa taifa! inamaana enzi hizo hawa viongoz wa dini hawakuwepo?? Sema chadema imeshamjua huyu mkulu wa sasa kwmba sio kama yule aliepita na pia ni kauzu ndo mana kwasababu hakuna kipind ambacho ilikuwa na maandamano kama awamu iliyoisha na kupigwa na askar ilikuwa kawaida tu kipind hicho,
Walicho Kitaka CHADEMA Wameshakipata!
Cha kushangaza hata waliotangaza kuwa leo watafanya usafi na wale wapiga kwata mitaani wote hawaonekani kwa sasa. Magari na ndege za kivita nazo zimepaki; hakika watawala wamepigwa bao la kisigino
ahahaha,ni kweli mkuu!
 
Ukuta ni operation iliyofanikiwa kwa asilimia zaidi ya mia kila mwenye dhamana na aliyefikia kudharau upinzani alikosa usingizi na akafikiri afanye nn kuokoa hilo maneno ya kamanda Sirro yametoka moyoni aliwaumizwa sana na kupiga wananchi ambao aliapa kuwalinda na wao na mali zao hakuna mshindi kwenye hili wenye akili wameelewa
Chadema wahuni mnazamia ht jubilei za watu kutafuta umaarufu
 
Wewe jamaa unabusara sana..Mungu akupe maisha marefu ili watu waendelee kuvuna HEKIMA NA BUSARA KUTOKA KWAKO.
 
Baada ya jana kuahirishwa maandamano ya UKUTA kwa mwezi mmoja zimefumuka post za kukejeli hiki kitendo

Kila mtu kasema lake, lakini wengi wakijikita kwenye kusema kuwa eti

-CHADEMA ni vigeugeu
-CHADEMA ni mabingwa wa kubadili gia angani
-CHADEMA inapoteza mwelekeo chini ya Lowassa (utafikiri ndio mwenyekiti)

Kejeli ni nyingi kweli na hili halina tatizo kwakuwa wale waliokuwa wamejiandaa kuumiza wananchi wasio na hatia hawataweza tena kufanya hivyo! Maandalizi yalikuwa mengi na kabambe mno ya kukipaka damu chadema kama maandamano haya yangefanyika
Kichekesho na dhikaha ya kukera sana ni wale wanaojifanya kutaka kuihama CHADEMA eti tu kwakuwa wameahirisha maandamano! Hilo tu likufanye uhame chama? Maandamano yangefanyika wewe ungeenda? Uhame Chadema uende chama gani? CCM? kama kuhama chama kungekuwa rahisi hivyo Lipumba asingeng'ang'ania cuf....unazi wetu uko nyuma ya keyboard tuu lakini waandamanaji wa kweli wasioogopa chochote iwe virungu iwe maji ya kuwasha ile jela, hawapo hapa na hawa wamekubaliana na maamuzi! Hakuna haja ya kutishia kuhama FANYA SASA

Dhima ya CHADEMA haikuwa kuandamana!maandamano huwa silaha ya mwisho kabisa kwenye nchi ya kidemokrasia kama njia zote zikishindikana

CHADEMA kwenye hili wamefanikiwa sana tena sana, harakati za ukuta zimeleta matunda mengi

Maamuzi mengi ya kibabe yamepungua ama kubatilishwa

Kupayuka payuka kumepungua

Utawala wa sheria unaanza kurejewa

Utawala ulioanza kujisahau umekuwa makini zaidi sasa

Viongozi wengi wameamua kuingia kwenye mazungumzo

CHADEMA SASA IMEANZA KUSIKILIZWA NA ITASILIKOLIZWA..hii ndio ilikuwa dhima ya yao KUSIKILIZWA

CHADEMA itasikilizwa bila kusababisha madhara kwa wananchi bila uharibifu wa mali na kwa gharama bei chee kabisa

CHADEMA imepiga hatua kumi zaidi mbele waliokamatwa kwa mashtaka ya kutunga na kunjuka ni viongozi tuu raia hawafiki watano! Huu ni ushindi mkubwa sana
Kama unahama CHADEMA Salam zao huko uendako

una roho ngumu sana
na una mahaba ya dhati hongera
 
Hahahaha kamanda. Hizi ndizo mbinu za kujihami. sawa basi maana naona mishipa ya shingo imekutoka kisa watu wanataka kuhama chama.
 
Kuna watu natural wamezaliwa wanapenda ugomvi kwa hiyo walijipanga kwa ugomvi sasa umezuilika wanaanza kutapa tapa
 
Mimi hasira yangu kutumia viongozi wa dini kujitafutia umaarufu. Nahisi hao ni wale viongozi wa dini njaa tuliyowaona wkt mchakato wa urais ndani ya ccm
Hapana hawa ndio wameombwa na mamlaka za juu wafanye hivyo katu CHADEMA haikuwaomba mazungumzo
 
yaani uko uchi, unajitetea macho ya waonaji nfuo hayaoni
 
Chadema ni sawa na mgonjwa anayepata nafuu na kuumwa. Ni mgonjwa asiye na matumaini ya kupona. Nafuu huja pale kunapokuwa na operation, baada ya operation, mgonjwa hurudi kwenye hali yake. Baada ya operation ukuta ku fail, mgonjwa amerudi kwenye hali yake. Mwenyekiti anapaswa kubuni operation nyingine ya kumfanya tena mgonjwa apate nafuu maana huyu c mgonjwa wa kupona.
 
una roho ngumu sana
na una mahaba ya dhati hongera

Hahahaha kamanda. Hizi ndizo mbinu za kujihami. sawa basi maana naona mishipa ya shingo imekutoka kisa watu wanataka kuhama chama.
Kwenye mjadala kama huu lazima kuwe na mawazo tofauti kama haya..na mtu akikwazika kwa mitazamo kama hii atakuwa mpuuzi kiwango cha lami
 
ndugu yangu inaonekna hukuwa unaelewa dhana ya ukuta, ulidhani suala ni maandamano. suala halikuwa ni maandamano tu.. suala lilikuwa ni kujenga sababu za kusikilizwa ,kuishinikiza serikali.kama serikali inakuwa tayari kuzungumza then muandamane kwa misingi gani? huo utakuwa ukosefu wa akili. na suala hapa si msimamo ninyi ni CCM ndo mnaobaki kuzungumza wakati wa slaa wakat wa slaa kama slaa unampenda sana si ukaishi naye? au mshauri aanzishe chama uhamie huko. nenda kaolewe naye au mpe dada yako. maana hizi reasoning nyingine ni za kitoto dada yangu. wakati wanaume wanapoandamana sidhan kama nawe ulikuwa ni mmoja wapo. ninyi wengine huwa mnakuwa mmekaa mbele ya keyboard kupost picha n.k wakati huo wanaume wapo field. then unakaa hapa eti umekata tamaa. si uhame chama?

Mkuu, kubali tu kuwa THIS IS THE SAD ENDING OF UKUTA, mbona enzi za Slaa chadema walikuwa na msimamo wakisema tunaandana wanaandamana?? Au enzi hizo hakukuwa na viongozi wa dini wa kusuluhisha??
On the positive side, angalau mmewaweka police force on their toes.
 
Siku zote na kili kuwa mwanaccm kindakindaki ila nitamlaani siku zote anayeombea upinzani kufa nchi hii...!
 
Igenja ushawahi Soma katiba ya jmt? Kama umesoma tuambie kipengele kipi tunapigania? Kama hujasoma no right to speak shut up ur mouth
 
Asante mkuu kwa kuliona hili.
Hakuna kiongozi anayetaka
wanachama wake wauawe.
Na hapa ndo tunaipongeza CDM
kwa uamuzi huu,naamini kama ni ujumbe
wameufikisha kwa njia ya amani
kazi imebaki kwa watawala kuufanyia
kazi.
 
You nailed it, CCM kamwe hawataki amani, CCM ni wachonganishi, hapa CCM wamepigwa mbele wakageuzwa nyuma piga kabisa wakagalagazwa. Kumbuka maneno ya Lissu kuwa kuna aina nyingi za Vita kwenye siasa....
 
Ila ni ukweli kua chadema haina maana tena, ipo ipo tu, mradi ipo.
 
Back
Top Bottom