ChaMtuMavi
JF-Expert Member
- Oct 15, 2008
- 330
- 10
Wajamani tuwe waangalifu, it could be "Money Roundering"
Wajamani tuwe waangalifu, it could be "Money Roundering"
Biashara za kufanya upate faida ya kulipa watu zipo ila practicability yake ndio ngumu.
Mfano creti moja ya bia ina faida ya 5000. ukimanage kuuza daily kwa mwezi una 150,000/=. Assuming operation cost zinakuwa covered na muuza chipsi na initial cost isiwe considered. Just consider circulation of the cash.
Naa hii inatoka kwenye circulation ya less than 30,000/=.
Lets think big on the manufacturing industry and something else and conside hawa ni walokole walioamua kushare profit 100% inawezekana.
Just imagine kama wanalink na forever living products and just imagine how much those people wanachuma from the product users and assume all this cash is going to be invested in farming aloevera somewhere???
Lets think +vely and hope hawatutapeli.
ila wahusika TRA please lets have data za uhakika maanake google haionekani hii kitu kabisa.
.....Naungana na wenye wasiwasi na huu mradi ambao una kila dalili ya kuwa Dollarjet na upatu vilivyopata kuwaliza watu siku za nyuma LAKINI maybe, just maybe, inawezekana;
Benki ya CRDB wanatoa riba ya 2% kwa SIKU 30 kwa kila shilingi milioni 100 utakazoweka kwenye fixed account. Hii ina maana kuwa kila bada ya siku 30 milioni mia moja yako itakupa shilingi milioni 2.
Suppose hawa jamaa wana mafungu 10 tu ya shilingi milioni 100 kila moja, ina maana kila mwezi wanaingiza shilingi milioni 20 na kwa maana hiyo baada ya miezi minne wana milioni 80!!
Surely, hii sum can be enough to pay 'wawekezaji' kadhaa walioweka tulaki mbili twao miezi minne kabla, bila kusahau kuwa hao jamaa bado wata-retain asilimia fulani ya hela hiyo kama alivyosema mchangiaji mmoja hapa?
going by this hesabu, maybe, just maybe inawezekana...?!
.....debate sasa basi maana huu ni wizi wa mchana kila mtu anajua, mlio Dar naomba msaidie kuwaripoti hawa watu kwenye vyombo vya sheria kabla ya mwanawamungu na wasioelewa hizi game hawajapoteza mitaji yao,mtakuwa mmefanya good public service na itapunguza umaskini kwa wale wanaoelekea kupoteza pesa zao soon or later,mnaweza kureport police,TRA au wizarani!
.....Naungana na wenye wasiwasi na huu mradi ambao una kila dalili ya kuwa Dollarjet na upatu vilivyopata kuwaliza watu siku za nyuma LAKINI maybe, just maybe, inawezekana;
Benki ya CRDB wanatoa riba ya 2% kwa SIKU 30 kwa kila shilingi milioni 100 utakazoweka kwenye fixed account. Hii ina maana kuwa kila bada ya siku 30 milioni mia moja yako itakupa shilingi milioni 2.
Suppose hawa jamaa wana mafungu 10 tu ya shilingi milioni 100 kila moja, ina maana kila mwezi wanaingiza shilingi milioni 20 na kwa maana hiyo baada ya miezi minne wana milioni 80!!
Surely, hii sum can be enough to pay 'wawekezaji' kadhaa walioweka tulaki mbili twao miezi minne kabla, bila kusahau kuwa hao jamaa bado wata-retain asilimia fulani ya hela hiyo kama alivyosema mchangiaji mmoja hapa?
going by this hesabu, maybe, just maybe inawezekana...?!
Tatizo, hili jambo halikuwa kwa watu wote ninyi, lilikuwa kwa watz wachache ambao ni walokole, hata halikuwa linawahusu. tumewahusisha mmeanza kutuchefua? tutarudisha liwe kwa walokole tu. sisi kama walokole tunaridhika, na maadam tumesha vuna kwa mara nyingi tukapata faida, hatuna shida. hata ikiisha leo hatuna hasara. pilipili usoila inawawashia nini? wanaotumia wamenyamaza kimya, ninyi ambao hamjatumia mnaongea. mnaweza mkamkomvisi vipi mtu ambaye ameshavuna pesa mara kibao, aliweka laki mbili amesha vuna mle takribani million nne tayari, sasa. tunapata faida, na hatutaiacha, na hata kama watu watasema sana, mnachelewa bure, mtasema matokeo yake mtakuja kuujua ukweli wake muda wakati umeisha na ninyi nafasi ya kufaidika imefungwa. kalaga baho.
deci aka tushikamane revolving fund wamesajiliwa na wana tin number
105 797 095.
Maelezo ya waliotangulia yana mapungufu ambayo nitarekebisha hapa.
Kiwango cha chini '' kupanda'' ni sh. Elfu kumi na kiwango cha juu ni sh. Laki mbili. Hata hivyo mtu anaweze kupanda zaidi ya sh. Laki mbili kwa mafungu, mfano ukipanda laki nne unahesabiwa umepanda laki mbili mara mbili. '' kuvuna'' ni mara moja kwa wiki hivyo basi hata kama ukipanda laki nne kwa siku moja lakini wakati wa ''kuvuna'' utazivuna kwa wiki mbili tofauti.
Mahesabu ya kuvuna kwa aleyepanda sh. Laki mbili yako hivi: Baada ya miezi minne laki mbili inakuwa laki tano. Ni lazima utrudishe sh. Laki mbili shambani na wewe unabaki na laki tatu. Katia hiyo laki tatu unakatwa tax ya asilimia 15 ambayo ni sh. Elfu 45. Kwa hiyo unabakiwa na sh. 255,000. Kila baada ya miezi minne cycle hiyo inajirudia. Hivyo basi kwa kupanda sh laki mbili unavuna sh. 765,000 kwa mwaka (miezi 12).
Well cha msingi ni kwamba mpaka sasa waliojiunga hawana malalamiko,ingawa ukweli ni kwamba kuna siku deci itatetereka kwa sababu kadhaa nilizozibaini. Sitazitaja zote hapa kwa usalama wa walioweka pesa zao ila sababu moja kubwa ni ukosekanaji wa professionalism katika money handling.naomba nisilielezee hili kwa undani pia kwa sababu za kiusalama.
Idara ya fedha kama deci ambayo sasa ina pesa nyingi ilitarajiwa kuendeshwa kitaalamu zaidi ya ilivyo sasa.mfano rahisi wa kuchallenge jinsi inavyoendeshwa ni email address yao ambayo ni decitanzania@yahoo.com
deci kama multibillion project inatarajiwa kuwa na domein yake na si kutumia yahoo etc...!!!
Ushauri ninaoutoa ni kwa walio na access na deci wajiunge mapema ili waweze kunufaika kabla muda wake wa kutetereka haujafika. Hakuna anayeweza kusama hadharani muda huo ni lini lakini tukumbuke kuwa no risk, no profit.