DECI Tanzania: Ilivyoanza, ilipo na hatma yake

DECI Tanzania: Ilivyoanza, ilipo na hatma yake

Ukistaajabu ya "credit crunch" utayaona ya DECI!!
Its either they engage in an illegal business or they do the legal business illegally,mayb both.
 
Hizi zinaitwa "pyramid schemes". Hakuna "investment" yeyote inayofanyika kupata faida. (Ukiwauliza watajibu ni siri ya biashara). Ukweli ni kwamba michango ya Members wapya ndiyo waliotangulia wanalipwa......tatizo ni kwamba, baada ya muda fulani wanashindwa ku recruit members wapya kwa vile watu wote wenye interest ni members tayari....inayaofuata ni the BIG CRASH, wanashindwa kulipa faida walizoahidi....na jamaa wanatoweka!! KWA HAKIKA , big crash inakuja...it is only a question of time.
 
hivi watanzania wasichoelewa ni nini??
hao watu wanachofanya ni kukusanya fedha kutoka kwa wanachama wapya na kuzigawa kwa wanachama wa zamani.

here is the catch:
utafika wakati wanachama wapya watakuwa wachache na hawatoshelezi mahitaji ya wanachama wapya.kinachofuata hapo ni hao jamaa wa DECI kutokomea.kwa kuwa nchi yetu hamna anayejali basi jamaa watapeta tu mtaani.

weka pesa zako kwa hao jamaa ila ukae ukijua siku rate ya cash outflow ikiwa kubwa kuliko cash inflow utakuwa mhanga wa utapeli.

najua ni maisha magumu na TAMAA ndio inasababisha haya yote.

Vyombo Vya sheria viko wapi?Hivi TRA and the like ndio wanatoa leseni kwa watu wa aina hii siku hizi??
 
Kwa mtu yeyote mwenye kuifahamu vizuri HIki chombo kinachojishugulisha na biashara ya pesa wao wasema kupanda na kuvuna.. Kila kona ya Dar na baadhi ya Mikoa hapa nyumbani TZ DECI wanakusanya pesa na kurudisha kwa faida kubwa. Tunaomba kuwafahamu vizuri ili tukiamua kujiunga nao tusiwe na mashaka kama yale yaliyowahi kutukuta ya UPATU. Plz wenye data zitakazo tusaidia msisite.


Na ukiamua kujiunga naomba uelewe kuwa ukipanda wakati mwingine jua linakuwa kali na mazao yanaungua... unatoka kapa...
 
Duh kazi kweli kweli.... kama mtu mwenye access na keyboard anaweza kutetea wizi huu wa mchana, tutarajie nini wale wa ndundunyikanza aweze kulinda sanduku la kura.

I thought tunakaribia kufika kumbe bado safari ni ndefu.....
 
Mr. Impossible hakuna anayebisha "mavuno" kuwa hayafanyiki. Hakuna anayekataa kuwa watu wanapata mavuno!! Tatizo hizo mbegu zinapandwa wapi!?

Labda itabidi nitumie vielelezo kufafanua hili; tunachosema ni kuwa hii scheme will have to collapse. Itakapocollapse watakaolia watakuwa wengi zaidi kuliko wale waliovunja na kuchomoka zao! It is not sustainable.

Jamani ninyi mbona mnaingilia mambo ya watu.

Leo mimi hapa nikiwa na mamilioni ya fedha nikaamuwa kuyagawa kwa njia ninayotaka utakuja kuhoji? kwanini nagawa fedha?.

Wakuulizwa ni yule aliyewasajili hao jamaa
 
Wajinga ndio waliwao na kwa walokole hapo wamepata soko. Hata hivyo sishangai sana kwa sababu nchi nayo inaendeshwa hivyo hivyo - kitapeli. Badala ya mlokole weka mtanzania na utaweza kuelewa kwa nini CCM iko madarakani hadi leo. Si mnaona hao wezi wanavyotetewa ?
 
Wajinga ndio waliwao na kwa walokole hapo wamepata soko. Hata hivyo sishangai sana kwa sababu nchi nayo inaendeshwa hivyo hivyo - kitapeli. Badala ya mlokole weka mtanzania na utaweza kuelewa kwa nini CCM iko madarakani hadi leo. Si mnaona hao wezi wanavyotetewa ?
Na CCM inaingia vipi hapo?
 
Swali kubwa hapa ni- ni deal gani hawa jamaa wanafanya hadi kuweza kupata faida kubwa kiasi hicho kwa kipindi cha muda mfupi kama huo? Hakuna mwenye jibu kamili la hili hapa kwenye hii forum, majibu yaliyopo hapa ni assumptions na guess works tu. Ni vigumu kuwadicourage watu wasijiunge wakati kuna mifano hai kibao ya watu kuendelea 'kuvuna'.

Kuna umuhimu wa kulifanyia uchunguzi suala hili- MMK nitashukuru kama utawaandikia hawa mabwana.
 
Sijui hii DECI imeanza lini lakini wachangiaji wanasema miaka almost 3 iliyopita. Kumbu kumbu zangu zinaniambia kuna sheria ya Fraud na money laundering imepitishwa Tanzania within that time frame. Hivyo basi: DECI Ipo kwaa ajili ya kamchezo fulani cha kusafisha hela ''chafu'' kuzifanya zing'ae na kuonekana ni genuine. Hela zinaweza kutokana na madawa ya kulevya, ukwepaji wa kulipa kodi, ufisadi n.k Hivyo capital wanayopokea kwa wanachama ni camaouflage tu.

Kama ni biashara nimewahi kufanya due delligent ya biashara zaidi ya 100 Tanzania kwenye mikoa 17 ya Tanzania bara the only business which has high return ni kilimo cha umwagiliaji, na hasa kilimo cha miwa na stocking ya mazao ambayo unaweza kupata hadi 65% Net profit.

DECI wanapata wapi hiyo faida?
kama ni hiyo scheme ya mmoja anaweka leo kesho mwingine anapewa still kama hakuna anayotozwa riba mwisho wa siku kila mmoja atapata kiasi alichowekeza na sio zaidi ya hapo. Ukipata zaidi ya hapo maana yake kuna mtu anatozwa riba (300%) ama fine ya (300%) Vinginevyo it must be from illegal business.

Je kama wanabiashara fulani wanafanya, je wanahitaji mtaji kiasi gani??? hadi leo haujatosha? (Haijafikia point of diminishing return?). Na kama kuna products wanayouza, je hiyo demand yake ni kubwa kiasi gani kila wakiongeza mtaji wa kununua bado mzigo unauzika faida haipungui na shareholders wanapiwa kwa wakati... HIYO NI MABIBO TU ndani ya DECI hata SIO TANZANIA. Je wamewezaje kukeep secret ya hiyo biashara watu wengine wasiingie? ukijiuliza sana utaconclude ni illegal business tu ndio inatabia hizi.

Vyombo vyote vya fedha vinahitaji kusajiliwa either na BoT ama wizara ya viwanda, Ushirika na masoko kwa maana ya SACCOS, ASCAS, ROSCAS e.t.c Na kunasheria za kuziendesha hizi na SACOOS kubwa kama zilizopo Morogoro Kilombero, Mtibwa, kariakoo na kwingineko pamoja na kutengeneza faida kubwa hazijawahi kutoa faida ya even 40% annual returns. The mentioned saccos have capital of 100millins and two have billions.

Maoni yangu kwa wadau wote hawa ni matapeli ama wamesafisha pesa zao ama wanakula timing tu muda utimie NYANI WOTE NA NGEDERE WATANUNULIWA KWA BEI YA AJABU NA NDIO MWISHO WA SINEMA HIII.

Nitafanya kazi kupata utajiri ama nitacheza lotto ambayo kila mtu anayoprobability sawa ya kushinda- kwa herini
 
Mr. Impossible hakuna anayebisha "mavuno" kuwa hayafanyiki. Hakuna anayekataa kuwa watu wanapata mavuno!! Tatizo hizo mbegu zinapandwa wapi!?

Labda itabidi nitumie vielelezo kufafanua hili; tunachosema ni kuwa hii scheme will have to collapse. Itakapocollapse watakaolia watakuwa wengi zaidi kuliko wale waliovunja na kuchomoka zao! It is not sustainable.


Mwanakijiji:

Baada ya kuvunjika kwa ukomunisti niliwahi kuishi katika nchi zilizokuwa za kikomunisti. Michezo hii ya Pyramid scheme ilikuwa mingi sana. Nchi ikiwa na unemployment kubwa na desperation ya kupata kipato wanakuwa rahisi kujiingiza kwenye mitego. Na hakuna mitego mizuri kama mahekalu ya Mungu.

Watu watuletee basi background za wanaoongoza hiyo taasisi kama hawatakuwa wahitimu wa Washington International University.
 
Sijui hii DECI imeanza lini lakini wachangiaji wanasema miaka almost 3 iliyopita. Kumbu kumbu zangu zinaniambia kuna sheria ya Fraud na money laundering imepitishwa Tanzania within that time frame. Hivyo basi: DECI Ipo kwaa ajili
ya kamchezo fulani cha kusafisha hela ''chafu'' kuzifanya zing'ae na kuonekana ni genuine. Hela zinaweza kutokana na madawa ya kulevya, ukwepaji wa kulipa kodi, ufisadi n.k Hivyo capital wanayopokea kwa wanachama ni camaouflage tu.

Kama ni biashara nimewahi kufanya due delligent ya biashara zaidi ya 100 Tanzania kwenye mikoa 17 ya Tanzania bara the only business which has high return ni kilimo cha umwagiliaji, na hasa kilimo cha miwa na stocking ya mazao ambayo unaweza kupata hadi 65% Net profit.

DECI wanapata wapi hiyo faida??????
kama ni hiyo scheme ya mmoja anaweka leo kesho mwingine anapewa still kama hakuna anayotozwa riba mwisho wa siku kila mmoja atapata kiasi alichowekeza na sio zaidi ya hapo. Ukipata zaidi ya hapo maana yake kuna mtu anatozwa riba (300%) ama fine ya (300%) Vinginevyo it must be from illegal business.

Je kama wanabiashara fulani wanafanya, je wanahitaji mtaji kiasi gani??? hadi leo haujatosha?????? (Haijafikia point of diminishing return??????). Na kama kuna products wanayouza, je hiyo demand yake ni kubwa kiasi gani kila wakiongeza mtaji wa kununua bado mzigo unauzika faida haipungui na shareholders wanapiwa kwa wakati... HIYO NI MABIBO TU ndani ya DECI hata SIO TANZANIA. Je wamewezaje kukeep secret ya hiyo biashara watu wengine wasiingie?????? ukijiuliza sana utaconclude ni illegal business tu ndio inatabia hizi.

Vyombo vyote vya fedha vinahitaji kusajiliwa either na BoT ama wizara ya viwanda, Ushirika na masoko kwa maana ya SACCOS, ASCAS, ROSCAS e.t.c Na kunasheria za kuziendesha hizi na SACOOS kubwa kama zilizopo Morogoro Kilombero, Mtibwa, kariakoo na kwingineko pamoja na kutengeneza faida kubwa hazijawahi kutoa faida ya even 40% annual returns. The mentioned saccos have capital of 100millins and two have billions.

Maoni yangu kwa wadau wote hawa ni matapeli ama wamesafisha pesa zao ama wanakula timing tu muda utimie NYANI WOTE NA NGEDERE WATANUNULIWA KWA BEI YA AJABU NA NDIO MWISHO WA SINEMA HIII.

Nitafanya kazi kupata utajiri ama nitacheza lotto ambayo kila mtu anayoprobability sawa ya kushinda- kwa herini

Unajua shetani hatafuti wa kumfuata kwenye mabaa. Kwa sababu hao tayari anao.
 
Kuna njia kubwa nne za mtu kutengeneza fedha, kuuza kitu (bidhaa, nguvu kazi, huduma n.k), kukopa (ahadi ya kurudishiwa baadaye), kuwekeza kwenye chombo cha fedha (kupata riba n.k), na kupewa za bure (urithi, zawadi, kushinda bahati nasibu n.k)

Sasa kwenye hii DECI jambo moja inaonekana ni wazi:

a. Mtu anawekeza fedha zake baadaye anapata malipo yakiwa na faida ya kuliko kile alichowekeza. Njia hii inatumiwa na benki nyingi (kama siyo zote) ambapo mteja anaweza kuwekeza fedha kwa masharti fulani akitarajia kwamba baada ya muda fulani atapata faida ya kiasi fulani kutokana riba ambayo anaijua tangu awali. Huu ndio msingi wa Akaunti za Akiba, CDS, IRAs na wenzao. Hivyo kwa mteja wa kawaida yeye hajali sana benki zinafanya nini na hela yake lakini anajua kuwa baadaya muda fulani atapata riba (iwe compounded au simple).

b. Kwa benki hazifanyi huduma ya bure. Zinapofanya hilo la (a) hapo juu (yaani kuchukua fedha za wateja) hawazikalii fedha hizo bali wanazizungusha katika biashara mbalimbali au hata kuziuza kwa taasisi nyingine n.k ilimradi kwamba zile fedha zinatumika kuzalisha faida huko zinakozungushwa. Wanafanya hivyo wakijua kwamba mteja hatorudi kuzichukua fedha zake hadi miezi sita ipie. HIVYO, benki itazungusha fedha hizo ili hatimaye ziwe na faida zaidi ya faida ambayo ataipata mteja. Kwa mfano, kama mteja aliweka Shs 100,000 na anajua kuwa baada ya miezi sita atapata 50,000 zaidi, basi ile benki lazima iwe na uhakika kuwa itakapozungusha hizo fedha huko itapata faida ya zaidi ya 150,000 (say 175000).

Hii ina maana ya kwamba, mteja atakapokuja baada ya miezi sita atachukua hela yake ya awali na faida (150,000) na Benki itabakiwa na 25,000 kama faida yake.


c. Sasa Benki haiwezi kutoa fedha tu za faida bila yenyewe kutengeneza faida vile vile. Hivyo kwenye hii DECI maswali yanayokuja ni kwamba hao jamaa wao wanapata faida gani?

- i. Haiwezi kuwa ni ada, kwani kwa kadiri ya kwamba wanacholipa wateja wao ni zaidi sana ya fedha waliyoingiza ile ada inakuwa cancelled na malipo hayo.

- ii. Bila ya wao wenyewe kuwekeza kwenye mzunguko mwingine wa fedha (aidha kwa kuchukua fedha hizo na kufungua akaunti yenye riba kubwa) wao wanapataje faida? Kama wamekusudia kuwekeza fedha benki, lazima hiyo riba iwe kubwa mno. Nimeangalia CRDB ambao rate yao ya juu ni asilimia 7 (kwa miezi 12, 24) kwa kiasi chochote kuanzia bilioni moja kwenda juu.

Kwa Wekezo la miezi tisa kwa shilingi milioni 100 rate yake ni asilimi 4.5. Hii ina maana ya kuwa baada ya miezi tisa ukiwekeza milioni 100 unapata milioni 4.5 kama faida. Sasa kama ni mtu mmoja hiyo siyo mbaya sana hasa ukijua kuwa kila baada ya miezi tisa unapata karibu milioni tano unaweza usifanye kazi yoyote ile! Sasa hawa DECI wao wanawekeza kwenye nini?

d. Njia ambayo naweza kuiona kwa jinsi ilivyosimuliwa humu ni kuwa wao wanazungusha fedha za mteja wa leo kwenda kumlipa mteja wa jana! na gurudumu linaendelea vivyo hivyo. Katika mtindo wa namna hiyo haijali sana riba wala nini inajali idadi ya watu wanaojiandikisha na muda wanaotakiwa kusubiri kupata "mavuno yao".

HIvyo ukijiunga leo na kutoa laki mbili. Watakuambia usubiri hadi miezi minne ipite halafu ukija baada ya miezi minne unapewa laki tano (yaani laki tatu zaidi). Sasa unajiuliza wao wametoa wapi hizo laki tatu? Jibu ni kwa wale waliojiunga nanyi ndani ya miezi ile minne. Fedha uliyotoa wewe ya laki mbili inatumika kuwalipa wale waliokuwa kabla yako.

Hii ina maana gani? Ina maana ya kwamba ili kumlipa aliyeahidiwa laki tano baada ya miezi minne inahitajika watu wengine wawili walijiunge!

TATIZO:
Kwa kadiri ya kwamba mtindo huo unategemea wateja wapya na unaendelea kuahidi mavuno makubwa, basi hatima yake ni kuanguka au kuporomoka kwani baada ya watu wote kujiunga na mtandao huo wale wanaoingia mwisho watajikuta hakuna wa kuwalipa wakati wale walioingia mwanzoni watakuwa wameshakuwa matajiri wa haraka haraka!

So, mtu atutafutie majibu kuwa hawa jamaa wanauza nini na wao wanatengenezaje faida ya kuwalipa watu kiasi hicho kikubwa cha fedha?

Hii Narrative ya MMJ imeelezea vizuri sana scheme yenyewe. Kwa watakaowahi, watafaidika. Shida itakuja pale pool itakapokuwa exhausted, hapo ndio kutakuwa na vilio na kusaga meno. Vyombo vyetu vya sheria vilitakiwa kuliona hii mapema. Mradi huu ni pure Ponzi scheme.
 
Mwenye macho haambiwi tazama. Kwa vile tumesema lakini hawatusikilizi, tuna haki ya kunawa mikono kama Pilato. Pia sikio la kufa halisikii dawa.

Kwa sababu watu wengi (hasa hasa WaTz) wanapenda vitu vya dezo bila kufanya kazi, ndio maana wamegeuka omba omba kwa viongozi (wabunge, Mawaziri na hata JK). Kwa hiyo hapa watakimbia tu kama nguruwe kuwahi DECI, bila kujua kama huko ni machinjio au la. Lawama zangu ni kwa serikali yenye jukumu la kusimamia sheria. Kama hili hawalishughulikii basi ni kosa lao. Hata hivyo sitashangaa kama na wakubwa nao wamepeleka vijisenti vyao huko!! Maoni ya watu wengine humu ndani yanadhihirisha kuwa baadhi yetu tumepoteza muda bure kwenda shule!!
 
This is another Ponzi Scheme we have seen people losing money from Dollar Jet and Women Empowering Women, those who were conned from these schemes will never forget.
 
Mwenye macho haambiwi tazama. Kwa vile tumesema lakini hawatusikilizi, tuna haki ya kunawa mikono kama Pilato. Pia sikio la kufa halisikii dawa.

Kwa sababu watu wengi (hasa hasa WaTz) wanapenda vitu vya dezo bila kufanya kazi, ndio maana wamegeuka omba omba kwa viongozi (wabunge, Mawaziri na hata JK). Kwa hiyo hapa watakimbia tu kama nguruwe kuwahi DECI, bila kujua kama huko ni machinjio au la. Lawama zangu ni kwa serikali yenye jukumu la kusimamia sheria. Kama hili hawalishughulikii basi ni kosa lao. Hata hivyo sitashangaa kama na wakubwa nao wamepeleka vijisenti vyao huko!! Maoni ya watu wengine humu ndani yanadhihirisha kuwa baadhi yetu tumepoteza muda bure kwenda shule!!

Mchelewa Bus husafiri amesimama au huwachwa kabisa.

Hakuna biashara duniani isiyokuwa na hasara, tatizo linakuja ni jinsi gani umejipanga na kuamua kuingia kwenye biashara husika.

Watanzania wengi ni waoga sana kujiingiza kwenye biashara. zitokeapo nafasi za kujikwamua watu wataleta mashaka ya kila namna. lakini ukweli wale wasiokuwa waoga kwenye kuwahi nafasi za mafanikio ndio hao wanaofakiwa, na wale wanaositasita kama wengi wa humu JF mtabaki kuwa mashabiki wa maneno ya kudauti na kupinga wakati wengine wakiendelea kufaidika.

DECI inatambulika na BOT na ina vibali vyote vya kisheria vya kufanya huo mradi wa uzungushaji hela. Hicho kiwango cha 200 000 waliekewa na BOT kwa asbabu hizo hizo za udhibiti wa mzunguko wa hela. Kama serikali imekuwa tayari kutoa hadi ulinzi wa kipolisi kwenye hichi chombo hiyo inaashiria kuwa Serikali unauelewa vizuri huo mfumo wa DECI na ina uhakika wananchi hawatoumizwa kwa namna yoyote.

Tatizo la DECI ni matatu haswa

1. Maeneo wanakofanyia kazi zao hakujakaa vizuri, kuko hatarishi kiusalama japo kweli kuna Polisi pale kila wakati.

2.System yao ya kuendesha huo usajilini hauko madhubuti kabisa, kiasi kuwa hata ikitokea leo wamesitisha mradi hakuna atakaeweza kudai na akaweza kulipwa. watu wanatambuliwa kwa risiti, ambapo kama leo risiti yangu ikiibwa au ikipotea sina jinsi tena ya kudai hela.

3. Watu wanaruhusiwa kuwa na accounts za idadi yoyote kwa majina yoyote. Hivyo kwa hiyo kama ikitokea mtu husika amefariki na hakuacha wazi kuwa mrithi wa fedha zake ni nani basi DECI itazifaidi hizo fedha maana hakuna mfumo wa madai ambao unaweza kutumiwa na ndugu wa marehemu kwenda kudai hela za marehemu wao.

Kwa kweli yapo mambo mengi sana ya kiutawala yanatakiwa yaboreshwe pale la sivyo siku ukitokea mkanganyo itakuwa balaa maana kwa uhakika hawa watu wanazungusha hela nyingi sana kwa siku. na nina imani Account zao zitakuwa na Bilions of money.

Anaetaka hela za faster ajiunge. humu hadi wabunge wetu na watu wengine wakubwa tu wa serikali na taasisi binafsi na za umma wamejiunga na hii network ya DECI.

Tokea DECI ianze kuna watu wamejenga, wamefungua miradi mikubwa tu, wanasomesha na kulea familia zao kwa hela za DECI. Huu usemi wa DECI itakufa haukuanza mwaka huu. Kweli inaweza kuja kufa lakini wanasema "kifo cha wengi Harusi" Chukua Chako Mapema, Chelewa chelewautakuta mwana si wako, kelele za chura hazizuii tembo kunywa maji, KABLA HUJALA LAZIMA UWE TAYARI KULIWA KWANZA.

Mwanakijiji na wengine karibuni Deci tuzikong'oli noti
 
Duh kazi kweli kweli.... kama mtu mwenye access na keyboard anaweza kutetea wizi huu wa mchana, tutarajie nini wale wa ndundunyikanza aweze kulinda sanduku la kura.

I thought tunakaribia kufika kumbe bado safari ni ndefu.....
Masatu hii haina Msomi wala kabila, Watanzania kwa dezo acha kabisa, wakati wa UPATU ndugu yangu msomi mzuri (Graduate) tena mwalimu wa A level yeye kwa miezi kadhaaa alinishupalia nijiunge nilikuwa nikimuuliza maswali haya haya kwamba Upatu wanabiashara gani kuweza kulipa vile?

Hakuwa na jibu ila mifano hai ya waliolipwa pamoja na yeye, Siku ya siku akaanza safari za siri na sikujua anafuatilia nini Dar mara ikatangazwa redioni kuwa wameliwa ndipo niliishia kumpa pole, na kwa hawa hata upige risasi sikioni hawatasikia milele hivyo tukae tusubiri kishindo kwani kama kuna nyomi ya wanaojiunga sasa bila kificho basi tusikilizie kishindo hivi karibuni
 
Sikujua hata Bernard Madoff keshafika TZ. Huko mbele kuna watu watalia kwenye hili.

Thank you for this. The scheme DECI operates is exactly like what Madoff did. DECI will DEFINITELY collapse - Its just a matter of time!
 
Wtz wengi ni waoga wa kujaribu vitu. Deci mwanzoni ilikuwa ni organisation ambayo ilikuwa ni special kwa walokole tu. walioianzisha ni walokole, na wanaoiendesha hadi sasa ni walokole, yaani watu kama mimi hapa ninayeandika, mlokole. ninaifahamu kiundani sana. the main purpose of this Deci, ilikuwa kama kuwainua walokole, waumini wa kanisa. lakini, kwasababu ulokole/wokovu unahitaji upendo, na watu walipolalamika(wasiokuwa walokole), Deci ikaamua kupokea hata wasio walokole. hadi sasa hivi inaendeshwa na watu wa Mungu, ninao wafahamu. wachungaji kibwena wameweka pesa zao kule na wanakula faida kila wakati. kuna waislam pia wengi sana, wengi wao wanawake, wameweka pesa hapo na wanapokea pesa kibao. wengine wamejenga kwa njia hii. kuna wakati mwingine huwa wanakatishwa tamaa halafu wanajaribu kuirudisha kwa walokole(kwasababu watu wengine wanawaletea fujo...sina uhakika na hilo ila) lakini huwa wanajirudi na kuendelea kuwapenda. in short, hii ilikuwa ni njia ya kusaidia walokole lakini kwa upendo, wamewapokea hata wasio walokole. walokole wanafaidika sana na hii, na wasio kuwa walokole pia. kila mtu anakaribishwa, lakini halazimishwi.

hii ni challenge kubwa kwa watu wa dini zingine, hasa zinazojifanya zina pesa. walokole wanasapotiana sana wao kwa wao, lakini wengine wamelala fofofo. hii nchi kwa kifupi, inaenda kuendeshwa na walokole, na ndio walioishika hii nchi kwa sasa. Mungu wao anawasaidia. angalia makanisa makubwa yanayojaa kila siku, na wachungaji wao wana influence kubwa sana, wanaweza wakafanya hivyo hata kisiasa mtu asipigiwe kura, na ikawa hivyo. kwasababu waumini wana imani sana na mchungaji. walokole wamejenga mashule mengi(pamoja na kwamba roman catholic na lutheran ndio vinara kwa hili). hii ni muhimu pia kwasababu, ulokole sasa haujawa wa dini moja, kuna walokole lutheran,roman na dini zingine, hivyo nawezakusema ukristo sasa umekuwa ulokole kwasababu movement ya waumini kwa sasa si kitu cha kushangaza toka dini moja kwenda ingine, zote zina feel one. kwa kifupi, kila kanisa kubwa hapa bongo, hata mikoani, yanajenga shule za kilokole, na watoto wanakuzwa kimazingira ya kilokole. wanapata sapoti hata kama hawana hela. wanasaidiana sana, na tunajivunia kwa hilo. Deci imesaidia walokole lukuki, mimi na my wife wangu pia, tuliweka hela ya mboga, na huwa tunachuma kila baada ya miezi mitatu zaidi ya million. hiyo ya mboga tu na mafuta ya gari. inatupa faida infact.

Wanaowekeza wasubiri maumivu. Yatakuja tu.
 
Back
Top Bottom