Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,786
- 1,710
Well mimi katika DECI nimepanda 2Million ambazo zimepelekwa kwa laki 2 kila mpando so mpaka sasa zote zimeshatoa mavuno ya kwanza ambayo ukishatoa makato ya 15% nimepata 2,550,000 ambayo ni kutoka July 08 mpaka Jan 09. Nilipovuna nilipanda tena so kati April na June 09 nitavuna tena 2,550,000. Ukilinganisha hizo hela kama ningeziweka bank nisingeweza kupata hiyo faida. Hivyo si lazima uweke mahela kibao weka kidogo ikusaidie katika mambo madogo kama fees za watoto au hata biashara za kawaida.
Mimi ushauri wangu ni kuwa ni kweli hii system haileweki kwa undani lakini office ziko wazi pale mabibo na kwenye attachment zangu za jana nimeonyesha kuna simu wapigie watakupa majibu.
Hawa jamaa wanautaratibu kwani ukilipa unapewa receipt ambayo utakwenda nayo ukienda kuvuna na pia kuna registration ambayo unapewa kitambulisho. Kwenye receipt yao kuna mpaka TIN NUMBER kwahiyo wanafanya kazi ya halali kabisa.
Tufuatilie kwa undani tusiwakatishe tamaa wengine ambao kwa kweli wana mahitaji ya kweli katika huduma kama hizi. Tusiwe sana negative katika kila kitu. Tufuatilie ili kama kuna utata tuambiana.
Thanx
Kwamba tayari watu wamenufaika hakuna anayekataa.
Kwamba kuna watu wanataka kukatisha tamaa wengine wasipate kipato, sidhani kama ni hivyo.
Kwamba wanaopinga hawajafanya utafiti sawasawa. Sina hakika.
Nilicho na hakika, watu wanahoji msingi wa hili. Na wanaoohoji msingi, naamini ni watu wa fikra, si watu wa juu juu.
Ndugu zangu sehemu mbalimbali duniani watu wameamini michezo hii na wakalizwa. Naweka link hii hapa muone jinsi Columbia watu walivyopoteza mabilioni ya pesa, kwa scheme kama hizo ambazo waliziamini mno, ndo maana wakajiunga kwa wingi.
http://www.latinalista.net/linkinglatinas/2008/11/colombia_pyramid_money_scams_fall_down_a.html
Moja ya picha ya waliolizwa ni hii hapa kwenye attachment. Wakati huo too late!
Well, kama systems kama hizo zingedumu milele, kwa nini watu wangehangaika na pesa za kutokea jasho????
Lakini kama watu wote pia wangepata mahitaji yao katika system kama hizo, uzalishaji wa mahitaji muhimu ungekoma..... Well, at least sioni kama mapato ya hivyo ni sustainable, unless DECI watuoneshe huo mgodi wa dhahabu wanaozalisha za kuvunisha watu.
Mnapojibu mjue tunatafiti.
Attachments
Last edited: