Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,232
- 113,610
I hate Silencer and Painkiller
kama ni wezi wamemuibia nani? ninao ndugu zangu wengi tu, nimewakopesha pesa, wakaenda kuziweka huko. wameshavuna mavuno karibia mawili. unaweza ukaweka hela za mtoto wako mmoja mmoja,dada zako hata shangazi nk. na utapata. kuna watu wanavuna karibia kila baada ya miezi mitatu, kutu kama million hadi tano pale, kwasababu waliweka zamani, na ile pesa waliyoingilia walishaipokea na wana kulaga faida. Kwa kifupi DESI SIO KWAMBA WANAKOPESHA AU NINI, NI SAWA NA UMEPANDA MTI WA MATUNDA, HIVYO UNAKUWA UNAVUNA KILA WAKATI HADI MTI HUO UTAKAPOZEEKA. unaweza ukavuna pesa za deci hadi miaka 50. ina faida sana. mimi nilifikiri ni wanigeria mwanzoni, nikaenda kuweka pesa pia, na nimepokea mihela kibao. wapo pale mabibo mwisho, watu wanapaki magari yao pale wanaweka hela na kuondoa. inasaidia sana, na kuna watz wengi wanaishi kwa hiyo.
...acha kutetea upumbavu,hawa matapeli wanatakiwa kusimamishwa kabla ya kupelekea watu vilio!
Recta, wanazungusha hizo fedha kwenye biashara gani inayoweza kulipa faida ya zaidi ya asilimia 300 kwa mwekezaji mmoja? ukinionesha na mimi nitawatumia dola 200 niingie maana KLHN inahitajia kamtaji kanguvu! shoot..
Hahahaha, Mkuu MKJJ, zipo biashara kadhaa zinazoingiza pesa nyingi tu. Miezi minne kupata faida ya mtaji wako mwenyewe ya 250% si nyingi, hasa kama unaijua vyema biashara hiyo. Mabenki hufanya biashara kubwa na pesa zetu kidogo kidogo tunazoziweka (kwa siku). Inawezekana. Swala ni je, itadumu?
Nafahamu zipo biashara za namna hiyo hata bahati nasibu, n.k sasa hawa Deci wao wanazungusha kwenye biashara gani? Wanawekeza kwenye vitu gani?
...kwenye stock market
...unapata ngapi kwenye biashara yako ya bongflava na camcorder?
mama yangu mzaazi aliniomba million moja nikampa laki tano akachanganya laki tano zake akapeleka kweli amevuna na akataka kunirudishia namwambia apande tena aiongezee so tunasubiri mwezi wa tatu tena kama neeme itaendelea hivi ...nitawakumbuka na nduguzangu wa JF....