DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Na kwann pia wananchi wanachangishwa pesa kuunganishiwa maji? Tukija ofisini kwenu mnatoa visingizio vya vifaa hakuna itachukuwa mda mrefu mno kupatikana. Mtu aingie mfukoni kununua marola ya mipira konektaz sijui makitu gani huko....kwann inakuwa hivi?

Unanunua mipira na migarama mingine ili upate maji wanakufungia af maji enyewe wanakua wanatoa mara 2 kwa mwezi tena kwa nusu saa
 
Unanunua mipira na migarama mingine ili upate maji wanakufungia af maji enyewe wanakua wanatoa mara 2 kwa mwezi tena kwa nusu saa
Halafu wakija wana majibu rahisi rahisi tu kwamba kama una haraka lipia kuna huna haraka basi endelea kuwepo kuwepo
 
Ninakaribia kuwafungulia kesi ya jinai kwa kuja kufanya uhalifu nyumbani kwangu
 
DAWASA bwana, mnanifurahisha sana, rangi nzuri ila watendaji wenu wamejaa ukiritimba wa hali juu.,. Waambieni hii ni biashara sio huduma ya bure...
 
Dawasco kulikoni kiwalani mmetuondoa kwenye maji yetu ya visima mkatuletea yamgao na saa nyingine hayapo kabisa tuambieni
Kuna shida gani tujue
 
Tabata Segerea kwa kweli bado hatujajua kosa letu, maji hamna wiki ya tatu na yakija yana toka kidogo mno kuna tatizo?
 
Watanzania amkeni, Dawasa inafanya biashara ya kuuza mipira ya maji mita pamoja na koki.

Dawasa hawana uwezo wa kutowa huduma ya kusambaza maji.

Mwenye masikio na asikie na mwenye kuelewa aelewe.

Mkombozi pekee wa tatizo la maji ni wananchi wenyewe, chaguweni viongozi imara wa mitaa, undeni kamati zenu hakikisheni mnapata visima vikubwa vya kuhudumia mtaa mzima mpaka kata.

Dawasa ni chombo cha propaganda za kisiasa kutowa takwimu za mafanikio ya serikali na siyo taasisi ya kuwapa huduma bora za maji wananchi.

Kama una pesa ya kununuwa gari IST used ni bora pesa hiyo uchimbe kisima kirefu nyumbani kwako na hawa Dawasa achana nao kabisa.
 
Dawasa Tabata nimeleta form za maombi ya maji nikaambia surveyor atakuja ndani ya wiki moja. Wiki ya pili sasa hamjafika. Kama survey tu wiki mbili kuubganishiwa maji si itakuwa miaka miwili.?
 
Hivi inakuwaje hawa vijana wenu mnaowatuma kufatilia bili wanakosa lugha nzuri ya kuongea na wateja,
Na wana mihemko sana, muwafundishe vizuri namna ya kudeal na wateja....

Ndio gharama ya kupeana kazi kwa kuwekana mtoto wa mjomba mwisho mnaweka watu wasiojielewa
 
Dawasa tabata nimeleta form za maombi ya maji nikaambia surveyor atakuja ndani ya wiki moja. Wiki ya pili sasa hamjafika. Kama survey tu wiki mbili kuubganishiwa maji si itakuwa miaka miwili.?
Mie Surveyor alikuja ila wanasema vifaa hamna.Sijui mwaka gani vitakuja kupatikana.Eti Corona.

Sasa najiuliza mbona magari yanakuja tu toka nje,tulikuwa DT Sasa hivi DU tena namba zinatembea hatari, inakuaje vifaa vya DAWASA ndio visije?
 
Segerea karibia week ya pili hamna maji ,hivi mnajielewa kweli ?
 
Dawasa hii imekaaje!!unakuta mtaa wa kwanza haupati maji!!! Ila mtaa wa pili unapata maji?? Wakt bomba ni hilo hilo
 
Mie Surveyor alikuja ila wanasema vifaa hamna.Sijui mwaka gani vitakuja kupatikana.Eti Corona.Sasa najiuliza mbona magari yanakuja tu toka nje,tulikuwa DT Sasa hivi DU tena namba zinatembea hatari,inakuaje vifaa vya DAWASA ndio visije?
Ndiyo wanavyodai corona imesababisha ukosekanaji wa vifaa.
 
Asante kwa huduma yenu lakin hiz mita mnasomaje kwasababu naona bill inaongezeka kila mwezi wakati matumiz Ni yaleyale nikiuliza wanaosoma izo metre wanajibu utatumiwa message
 
Back
Top Bottom